Saturday, 25 March 2017
WAPENZI WADONDOKA NA KUFA WAKATI WAKIFANYA MAPENZI DIRISHANI...!!!
Jinsi Maulid Kitenge alivyomnusuru Nape na bastola
MWANDISHI wa habari, Maulid Kitenge, ambaye juzi alimnusuru aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye dhidi ya mtu aliyemshikia bastola wakati akielekea kuzungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Protea, jijini Dar es Salaam, amefunguka na kueleza kile kilichomsukuma aingilie kati.
Juzi, mara baada ya Nape kuwasili karibu na hoteli hiyo, ambayo inapakana na Kanisa la Mtakatifu Petro, lililoko eneo la Oysterbay, aliposhuka tu ghafla kijana huyo mrefu mweusi akiwa amevalia suruali ya jinzi, shati la mikono mirefu la mistari mistari pamoja na kofia, alimkimbilia na kumshika mkono kiongozi huyo akimtaka arudi kwenye gari.
Nape hakukubaliana na hatua hiyo, ambaye alimtaka kijana huyo aonyeshe kitambulisho, lakini hakufanya hivyo, zaidi alirudi hatua chache nyuma na kisha kutoa bastola iliyokuwa kiunoni kwake na kumtishia.
Wakati tukio hilo likitokea, ghafla alitokea kijana mwingine aliyekuwa amevalia suruali na fulana nyeusi akimsaidia yule aliyekuwa ameshika bastola kumsukuma Nape, ili arudi kwenye gari lake.
Ni katika mazingira kama hayo, ndipo waandishi wa habari waliokuwa ndani ya Hoteli ya Protea wakimsubiri Nape walipoanza kusogea, huku Mwandishi wa habari mashuhuri wa michezo nchini, Kitenge, akiwahi kufika na kwenda moja kwa moja katika eneo ambalo Nape alikuwa akisukumwa aingie ndani ya gari lake.
Kitenge alimsihi kijana huyo aache kumsukuma Nape na alipoonekana kubisha aliamua kumsukuma pembeni.
MTANZANIA Jumamosi jana lilizungumza na Kitenge, ambaye alisema:
“Niliona mtu anamtolea Nape bastola nikashangaa, kwani muda mfupi uliopita alikuwa waziri na isitoshe ni mbunge, sasa yule mtu aliambiwa ajitambulishe, lakini hakujitambulisha,” alisema.
Alisema tukio lile lilimshtua, kwani mtu huyo aliyekuwa ameshika bastola alikuwa akitetemeka sana, huku jasho likimtoka.
“Hatukumwelewa, kwanza hakutoa kitambulisho,” alisema Kitenge, ambaye juzi wakati akimwokoa Nape alisikika akimwambia kijana huyo aliyeshika bastola; “unaharibu bwana mwache, mwache bwana….”
Wakati tukio hilo linatokea walikuwapo waandishi wa habari wachache, huku wengi wao wakiwa ndani ya hoteli hiyo wakimsubiri Nape, lakini purukushani hizo ambazo ziliambatana na kelele ziliwashtua na hivyo kulazimika kukimbia kuelekea eneo la tukio.
Waandishi wa habari walivyofika wengi mtu huyo hakuweza kuonekana tena na ndipo Nape alifanikiwa kuzungumza nao.
Tukio hilo la kutolewa bastola lilitanguliwa na lile la Meneja wa Hoteli ya Protea, aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Suleiman, kutangaza kuzuia mkutano wake na waandishi wa habari usifanyike katika hoteli hiyo, kwa kile alichodai kuwa, ni maelekezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Susan Kaganda.
KITENGE GUMZO
Kutokana na kitendo hicho, mwanahabari huyo sasa amegeuka gumzo katika maeneo mbalimbali, hususan katika mitandao ya kijamii.
Andiko ambalo linasambaa sana kwenye mitandao ya kijamii, lakini halijulikani aliyeandika, ni lile lililoambatana na picha yake inayomwonyesha akikimbia huku likisomeka;
“Wanaume wa Dar walikuwa wanadharaulika sana, Kitenge kawaokoa…”
Si hilo tu, baadhi ya watu wamekwenda mbali na hata kuanza kuhoji nguvu alizonazo mwanahabari huyo kiasi cha kuweza kuhimili kumwondoa mtu huyo aliyeshika bastola.
Hii kali ya Mwaka!!..Matajiri Wajenga Mahandaki Kujiandaa na Mwisho wa Dunia..!!!
UKITAMKA “handaki la kujificha kwa ajili ya mwisho wa dunia” watu wengi watadhani kuwa ni chumba kilichojengwa kwa uimara wa hali ya juu kikiwa kimesheheni vyakula vilivyosindikwa na vitu vingine ili kuwezesha watu kuishi kwa muda mrefu.
Tishio la kuangamia kwa dunia kwa sasa ni kubwa kama ilivyokuwa wakati wa Vita Baridi, lakini mahandaki haya ya leo ni tofauti kabisa na zile za karne ya 20.
Kampuni nyingi duniani kote zimekuwa zikishughulikia kuongezeka kwa mahitaji ya majengo yenye uwezo wa kuwalinda watu dhidi ya hatari ya aina yoyote, iwe ni magonjwa hatari ya kuambukiza, dunia kugongana na sayari au kitu chochote kutoka anga za juu, Vita ya Tatu ya Dunia – lakini wakati huo huo jengo hilo liwe ni sehemu yenye starehe.
“Mahandaki wakati wa baba au babu yako hayakuwa yanakalika,” anasema Robert Vicino, mfanyabiashara wa majengo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Vivos, kampuni ambayo hujenga na kusimamia majumba ya kifahari duniani kote.
