MPYA: HAYA HAPA MAJINA YA WALIMU WALIOTUMA VYETI VYAO WA STASHAHADA NA SHAHADA YA SAYANSI UALIMU | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday 13 January 2017

MPYA: HAYA HAPA MAJINA YA WALIMU WALIOTUMA VYETI VYAO WA STASHAHADA NA SHAHADA YA SAYANSI UALIMU


Image result for serikali ya tanzania 


TAREHE 12/12/2016 WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILITANGAZA KUWA WAHITIMU WA STASHAHADA NA SHAHADA ZA UALIMU KATIKA MASOMO YA SAYANSI (FIZIKIA, KEMIA, BIOLOJIA) NA HISABATI WA MWAKA 2015 WAWASILISHE VYETI VYAO KWA


     AJILI YA UCHAMBUZI WA WAHITIMU WENYE SIFA.

WAHITIMU WALIOKUWA NA MAPUNGUFU KATIKA NYARAKA ZAO WANATAKIWA WAWASILISHE TENA. WAHITIMU HAO NI KAMA IFUATAVYO:-
     (1) WALIOTUMA NAKALA ZA “RESULTS SLIPS” AU “ACADEMIC TRANSCRIPTS” BILA NAKALA ZA VYETI HALISI VYA KIDATO CHA 4, 6, STASHAHADA AU SHAHADA
     (2) WALIOTUMA NAKALA ZA VYETI VYA STASHAHADA ZA UZAMILI (POSTGRADUATE DIPLOMA IN EDUCATION – PGDE) BILA NAKALA ZA “VYETI VYA SHAHADA YA KWANZA PAMOJA NA “ACADEMIC TRANSCRIPTS” ZAKE;
WAHITIMU AMBAO HAWAKUTUMA KABISA NAKALA ZA VYETI VYAO WANAPEWA FURSA YA MWISHO KUTUMA.
WAHITIMU AMBAO NYARAKA ZAO ZILIWASILISHWA MAJINA YAO YANAPATIKANA KATIKA LINK HIZI .
WAHITIMU WALIOPO KWENYE ORODHA HAPO JUU WASIWASILISHE NYARAKA HIZO TENA.
UTARATIBU WA KUTUMA VYETI NI KAMA IFUATAVYO:-
  1. WAOMBAJI LAZIMA ‘WA-SCAN’ VYETI HALISI (ORIGINAL CERTIFICATES - KIDATO CHA 4, 6, STASHAHADA, STASHAHADA YA UZAMILI AU SHAHADA) NA SIYO KIVULI CHA CHETI (PHOTOCOPY) ;
  2. WAOMBAJI WA STASHAHADA YA UZAMILI (PGDE) NA SHAHADA LAZIMA ‘WA-SCAN’ NA KUTUMA NAKALA ZA “ACADEMIC TRANSCRIPTS” ZA SHAHADA YA KWANZA.
  3. WAOMBAJI LAZIMA WAWEKE NAKALA ZA VYETI VYAO VYOTE KWENYE ‘FILE’ MOJA LIKIWA KATIKA ‘PDF’ NA LIPEWE JINA LA MWOMBAJI HUSIKA KABLA YA KUTUMA. NYARAKA ZITUMWE KUPITIA ‘BARUA PEPE’ ZAO WENYEWE NA SIYO ZA WATU WENGINE.
TANBIHI:
  1. WAOMBAJI WATUME TAARIFA ZAO KUPITIA BARUA PEPE YA WIZARA info@moe.go.tz
  2. TAREHE YA MWISHO KUPOKEA NYARAKA NI 17 JANUARI,2017.
  3. BARUA PEPE ZA KUWASILISHA NYARAKA ZA WAOMBAJI ZITUMWE MARA MOJA TU NA SI KWA KURUDIA RUDIA ILI KUEPUKA USUMBUFU WA KUTAFUTA ZILIZO SAHIHI.

IMETOLEWA NA
PROF. SIMON S. MSANJILA
KAIMU KATIBU MKUU
12/01/2017

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us