Dada wa kazi auawa kwa kisu, DSM | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday 6 May 2017

Dada wa kazi auawa kwa kisu, DSM

Katika hali isiyo ya kawaida dada wa kazi aliyetambulika kwa jina la  Christina Mabuga (37), amekutwa ameuawa ndani ya chumba chake, huko Moshi Baa, Gongo la Mboto, Dar es Salaam kwa kujichoma kisu kifuani.

Jeshi la Polisi katika mkoa wa kipolisi Ilala limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, lililofanyika katika nyumba ya mwajiri wa dada huyo wa kazi, ambapo mpaka sasa haijafamika chanzo cha dada huyo kujiua.


Mwajiri wa binti huyo, Anna Kasanda alisema alipokea taarifa saa 9:00 alasiri kwamba kuna tatizo nyumbani kwake, na ndipo alipoamua  kurudi nyumbani na kukuta mfanyakazi huyo amejiua.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us