Habari njema kwa wasomaji wetu!!
Sasa Unaweza kuwa wa kwanza kupata habari za uhakika kutoka pande zote za dunia kwa ku download APP yetu ambayo iko tayari Google Playstore
Au unaweza kuipata kwa kubonyeza hapa 👇👇👇👇👇
Wednesday, 19 April 2017
HABARI NJEMA!!! DOWNLOAD KINGAZI BLOG APPLICATION ON PLAYSTORE BONYEZA HAPA
Kenya Nao Waiga usafiri wa Mwendokasi kama Tanzania..!!
Mara nyingi watanzania wamekuwa wanataja mafanikio ya nchi nyingine wakilinganisha na mazingira hafifu ya hapa nchini katika masuala ya Maendeleo.
Lakini orodha ya mazuri yanayoigwa na nchi nyingine kutoka Tanzania itakuwa imeongezeka kwa jambo moja lingine ambalo ni Mabasi ya mwendo kasi.
Aidha, Mamlaka ya usafiri jiji la Nairobi imefufua mpango kupunguza foleni za magari kwa kuanzisha usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi kama yanayotumika kwa sasa nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Katibu wa Masuala ya usafirishaji Mwangi Mariga alisema ujenzi wa mradi huo wa Mabasi ya Mwendokasi utahusisha miji mitano.
Naye Katibu wa Baraza la Mawaziri James Macharia alishauri mwaka jana kwamba mapendekezo maalum ya mfumo wa Mabasi ya usafiri yalikuwa na changamoto kutokana na miundombinu iliyopo ya barabara kwa mabasi kuwa na msongamano.
Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi umebuniwa kufuatia idadi ya watu wa Nairobi kuongezeka hadi milioni 3.3 kutoka 350,000 mwaka 1963 na idadi ya magari inakadiriwa kufikia 300,000 bila ongezeko sawa katika mtandao wa barabara.
Sakata la vyeti feki lachukua Sura Mpya!!! Habari katika magazeti yq leo Jumatano April 19,2017
Askari 17, Viongozi 18 Wameuawa Mkuranga, Kibiti
Idadi na watu, raia na askari polisi waliouawa kwa kupigwa risasi katika Wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga mkoani hapa imekuwa kubwa hivyo kutia wasiwasi kwamba, maisha katika eneo hilo ni ya roho mkononi, Uwazi limechimba na kuchimbua.
Uwazi limebaini hayo kufuatia Aprili 13, mwaka huu, askari polisi wanane wilayani Kibiti kuuawa kwa kupigwa risasi kisha kuporwa bunduki 7 na watu ambao jeshi hilo linasema ni majambazi.
Askari hao ni A/INCP Peter Kigugu, F.3451CPL Francis, F.6990PC Haruna,G.3447 PC Jackson, H.1872PC Zacharia, H.5503 PC Siwale, H.7629PC Maswi na H.7680PC Ayoub ambao wote wamezikwa Jumapili iliyopita.
KWA NINI MKURANGA, KIBITI NA RUFIJI?
Matukio ya askari kupigwa risasi wilayani humo si mageni lakini mbali na askari, pia viongozi wa vijiji wapatao 18 katika wilaya hizo nao wameuawa kwa kupigwa risasi. Inauma sana!
WANANCHI WA KIBITI
Wakizungumza na Uwazi baada ya mauaji ya askari hao, baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mkengeni Kibiti, walisema kuwa, Mkoa wa Pwani umekuwa si salama kwa maisha ya watu na mali zao kwani mpaka sasa, hesabu za haraka zinaonesha kuwa, unaongoza kwa mauaji ya risasi huku viongozi na askari wakiwa wanashika namba kubwa.
“Mimi kumbukumbu inaniambia, katika Mkoa wa Pwani na wilaya zake hizo, tayari askari kumi na saba (17) wameshauawa kwa kupigwa risasi na viongozi wa vijiji kama kumi na nane (18) nao pia wameuawa.