“Hayakuwa yanavutia. Yalikuwa yanajengwa kwa chuma, kama ilivyo meli au kifaa cha kijeshi. Na ukweli ni kwamba, binadamu hawezi kuishi kwa muda mrefu katika mazingira ya namna hiyo.
Mahitaji ya mwisho wa dunia
Matajiri wengi duniani, wakiwemo mameneja wa mifuko ya fedha, nyota wakubwa wa michezo mbalimbali na matajiri katika nyanja ya teknolojia (kuna uvumi kuwa Bill Gates amejenga handaki kwenye kila sehemu ambapo ana mali isiyohamishika kama ardhi) wamechagua kubuni makazi yao ya siri kwa ajili ya familia na wafanyakazi wao.
Gary Lynch, meneja mkuu wa kampuni ya Rising S Company ya huko Texas nchini Marekani, anasema kuwa mauzo kwa ajili ya majengo ya chini ya ardhi yameongezeka kwa asilimia 700 mwaka 2016, ukilinganisha yalivyokuwa mwaka 2015, wakati kwa ujumla mauzo hayo yameongezeka kwa asilimia 300 tangu uchaguzi mkuu wa Marekani Novemba mwaka jana.
Majengo ya chuma ya kampuni hiyo, ambayo yamebuniwa kwa ajili ya kudumu kwa vizazi kadhaa, yanaweza kuchukua chakula cha kutosha matumizi ya mwaka mzima kwa kila mkazi wa majengo hayo na pia yana uwezo wa kuhimili matetemeko makubwa ya ardhi.
Lakini wakati wengine wanataka kukaa kwenye majengo hayo peke yao, wengine wanataka kukaa huko na jamii zao ili kuwa na mfano wa maisha yanayofanana na yalivyo sasa.
Wabunifu wa majengo maalumu kwa ajili ya jamii mara nyingi hununua mahandaki ambayo hapo awali yalikuwa yakitumiwa kijeshi au mahandaki maalumu ambayo yalijengwa na serikali ya Marekani kwa ajili ya kuficha silaha kali – maeneo ambayo yanaweza kugharimu mamilioni ya dola kwa ajili ya kuyajenga leo hii.
Majengo hayo ambayo yameimarishwa, yamebuniwa kuweza kuhimili shambulio la kinyuklia na yamewekewa mifumo maalumu ya umeme, mifumo ya kusafisha maji, mifumo kwa ajili ya kuhimili matetemeko makubwa ya ardhi, na pia kuhimili mashambulizi ya silaha za kibiolojia na kikemikali. Lakini pia, majengo hayo yana mifumo kwa ajili ya kusafisha hewa.
Majengo hayo yanaweza kuchukua kiasi cha chakula cha kuweza kukaa kwa mwaka mzima au zaidi, na mengi ya majengo hayo yana bustani maalumu ambazo zinaweza kutumiwa kupanda mimea kwa kutumia madini fulani ambayo huwekwa kwenye maji, hivyo kuondoa umuhimu wa kutumia udongo, na hivyo kuweza kuwapatia wakazi wa majengo hayo virutubisho maalumu ambavyo vinapatikana kwenye mimea.
Wajenzi wa majengo hao pia wanafanya kazi ili kuhakikisha kuwa jumuiya ambazo zitakuwa zinaishi kwenye majengo wanakuwa na vipaji mbalimbali ili kuhakikisha kwamba watu wataweza kuishi katika majengo hayo kwa muda mrefu, kuanzia madaktari hadi walimu.
Vicino anasema Vivos imepokea maombi mengi kwa ajili ya majengo yake wakati wa uchaguzi nchini Marekani mwaka jana.
Safina ya mbunifu
Moja ya makazi hayo, Vivos xPoint, yapo karibu na Black Hills huko South Dakota nchini Marekani, na lina jumla ya mahandaki 75 ya kijeshi ambalo zamani lilikuwa ni sehemu maalumu kwa ajili ya kuhifadhi silaha za jeshi hadi mwaka 1967.
Sehemu hiyo sasa inabadilishwa ili kuwa ni sehemu yenye uwezo wa kuchukua jumla ya watu 5,000. Marekebisho ndani ya mahandaki hayo yanafanywa kwa gharama ya kazi ya dola 25,000 hadi 200,000 kwa kila moja. Bei ya handaki hutegemea ukubwa wake.
Jengo lenyewe litawekwa starehe zote ambazo hupatikana kwenye mji mdogo, zikiwemo ukumbi wa burudani, madarasa, bustani maalumu, kliniki na sehemu ya kufanya mazoezi ya mwili.
Kwa wateja ambao wanatafuta vitu adimu na vya starehe zaidi, kampuni hiyo inauza Vivos Europa One, ambayo imepewa jina la “safina ya kisasa ya Nuhu” katika ghala za zamani za kuhifadhi silaha wakati wa vita baridi nchini Ujerumani.
Jengo hilo, ambalo limejengwa kwenye jabali, lina makazi 34 binafsi, kila moja likiwa na ukubwa wa futi za mraba 2,500, na likiwa na uwezekano wa kuongeza ghorofa hivyo kufikia ukubwa wa futi za mraba 5,000.
Nyumba zilizoimarishwa kuhimili nyuklia
Majumba kwa ajili ya matajiri yaliyojengwa na Larry Hall zinazofahamika kama Survival Condo huko Texas nchini Marekani zinatumia maeneo mawili yaliyokuwa yanatumiwa kuhifadhi makombora ya masafa marefu, ambayo yalijengwa na mainjinia wa Jeshi la Marekani ili kuhifadhi vichwa vya mabomu ya nyuklia wakati wa miaka ya 1960.
“Wateja wetu wanapewa faida ya kuwa na nyumba ya kifahari na ambayo inakuwa imeimarishwa kuhimili shambulizi la kinyuklia,” anasema Hall, ambaye tayari amesjaanza kazi ya ujenzi wa nyumba nyingine ya aina hiyo sehemu nyingine.
