KINGAZI BLOG: 02/11/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 11 February 2017

Picha:Inasikitisha!!!! Defoe akubali kulala na Bradley Lowery kwenye siku yake ya mwisho duniani ambayo ni leo jumamosi.



Jumamosi ya leo ndio siku ambayo ilidaiwa kuwa mtoto ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu ya soka ya Sunderland, Bradley Lowery atafariki dunia kutokana na ripoti ya madaktari ambapo anasumbuliwa na maradhi ya kansa ambayo imedaiwa kufika mwisho hadi kushindikana kutibika.

Bradley amemuomba Jermain Defoe kulala naye kitanda kimoja hospitalini ambapo amelazwa katika siku yake hiyo ya mwisho duniani ambayo alidaiwa kuwa atafariki ambapo mshambuliaji huyo amelikubali ombi hilo.

Miezi kadhaa iliyopita ilidaiwa kuwa matibabu ya mtoto huyo yatagharimu kiasi kisichopungua bilioni mbili ambapo timu za Everton, Man City na Sunderland pamoja na wadau wengine walijitolea kumchangia lakini baadae jopo la madaktari lilitoa taarifa ya kushindikana kwa matibabu hayo.

HAYA HAPA MAJINA YA WALIOPATA MKOPO WA CHUO KIKUU BAADA YA KUKATA RUFAA (APPEAL) 2016/17

Image result for bodi ya mikopo



LIST OF SUCCESSFUL LOAN APPELLANTS 2016/2017
The Higher Education Students’ Loans Board wishes to announce successful loan appellants.
Details of the loan allocations will be available in their respective institutions by end of 13th February, 2017.
Issued by:
EXECUTIVE DIRECTOR
HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD
11th February, 2017.

Baada ya kutoka selo wiki iliyopita Paul Makonda amualika T.I.D nyumbani kwake Masaki leo.

Ni siku 3 toka mwimbaji wa bongofleva T.I.D aachiwe kwa dhamana kwenye sakata la dawa za kulevya ambalo lilianzia kwenye orodha aliyoitaja mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.Leo February 11 2017 Mkuu huyo wa mkoa amemuita T.I.D nyumbani kwake Masaki na kufanya nae mazungumzo ikiwa ni siku mbili zimepita toka Makonda amsifie T.I.D kwa kukiri kuwa tayari kusaidiwa kuachana na dawa za kulevya.Baada ya kufanya mazungumzo na T.ID Paul Makonda alisema “Mungu wetu hajalala na siku zote anampenda amtafutae, karibu tena nyumbani T.I.D”

Donald Trump asema atatoa marufuku nyingine mda si mrefu

 Marufuku hiyo ya Trump ilizua ghasia katika viwanja vya ndege na kusababisha maandamano nhcini humo

Donald Trump anasema kuwa huenda akabadilisha marufuku yake dhidi ya wahamiaji na agizo jingine la rais litakalopiga marufuku raia wa mataifa kadhaa kutoingia Marekani baada ya jaribio lake la awali kubadilishwa na mahakama.

Bw Trump aliambia wanahabari katika ndege ya Airfoce One kwamba amri mpya huenda ikatolewa mapema siku ya Jumatatu ama jumanne .

Inajiri baada ya mahakama ya rufaa mjini San Fransisco kupinga amri yake ya hapo awali.

Agizo hilo lilikuwa limepiga marufuku raia kutoka mataifa saba ya Waislamu.

Haijulikani ni vipi amri hiyo mpya itakuwa.

Bw Trump amesema kuwa amri hiyo itakuwa na mabadilik kidogo lakini hakutoa maelezo zaidi.

Serikali ya Marekani

Licha ya pendekezo lake siku ya Ijumaa ,serikali ya Trump huenda ikafuatilia rufaa yake mahakamani kuhusu agizo lake la kwanza ambalo lilipingwa wiki moja iliopita na jaji wa Seattle.

''Tutashinda vita hivi,Trump aliwaambia maripota akiongezea:Tatizo ni kwamaa inachukua muda mwingi.Lakini tutashinda vita hivyo.Lakini pia tuna njia nyengine mbadala ikiwemo kuanzisha upya marufuku nyengine''.

PICHA 2: Hatimae Diamond Platnumz aonyesha sura ya mtoto wake wa pili na hizi ndizo picha zake.


Mashabiki wengi wa Mwimbaji wa bongoflevaDiamond Platnumz walikua wanasubiria hii siku Diamond apost picha ya mtoto wake wa pili aitwae Nillan ambaye toka amezaliwa hakuna shabiki aliepata nafasi ya kuona sura yake.

Wengi walikua wanasubiria kumuona wajue kama kafanana na Baba au mama? sasa picha zenyewe ndio hizi na ukishamaliza kuzitazama usiache kuniandikia mfanano ukoje



Baada ya Kukataa Wito wa Polisi,Mbowe Aamua Kumpeleka Makonda Mahakamani,..!!


Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe (MB) leo tarehe 10 February 2017 amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu DSM na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dsm.

Kesi hiyo ilisajiliwa kama Kesi ya Kikatiba namba 1 ya 2017 imefunguliwa kwenye Mahakama ya Kuu masijala ya Katiba (Masijala Mkuu).

Kwenye Kesi hiyo Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke na kuwa Mkuu wa Mkoa hana mmalaka ya kudharilisha, na kukamata.

Mbowe pia ameiomba mahakama itengue vifungu vya 5&7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwakua ni batili na vinakiuka haki za kikatiba.

Katika kesi hizo Mbowe atawakilishwa na Mawakili toka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya CHADEMA.

RAIS AFANYA UTEUZI HUU MKUBWA KUONGEZA NGUVU ZAIDI KWENYE VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA.





Habari kuu Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya February 11


 

Gallery

Popular Posts

About Us