KINGAZI BLOG: 10/23/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday, 23 October 2016

Malkia Wa Shindano La Urembo Kwa Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi ‘Albino’ Kenya Apatikana

 Akina dada walioshiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.Mamia walijitokeza kushuhudia maonyesho ya urembo ya Mr na Ms Albino nchini Kenya. Kila siku Albino wanakabiliwa na hatari ya kuuawa na viungo vyao vya mwili kuuzwa kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na Afrika kusini.

 Malkia mpya! Louise Lihanda, aliyeshinda taji la urembo kwa akina dada atembea jukwani akiwa amevalia vazi la kupendeza lililotengenezwa kwa kutumia puto. Loiuse ambaye ni mwanafunzi, amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda taji hilo, katika mashindano yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016

 Wanaume walioshiriki katika mashindano hayo wasimama  jukwaani. walishiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.

 Mfalme! Jairus Ongetta, ambaye amekabidhiwa taji ya uanamitindo bora kwa wanaume akiwa jukwaani na mavazi ya kupendeza.

 Erick Thomas, awaongoza wanamitindo wenzake kwenye jukwaa wakati wa mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi. Lengo lake ni kuhakikisha kwamba watu walio na ulemavu huo wamejivunia ngozi yao.

 Msichana huyu aliduwazwa na maonyesho hayo! Yeye ni miongoni mwa watu ambao kila siku wanakabiliwa na hatari ya kuuawa kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na Afrika kusini.

 Miraba minne! John Ngatia, ambaye pia huwa anasakata densi, avalia sare ya mapigano ya ndondi katika maonyesho hayo, jijini Nairobi Kenya tarehe 21 Oktoba 2016

 Majaji walikuwa macho! Waliongozwa na mwanamitindo wa kimataifa Deliah Ipupa (katikati) tarehe 21Oktoba 2016.

 Naomi Wafula, ajitokeza jukwaani akiwa amevalia vazi lililotengenezwa kwa sahani za plastiki katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016

 Mamia walihudhuria maonyesho hayo kuonyesha umoja wao na watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi katika mgahawa wa Carnivore jijini Nairobi Kenya, tarehe 21, Oktoba 2016

  Amina Makokha ajitokeza jukwaani akiwa amevalia sare ya mchezo wa raga katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016

Kutoka kulia, naibu rais wa Kenya William Ruto, Mbunge Isaack Mwaura na mkurugenzi mkuu wa bodi ya filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua pia walikuwemo.

MPENZI MPYA WA WEMA SEPETU ANYOOSHA MAELEZO FNL, ADAI HAMJUI IDRISS

‘Model’ anayedaiwa kuchukua nafasi ya Idriss kwa kutoka kimapenzi na mrembo Wema Sepetu, amejikuta akiweka hadharani mahaba yake kwa mrembo huyo kwa kutoa maelezo yanayothibitisha kuwa hivi sasa yeye na Wema ni wapenzi.

Calisah
Kijana huyo anayefahamika kwa jina la Calisah, alikumbana na kibano kizito kupitia kipindi cha FNL kinachuruka kila Ijumaa kupitia EATV, pale alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa mahusiano yake na mrembo huyo ambaye alikuwa Miss Tanzania mwaka 2006.
Calisah alisema Wema ni msichana mrembo na mwenye mvuto kwa kila mwanaume, hivyo hata yeye anavutiwa naye na anapenda kuwa naye katika mahusiano, lakini akagoma kusema iwapo tayari wameanza mahusiano au la.
Calisah pia alijifagilia kuwa uzuri wake ndiyo uliomfanya Wema kumzimikia na kuwatosa wote aliokuwa kuwa nao.

