Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Akamatwa Kwa Rushwa ya Ngono Dar es Salaam | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday 13 January 2017

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Akamatwa Kwa Rushwa ya Ngono Dar es Salaam

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usifirishaji (NIT) amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Konondoni baada ya kunaswa katika mtego wa rushwa ya ngono.

Mhadhiri huyo anayefahamika kwa jina la Samson Jovin Mahimbo (66) mkazi wa Makongo Juu, Dar es Salaam alikamatwa jana Januari 12, 2017 katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kama Camp David iliyopo eneo la Mlalakua, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Samson Mahimbo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego kufuatia taarifa iliyotolewa na mwanafunzi huyo aliyeombwa rushwa ili aweze kumpatia alama (marks) nzuri  katika mtihani wake wa marudio (supplementary examination) alioufanya tarehe 5 Januari 2017.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa tuhuma za kufanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2017.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us