Sakata la Nape Lazidi Kumpasua Kichwa Magufuli..Habari Katika Vichwa vya Magazeti ya Leo 25/3/2017...!!!
Hivi ndivyo Nape Alivyojitabiria Kuvuliwa Uwaziri wa Habari..
Mtu anapopatwa na jambo, ni kawaida ya binadamu kuangalia mambo au kauli zake alizokuwa akitoa kabla ya kufikwa na tukio hilo.
Mara nyingi mambo au kauli hizo huonyesha kama vile alikuwa akiona tukio likimjia au kumtokea.
Unaporejea kauli za hivi karibuni za Nape Nnauye, unaona dhahiri kuwa alikuwa kama anaona kinachokuja na kujitabiria kuwa angevuliwa uwaziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo.
Kauli ya mwisho na yenye nguvu aliitoa juzi mchana wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tukio la uvamizi wa studio za televisheni za kampuni ya Clouds Media Group.
“Niseme tu kwamba nimepokea ripoti na kama nilivyosema kazi hii si rahisi sana, ina gharama kubwa sana. Gharama ya kusimamia haki, kusimamia ukweli,” alisema juzi.
Kauli hiyo aliirudia jana wakati akiongea na waandishi wa habari nje ya Hoteli ya Protea baada ya kuzuiwa kufanya mkutano wake ndani.
Nape aliondolewa katika nafasi hiyo katika mabadiliko madogo yaliyofanyika jana asubuhi, siku moja baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo ambayo aliahidi angeiwasilisha kwa mamlaka za juu, ambazo alizitaja kuwa ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais.
Katika mabadiliko hayo, Rais Magufuli amemteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Dk Harrison Mwakyembe ambaye anaziba nafasi ya Nape.
Ni kama Nape alikuwa akiona gharama za kusimamia haki za Clouds Media za kutoingiliwa katika shughuli zake na viongozi baada ya kituo hicho kuvamiwa na askari waliokuwa na silaha za moto wakimsindikiza kiongozi aliyekwenda kuhoji sababu za kituo hicho kutorusha habari ya ‘umbea’ iliyokosa sifa stahiki.
Maneno hayo ya Nape ni sehemu ya mlolongo wa kauli za utabiri ambazo amekuwa akizitoa kwa siku chache zilizopita wakati akizungumza na waandishi na kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya kituo cha Clouds kuvamiwa, Nape alituma ujumbe kwenye akaunti yake ya Tweeter Machi 20 akisema “No Longer at Ease”, ikiwa ni nukuu ya kitabu cha fasihi kilichoandikwa na Chinua Achebe mwaka 1960 kumaanisha hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho.
Siku hiyo, Nape alituma ujumbe mwingine katika akaunti hiyo akisema “each day is a day of decisions, and our decisions determin our destiny” akimaanisha “kila siku ni siku ya uamuzi na uamuzi wetu huamua mustakabali wetu”.
Kama vile haitoshi, Nape alituma ujumbe mwingine siku hiyo akisema “majaribu huja ili kutuinua kutoka utukufu hadi utukufu. Kikubwa tusikate tamaa, utukufu mkubwa upo mbele. Quaresma njema”.
Nape aliandika hayo wakati mchakato wa kamati aliyoiunda ikiendelea kuchunguza tukio la Clouds kuvamiwa.
Na alikuwa na ushauri kwa wanasiasa wengine. “Na kwa kuwa sisi wengine tuliopewa dhamana ya kuwatumikia watu ni vizuri kujifunza kuwa wanyenyekevu, kwanza ina baraka kwa Mwenyezi Mungu, lakini pia tutakuwa tunawatendea haki Watanzania ambao ndiyo wametuchagua na kutuweka kwenye madaraka.”
Baada ya kuvuliwa uwaziri, Nape jana alituma tena ujumbe katika akaunti yake ya Tweeter akiandika kwa herufi kubwa baadhi ya maneno kuweka msisitizo.
“Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO (jana) mchana nitakutana na wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali. Kwa sasa naomba TUTULIE!”
Baadaye akatuma ujumbe mwingine akisema “tukutane saa nane kamili Protea Hotel karibu na St. Peter. Nitakutana na wanahabari. Karibuni sana!”
Kauli za wadau
Wadau wa habari wakiwamo wanasiasa, wasomi, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na wanahabari wameeleza kushtushwa na mabadiliko hayo na kummimia sifa mbunge huyo wa Mtama.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Nevile Meena alisema tasnia ya habari imepokea kwa huzuni taarifa hiyo, hasa kutokana na ukweli kuwa ameondoka katika kipindi ambacho alikuwa karibu na wadau akitetea uhuru wa habari.
“Tulitegemea Nape angeondoka wizara hiyo, lakini hatukutegemea ingekuwa kwa mtindo huu. Katika sakata hili Nape alionyesha wazi kutoegemea upande wa Serikali na alisimamia haki,” alisema Meena.
Kuhusu nafasi hiyo kuchukuliwa na Dk Mwakyembe, Meena alisema tasnia inamkaribisha, ikitegemea atafanya vizuri, “asipokwenda sawa tutaenda naye hivyohivyo”.
Kauli ya masikitiko pia ilitolewa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC) ambayo rais wake, Deogratius Nsokolo alisema, “Nape alikuwa karibu mno na waandishi na wadau wote wa habari na alikuwa akisimamia haki”.
Alisema huenda kilichomgharimu Nape ni kwenda kutembelea kituo cha Clouds na kuunda kamati ya kuchunguza uvamizi huo.
“Nimsihi Nape asikate tamaa. Yeye ni mwanasiasa mzuri na mkomavu. Hakuna ubishi tena, ni shujaa ambaye amejitoa kusimamia haki. Sina uhakika sana kama atakayeshika nafasi yake atakuwa kama yeye,” alisema.
