Kurudisha nguvu za kiume
Makala hii ni maalumu kwa ajili ya
wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope
Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.
Katika kilele cha juu kabisa cha
furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo
lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe
limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.
Nguvu za kiume ni neno linalotumika
mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa
tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa
kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni
hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa
kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.
Pamoja na hayo yote, elimu mhimu
ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa
kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula
tunavyokula kila siku.
Sababu za Wanaume kuishiwa nguvu za
kiume:
Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la
kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili
ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.
Tatizo la kupungukiwa nguvu za
kiume huongezeka sababu ya umri. Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wa umri
kuanzia miaka 61 na kuendelea ndiyo wanapatwa na tatizo hili zaidi kuliko
wanaume wenye umri wa miaka 41 Kushuka chini.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya
utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni
kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza
nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza
janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo. Mazoezi
ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.
Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza
pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’.
Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na
magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.
Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume
wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama
vizuri. Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni
miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za
kiume. Walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji
mchache wa mbegu za kiume (manii).
Wengine wenye hatari ya kupatwa na
tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye shinikizo la
juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo
vya uzazi wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela
bila kushauriwa na wataalamu na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo
wa damu kwenda katika mishipa ya uume.
Pamoja na hayo, tatizo la upungufu
wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.
Kabla dakatari hajaanza kukutibu
tatizo kupungukiwa nguvu za kiume, atataka kujuwa:
Umri wako
Utendaji wa tendo la ndoa kabla na
baada ya kuugua
Afya yako kwa ujumla
Matatizo katika ndoa ikiwa kuna
ugomvi wowote n.k
Nini sababu ya wewe kutaka kupona
Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya
kwanza katika kupata uponyaji sahihi. Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kuwa na
imani na daktari wako. Kwa kufanya hivi utakuwa umepiga hatua nzuri kelekea
kwenye ufumbuzi wa tatizo lako.
Nini Sababu ya uume kushindwa
kusimama?
Kushindwa kwa uume kusimama pia
hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa
kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya
tendo la tendo na mwenza wake. Pamoja na ukweli kuwa mara zote Mwanaume lazima
atafika kileleni, hali huweza kuwa tofauti kwa upande wa pili kwani mwanamke
anahitaji mwanaume akawie zaidi ili na yeye (mwanamke) aweze kutosheka.
Mkeo hupendelea ukawie na
ikiwezekana ukawie zaidi. Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa
hapati raha kamili.
Ingawa, kama una tatizo la kuwahi
kufika kileleni hauko peke yako. Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote
wanakabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za
kiume. Hata hivyo kutambuwa tu kwamba wanaume wengine pia wana tatizo kama lako
siyo sababu ya wewe kukaa tu bila kutafuta suluhisho la tatizo lako.
Habari njema ni kuwa zipo njia
zinazoweza kuleta matokeo mazuri na hatimaye kulimaliza tatizo hili bila
madhara mabaya hapo baadaye.
Wakati mwingine uume kushindwa
kusimama inaweza kuwa si tatizo, lakiini jambo hilo linapojitokeza kila mara na
kwa kipindi kirefu inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke.
Sababu nyingine amabzo zinaweza kupelekea uume usisimame vizuri ni pamoja na
matatizo ya mhemko kama;
Wasiwasi
Hasira
Msongo wa mawazo (Stress)
Huzuni
Hofu na mashaka
Kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
Ili uume usimame vizuri ni lazima:
Mfumo wako wa neva uwe na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve
impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
Mishipa ya ateri iliyo na afya ya
ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
Misuli laini yenye afya na tishu za
ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa
Kiwango sahihi cha oksidi nitriki
(nitric oxide) ndani ya uume.
Uume kshindwa kusimama vizuri
kunaweza kusababishwa pia kama kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi
vizuri. Mambo mengine yanayopelekea kupunguwa kwa nguvu za kiume, uume
kushindwa kusimama vizuri na kuwahi kufika kileleni ni:
Uzee
Kisukari
Kujichua/Punyeto
Uzinzi
Kukosa Elimu ya vyakula
Kutokujishughulisha na mazoezi
Shinikizo la juu la damu
Ugonjwa wa moyo
Uvutaji sigara/tumbaku
Utumiaji uliozidi wa kafeina. Na
kama hujuwi kafeina ni kitu gani, bonyeza => hapa.
Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
Madawa ya kulevya
Kupungua kwa homoni ya testerone
Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
Pombe
Nguvu za kiume na mzunguko wa damu:
Kitu gani husababisha uume usimame?
Unaweza kujibu ni msisimko. Ni
kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi. Hata hivyo msisimko ni matokeo. Kipo
kinachosababisha kutokea huo msisimko. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza
kutokea.
Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu
sahihi la swali hili ili atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa
kuishia. Siyo lazima uwe daktari, Elimu ya kutambua mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu
sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama watu wengi mnavyodhani.
Kutokusoma soma lolote kuhusu miili
yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela
na hivyo kujikuta tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu.
Mzunguko wa damu ndicho kitu
kinachofanya uume USIMAME. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu;
‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu,
lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini,
nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU.
Mzunguko wa damu unaofanya kazi
vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana
katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.
Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?
Mzunguko wa damu wenye afya bora
husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili ikijumuisha pia damu
iliyo katika mishipa ya uume. Hivyo, hata kama utagusana na mwanamke hautaweza
kufanya lolote ikiwa damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa.
Mtazame mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je anaweza kufanya lolote? Hata
hivyo huo ni mfano mkubwa sana.
Hii ni kusema kuwa, chochote
ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama
kwa uume. Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza
kusimamisha uume vizuri. Hii ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya
kutosha.
Mara nyingi vena zilizoziba
kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa
wanaume wengi wenye miaka 60 kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume
wenye hali ya kukauka kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.
Baadhi ya wanaume wanapatwa na
tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta
mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa
pia kuepuka vinywaji na vyakula ambavyo husindikwa viwandani.
Katika tendo la ndoa kwa mwanaume,
mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya
usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa
kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa
damu mwilini mwako.
Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu
wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na
tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza
afya yako mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu
hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi
wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda mwenyewe.
Kurudisha nguvu za kiume
Katika kujitibu tatizo hili jambo
la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.
Njia 13 za kujitibu tatizo la
kupungukiwa nguvu za kiume:
1. Acha mawazo
Mawazo na mfadhaiko huondoa
mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu
za kiume na hata uume wenyewe.
Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au
stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika
hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano,
wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama
mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda
akaenda kukutangaza kwa majirani!.
2. Jitibu magonjwa yafuatayo
Kama tatizo limesababishwa na
magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito
kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu
wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.
Kisukari, shinikizo la juu la damu,
vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa
hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa
kwa kipindi cha majuma kadhaa.
3. Acha vilevi
Kama tatizo linatokana na matumizi
ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha
kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo
vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.
Kuna watu wanajidanganya kwamba
ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo
mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo
utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho
kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako
itakapojitokeza.
4. Fanya mazoezi ya viungo
Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya
viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu
sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Kutengeneza mishipa na kupunguza
uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume na
uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara
ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu
kwenda kwenye uume.
Kama uzito wako upo juu sana na ni
mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka
miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya sana
mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama. Una chuchumaa na kusimama mara 25 mpaka 30,
unaweza kupumzika dakika mbili unaendelea tena kuchuchumaa na kusimama hivyo
hivyo unapumzika dakika 2 mpaka mizunguko (rounds) mitano kila siku.
5. Tumia kitunguu swaumu
Chukuwa punje 6 za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande
vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja.
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu
swaumu kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kule kuwa kwake na viasili
kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa
kiutendaji unatokana na sifa zifuatazo:
Vina uwezo wa kusababisha kutanuka
kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani
yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
Husaidia uthibiti wa kiwango cha
sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na hivyo
kupunguza madhara ya kisukari.
Ukivikata vipande vidogo vidogo
hivi (chop), vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo kwa kitaalamu kama
‘Allicin’ ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na ‘Phytoncide’ ambayo huua fangasi
mbalimbali mwilini.
6. Kula tikiti maji
Tunda hili lina faida nyingi pamoja
na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium,
Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B6,C. Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins
na Virutubisho vingine vingi.
Tunda linasaidia kuwa na uwezo
mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na
kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu.
Faida nyingine 12 za tikiti maji
kiafya ukiacha hii ya nguvu za kiume
• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha
afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha
kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo
kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Chanzo cha madini ya potasiamu
• Husaidia kushusha na kuponya
shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu
mwilini
• Huondoa sumu mwilini
Kula tikiti maji kila siku huku
ukitafuna na zile mbegu zake, fanya mara hivi mara kwa mara.
