Mtangazaji wa Clouds Tv ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday 10 September 2016

Mtangazaji wa Clouds Tv ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya

Leo Septemba 10, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.

Miongoni mwa Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa, yumo pia mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv kinachorushwa kila siku kuanzia jumatatu hadi Ijumaa.

Hudson Stanley Kamoga ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuteua watangazaji kushika nyadhifa mbalimbali kwani alimteua aliyekuwa Mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Wakurugenzi wengine walioteuliwa leo ni pamoja na;-

Mwailwa Smith Pangani – Halmashauri ya Wilaya ya NsimboGodfrey Sanga – Halmashauri ya Wilaya ya MkalamaYusuf Daudi Semuguruka – Halmashauri ya Wilaya ya UlangaBakari Kasinyo Mohamed – Halmashauri ya Wilaya ya NachingweaJuma Ally Mnwele – Halmashauri ya Wilaya ya KibondoButamo Nuru Ndalahwa – Halmashauri ya Wilaya ya MoshiWaziri Mourice – Halmashauri ya Wilaya ya KaratuFatma Omar Latu    – Halmashauri ya Wilaya ya BagamoyoGodwin Emmanuel Kunambi – Manispaa ya DodomaElias R. Ntiruhungwa – Mji wa TarimeMwantumu Dau – Halmashauri ya Wilaya ya BukobaFrank Bahati – Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us