Wanasiasa
Akizungumzia kuondoka kwa Nape, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe alisema haitoshi kumlilia Nape, bali wananchi wanapaswa kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.
“Haifai tu kumlilia Nape kwamba anaonewa, tunapaswa kumuwajibisha Rais ambaye amechaguliwa na wananchi. Anapaswa kuwa mnyenyekevu kwa wananchi na hatupaswi kuendekeza tabia zozote za utawala wa kiimla,” alisema kiongozi huyo wa ACT Wazalendo.
“Ni lazima sisi viongozi tuwaelekeze wananchi mabaya au mazuri na tuwaelekeze kuchukua hatua.”
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kilichotokea ni uthibitisho wa madai ya muda mrefu ya wapinzani kuwa Rais Magufuli anapingana na mawazo ya wananchi wake.
“Huu ni uthibitisho kuwa tuna Rais ambaye anapingana na maoni ya watu anaowaongoza. Kinachoendelea hapa si Rais au Nape, bali ni hisia za wananchi. Nape amejipambanua hivi karibuni kama waziri makini na alichokifanya kiko ndani ya uwezo wake,” alisema Mbowe.
“Sisi kama wapinzani tunaona tunashamiri kwa sababu CCM inasambaratika, lakini si jambo la kufurahi tu, bali tuisaidie nchi yetu.
“Kitu cha msingi Rais anapaswa kuwa mwepesi wa kusikiliza kuliko kuongea. Marais wengi wamefanikiwa kwa kusikiliza wananchi wao, lakini Rais Magufuli ni tofauti, anaongea kuliko kusikiliza maoni ya wananchi wake. Ndiyo maana mawaziri wanajiuzulu, wabunge wanajiuzulu kwenye kamati zao, yote kwa sababu Rais hataki kusikiliza maoni yao,” alidai Mbowe.
Lakini Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora (Fordia), Bubelwa Kaiza aliunga mkono hatua ya Rais Magufuli akisema kuwa aliitarajia.
“Binafsi hatua hii niliitegemea kwa sababu vitendo alivyovifanya Nape ni kama hakujua kuwa Serikali ndiyo inayojisimamia. Alipaswa kuomba ushauri kabla ya kuunda ile kamati yake,” alisema Kaiza.
“Ni kweli kama Waziri wa Habari angekwenda kutembelea Clouds Media, lakini asingesema chochote. Lakini yeye aliunda kamati na kufanya aliyofanya jana (juzi). Kwa Serikali iliyo makini ni lazima izibe vaccum (ombwe) inayojitokeza.”
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai alisema kama wamiliki wa vyombo vya habari wako tayari kufanya kazi na waziri yeyote anayeteuliwa na Rais, ilimradi tu afuate misingi na weledi wa kazi hiyo.
“Kitakachotukosanisha naye ni kama atakandamiza uhuru wa habari,” alisema Nanai.
“Tunampongeza waziri mpya, Dk Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa na pia tunampongeza Nape Nnauye anayeondoka kwa kazi kubwa aliyoifanya. Kuondoka kwake kumetushtua kwa sababu tulikuwa naye kwenye kazi na sasa itabidi tuanze na mtu mpya.”
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi alisema Nape ameondoka kishujaa kwa sababu alikuwa amebeba matumaini ya Taifa.
Alisema kutokana na kuondoka kishujaa, anayo nafasi ya kuteuliwa tena kuongoza wizara nyingine na alimsifu kwa jinsi alivyosimamia suala la kuvamiwa kwa studio za Clouds Media.
Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Mohamed Bakari alisema kitendo cha kuondolewa kwa Nape saa chache baada ya kupokea ripoti, kinaashiria kuwa Rais John Magufuli hapendi kushauriwa.
“Waziri aliyewekwa, Dk Harrison Mwakyembe ameonyesha kutosimamia mambo yake katika wizara alizotoka. Hana msimamo,” alisema Dk Bakari na kuongeza kuwa ni mapema kumzungumzia waziri mpya wa Katiba, Profesa Kabudi kwa kuwa ndio kwanza ameteuliwa.
Askofu Gwajima
Askofu Josephat Gwajima, ambaye alisema habari iliyomtuhumu kuwa amezaa na mwanamke mmoja wa jijini Dar es Salaam ndiyo iliyosababisha Clouds kuvamiwa, jana pia alijibebesha mzigo wa Nape.
Akiwa katika ziara ya kituo cha redio cha EFM, Askofu Gwajima alisema: “Sababu zilizofanya Nape aenguliwe zinanihusu sana mimi, sababu mkuu wa mkoa alivamia mahali kuwalazimisha warushe kipindi kinachonihusu. “Nataka kila mtu ajiulize je, ni nani aliyekwenda kushinikiza Clouds kwamba material (kipindi) za kumchafua Askofu Gwajima zipigwe, ni nani? Nani alikuwa nyuma ya Mkuu wa Mkoa hata kiasi kwamba Nape aondolewe uwaziri?”
Wanamuziki wazungumza
Nape pia alikuwa anaongoza wizara inayowahusu wasanii, ambao pia wameeleza kushtushwa.
“Nape endelea kuwa mwerevu,” alisema mwanamuziki wa miondoko ya Bongo Fleva, Nick wa Pili alipozungumza na gazeti hili.
Nick alisema inauma ingawa haijulikani kwa nini amebadilishwa na kuwekwa mwingine, lakini kitendo cha kuondolewa kwake ni pengo kwa wasanii kwa sababu alikuwa ni mtu anayepatikana kirahisi.
“Tusubiri tuone huyu mpya itakuwaje. Inawezekana akaendeleza mazuri tuliyoanza Nape,” alisema Nick wa Pili.
