KINGAZI BLOG: 11/14/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday, 14 November 2016

Haya ndio madhara 6 ya kutoa Mimba

Kutoa mimba ni nini?
Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.

Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?

Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.

Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

1. Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

2. Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.

3. Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..

4. Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu  na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

5. Kansa ya mlango wa uzazi:
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

6. Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…

Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako yote..kwa maelezo zaidi

Wadaiwa Sugu Bodi ya Mikopo wapewa siku 30



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema kuwa hadi sasa kuna jumla ya wadaiwa sugu 142,470 wenye mikopo ya shilingi 239,353,750,170.27 iliyokwishaiva hawajajitokeza wala kuanza kulipa mikopo yao.

Akitolea ufafanuzi wa maana ya neo "Wadaiwa Sugu", Badru amesema kuwa ni wanufaika waliokopeshwa, muda wa matarajio ukapita bila kuwasilisha taarifa zao na kulipa madeni ya mikopo waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/1995.

Kuhusu hatua zinazochukuliwa na bodi hiyo, Badru amesema mbali na kutoa siku 30, bodi hiyo inakamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa kuvunja sheria ya bodi ya mikopo kifungu cha 19A(1).

Hatua nyingine ni pamoja na kuyawasilisha majina hayo katika taasisi za mikopo, kuwasiliana na wadhamini wao pamoja na kuyatangaza hadharani majina ya wadaiwa sugu wote ili waajiri, wadhamini na wadau wengine wayajue na kutoa taarifa katika bodi hiyo.

Kuhusu takwimu za mikopo iliyotolewa, amesema tangu 1994/95 hadi 2015/16 jumla ya shilingi 2,595,932,575.56 zimekopeshwa kwa jumla ya wanufaika 379,179.

Amesema kati ya mikopo yote iliyokopeshwa, mikopo iliyoiva ni shilingi 1,425,708,285,046.48 kwa wanufaika 238,430 ambao tayari wamemaliza kipindi chao cha matazamio.

Badru amesema kuwa jumla ya wanufaika wa mikopo 93,500 wamebainika na kupelekewa ankara za madeni yao, ambapo kati yao wanufaika 81,055 wanaendelea kulipa.

Mikopo elimu ya juu yapeleka kilio Udom


ZAIDI ya wanafunzi 200 waliodahiliwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kwa mwaka (2016/17), wamelazimika kuacha masomo na kurejea nyumbani baada ya kukosa mikopo ya elimu ya juu kutoka serikalini.

 

Imeelezwa kuwa wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza walifika mapema chuoni hapo kabla ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutoa majina ya wanufaika na wamefikia uamuzi huo baada ya bodi hiyo ’kuwatosa’ kutokana na kukosa sifa za kupata mikopo hiyo.

Aidha, zaidi ya wanafunzi 100 waliokuwa wanaendelea na masomo chuoni hapo wamelazimika kusitisha kwa muda masomo yao kutokana na kuondolewa kwenye orodha ya wanufaika kutokana na kubainika kuwa awali waliingizwa kwenye orodha hiyo pasi na sifa za kupatiwa mikopo.

Saipulani Abubakar, waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, aliiambia Nipashe jana kuwa kutokana na kukosa mikopo kutoka HESLB, wanafunzi hao wameshindwa kujilipia ada na kumudu gharama za maisha ya chuo na wameamua kurudi nyumbani.

“Nusu ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wameamua kurudi nyumbani kutokana na kukosa mikopo kutoka serikalini, wengi ni watoto wa maskini, wameshindwa kujilipia na kuamua kurudi nyumbani kufanya shughuli zingine,” alisema Abubakar.

Alisema hadi mwishoni mwa wiki, ni wanafunzi wachache waliosajiliwa chuoni hapo na hawafiki hata nusu ya waliodahiliwa kwa ajili ya mwaka huu wa masomo.

Aidha, Abubakar alisema wapo wanafunzi wanaosubiri hatma yao kutokana na HESLB kupeleka majina kwa mafungu katika vipindi tofauti chuoni hapo. Alisema wanafunzi hao kwa sasa hawakai chuoni na wamekuwa wakiondoka na kurejea chuoni kujua hatima yao.

