KINGAZI BLOG: 11/10/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday 10 November 2016

Mfahamu kiundani kwa historia Rais mteule wa Marekani, Donald Trump 1946 - 2016


New York. Donald John Trump alizaliwa Juni 14, 1946 Jamaica Estates, Queens karibu na New York. Ni mtoto wa pili kati ya watoto watano wa Fred Trump na Mary. Ndugu zake watatu; Maryanne, Elizabeth na Robert wako hai wakati kaka yake mkubwa, Fred Junior alifariki mwaka 1981 kutokana na unywaji pombe wa kupitiliza. Donald anasema jambo hilo ndilo lililomfanya yeye kujiepusha na pombe na uvutaji sigara.

Baba yake Trump kwa asili ni Mjerumani wakati mama yake asili yake ni Scotland. Bibi na babu zake Trump wote ni watu waliozaliwa Ulaya. Jina lao la asili la Kijerumani ni Drumpf baadaye katika karne ya 17 ndiyo likawa Trump. Trump anasema anajivunia asili yake.

Trump alizaliwa na kukulia mjini New York, alipata shahada yake ya kwanza ya uchumi katika shule ya uchumi ya Wharton ya Chuo Kikuu cha Pennyslvania mwaka 1968.

Mwaka 1971 alikabidhiwa udhibiti wa kampuni ya ujenzi ya baba yake Fred Trump ambayo baadaye aliibadilisha jina na kuiita The Trump Organization. Trump ni mwenyekiti na Rais wa Jumuiya ya Trump ambayo ni kampuni tanzu ya ujenzi, wadhifa ambao alisema atauacha mara atakapochaguliwa kuwa Rais wa Marekani.

Katika sekta ya ujenzi Trump amejenga ofisi, hoteli, casino na viwanja vya golf katika sehemu mbalimbali.

Mwaka 1996 hadi 2015, Trump alikuwa muandaaji wa mashindano ya urembo ya Miss USA na hapo pia akawa anaonekana katika filamu na vipindi mbalimbali vya runinga.

Mwaka 2016 aliorodheshwa katika jarida la Forbes kuwa mtu wa 324 kwa tajiri duniani, lakini anashika nafasi ya 156 ya utajiri nchini Marekani.

Ujana wake

Familia ya Trump ilikuwa na nyumba ya ghorofa mbili huko Wareham Jamaica Estates ambako Trump alikuwa akiishi wakati anasoma shule ya The Kew-Forest. Kutokana na tatizo la kimaadili, Trump aliacha shule akiwa na miaka 13 na kupelekwa chuo cha kijeshi cha New york (New York Military Academy - NYMA) ambako alimaliza sekondari mwaka 1983.

Baba yake (Fred Trump) wakati alipohojiwa kuhusu tabia za mwanawe alisema: “Donald alikuwa mkorofi alipokuwa mdogo.”

Mwaka 2015 Trump alimwambia mwandishi mmoja kuwa NYMA imempa mafunzo mengi ya kijeshi kuliko mtu yeyote aliyeingia jeshini.

Trump alisoma Chuo Kikuu cha Fordhan kwa miaka miwili kuanzia Agosti 1964 na kuhamia shule ya biashara katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania ambacho hutoa mafunzo kuhusu usimamizi wa ujenzi. Wakati akiwa chuoni hapo alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya familia iliyojulikana kama Elizabeth Trump & Son, jina la bibi yake mzaa baba.

Mwekezaji majengo

Trump hakuandikishwa kupigana vita ya Vietnam, lakini kati ya 1964 hadi 1968 akiwa chuoni alisimamishwa masomo mara nne.

Kuanza kazi

Trump alianza kazi katika kampuni ya baba yake mara tu baada ya kumaliza chuo. Kampuni hiyo ilikuwa ikijenga nyumba za makazi na kuzikodisha huko Brooklyn, Queens na Staten Island. Mradi wake wa kwanza aliousimamia ulikuwa ni kuboresha makazi ya Swifton Village apartment huko Cincinnati, Ohio sehemu ambayo ilinunuliwa na baba yake kwa dola 5.7 milioni mwaka 1962.