“Hii idadi ni kubwa sana, siamini kama kuna mkoa umefikia, labda Dar es Salaam kwa sababu ya ukubwa wake wa makazi, lakini nje ya hapo sidhani,” alisema mkazi mmoja wa aliyejitambulisha kwa jina la Masaidi Khalidi. Anaongeza:
“Jeshi la Polisi likitaka kumalizana na hii hali ni kuingiza ushirikiano na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waingie msituni na kufanya kazi kama wako vitani, naamini wahalifu wote watakamatwa na itajulikana nguvu yao ilipo.”
KUHUSU POLISI NI KWELI?
Kufuatia madai hayo, Uwazi lilichimba kwenye kumbukumbu za nyuma na kukuta kweli idadi ya askari waliopoteza maisha Pwani inatisha, lakini pia idadi ya viongozi wa vijiji ambao pia wameuawa kwa kupigwa risasi pia inatisha.
WALIANZA POLISI HAWA
Juni 11, 2014, watu wenye silaha za jadi walivamia Kituo cha Polisi cha Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga mkoani hapa na kumuua kwa kumshambulia kwa mapanga askari Joseph Ngonyani kisha kupora bunduki tatu aina ya SMG na risasi 50.
Mwaka 2015 nao ukaingia na balaa, matukio ya mauaji yaliendelea kuukabili mkoa huu kufuatia askari wanne wa Kituo cha Polisi Ikwiriri kuvamiwa na kuuawa na watu ambao jeshi hilo lilisema ni majambazi. Askari hao ni Koplo Yahya Malima, Koplo Tito Mapunda, Koplo Gaston Lupanga na Koplo Khatib Ame Pandu.
KIZUIZI CHA POLISI VIKINDU
Machi 30, 2015, saa 1:30 usiku wa kuelekea Sikukuu ya Pasaka, askari wawili waliuawa kwenye kizuizi cha barabarani katika Kijiji cha Kipara, maeneo ya Vikindu, Pwani. Waliouawa ni Sajenti Michael Aaron Tuheri na Koplo Francis Mkinga. Mauaji hayo yaliliacha jeshi la polisi nchini katika hali ya huzuni huku yakifananishwa na yale yaliyotokea katika vituo mbalimbali vya polisi nchini.
IKWIRIRI TENA
Januari 21, 2016, watu wasiojulikana walivamia Kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani humu na kuwaua askari wawili, Koplo Edgar na WP Judith na kupora silaha zilizokuwepo kituoni hapo.
KIJIJINI VIKINDU
Agosti 26, 2016, askari wa ngazi ya juu katika kikosi cha kupambana na majambazi nchini, SSP Thomas Njiku aliuawa kwenye Kijiji cha Vikindu, Mkuranga akiwa katika oparesheni ya kuwasaka watu waliodaiwa kufanya uhalifu maeneo na Mbande, Temeke jijini Dar es Salaam.
JARIBU MPAKANI
Februari 22, 2017, taarifa kutoka Kibiti zilisema, mpelelezi wa wilaya hiyo (OC-CID), SP Peter Kubezya aliuawa kwa kupigwa risasi ya tumboni na watu hao wanaosadikiwa kuwa ni wahalifu. Tukio hilo lilijiri usiku wa saa 1, ambapo watu sita wenye bunduki zinazosadikiwa kuwa ni aina ya Sub Machine Gun (SMG) walivamia Kituo cha Kutoza Ushuru wa Mazao ya Kilimo na Misitu Kijiji cha Jaribu Mpakani na kumuua kwa kumpiga risasi afande huyo na raia wengine wawili.
KUHUSU VIONGOZI WA VIJIJI
Kwa upande wa viongozi wa vijiji si rahisi kuamini lakini ndiyo ukweli ulivyo kwamba, idadi yao ilifikia kumi na nane (18) wakiwa wameuawa kwa nyakati tofauti. Usiku wa Machi 28, mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Makondeko, Kijiji cha Ikwiriri Kaskazini, Emmanuel Lukanga aliuawa kwa kupigwa risasi.
MUDA MCHACHE KABLA
Akizungumza na Uwazi, kwenye mazishi ya kiongozi huyo, Katibu Kata wa Ikwiriri Kaskazini, Sauda Mningi alisema saa chache kabla ya Lukanga kufikwa na mauti walikuwa kwenye kikao cha kujadili suala la ulinzi na usalama wa eneo hilo.
