Hivi Wajua, kunywa maji mengi ni janga kwa afya yako? | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 1 December 2016

Hivi Wajua, kunywa maji mengi ni janga kwa afya yako?


KUISHIWA maji mwilini ni adui wa siku zote wa mwanariadha. Dhana hiyo iko mara zote akilini kwa mshiriki wa mashindano ya mbio ndefu za Marathon.

Lakini, unafahamu kwamba kwa upande wa pili wa shilingi ni kwamba, mtu akinywa maji mengi kupita kiasi nayo ina athari zake na hasa tendo hilo linapokosa usimamizi sahihi?

Hivyo katika hilo, hupaswi kuwa kama wanariadha wa Marathon, ambao wanaishia kuwa waathirika wa kile madaktari wanachokiita ‘sumu ya maji.’

Sumu ya maji hutokea pale mtu anapotumia maji kupitia kiasi na kupunguza kiwango cha chumvi mwilini kutokana na ziada ya maji.

Mtaalamu, Dk. Aaron Baggish, wa jijini Boston, Marekani, anasema sumu ya maji hutokea maji yanapozidi kwenye damu na kupunguza kiwango cha chumvi, hali inayoleta madhara katika afya ya mwanadamu.

“Inapotokea kiwango cha sodium (chumvi)ni kidogo katika damu, inawezesha maji kuingia katika mishipa midogo, “ anasema Dk. Baggash.

Mtaalamu huyo ambaye pia ni bingwa wa maradhi ya moyo katika kituo cha afya kilichoko jijini Massachuset, Marekani anafafanua kuwa hali hiyo kitaalamu inajulikana kama Hyponatremia.

Kwa mujibu wa daktari huyo, ubongo wa binadamu ni moja ya viungo vinayoathirika na mabadiliko ya kiwango cha maji katika damu, kwani ina kawaida ya kuvimba maji ya kwenye ubongo yanapohama kwenye mishipa midogo.

Miongoni mwa athari ni mtu kujihisi kuchaganyikiwa, maumivu ya kichwa na anajihisi kutapika na mwisho wake si mzuri, kwani mtu anapata magonjwa makubwa ya yanayohusiana ubongo, ukiwamo unaojulikana kama ‘brain stem herniation.’

"Ubongo ni kituo laini ambacho kipo kwenye fuvu. Inapotokea ubongo, kuna sehemu moja tu inapoweza kujitoa, nako ni chini ya fuvu ambako kuna uwazi unaounganisha ubongo na uti wa mgongo," anasema Dk. Baggish.

Mtaalamu Dk. William Roberts, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Madaktari wa Wanamichezo wa Marekani, anasema ni mara chache kushuhudiwa vifo vinavyotokana na matumizi ya maji yaliyopitiliza.

"Pengine inagusa vifo vya kama nusu dazeni (watu sita) kati ya watu milioni tatu hadi nne, kwa hiyo siyo sababu ya vifo vingi," anasema Prof. Roberts kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota, Marekani.

Pia anafafanua kwamba, kulingana na mazingira yao kiafya, kuna uwezekano mkubwa wa wakimbiaji wa Marathon wakafa kwa maradhi ya moyo

Hata hivyo, Dk. Baggish anasistiza kuwa ni rahisi mtu kushuhudia suala la ufuatiliaji matumizi ya maji katika michezo ya Marathon, kuliko watu wengine hospitalini.

Suala la ‘sumu ya maji’ athari zake zinaenda mbali zaidi, kwani hata kwa wacheza soka kuna tukio la mwaka juzi, kijana mwenye umri wa miaka 17 alifariki jijini Georgia, Marekani baada ya kudaiwa kunywa vitu vya maji wakati akiwa mchezoni.

MATUKIO YA VIFO

Pia nchini Uingereza, kuna mwanamke mwenye umri wa miaka 47, mwaka 2006 alifariki baada ya kunywa maji mengi, huku akitembea umbali mrefu.

Pia huko California, mwanamke mwenywe umri wa miaka 28 naye alikufa mwaka 2007 kwa ‘sumu ya maji’ baada ya kushiriki shindano la redioni la kunywa maji,.

Mapema mwaka huu, kijana Andrew Schlater mwenye umri wa miaka 27, alifariki alipokuwa akifanya mkakati binafsi wa kusafisha mwili kupitia kunywa maji mengi.

Kwa mujibu wa baba wa marehemu, Frank Schlater, mkazi wa Rowayton, Marekani, marehemu alishuhudiwa akinywa mengi kupita kiasi hali iliyowatia shaka, ingawaje hakuonyesha mabadiliko ya kiafya.

Wazazi walimuasa aache mwenendo huyo, akakataa na siku moja alikutwa jikoni yuko hoi na alipowaishwa hospitalini kwa matibabu, aligunduliwa ana tatizo la ubongo litokanalo na kunywa maji mengi. Alifariki muda mfupi baadaye.

"Huwezi kuamini maji yanaweza kukudhuru," anasema Mzee Schlater.

BALAA LA MARATHON

Prof. Roberts anasema kuwa, wanariadha wa Marathon, wako katika balaa zaidi, kwani wanapokimbia kwa kipindi kirefu, maana yake ni kwamba wanakunywa maji mengi zaidi ndani ya kipindi kifupi, kuliko wenzao wa mbio fupi.

"Wakimbiaji wa mbio fupi wana muda wa kutosha wa kunywa maji,” anasema Prof. Roberts na kuongeza:

"Kama upo pale pale kwa saa sita na unasimama katika vituo vya maji na kunywa zaidi ya mahitaji yako, utaishia katika hali hii (kuugua).”

Daktari mwingine, Robert Glatter, anapendekeza mbadala kuwa mtu atumie chumvi wakati akiwa mbioni hali inayomuweka mbali na balaa litokanalo na kunywa maji mengi.

Dk. Baggish anawashauri wanariadha wanywe maji pindi wanapokuwa na kiu na si vinginevyo, hali itakayowasaidia kuondokana na na athari itokanayo na maji mengi kwenye damu.

Je, mtu anatakiwa kunywa kiasi gani cha maji kwa siku? Kimsingi, hakuna kiwango sahihi kilichokubalika kwa jumla, ingawaje kuna watu waliofanya utafiti na kupata majibu ya kiwango.

Wataaluma kutoka Taasisi ya Afya ya Marekani, wanapendekeza kwamba mwanaume mwenye umbile la kawaida, anapaswa kunywa wastani wa lita tatu za maji kwa siku, ambayo ni sawa na vikombe 13 na mwanamke ni lita 2.2, sawa na vikombe tisa.

Hata hivyo, wataalamu wa Kituo cha Kliniki cha Mayo Marekani, wanaenda mbali na ushuri wai kwamba wastani wa kile anachokunywa mtu kwa siku ni cha unyevu kwa ujumla ikijumuisha maji na vingine kama vile juisi na chai.
Muungwana blog

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us