Donald na baba yake walisimamia mradi huo uliokuwa na uwekezaji wa dola 500,000 na kuweza kujenga nyumba 1,200. Trump anasema wakati anahitimu chuo mwaka 1968 alikuwa na utajiri wa kiasi cha dola 200,000 (sawa na dola 1,020,000 kwa mwaka 2015).

Mradi wa kwanza mkubwa wa Trump ulikuwa ni ujenzi wa Grand Hyatt Hotel mwaka 1978.

Mwaka 1981, Trump alinunua na kukarabati jengo huko Third Avenue mjini New York ambalo kwa sasa linajulikana kama Trump Plaza.

Mwaka 1983, Trump alikamilisha ujenzi wa Trump Tower yenye ghorofa 58 iliyopo Midtown Manhattan. Mwaka 1978 wakati Trump ananunua eneo hilo na kuweka mipango yake ya ujenzi kulikuwa na sintofahamu na majirani zake, ikabidi majadiliano yawe makali kwanini anataka kujenga jengo refu na kuwanyima haki ya eneo la anga jirani zake. Majadiliano yalipomalizika mwandishi mmoja wa The New York Times aliandika: “Trump alifanikiwa kulipata eneo… huo ni ushuhuda wa jinsi alivyo king’ang’anizi na uwezo wake wa kujadili na kufikia mwafaka.

Ndoa za Trump

Trump ameoa mara tatu na ana watoto watano na wajukuu wanane.

Mke wa kwanza wa Trump alikuwa ni Ivana. Huyu alikuwa ni mwanamitindo kutoka Jamhuri ya Czech, alimuoa mwaka 1977 na kuzaa naye watoto watatu: Donald Trump Jr, Ivanka na Eric. Ndoa hii ilivunjika rasmi 1992.

Ivana alizungumza na New York Post na kusema kwa sasa yeye na Trump ni marafiki na mara nyingi amekuwa akimshauri kuhusu hotuba zake. “Tulikuwa tunazungumza kabla na baada ya mikutano yake na alikuwa akiniuliza nafikiri nini? Nami humuambia kuwa atakuwa rais mzuri kwa sababu anasema kila kitu kama kilivyo.”

Aliyekuwa mke wa pili wa Trump ni Marla Maples, alimuoa 1993 na mwaka huohuo walipata mtoto wa kike waliyempa jina la Tiffany. Marla na Trump waliachana mwaka 1999.

Mwaka 2005 Trump alimuoa mwana mitindo mwingine Melania Knauss, huyu ni mzaliwa wa Slovenia. Mwaka 2006 akawa raia wa Marekani. Wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Barron.

Melania alipoulizwa katika mahojiano na CNN alisema: “hakuna nafasi ya kufikiri mambo madogo, hakuna nafasi ya matokeo madogo. Donald hufanya vitu vifanyike.

Hata hivyo, katika hali tofauti Melania aliwahi kumfananisha Trump na mtoto mdogo kwa kusema: “Mara nyingine husema nina wavulana wawili nyumbani. Ninaye mtoto wangu mdogo na ninaye mume wangu.”

Makala haya yameandaliwa na Hawra Shamte kwa msaada wa mtandao.

Maelfu waandamana kupinga ushindi wa Trump Marekani


 Rais wa Marekani Donald Trump amemwalika Rais mteule wa Marekani Donald Trump katika White House, huku maandamano ya kupinga ushindi wa Trump yakifanyika miji mingi Marekani.

Rais Obama amesema lengo la mkutano wao litakuwa kujadiliana kuhusu shughuli ya mpito na kupokezana madaraka.

Amesma anataka shughuli hiyo iwe laini na bila matatizo.

Bw Trump wa Republican atakuwa rais wa 45 wa Marekani baada ya kupata ushindi wa kushangaza dhidi ya Hillary Clinton wa chama cha Democratic, chake Rais Obama.

Bw Obama alifanya kampeni kali kumzuia Bw Trump kushinda, na alisema hafai kuongoza. Wakati mmoja alisema hata hafai kuwa mwuzaji dukani.