STAILI YAO YA KUUA
Staili ya watoa roho hao ni kuua kwa risasi wakitumia bunduki aina ya SMG bila kuchukua pesa wala mali yoyote kutoka kwa marehemu huku wakiwa wamevaa kininja na wakitumia bodaboda hali inayotafsirika kuwa, ni mauaji ya visasi. “Huku jamani sisi wananchi, giza linapoingia wasiwasi tupu. Tunakuwa hatujui nani atauawa. Hawa watu wameanza zamani, tangu mwaka 2015,” alisema kiongozi mmoja huku akiomba hifadhi ya jina lake.
VIONGOZI WALIPOKEA MESEJI
Ilielezwa kuwa, viongozi mbalimbali wakitimia 18 wa vijiji vya wilaya hizo walianza kupokea meseji za vitisho kutoka kwa kundi moja la wahalifu wakidai roho zao ziko mikononi mwao, watawaua mmoja baada ya mwingine.
MAUAJI YA KWANZA
Mapema mwaka 2015, kundi hilo lilidaiwa kumuua kwa kumchinja karani wa Mahakama ya Mwanzo Mkuranga aliyetajwa kwa jina moja la Pazi.
MACHI MOSI, 2016 Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambunda, Said Mbwana aliuawa kwa kupigwa risasi na watu hao waliovamia nyumbani kwake. JULAI 17, 2016 Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimanzichana, Ramadhani Mkagile naye aliuawa kwa kupigwa risasi na watu hao waliofika nyumbani kwake kwa njia ya bodaboda wakiwa wamevaa kininja.
AGOSTI 12, 2016 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mkuruwili wilayani Mkuranga, Salum Kiswamba ambaye pia alikuwa imamu wa msikiti, naye aliuawa nje ya nyumba yake kwa kupigwa risasi.
OKTOBA 6, 2016 Katika Kijiji cha Kimanzichana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Bakari Simkole akiwa ofisini, alipigwa risasi ya kifuani na kufariki dunia papohapo. OKTOBA 24, 2016 Kundi hilohilo lilimuua Mtendaji wa Kijiji cha Nyambunda, Ally Omar kwa kumpiga risasi akiwa nje ya nyumba yake.
DESEMBA 6, 2016 Mohammed Ally Thabiti ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyambunda, Kijiji cha Nyang’hundu naye aliuawa kwa kupigwa risasi na watu waliovaa kininja.
WAWILI WALIUAWA
Nyuma ya mauaji ya viongozi hao wa kijiji hicho, waliuawa viongozi wengine wawili ambao Uwazi halikupata majina yao wala tarehe. Kijiji kikabaki hakina viongozi. JANUARI, 2017 Mauaji ya viongozi hao hayakuishia hapo, Januari mwaka huu, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambunda Wilaya ya Kibiti mkoani hapa, Said Mkandambuli naye aliuawa kwa kupigwa risasi na kundi hilo, nyumba yake imeota majani baada ya familia yake kukimbia.
JANUARI 19, 2017
Katibu Mtendaji wa Kijiji cha Nkwandala wilayani Kibiti (zamani kilikuwa katika Wilaya ya Mkuranga), Oswald Mrope naye aliuawa na wauaji hao ambao walimkuta akiwa amejipumzisha nje ya nyumba yake.
FEBRUARI 9, 2017 Saa 6 usiku, kundi hilo linaloaminika kuwa ndilo linalotoa roho za viongozi, lilimuua Kamanda wa Mgambo Kata ya Bupu, Mussa Koti na kuichoma moto nyumba yake.
SIKU HIYOHIYO
Wauaji hao siku hiyohiyo walimuua kwa risasi, Kamanda Msaidizi wa Mgambo, Mohammed Cheleu na kuzichoma moto nyumba zake mbili, ya mke mdogo na mke mkubwa na kuacha ujumbe kupitia vipeperushi kuwa, roho zaidi zitaendelea kutolewa.