Alibainisha kuwa miongoni mwa wanafunzi waliorudi nyumbani, wamo waliopata asilimia ndogo ya mikopo ukilinganisha na ada wanazotakiwa kulipa na hawana uwezo wa kumalizia kiasi kilichobaki.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa wanafunzi alisema serikali yake iliangalia vigezo vipya vilivyowekwa na bodi na kubaini kuwa baadhi ya wanafunzi wanakidhi, lakini hawamo kwenye orodha ya wanufaika wa mikopo hiyo mwaka huu.

Aliiomba serikali kuangalia upya mustakabali wa wanafunzi hao waliorudi nyumbani kwa kuwa wanapoteza ndoto zao.

“Ni kweli bodi iliweka vigezo vya wanafunzi kupata mikopo, lakini tunashangaa kuona baadhi ya wanafunzi wenye sifa wanakosa, kuna wanafunzi walisoma shule za kata, wengine hawana wazazi na wanaishi vijijini ambako maisha ni magumu na wamenyimwa mikopo,” alisema.

"Wapo baadhi ya wanafunzi waliokosa mikopo hiyo, wakaamua kujilipia ada, lakini kutokana na ugumu wa maisha hasa kukosa fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida, wameamua kuahirisha mwaka ili wakajipange kwa ajili ya mwaka ujao," aliongeza.

NUSU MWAKA

Alisema zaidi ya wanafunzi 100 waliokuwa wakiendelea na masomo lakini waliokosa na kuamua kujilipia ada ya nusu mwaka, walifika ofisini kwake kuandika barua za kuahirisha mwaka hadi pale hali ya maisha itavyokaa vizuri na kuwapa fursa ya kuendelea na masomo.

Alisema kuwa kwa taarifa waliyopewa na HESLB, inaeleza kuwa wanafunzi walioondolewa kwenye orodha ya wanufaika wa mikopo kwa mwaka huu wa masomo licha ya awali kupewa, wamebainika kutumia vyeti feki vya vifo, majina yao kutoonekana kwenye vitivyo wanavyopangwa na kutosaini uthibitisho wa kupatiwa fedha.

Kiongozi huyo pia alibainisha kuwa kuna wanafunzi wanaondelea na masomo lakini hawana uhakika kama wataendelea kunufaika na mikopo hiyo kwa kuwa usajili kwa ajili ya mwaka huu wa masomo umesitishwa kusubiri HESLB itoe majina ya wanafunzi inaoendelea kuwapa mikopo.

Kutokana na hali hiyo, Abubakar alisema serikali ya wanafunzi chuoni hapo imeamua kukutana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarish na Mkurugenzi wa HESLB, Abdul- Razaq Badru, Novemba 20, mwaka huu kuzungumzia hatima ya wanafunzi waliokosa mikopo.

Alipotafutwa na gazeti hili jana, Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa, alisema wanafunzi watakaopata fedha mwaka huu ni wale waliokidhi vigezo vilivyowekwa.

Alisema bodi imefanya uchambuzi yakinifu wa kujua nani anastahili kupata mikopo hiyo na nani hastahili.

Mwaisobwa alisema bodi haiwezi kutoa msaada wowote kwa wanafunzi waliokosa mikopo na kuamua kurejea nyumbani kwa kuwa kutokana na mfumo wa kielektroniki uliotumika kufanya uchambuzi, imeweza kubaini wanafunzi wenye sifa na wasio na sifa.

Mwaisobwa alisema “Sisi tunafuata sifa na vigezo vilivyowekwa vya utoaji wa mikopo, hata kama wangerudi wote nyumbani, tunachoangalia ni vigezo vya kupata huo mkopo”.

Alisema mwaka wa masomo 2016/17 Udom ulianza Oktoba 29, mwaka huu na kwamba baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliobahatika kupata mikopo, walipewa fedha kwa ajili ya chakula na malazi Ijumaa iliyopita.

Hivi karibuni, HESLB ilitangaza kuwaondoa zaidi ya wanafunzi 3,000 kwenye orodha ya waliotarajiwa kunufaika na mikopo hiyo kwa mwaka huu wa masomo kutokana na kile ilichokielezwa kuwa ni kupungukiwa sifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru, alisema mbali na kuondoa wanafunzi hao, wengine 87 ambao awali hawakujumuishwa kwenye orodha ya wanufaika kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kusoma shule zisizo za serikali, sasa watapata mikopo baada ya kubainika walisomeshwa na wafadhili.