Rais wa Mfuko wa Muziki Tanzania, Dk Donald Kisanga alimtaka Nape kusonga mbele.
“Mapambano bado yanaendelea. Wewe bado kijana tena jasiri, bado una fursa ya kufanya vitu vingi zaidi,” alisema.
Alisema kinachosikitisha ni kuondolewa kwenye nafasi aliyopo kwa sababu alionekana kuimudu, ingawa matumaini yapo pia kwa anayekuja.
Muigizaji aliyebobea, Dk Cheni alisema hakuna anayefahamu Rais anawaza nini, hivyo ni vyema kusubiri kitakachotokea.
Mwigizaji mwingine wa filamu, Johari Chagula alisema uamuzi huo umemuuma kwa sababu Nape alikuwa waziri pekee aliyejitokeza hadharani na kupigana vita moja, akisikiliza matatizo ya wasanii bila kupitia mtu mwingine.
“Kiukweli alitutoa eneo moja kutupeleka jingine. Alikuwa amesimama katikati ya masilahi yetu,” alisema Johari.
Mstuko kwa wanamichezo
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (Tava), Agapa Agostino alisema ni mapema Nape kuondolewa kwa kuwa tayari alikuwa na mikakati mingi katika kuboresha tasnia ambayo ameiachia njiani.
“Naheshimu uteuzi wa Rais. Ni maamuzi yake, lakini naona kama imekuwa mapema mno Nape kuondolewa. Pamoja na yote, namshauri mrithi wake kuendeleza mipango yote mizuri iliyoachwa na Nape na mabaya kuyaweka kando,” alisema.
Kocha wa judo, Zaid Hamis alisema misimamo ya Nape katika kutetea masuala ya habari ndiyo imechangia kuenguliwa katika nafasi hiyo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Arusha, Alfredo Shahanga alisema mwenye uamuzi ni Rais, na kwamba watafanya kazi na yeyote yule watakayeletewa.
“Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua mawaziri hivyo maadamu kaona inafaa Nape aondoke ni sawa na sisi tutafanya kazi na waziri yeyote tutakayeletewa,” alisema.
Makosa Unapodeti Mwanamke Ambayo Unapaswa Kuyaepuka
Hebu soma stori hii kali ya mahaba
Alikuwa ni rita niliyempenda zaidi pale kazini kwetu , kazi yake sikujua ni nini haswa , lakini nilimwona mara kwa mara akipita huku na kule katika shuguli , mimi kazi yangu ilikuwa ni nyingine kabisa .
Kampuni yetu ilikuwa kubwa na wafanya kazi wengi , ilikuwa sio rahisi kujua watu wote koz wengine wako idara zingine na shuguli zao ni zingine , ndio kama rita sikujua yeye kazi yake wala yuko idara gani .
Lakini alikuwa akipita idara yetu , nikikaa pale katika computer huwa namwona akipita na kuchugulia wakati mwingine anaongea na kiongozi wa idara yetu kisha anaondoka , kweli nilimpenda , siri ilikuwa ni rohoni mwangu .
Kwanza nilivutiwa na sauti yake alivyokuwa anaongea upole na taratibu , ngozi yake nyeupe laini sio ya mkorogo , nilivutiwa na macho yake , nywele zake na mwisho kabisa kuliko zote ni miguu yake , vile vimini nilinichanganya kwa hakika .
Wakati mwingine nilihisi anakuja kwangu labda kunisalimia hivi au kuniuliza kitu Fulani lakini wapi , hata salamu hatowi , nilitafuta contact zake mpaka nikachoka , niliwauliza wafanya kazi wengine walikataa kunipa .
Nilihisi nao wanampenda ndio maana hawataki kunipa contact zake , pia ni mimi mwenyewe nilikuwa ni mtu wa aibu sana , sidhubutu kuongea na mwanamke haswa yeye anayevutia , niliendelea kuvumilia tu .
Siku moja asubuhi , alikuja chumbani kwangu kule kazini , nilikuwa nimekaa mwenyewe ,tu , sikumbuki alikuja kutazama nini , ila alikuja mpaka kule ninapokaa , alipofika nilisimama na kumshika mkono , nilimweleza kwamba nampenda sana .
Hakuamini , aliomba nimnongoneze , nikafanya hivyo , kisha akani hug , nami nilimpiga busu na mdogo tukashikana mikono mpaka mlangoni wakati anatoka nilimwomba tuonane jioni ya siku hiyo kwa maongezi , alikubali kwa furaha .
Nilihisi roho yangu imeingia dhahabu , nilijiona kweli mimi ni mwanajeshi wa mapenzi ,nikaanza kupanga mambo ya jioni , siku hiyo nzima sikufanya kazi nilikuwa na furaha ya kukutana na rita jioni hiyo mambo poa .
Jioni ilifika , rita akanikumbuka alinipitia chumbani kwangu , tulianza safari ya kwenda sehemu Fulani inaitwa sunrise , tulipanda taxi mpaka kule , tulipofika kule tulikaa chini ya mchanga huku tukiongea na tabasamu kwa mbali .
Hapo sunrise kukawa na speaker kubwa tulisikia sauti mpaka kule mchangani , muda huo ilikuwa ni saa 12 jioni , nyimbo iliyokuwa inapigwa ni butterflies ya Michael Jackson , maneno ya nyimbo ile ni matamu yaliendana na wakati ule .
Nyimbo ile iliendana na wakati wetu pale , wote tulilala mchangani tukipigana mabusu , kuchezeana miguu na kutekenyana , taratibu , nilikuwa nimefunga tai wakati wote huo alinivua tai yangu , wakati tukiendelea na mambo mengine .
Aliniambia ananipenda sana kwa mara ya kwanza , hapo moyo ulienda mbio sana , nami nilimwambia pia jinsi nilivyokuwa najisikia siku zote anakuja katika office yetu , tuliongea kwa muda kisha tukasimama kurudi zetu ukumbi mkuu .