7. Kula ugali wa dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni
mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho
vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera
jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa
pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga
yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia
yako kwa maisha yako yote.
8. Tumia chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile
ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika
kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.
9. Kunywa maji mengi kila siku
Kunywa maji ya kutosha kila siku
bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji
ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.
10. Tafuna mbegu za maboga
Maajabu mengine ya mbegu za maboga
ambayo ulikuwa huyajuwi bado. Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni
namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha
lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya
ngiri nk), zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya kuliko zote
ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye
upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Bado huelewi? Zina madini ya chuma
pia
Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina
uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ofisini
unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Sambamba na
hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha
kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count)
ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukipiga bao linatoka la kutosha
na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga.
NAMNA NZURI YA KUTUMIA MBEGU ZA
MABOGA KAMA DAWA:
Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo
utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 5
hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa
mbali ili kupata radha.
Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja
cha mkono wako cha mbegu za maboga, ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi
kila siku. Unatafuna na ganda lake hasa kama zimekaangwa tayari
Kwa muda gani? Kwa wiki 3 mpaka 4
kwa ugonjwa wowote kati ya haya niliyoeleza. Kumbuka pia unaweza kutumia mbegu
hizi hata kama huumwi chochote!
11. Tumia asali yenye mdalasini
Chukuwa lita moja ya asali safi ya
asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 8 vya mdalasini ya unga
changanya vizuri pamoja. Acha ndani ya bakuli kubwa ili iwe rahisi kuikoroga
vizuri kila unapoitumia. Lamba vijiko vikubwa vitatu kila unapoenda kulala.
Fanya hivi kwa mwezi mmoja.
Hata baada ya mwezi mmoja kuisha
bado nakushauri uendelee kuitumia asali hivi maisha yako yote au hakikisha
haipiti siku bila kunywa au kula chakula chenye asali yenye mdalasini ndani yake.
Unaweza kuitumia kila siku kwenye mkate kama mdabala wa siagi au blueband au
ukaitumia kwenye juisi na kwenye chai kama mbadala wa sukari. Au unaweza kuweka
vijiko vikubwa vitatu ndani ya glasi moja ya maji na unywe yote kutwa mara 2
amabapo husaidia pia kutibu uchovu mwilini.
12. Kunywa chai ya tangawizi
Tangawizi ni chakula ambacho
husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana
sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume.
Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.
Ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa
kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa.
Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza
ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima
nusu saa kabla ya tendo.
Kunywa chai ya tangawizi mbichi
kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na Tangawizi
mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi
inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje.
Sasa badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya
tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. Tangawizi
peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!
13. Tumia unga au juisi ya msamitu
Unga au juisi ya msamitu (mtishamba
wa porini) ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia
unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume hasa lililosababishwa
na kujichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani unaimarisha sana mishipa ya
uume. Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari.
Msamitu unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina
mama pia.
Msamitu pia unatibu magonjwa
yafuatayo bila shida yoyote; Pumu, Chango la uzazi, Kupooza mwili, Unaondoa
kabisa gesi tumboni na Kuongeza nuru ya macho kuona.
Msamitu unao uwezo pia wa kuongeza
ukubwa wa uume wako. Labda utauliza kwa namna gani?, kwa sababu moja ya kazi
zake mwilini ni kuponya mwili uliokuwa umepooza, mwili unapokuwa umepooza ina
maana hata damu yako pia inakuwa haitiririki vizuri kama inavyotakiwa na
tuliona hapo juu kwenye somo hili umhimu wa mzunguko wa damu ulio bora katika
nguzu za kiume.
Kwa kuwa mwili ulikuwa umepooza,
Msamitu unapokuja kukutibu unakufanya kuwa mtu uliyechangamka na damu yako
itaanza kuwa inatiririka kwa mtiririko mzuri zaidi na kama matokeo yake utaanza
kuona hata ukubwa wa mheshimiwa unaanza kuongezeka kidogo kidogo. Na hii ni
hasa kwa wale ambao walizaliwa na uume wa kawaida lakini sababu ya punyeto,
lishe duni au stress walijikuta maumbile yao yanaanza kusinyaa au kupungua
badala ya kuongezeka.