Trump: Kura zinaibiwa vituoni Marekani | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday 17 October 2016

Trump: Kura zinaibiwa vituoni Marekani

 Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amedai uchaguzi nchini humo "unaibiwa" na vyombo vya habari pamoja na "kwenye vituo vya kupigia kura" kumzuia kushinda.

Matamshi hayo yanaonekana kukinzana na ya mgombea mwenza wake Mike Pence, ambaye awali aliambia kituo cha runinga cha NBC kwa Bw Trump bila shaka atakubali matokeo ya uchaguzi, licha ya "kuonewa" na vyombo vya habari.

Mshauri wa Bw Trump, Bw Rudy Giuliani pia amewatuhumu wanachama wa Democratic kwa "udanganyifu".

Kura za maoni zinaonesha kwamba Bw Trump anapoteza ushawishi katika majimbo mengi muhimu yanayoshindaniwa.

Hayo yakijiri, mgombea mwenza wa mpinzani wa Trump, mgombea wa chama cha Democratic Bi Hillary Clinton, Bw Tim Kaine amejibu vikali madai hayo ya Bw Trump kwamba kuna njama ya kuiba kura uchaguzini na kusema ni mbinu tu za kutaka kuzua wasiwasi.

Bw trump ametilia shaka uhalali wa shughuli ya sasa ya uchaguzi kwenye msururu wa ujumbe kwenye Twitter.

Ameandika hatimaye kwamba: "Uchaguzi huu bila shaka unaibiwa na wanahabari wasio wa kweli na wa kupotosha ambao wanamtetea Hillary mwovu - lakini pia katika vituo vingi vya kupigia kura - Inasikitisha."

Awali, Bw Trump alikuwa amewatuhumu wanahabari kwa kuchapisha habari za uongo.

"Uchaguzi huu unaibiwa na wanahabari, kwenye juhudi za pamoja wakishirikiana na wanakampeni wa Clinton, kwa kuchapisha habari za mambo ambayo hayajawahi kutokea!"

 Hata hivyo akiongea katika kipindi cha NBC cha Meet The Press (Kutana na Wanahabari), Bw Pence amesema Wamarekani wamechoshwa na mapendeleo ya wazi kwenye vyombo vya habari vya taifa ambapo kunaonekana dalili za "wizi wa uchaguzi".

Hata hivyo alisema: "Bila shaka, tutakubali matokeo ya uchaguzi."

"Uchaguzi daima huwa si rahisi," aliongeza, lakini akasema kwamba Marekani ina desturi ya "kukabidhi madaraka kwa njia ya amani".

Mike Pence alitofautiana na kauli ya Bw Trump awali

Hayo yakijiri, meya wa zamani wa New York Rudy Giuliani, ambaye ni mshauri wa kampeni wa Bw Trump aliambia kipindi cha State of the Union cha CNN kwamba ni "juha" peke yake anayeweza kuamini kwamba uchaguzi, mfano katika maeneo kama vile Philadelphia na Chicago, utakuwa wa haki.

"Nimepata visa vichache sana ambapo Republicans hutumia udanganyifu uchaguzini .... hawadhibiti maeneo ya ndani mitaani kama ilivyo kwa Democratic. Labda kama Republican wangedhibiti maeneo ya ndani mitaani, wangetumia udanganyifu kama wafanyavyo Democratic," alisema.
"Samahani. Wafu kawaida hupigia sana Democratic kuliko Republican" aliongeza.

Trump 'aliwapapasa wanawake kama pweza'

Mgombea mwenza wa Democratic Bw Kaine aliambia kipindi cha ABC cha This Week Mr Trump kwa sasa anatafuta kila "kivuli" na kuanza kukishambulia kwa sababu "anajua kwamba anashindwa".

"Anawalaumu wanahabari. Analaumu GOP (Chama cha Republican). Anasema Marekani haiwezi kuwa na uchaguzi huru na wa haki."

Wanawake kadha wamejitokeza na kumtuhumu Bw Trump kwa kuwadhalilisha kimapenzi kwa kuwapapasa au kuwapiga busu kwa lazima wiki iliyopita kwenye vyombo vya habari.

Hii ilijiri baada ya ukanda wa video wa mwaka 2005 kutolewa ukionyesha Bw Trump akitumia lugha ya kuudhi kuwarejelea wanawake.

Amekanusha madai hayo na kuwataja wanawake hao kama "waongo" na akawalaumu wanahabari akisema wamekuwa mawakala wa "mashine ya Clinton".

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us