Njiani katika mchanga tulikutana na vijana 3 , hao vijana walitusimamisha walikuwa wamevaa jeans wote , mmoja nilimwona na kitu kama bisi bisi hivi , mimi nilimshika rita mkono kumwamuru asijibu chochote tuendelee kwenda zetu .
Ghafla upande wa kulia walitokea vijana wengine 2 wakawa wanakuja kwa kasi kutuvamia , yule mmoja mwenye bisi bisi akachomoa ile bisi bisi yake alitaka amchome nayo rita , ilibidi nimpige ngwala rita adondoke chini , alipofika chini hiyo bisi bisi ilipita juu .
Nikainama chini , kubeba mchanga na kumwagia machoni , hapo alipofuka macho kwa muda , hakuweza kuona vizuri alianza kupiga kelele , wenzake walikuwa na mashaka kuhusu kuendelea na hiyo kasheshe .
Nilimbeba rita wangu , kuendelea na safari , tulipofika karibu na mwanga jamaa mwingine alikuwa na kisu , kwa kunutsukiza ,alirusha kisu kutokea nyuma , mimi na rita tulijidondosha kwa mbele , kukwepa paaa tulidondoka .
Nikawa chini , jamaa akaona ameshanipata nimedondoka , aliruka juu , ili anikanyage na viatu vyake , wakati anajiandaa kuruka nilimpiga mguu mmoja wa kushoto , kabla ya kudondoka chini , nilidaka mguu mwingine kwahiyo mguu mmoja juu mwingine nimeushika .
Niliugeuza na kuutengua , kisha nikachukuwa kisu na kumchomeka mwenyewe shingoni .Mimi na rita tulinyanyuka na kuendelea na safari yetu kurudi nyumbani .
Tulirudi nyumbani na maisha yalikuwa poa tu .
Kesho yake kazini , rita alikuwa akiwahadithia wenzake mambo yalivyokuwa
Kwaheri
Unapotokea kumpenda mtu aliye na mpenzi wake, Fanya haya!
Mapenzi yamekuwa yakichukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku na yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa furaha kwa kila mtu.
Kama huamini, angalia wale waliotokea kupenda na wao wakapendwa, utabaini nyuso zao zimetawaliwa na
furaha isiyo na kifani. Lakini mapenzi hayo hayo yamekuwa ni chanzo cha vilio kwa baadhi ya watu.
Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda.
Ilishawahi kutokea msichana akampenda kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake wakafunga ndoa.
Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyopendana lakini huko nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye na mbele wala nyuma.
Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume anaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake.
Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?
Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako.
Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.
Chunguza
Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye. Ndiyo maana nikasema chunguza uhusiano wake kwanza.
Usitafute uadui
Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.
Una nafasi kwake?
Sawa umetokea kumpenda msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.
Ni rahisi kubadili uamuzi wake?
Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.
Pingana na moyo wako
Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na demu ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.
Kwa hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha kumng’ang’ania msichana mwenye mpenzi wake licha ya ukweli kwamba, huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya kuwa mume wake na siyo huyo aliye naye.
Urafiki ni poa?
Umempenda sana na hauko tayari kumkosa katika maisha yako lakini imetokea kwamba tayari yuko na mtu na umebaini huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba angalau urafiki. Siyo urafiki wa kivile sana ila angalau pale unapotaka kusikia sauti yake kwa kumsalimia tu, upate nafasi hiyo.
Usiumie, yupo mwingine
Haina haja ya kujitafutia vidonda vya tumbo bure kwa kuwa tu umebaini uliyetokea kumpenda tayari ana mtu. Chukulia ni hali ya kawaida, mademu wazuri ambao wanaishi singo wapo kibao huko mtaani, ni suala la wewe kutulia tu. Amini yupo mwingine ambaye atayafanya maisha yako yawe ya furaha.
Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana kuhakikisha unampata kwa sababu ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa gizani. Ila pale utakapoona uwezekano wa kuwa naye haupo, usilazimishe ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha tu!
Kazi Immeanza Rasmi..Waziri Mpya wa Habari Aaanza na Sakata la Makonda Kuvamia Clouds,Ametoa Kauli Hii👇
Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo amejibu swali la waandishi kadhaa wa habari waliomhoji mapema leo baada ya kuapishwa katika viunga vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mwakyembe amenukuliwa akisema maneno yafuatayo juu ya sakata hilo lililotikisha vichwa vya habari nchini kwa juma moja sasa.
"Ninachokijua kuhusu tukio la Clouds Media kinatokana na vyombo vya habari, sidhani kama taarifa hizo zinatosha mimi kutoa uamuzi"-Waziri Mwakyembe
Hii kali sasa !!Familia ya Makonda Yaanika Ukweli Wote Juu ya Jina la Bashite..Soma hapa
Mzee Khamesse
Kutokana na kuwepo kwa taarifa za Paul Makonda kulelewa katika familia ya aliyekuwa Meya wa Jiji la Mwanza, Seleman Khamesse, JAMHURI limefika nyumbani kwa Mzee Khamesse, katika eneo la Nyamanoro, jijini Mwanza na kufanya mahojiano;
JAMHURI; Kuna taarifa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewahi kuishi nyumbani kwako. Je, ni kweli?
KHAMESSE; Ni kweli Daudi alikuja kwangu akiwa darasa la tano akitokea kijijini kwao, Koromije na kisha kuishi hapa na familia yangu.
JAMHURI; Mbona unasema uliishi na Daudi wakati nimekuuliza kuhusu Paul Makonda?
KHAMESSE; Ni kweli nimesema Daudi kwa sababu namfahamu kwa jina hilo. Amekuja kwangu akitokea kwa wazazi wake waliokuwa wakiishi Koromije, na jina lake ni Daudi Albert Bashite.
