Serikali Yalipa Madeni Ya Fedha Za Likizo Kwa Walimu 86,234 Nchini. | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday 21 April 2017

Serikali Yalipa Madeni Ya Fedha Za Likizo Kwa Walimu 86,234 Nchini.


Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imelipa madeni ya fedha za likizo kwa walimu 86,234 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/17.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella Manyanya wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.

“Serikali inaendelea kulipa madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha za likizo kwa walimu/Watumishi katika sekta ya Elimu”,Aliongeza Mhe.Manyanya.

Amesema kuwa katika kipidi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi mwezi Juni, 2016 jumla ya shilingi bilioni 22,629,352,309 zililipwa kwa walimu 63814, na pia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi kufikia mwezi Machi, 2017 jumla ya shilingi bilioni 10,505,160,275 zimelipwa kwa walimu 22420.

Aidha katika malipo haya jumla ya shilingi 13,415,410 zimelipwa kwa ajili ya madeni ya fedha za likizo kwa watumishi wa chuo cha ualimu Korogwe.Akizungumzia upande wa upandishaji madaraja Mhe.Manyanya amesema kuwakwa sasa uhakiki wa watumishi unaendela na ukikamilika watapandisha madaraja kama inavyotakiwa.

Aidha amesisitiza kuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imekuwa ikiwapandisha vyeo watumishi wake wenye sifa kila mwaka ambapo katika mwaka 2015/16 Wizara iliwapandisha vyeo watumishi 2272 kati yao watumishi 71 ni wa chuo cha ualimu korogwe.

Uhakiki wa madeni ya miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za malipo zitakamilishwa kwa wale wanaostahili.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us