KINGAZI BLOG: 10/27/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday, 27 October 2016

Picha zinatisha : BODABODA YATUMIKA KUSAFIRISHA MAITI, DEREVA AKAMATWA.



  1. Image result for BODABODA

    Bodaboda huyo amekamatwa akisafirisha maiti bila jeneza baada ya ndugu wa marehemu kutokua na uwezo wa kununua jeneza 1477558184581.jpg 1477558228184.jpg 1477558244676.jpg

Hii hapa Habari njema kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini

Fedha za mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini zimeanza kuingia katika akaunti zao, baada ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) kusema kuanzia Jumatano hii imeanza kuingiza fedha za wanafunzi wote waliokidhi vigezo vya kupatiwa mkopo.
Akizungumza na gazeti la Habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul Razaq Badru aliwahakikishia wanafunzi hao kuwa fedha hizo zinaanza kuingia siku tofauti tofauti.
“Napenda kuwahakikishia waombaji kuwa boom limeanza kuingia leo, kwa kuwa fedha hizo zinapitia benki baadhi wanapata kesho na wengine siku zinazofuata, ila sisi tumeshatimiza wajibu wetu,” alisema Badru.
“Kuna wanafunzi kama 90 wamekosa mikopo kwa sababu ya umri wao kuwa mkubwa, sisi tunatoa mikopo kwa wanafunzi wanaotoka sekondari. Pia kuna wanafunzi wengine kama 6,561 hawakuomba kabisa mikopo licha ya kudahiliwa na TCU hao nao tunasema hawana sifa ya kukopeshwa,” aliongeza Badru.
Katika ufafanuzi wa waliopata mikopo, Badru alisema kati ya wanafunzi hao yatima waliopata mkopo ni 873, wenye ulemavu wa viungo wako 118, wahitaji wenye mzazi mmoja 3,448, waliofadhiliwa na taasisi mbali mbali 87, wahitaji wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159 na Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine ni 9,867.
credt MUUNGWANA BLOG



Kwa upande mwingine SERIKALI YATOA SABABU ZA KUTOA MIKOPO KWA VIGEZO
Wizara ya elimu imefafanua kuwa wametoa mikopo kulingana na vigezo vya wanafunzi na pia sio wote wenye vigezo watapata kwa kuwa bajeti ina ukomo.

Naibu waziri amesema wanafunzi wengi walikuwa wanapata mikopo pasipo na vigezo na walikuwa wakitumia mikopo kufanyia mambo mengine kama kunywa pombe kununulia tv na kutembea ambavyo sio kusudio la mikopo hiyo.


Ufaulu darasa la saba wapanda kwa asilimia 2.52

Dkt. Charles Msonde, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani

Ufaulu wa mtihani wa Darasa la Saba umeongezeka kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.36 mwaka 2016. 

Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dkt. Charles Msonde amesema kuwa Jumla ya watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza.

Aidha Dkt . Msonde amesema Jumla ya watahiniwa 238 wamefutiwa matokeo ya mtihani huo kutokana na udanganyifu huku shule 6 waalimu, wamiliki wa shule na wasimamizi wa mitihani wakibainika kufanya udanganyifu na kuwafanyia mtihani wanafunzi.

Amesema katika mtihani huo mwaka huu jumla ya watahiniwa 795,739 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani wakiwemo wasichana 422,864. sawa na asilimia 53.14 na wavulana 372,875 sawa na asilimia 46.86. watahiniwa 789.479 sawa na asilimia 99.21 ya waliosajiliwa walifanya mtihani. wasichana wakiwa 419.932 sawa na asilimia 99.31.wavulana walikuwa 369.547 sawa nasilimia 99.11


BREAKING NEWS:HAYA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA(7)2016


                                                             Image result for matokeo darasa la saba 2015

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo limetangaza  matokeo ya mtihani wa darasa la saba uliofanyika mwezi septemba huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 2.52Kutokana na ukweli kwamba si kila mtu mwenye acces na mtandao na itambidi kwenda internet cafe kuangalia,KINGAZITZ BLOG tumekurahisishia mambo.

Endapo utahitaji huduma ya kuangaliziwa jina la mwanao au ndugu yako fanya yafuatayo;


1.Tuma  jina la mwanao,mkoa,wilaya na shule aliyosoma

(mfano:juma paul-PWANI,KIBAHA,UHURU PRIMARY) 

kwenda namba 0716528779

2.Huduma hii uatozwa tshs 1000 tu.(kwa ajili ya kuisuport kingazitz blog)

3.Tuma pesa kwenda namba 0755542721-MPESA
                                             0716528779-TIGO PESA   
5.Utajibiwa ndani ya dk.moja tu,tuma pesa kwanza ndio ujibiwe


====>>BOFYA  << HAPA>>  KUONA 


MATOKEO AU ===> UNAWEZA BOFYA  <<HAPA>> 


 KUYAONA

SEKOMU: Round 4 admitted applicants to join bachelor programmes 2016/2017


ROUND 4 -- > ADMITTED APPLICANTS\
 {<ARTS >|
|<ENC >|
|<LAW> | 

Habari kuu Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya Octoba 27


Maajabu!!! Kutana na Huyu Polisi ambaye ni roboti



Hatimaye hekaya za filamu za miaka ya 1980 zawa kweli kwani ndani ya muda mfupi  polisi roboti ataanza kutumiwa katika vituo vya usalama.

Katika tamasha la maonyesho ya roboti kwa jina la GITEX jijini Dubai ,mojawapo ya vitu vilivyowavutia watazamaji ni polisi roboti aliye na uwezo wa kufanya utambulisho wa uso wa mtu.

Roboti huyo polisi pia anaweza kutoa adhabu kwa wanaokiuka sheria za barabarani.

Roboti huyo anatarajiwa kupewa kazi ya kushika doria maeneo ambayo kuna wingi wa watalii jijini humo mwaka ujao.

 

Gallery

Popular Posts

About Us