Wema Sepetu
“Wema is a beautiful girl, sexy and every man’s dream, na mimi pia ni mvulana mzuri ambaye mwanamke yeyote angependa kuwa na mimi, akiwemo Wema mwenyewe, siwezi kusema moja kwa moja kwamba sisi ni wapenzi, lakini ujue kuwa Wema ni mzuri na mimi mzuri”
Alipotakiwa kutamka sababu za kumpora Wema kutoka kwa Idriss, Carissa amesema hamjui vizuri Idriss, na kwamba hakumbuki kama Tanzania imewahi kuwakilishwa na mtu anayeitwa Idriss katika mashindano ya Big Brother Afrika akisema “Who? Idriss, kwani amewahi kuwa Big Brother? Which year?”

MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANUFAIKA WA MKOPO 2016/2017-BATCH 1 & 2

                                                 Image result for bodi ya mikopo ya wanafunzi

Nimeamua kukuwekea hapo chini list ya vyuo ambavyohadi sasa vimetoa majina ya wanafunzi waliopata mkopo batch 1.



KWA CHUO CHA KCMC             <<BONYEZA HAPA>>
KWA CHUO CHA MAJI DSM       <<BONYEZA HAPA>>
KWA CHUO KIKUU UDSM          <<BONYEZA HAPA>>
KWA CHUO KIKUU DUCE           <<BONYEZA HAPA>>
KWA CHUO KIKUU MUCE          <<BONYEZA HAPA>>
 KWA CHUO KIKUU SUA               <<BONYEZA HAPA>> 
KWA CHUO KIKUU MUHAS        <<BONYEZA HAPA>>



N.B TUNAKUDIRECT KWENYE BLOG MARAFIKI AMBAYO NI MASWAYETU BLOG

CHECK LIST YA WASHINDI WA TUZO ZA MTV MAMA 2016,TANZANIA YATOKA KAPA

Tanzania imetoka kapa kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 zilizofanyika usiku wa Jumamosi hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee, Raymond, Navy Kenzo na Yamoto Band walikuwa wametajwa kuwania tuzo hizo.

Wizkid alikuwa man of the night
Ulikuwa ni mwaka wa Wizkid aliyeibuka na tuzo nyingi zaidi, ikiwemo ya msanii bora wa mwaka. Diamond na Alikiba walikuwa miongoni ma wasanii waliotumbuiza.
“Shukran sana sana kwa Kura na support Kubwa mlionipa na mnayoendelea kunipa,” ameandika Diamond kwenye Instagram.
“Pia S/O kwa my fellow Tanzanian Artist wote waliobahatika kuchaguliwa… Kuingia tunwengi kwenye MtvAwards ni Ushindi tosha kwa Tanzania…ila wanna congrats my brothers @sautisol for the Best Group award… my hommie @jahprayzah and @wizkidayo ya’ll deserve the Trophies,” ameongeza.
Alikiba amepost picha ya Sauti Sol na kuandika: Congratulations to my brothers @sautisol for The MTV Best Group Winner. You have had a great year and you deserve it.”
Naye Vanessa Mdee amepost picha ya Yemi Alade aliyekuwa akishindana naye kwenye kipengele cha msanii bora wa kike na kuandika: Congratulations to my lady love @yemialade na bado tunaenda #Juu and ALL the winners tonight. Thankyou @mtvbaseafrica for the recognition and your continued efforts to elevate Afrikan Music.Now lets get back to work kids.”

Kwa upande wao, Navy Kenzo wamewapongeza Sauti Sol kwa kuandika: With a Great pleasure we Thank God and all Fans, family, friends and all of our teams,Thank you Everyone for voting and it was a great exposure motivation and challenge towards major Goal…! We also Give thanks to @mtvbaseafrica @mtvbaseafrica For the Nomination and recognition we are very happy with a Great Gratitude. Until next Year. EAST AFRICA #KENYA AND AFRICA AT LARGE LET’S STAND TOGETHER AND SAY CONGRATULATIONS @sautisol @sautisol
@sautisol @sautisol #BESTGROUP #AFRICA.”
Hii ni orodha kamili ya washindi.



















Habari kuu kwenye Magazeti Ya Leo Jumapili ya Octoba 23



 

Gallery

Popular Posts

About Us