Lakini rais huyo sasa amewahimiza Wamarekani wote kukubali matokeo ya uchaguzi wa Jumanne.
"Sasa tunatafuta ufanisi wake katika kuunganisha na kuongoza nchi hii," Bw Obama alisema kuhusu Trump.

Licha ya Rais Obama kuhimiza umoja na Bi Clinton kuwaambia wafuasi wake kwamba Bw Trump anafaa kupewa "nafasi ya kuongoza", ushindi wake umezua maandamano katika miji na majimbo kadha Marekani.

Mamia ya waandamanaji wanaompinga Trump walikusanyika nje ya jumba kuu la Bw Trump, Trump Tower eneo la Manhattan jijini New York Jumatano jioni, wakibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe "Not my president" (Si Rais wangu), pamoja na mabango mengine.

Polisi hapo awali waliweka vizuizi vya saruji pamoja na kuchukua hatua nyingine za kiusalama nje ya jumba hilo refu linalopatikana barabara ya 5th Avenue, jumba ambalo huenda likawa makao makuu ya Bw Trump wakati wa kipindi cha mpito kabla yake kuingia White House.

 Waandamanaji wanaompinga Trump wakiwa New York

Polisi wameweka vizuizi vya Trump Tower 

Kuliripotiwa pia taarifa za waandamanaji kuziba lango la kuingia jumba la Trump Tower mjini Chicago Jumatano jioni, wakiimba: "No Trump, No KKK, No Fascists USA" (Hatumtaki Trump, Hatutaki KKK, Hatutaki Wafashi Marekani) na "Not my president!" (Si Rais wangu).

Mjini Oakland, California, na Portland, Oregon, waandamanaji waliteketeza bendera za Marekani.

Wakati wa hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi mapema Jumatano, Bw Trump aliahidi kuponya vidonda vya migawanyiko, baada ya uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali, na kuahidi kwamba atakuwa "rais wa Wamarekani wote".

Msemaji wa White House Josh Earnest amesisitiza kwamba Bw Obama atakuwa na uwazi kuhusu kuhakikisha shughuli laini ya mpito atakapokutana na Bw Trump, ingawa aliongeza kwamba: "Sijasema kwamba utakuwa mkutano rahisi."

Rais huyo mteule atasindikizwa kwenda White House Alhamisi na mkewe, Melania, ambaye atakutana na Mke wa Obama, Michelle.

 Wanafunzi wa shule ya upili ya Berkeley wakiandamana kupinga ushindi wa Trump

 Waandamanaji California

Bw Obama, aliyempongeza mrithi huyo wake kwa njia ya simu mapema Jumatano, alisema si siri kwamba yeye na Bw Trump wana tofauti nyingi.

Lakini aliongeza kwamba wanataka kuhakikisha wanalinda maslahi ya taifa na kwamba alitiwa moyo na yale Bw Trump alikuwa amesema usiku uliotangulia.

Kundi la kushughulikia shughuli ya mpito la Bw Trump litaongozwa na Chris Christie, gavana wa New Jersey, na lina wiki 10 kukamilisha maandalizi hayo.

Rais huyo mteule, ambaye hajawahi kuhudumu katika wadhifa wowote wa kuchaguliwa au kuteuliwa serikalini, amesema kipaumbele chake kitakuwa kufufua na kuimarisha miundo mbinu ya nchi hiyo pamoja na kukuza ukuaji wa uchumi wa taifa hilo maradufu.

Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha Republican Reince Priebus alisema: "Donald Trump anachukulia hili kwa uzito sana," na kuongeza kwamba mfanya biashara huyo tajiri atatumia uwezo wake wa kutetea na kufanikisha mikataba ya kibiashara kuhakikisha mambo mema "yanatendeka kwa Wamarekani" haraka iwezekanavyo.

Kama Rais mteule, Bw Trump ana haki ya kupokea taarifa za kila siku za ujasusi sawa na Rais Obama, ambazo ni pamoja na habari kuhusu operesheni za kisiri za Marekani pamoja na habari za kijasusi zinazokusanywa na mawakala 17 wa ujasusi za Marekani.