Wakati shangazi yake ambaye ni mke wangu mdogo (Mama Khamesse) anamleta hapa alikuwa akitumia jina hilo na hata alipopelekwa shule alikuwa akitumia jina la Daudi Bashite wakati anasoma Shule ya Msingi Nyanza.
Hata wakati anakwenda kuanza shule Pamba Sekondari alienda kwa jina la Daudi Bashite.
JAMHURI; Una uhusiano gani na Daudi?
KHAMESSE; Daudi ana uhusiano na mke wangu mdogo Bernadeta maarufu kama Mama Khamesse. Mama ndiye aliyemleta hapa kwani ni shangazi yake anaweza kukwambia zaidi kuhusu hilo.
JAMHURI; Tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na kisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mmekuwa mkiwasiliana?
KHAMESSE; Hatuna mawasiliano kwani tangu ateuliwe amewahi kufika nyumbani kwangu hapa tulipo mara mbili tu, tena alikuja usiku.
Mara ya kwanza alikuja saa saba usiku, hakuingia ndani aliishia nje akaongea na vijana wenzie akaondoka. Mwaka jana mwezi wa Ramadhan alikuja saa tano usiku akiwa amesindikizwa na vijana wawili hakuingia ndani aliishia nje akaongea na vijana wenzie, kwa vile nilikuwa sijalala tulisalimiana akanipatia mawasiliano yake kisha akaondoka.
Ukweli ni kwamba hatuna mawasiliano, kutokana na kwamba haoneshi kuhitaji kuwasiliana kwani namba alizonipatia nikipiga hapokei, hata nilipotuma ujumbe hakukuwa na majibu.
Ila wasiliana na shangazi yake anaweza kukueleza zaidi maana mie sikukaa naye sana kutokana na majukumu yangu yaliyokuwa yakinikabiri wakati huo. Pamoja na kwamba alikuwa akiishi nyumbani kwangu.
Ramadhani Khamesse
Ramadhani ni mtoto wa Mzee Khamesse, ambaye alikuwa akisoma shule moja na Paul Makonda, amesema kwamba amesoma na kuishi na Makonda katika kipindi chote alichokuwa nyumbani kwao.
“Tulikuwa naye shule moja ya Nyanza, na jina lake ni Daud Albert Bashite. Dada yangu, mimi, huyu Daudi tulikuwa tunalala naye chumba kimoja hivyo namfahamu. Pia tulikuwa rika moja hivyo hata michezo yetu ilifanana ingawa tulikuwa tunatofautiana baadhi ya tabia,” amesema Ramadhan.
Akimuelezea Makonda amesema anajua kuishi na watu pale anapohitaji jambo lake lifanikiwe kwani alikuwa anajua kunyenyekea kwa walimu ingawa alikuwa na tabia ya kubagua marafiki hasa wale ambao familia zao zilikuwa duni. “Alikuwa ni rafiki wa wenye uwezo,” amesema.
Pia ameeleza kwamba baada ya kujiunga na masomo ya jioni Pamba Sekondari alihamia kwa ndugu yake mwingine anayefahamika kwa jina la Mwana Zakhia.
Kuhusu mawasiliano kati yao, amesema ingawa wamekua pamoja hakuna mawasiliano yoyote kati yao kutokana na Makonda kumpatia namba ambazo hata akipiga simu hazipolewi.
“Alikuja hapa mara mbili usiku tukazungumza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukumbushana maisha tuliyoishi. Zaidi ya hapo hatuna mawasiliano kabisa zaidi ya kumsikia na kumuona kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,” amesema Ramadhani.
Mama Khamesse
JAMHURI lilifika nyumbani kwa Mama Khamesse Lumara na kufanya mahojiano;
JAMHURI: Una uhusiano gani na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam?
MAMA KHAMESSE: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni ndugu yangu kwani baba yake, Mzee Albert Bashite ni binamu yangu. Kwa hiyo Daudi ananiita mimi shangazi.
JAMHURI: Unaweza kunisaidia jila lake ni Daudi au Paul Makonda?
MAMA KHAMESSE: Mimi ninamfahamu kwa jina la Daudi Albert Bashite. Na hata wakati nampeleka kuanza shule katika shule ya mshingi Nyanza aliandikishwa kwa jina la Daudi Bashite.
JAMHURI: Ilikuwaje ukaanza kuishi naye?
MAMA KHAMESSE: Mama yake alikuja kuniomba mtoto wake aje kuishi na kusomea kwangu. Ukweli sikuona sababu za kumkatalia. Nilimkubaliana na kumpokea kisha ‘kumfanyia mpango wa kujiunga’ na shule ya Nyanza ambapo aliingia darasa la tano mpaka alipomaliza darasa la saba.
JAMHURI: Alipomaliza darasa la saba matokeo yake yalikuwaje?
MAMA KHAMESSE: Ukweli ni kwamba hakubahatika kufaulu ili kujiunga na kidato cha kwanza hivyo alilazimika kuanza kusoma masomo ya jioni katika shule ya sekondari ya Pamba.
Lakini hakuweza kukaa nyumbani kwangu kwa kipindi kirefu baada ya kuanza kusoma Pamba kutokana na sababu ambazo siwezi kukuelezea, kwani nilimuita mama yake tukazungumza kisha akamchukua na kumuhamishia kwa ndugu mwingine ambaye ni baba yake mdogo na Daudi.
Hata hivyo, wakati shangazi yake akigoma kutaja chanzo cha Makonda kuondoka kwa Mzee Khamesse, habari za uhakika ambazo familia ya Khamesse haikuthibitisha wala kukanusha zinasema Makonda alikuwa anachezea bunduki ya Mzee Khamesse risasi ikafyatuka na kupasua paa.
