NEWS: TAMISEMI YATOA TAMKO HILI KUHUSU AJIRA ZA UALIMU,UHAMISHO NA KUPANDISHA MADARAJA 2015/2016 | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday, 16 September 2016

NEWS: TAMISEMI YATOA TAMKO HILI KUHUSU AJIRA ZA UALIMU,UHAMISHO NA KUPANDISHA MADARAJA 2015/2016


Hivi karibuni kumezuka tabia za utapeli unaofanywa na wanaojisadikisha kuwa ni watumishi wa Umma au Mawakala wa kusimamia uhamisho wa Watumishi kuhama kutoka Mkoa mmoja kwenda Mkoa mwingine na pia kujihusisha  na kutoa taarifa za uongo kwa   kugushi nembo za Ofisi ya Rais.

– TAMISEMI kuhusu ajira, kupandisha madaraja ya walimu.

Yamekuwepo Malalamiko mengi kutoka kwa wahanga/waathirika wa tabia hiyo kwa nyakati tofauti ambayo watumishi wamehadaiwa kuwa watasaidiwa kuhamia sehemu yoyote wanayoihitaji baada ya kulipa kiwango cha fedha ambacho hupangwa na wahalifu hao. Miongoni mwa taarifa batili wanazosambaza ni Uhamisho na Ajira za Walimu.

Matangazo hayo pia yameonekana katika mbao za matangazo za baadhi ya Halmashauri. Mara nyingi watu hao huweka namba zao za simu kwa ajili ya kupokea fedha za uhamisho kutoka kwa watumishi pamoja na kuweka anuani za barua pepe zinazosadikiwa kutumika katika kukusanya barua za maombi ya uhamisho.

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) inapenda kuchukua fursa hii, kutoa taarifa hii kwa lengo la kuujulisha Umma wa Watanzania juu ya kuwepo kwa uhalifu huu ili waweze kujiepusha nao.

Ofisi ya Ras –TAMISEMI haitasita kuchukua hatua za Kisheria kwa wale wote watakaobainika kujihusisha na uhalifu wa aina hii.

Tunasisitiza kuwa wananchi wafuate taratibu na pia watambue kuwa hakuna malipo yoyote yanayotakiwa ili kuhamisha mtumishi. Wananchi wanaombwa kutoa taarifa pale watakapoona kuna utapeli unaoendelea katika masuala ya ajira na uhamisho.

Watumishi wanaweza kufahamishwa juu ya taratibu za uhamisho katika Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na pia kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI  (www.tamisemi.go.tz).

Ofisi ya Rais TAMISEMI haijatoa matangazo yoyote yanayohusiana na Ajira za Ualimu katika kipindi hiki.

Imetolewa na:-

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Ofisi ya Rais,

Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,

15 Septemba, 2016.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us