Bw Trump na kundi lake wanaaminika kuwa tayari kujaza nafasi kuu za usalama wa taifa haraka iwezekanavyo watakapoingia madarakani.

Lakini haijabainika nani atakuwa kwenye baraza lake la mawaziri au atakayejaza nyadhifa kuu wakati wa utawala wake kama vile mkuu wa majeshi.

Bw Chris Christie

Kunao wanaotarajiwa kupewa nyadhifa kuu wakiwemo Christie, spika wa zamani wa bunge Newt Gingrich na meya wa zamani wa New York Rudy Giuliani, mmoja wa washauri wakuu wa Bw Trump ambaye wengi wanasema huenda akafanywa mwanasheria mkuu au mshauri mkuu wa masuala ya usalama wa taifa.

Baada ya kupata hasara kubwa kutokana na ushindi wa kushangaza wa Bw Trump, masoko ya hisa yameanza kuimarika.

Trump ni nani? hii hapa historia yake kiufupi.


MAREKANI: Ni mtoto wa nne wa mmiliki raslimali za majengo jijini New York, Fred Trump.  Licha ya utajiri wa familia yake, alitumainiwa kufanya kazi za daraja la chini zaidi katika kampuni ya baba yake ambapo alipelekwa kujiunga na jeshi akiwa na umri wa miaka 13.

Baada ya hapo alijiunga na Chuo Kikuu cha Pennysylvania na akajiweka katika nafasi nzuri ya kurithi utajiri wa baba yake baada ya kaka yake mkubwa, Fred,  kuwa rubani.

Fred Trump alifariki akiwa na umri wa miaka 43 kutokana na ulevi na uvutaji sigara.

Ufanisi wake katika utajiri wa familia yake umemwezesha kuwa tajiri mkubwa anayemiliki miradi mbalimbali mikubwa ikiwa ni pamoja na majumba, mahoteli, na miradi mbalimbali iliyotapakaa Marekani, Mumbai, Istanbul na Ufilipino.

Utajiri huohuo umemfanya tangu mwaka 1996 hadi 2015  kuyamiliki mashindano ya urembo ya Miss Universe, Miss USA, na Miss Teen USA.

Pia amewahi kuandika vitabu kadhaa na ana biashara ya kuuza tai na maji ya kwenye chupa kwa kiwango cha kimataifa na gazeti la Forbes limeuweka utajiri wake katika kiwango cha Dola za Marekani bilioni 3.7 japokuwa yeye kila mara amesema utajiri wake ni Dola za Marekani bilioni 10.

Alichokisema Wizkid baada ya MTV EMA kumpokonya tuzo na kumpa Alikiba


Hapo awali, Wizkid hakuwa mtu aliyejishughulisha kabisa na masuala ya tuzo. Lakini siku za hivi karibuni baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo kwenye MTV MAMA, huenda aliamua kuufungua moyo wake.

Na sasa kuna kila dalili kuwa akarejea tena kwenye msimamo wa awali wa kuzichukulia tuzo kama si kitu cha maana baada ya kudaiwa kuwa MTV EMA wamesitisha ushindi wake na kuamua kumpa Alikiba kwakuwa ni dhahiri kwa mujibu wa kura ndiye aliyekuwa akistahili.

Baada ya hilo, mashabiki wengi wa Alikiba wameivamia page yake ya Instagram na kumporomoshea kila aina ya maneno, mengine yakiwa yamejaa kejeli.


Huenda maneno hayo yalimwongezea hasira zaidi alizozipata baada ya kupewa taarifa hiyo mbaya kiasi cha kuamua kufuta post alizokuwa ameweka kwenye Instagram kusherehekea ushindi.

Kupitia Twitter, huenda akawa ameamua kutupa jiwe gizani na wengi wametafsiri kuwa ndio ‘reaction’ yake baada ya kutokea hayo.



Habari kuu kwenye Magazeti Ya Leo Alhamisi ya Novemba 10





 

Gallery

Popular Posts

About Us