“Mzee Khamesse alisema huyu mtoto andoke haraka. Alisema kama amechezea bunduki yake kuna hatari anaweza akaua watoto wake kwa risasi kupitia michezo yake isiyokubalika,” kinasema chanzo chetu.
Mtu aliyeko karibu na Makonda amekiri lilitokea tukio hilo, ila akasema: “Hiyo ilikuwa michezo ya watoto. Mbona wengi tumemwaga uji wa mgonjwa? Ni hawa watu wa dawa za kulevya tu wanaochochea hata hayo mambo madogo.”
JAMHURI: Je, alimaliza masomo yake ya sekondari na kuhitimu?
MAMA KHAMESSE: Mh! Hapo kwenye kumaliza sekondari siwezi kukueleza lolote maana ni kautata kidogo kwani sikumbuki kitu kama hicho.
Ila ninachofahamu ni kwamba alianza kufanya kazi ya ukondakta wa daladala kwenye mabasi ya baba yake mdogo ambaye kwa sasa ni marehemu anayefahamika kwa jina la Mabina.
Baada ya muda kupita nilisikia kuwa amejiunga na Chuo cha Uvuvi Nyegezi, jijini Mwanza, na baadaye nikasikia yuko chuo huko Mbegani, Bagamoyo anasoma.
Lakini muda haukupita sana ndipo nikasikia kuwa amekuwa muhubiri hivyo alikuwa akihubiri injili na alikuwa akisafiri sana.
JAMHURI: Katika kipindi chote hicho uliwahi kusikia kuwa amebadili jina na kuitwa Paul?
MAMA KHAMESSE: Hapana nilikuwa sijawahi kusikia akiitwa jina zaidi ya tunalolifahamu wanafamilia la Daud Bashite. Na siku zote namfahamu kwa jina hilo hilo ingawa nilikuja kushangaa kuona kwenye luninga wakati yuko Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) alipotambulishwa kwa jina la Paul Makonda.
Nilishangaa jina nikadhani wamekosea, lakini kila siku zinavyokwenda niliendelea kumuona kwenye luninga akitambulishwa kwa jina la Paul Makonda huku akiwa ni Daud Bashite ninayemfahamu.
JAMHURI: Hili jina la Makonda unadhani amelitoa wapi?
MAMA KHAMESSE: Jina hili la Makonda ni jina ambalo lipo katika ukoo, upande wa babu na bibi zake, hivyo sio jina jipya katika ukoo. Lakini suala la yeye kuanza kuitwa hivyo labda yeye binafsi au wazazi wake wanaweza kulisema hilo.
Ndugu
Mmoja wa ndugu zake wa karibu (jina linahifadhiwa) amesema kwamba Daudi alishindwa kuendelea kuishi nyumbani kwa shangazi yake (Mama Khamesse) kutokana na tabia ya kupenda kuwa karibu na marafiki wenye uwezo mkubwa jambo lililokuwa linamnyima uhuru kwani alikuwa na tabia ya kuhamia huko na kutorudi nyumbani.
“Daudi alikuwa anaweza kutoka nyumbani kwao Nyamanoro akahamia nyumbani kwa rafiki zake baada ya siku kadhaa akarudi nyumbani tena kwa shangazi yake. Tabia hii ilimkera Mama Khamesse ikamlazimu kuwasiliana na wazazi wake ambao walimuondoa hapo na kumpeleka kwa ndugu mwingine,” amesema.
Amesema Mzee Albert Bashite alibahatika kuzaa watoto wawili tu ambao ni Daudi na mdogo wake wa kike ambaye hata hivyo alifariki akiwa mdogo, hivyo Daudi ni mtoto wa pekee wa Mzee Daudi Bashite na Susan Daud Malagila. Jina la Daudi alilithi kutoka kwa babu yake mzaa mama.
Shule ya Msingi Nyanza
JAMHURI lilifika Shule ya Msingi Nyanza na kukutana na Mwalimu Mkuu ambaye alikataa kujitambulisha kwa jina kwa madai kuwa hawezi kuzungumza chchote mpaka atakapopata kibali kutoka kwa wakubwa wake.
JAMHURI: Mimi ni Mwandishi wa Habari kutoka Gazeti la JAMHURI. Nimefika kwako kupata ufafanuzi kuhusiana na taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusoma katika shule yako ya Nyanza.
Mwalimu Mkuu: Siwezi kuzungumzia suala lolote linalohusu jambo hilo. Unatakiwa kuwa na kibali kutoka Ofisi ya Mkoa, nenda kwa RAS (Katibu Tawala wa Mkoa), RAS akishatoa kibali kitatakiwa kuthibitishwa na DAS (Katibu Tawala wa Wilaya), kisha utakipeleka kwa Afisa Elimu Wilaya, ambaye naye atakithibitisha na kukuelekeza kwa Mkurugenzi wa Wilaya ambaye atakupatia kibali cha kuja nacho hapa shuleni niweze kukujibu maswali yako.
Hapa unataka data (takwimu), na taratibu za kupata data unazifahamu. Hivyo siwezi kabisa kukusaidia chochote. Karibu tena.
JAMHURI limefanya mahojiano na mmoja wa walimu shuleni hapo (jina linahifadhiwa) ambaye amethibitisha Daudi Bashite kusoma katika shule ya Nyanza.
“Nashangaa hili jambo kukuzwa kiasi hiki! Hili suala lipo wazi kabisa, Daudi au Makonda kama anavyoitwa alisoma hapa na huyo Mwalimu Mkuu wa Nyanza, Jovenary anaweza kuwa anafahamiana naye kama hakumtangulia darasa kwani naye alisoma hapa hapa. Picha unayoiona kwenye mitandao Daudi aliipigia palee kwenye ngazi,” amesema Mwalimu huyo.
Source: Jamhuri.