Taarifa iliyotolewa na Badru Oktoba 30, ilibainisha sifa za wanufaika wa mkopo kuwa ni wanafunzi yatima na walemavu, wanaotoka familia za hali duni hususani waliosoma shule za umma na wale wanaosoma fani zilizo kwenye kipaumbele cha taifa.

Fani hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta na gesi asilia.

Fani nyingine ni sayansi asili huku ya mwisho ikiwa ni sayansi ya ardhi, usanifu majengo na miundombinu.

Katika mwaka huu wa masomo, upangaji wa mikopo hiyo unazingatia bajeti ya Sh. bilioni 483 zilizopitishwa na Bunge zikitarajiwa kunufaisha wanafunzi 119,012, kati yao 25,717 wakiwa ni wa mwaka wa kwanza na 93,295 wanaoendelea na masomo yao.

Trump afanya uteuzi wa awali


Rais mteule wa Marekani Donald Trump, amemteua Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Chama cha Republican, Reince Priebus, kutumika kama Mkuu wa Wafanyakazi.


Reince Priebus

Bwana Priebus ana uhusiano wa karibu na Spika wa Baraza la Wawakilishi Paul Ryan. Wandishi wa wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na Baraza la Congress kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo.


Stephen Bannon

Stephen Bannon, alikuwa ni mwenyekiti wa taasisi ya Breitbart News, ambayo ni tovuti yenye maoni ya mrengo wa kulia , naye ameteuliwa kwa nafasi ya mkuu wa mipango na mshauri mwandamizi.

Mkuu wa wafanyakazi ambaye anafanya kazi kama mruhusu na mtengeneza ajenda kwa rais, na kwamba ni mmoja wa chaguo muhimu la mapema kwa rais ajae.

Katika taarifa yake, Trump alinukuliwa akiwazungumiza Priebus na Bannon ni viongozi wenye sifa za hali ya juu waliofanya kazi pamoja wakati wa kampeni zake za kuingia Ikulu ya Marekani.

DONALD TRUMP KUWAREJESHA WAHAMIAJI MAREKANI KWAO



Donald Trump asema kati ya wahamiaji haramu milioni mbili ama tatu watasafirishwa kutoka Marekani baada ya kuapishwa kuwa rais wa chi hiyo.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani,CBS, Trump amesema wahamiaji wote wenye rikodi za uhalifu, ikiwemo makundi ya wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya ndio watakuwa kipaumbele chake .Hatma ya wahamiai haramu milioni nane na ushee waliosalia itafahamika mara tu mpaka utakapokuwa salama.Donald Trump ameongeza kuwa semhemu ya ukuta ambao aliahidi kujenga kwenye mpaka baina ya nchi yake na Mexico, unaweza kuwa ni uzio.

Habari kuu Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Novemba 14



KUNDI LA KIGAIDI LA ISIS LAPIGA MARUFUKU UVAAJI WA NGUO ZA NDANI KWA WANAUME


Kile kikundi cha kigaidi kijulikanacho na kuogopwa kwa ukatili wa kutisha hili kuleta hofu kimeenda hatua zaidi mbele kwa kuweka sheria kali.

Wahuni hao Wamepiga marufuku uvaaji wa boxer na Chupi kwa wanaume kwasabab ni kimagharibi badala yake unatakiwa uvae bukta ndefu inayovuka magotini ama kitambaa unachojifunga kiunoni kama taulo. Na ukibainika kuvaa hivyo hatua kali itachukuliwa dhidi yako.

Wanajeshi wa Iraq na Kurd walishangaa kukuta mabandiko hayo yanayokataza uvaaji wa Chupi na Boxers walipoukomboa mji wa Hammam Al Allil kusini mwa Mosul dhidi yao.

Pia ISIS imepiga marufuku kunyoa ndevu, kusikiliza mziki na kuvaa jeans zilizobana.

 

Gallery

Popular Posts

About Us