FEBRUARI 21, 2017 Watu watatu walipoteza maisha (mmoja kati yao akiwa OC CID wa Kibiti) baada ya kuuawa na kundi la watu wanaodhaniwa ni walewale wakiwa na silaha aina ya SMG/SAR. Mbali na OC-CID, wengine ni Peter Kitundu aliyekuwa Mkaguzi wa Maliasili Kituo cha Jaribu Mpakani na mgambo aliyekuwa akifanya kazi za ulinzi kwenye kizuizi hicho, Athumani Ngambo.
MACHI 12, 2017
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kazamoyo, Hemed Njiwa naye aliuawa kwa kupigwa risasi na watu hao akiwa nyumbani kwake.
GAZETI LA UWAZI
Gazeti la Uwazi, mara kadhaa tangu mwaka 2015 limekuwa likiandika habari za watu waliopo kwenye baadhi ya misitu kwenye wilaya hizo kwamba, ndiyo wanaopanga mauaji ya kutisha ya polisi kwa lengo la kuchukua silaha kwa matumizi wanayoyajua wao, ikiwemo kuwaua viongozi.
KINACHOTOKEA
Hata hivyo, licha ya mambo kuwa wazi, bado Uwazi limewahi kuitwa na uongozi serikalini na kuhojiwa juu ya habari hizo, hasahasa habari iliyowahi kuandikwa Julai 17, jana kwenye gazeti ndugu na hili, Amani yenye kichwa cha habari;
WANAOJIITA AL QAEDA WAUA IMAMU WA MSIKITI.
Katika habari hiyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mkuruwili Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Salum Kiswamba ambaye pia alikuwa imamu wa msikiti wa eneo hilo, aliuawa nje ya nyumba yake kwa kupigwa risasi na watu waliovalia kininja waliokuwa kwenye bodaboda.
Katika kusema ukweli huu, baadhi ya viongozi serikalini hutaka kuamini kuwa, magazeti ya Global Publishers yanazua hofu huku ukweli ukiwa unaonekana.
UWAZI NA BARUA KWA MAGUFULI
Pia, Uwazi liliwahi kumwandikia barua Rais Dk. John Pombe Magufuli ikimweleza namna wananchi wa mkoa huo, hasa Mkuranga, Kibiti na Rufiji wanavyoishi kwa wasiwasi wakimwomba msaada wake kwa imani kwamba, anaweza kutuma jeshi maalum na kuwaangamiza wahalifu hao.
KAMANDA KOVA ALIWAHI KUSEMA HAYA
Kabla ya kustaafu kwake, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova aliwahi kusema kuwa kuna mtu anaitwa Hery, alihusika katika kufadhili matukio ya mauaji huko Amboni (Tanga), Mkuranga (Pwani) na Stakishari (Dar) na mengineyo lakini aliongeza jeshi la polisi kwa kutumia kikosi cha intelijensia kiliweza kubaini nyendo zake na kuinasa picha yake.
UWAZI LILISEMA HOFU YATANDA MKURANGA
Gazeti hilihili liliwahi kuandika mwaka 2015 kuwa, hofu kubwa imetanda wilayani Mkuranga hasa katika Kijiji cha Mamndi Mkongo kufuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na wale wa Mkoa wa Pwani kunasa silaha za kivita zikiwa zimefukiwa kwenye shimo msituni. Tukio hilo la unasaji wa silaha lilifanikiwa Agosti 29, 2015 katika msitu mmoja uliopo katika kijiji hicho kilichopo umbali wa kilomita 23 kutoka mjini Mkuranga.
SILAHA ZILIZOKUTWA
Uwazi lilizungumza na kamati ya ulinzi na usalama kijijini hapo na kusema silaha zilizokutwa ni bunduki za kivita aina ya AK-47 (moja), SRA (mbili), RPG (mbili) Greana (moja) na risasi 388, tambi za milipuko mikali, kitabu cha muongozo wa kijeshi, kemikali za kutengenezea mabomu ya kutupa kwa mkono na kitabu chenye maelekezo ya namna ya kujibadili mwanaume kuwa mwanamke au mwanamke kuwa mwanaume.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Uwazi, wamemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu kufuatilia kwa kina matukio hayo kwani yanawatia hofu wananchi.
KUTOKA KWA MHARIRI
Ni vyema jeshi la polisi likaongeza nguvu ya ulinzi ili kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Tunalaani mauaji haya kwa nguvu kubwa tukiamini kwamba, waliouawa hawakuwa na hatia!
Credit - Uwazi/Globalpublishers
Huu ndo Uwezo wa Korea Kaskazini Kivita..Ana Makombora Zaidi ya 1000 Yanayoweza Kurushwa Toka Bara Moja Hadi Jingine
Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani.
Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90.
Mifumo ilio na uwezo mkubwa inadaiwa kufanyiwa utafiti.
Hivi karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambayo yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi.
Taifa la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa marefu zaidi ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong-13.
Makombora ya Hwasong yakiwa katika maonyesho
Ishara za kwanza kuhusu utengenezaji huo ulifanyika Septemba 2016 ambapo taifa hilo lilifanyia majaribio mashine mpya ya roketi ambayo baadhi ya watu wanasema inaweza kurusha kombora kutoka bara moja hadi jingine.
Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon inaamini kwamba Korea Kaskazini inamiliki makombora 6 aina ya KN-08, ambalo lina uwezo wa kufika hadi Marekani.
Korea kaskazini inaaminika kutengeza toleo jipya la kombora hilo linalojulikana kama KN-14. Haahivyo makombora hayo hayajafanyiwa majaribio.
Lakini mnamo mwezi Januari 2017, kulikuwa na ishara ya jaribio, muda mfupi baada ya kiongozi Kim Jong un kudai kwamba taifa hilo lilikuwa katika awamu ya mwisho ya kutengeza kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.
Mpango wa kisasa wa kutengeza makombora yaa Korea Kasakzini ulianza kwa kutengeza makombora ya scud ambapo yalipitia Misri mwaka 1976.
Kufikia 1984, taifa hilo lilikuwa likitengeza makombora yake kwa jina Hwasong.
Inaaminika kuwa na makombora tofauti tofauti ya masafa mafupi ambayo yanaweza kulenga taifa jirani la Korea Kusini.
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya Korea umeharibika na yamekuwa yakijiandaa kukabiliana kivita.
Kombora la Hwasong 5 na Hwasong 6 ambayo pia hujulikana kama Scud B na Scud C yana uwezo wa kwenda kilomita 300 na 500 mtawalia kulingana na kituo cha Marekani kinachofanya utafiti wa kuzuia kuenea kwa nuklia.
Makombora hayo yanaweza kubeba makombora ya kemikali na nyuklia.
Silaha hizo zimejaribiwa na kupelekwa katika maeneo yanayohitajika na kombora la Hwasong-6 limeuzwa nchini Iran.
Ramani ya Korea Kaskazini na majirani zake wa Korea Kusini
Korea Kaskazini ilianza mpango huo mapema miaka ya 80 kutengeza kombora la masafa ya kadri kwa jina Nodong likiwa na uwezo wa kusafiri urefu wa kilomita 1000.
Kombora hilo limetengezwa kwa muundo wa Scud ,lakini ni asilimia 50 kwa ukubwa na lina mashine yenye uwezo mkubwa.
Uchanganuzi wa mwezi Aprili 2016 wa taassii ya kimataifa kuhusu utafiti wa mikakati ,unasema kuwa makombora hayo yalithibtishwa yanaweza kupiga maeneo yote ya Korea Kusini na Japan.
Imeongezea kuwa maonyesho ya Oktoba 2010 yalithibitisha kuwa kombora hilo linaweza kufika urefu wa kilomita 1,600 ikimaanisha kwamba linaweza kupiga kambi kadhaa za Marekani zilizopo katika eneo la Okinawa.
Makombora hayo ya Nodong yanadaiwa kujaribiwa 2006, 2009, 2014 na 2016.
Kombora la Musudan
Korea Kaskazni imekuwa ikitengeza makombora ya Musudan kwa miaka kadhaa, na hivi karibuni ilifanya majaribio 2016.
Makadirio yanatofautiana kuhusu viwango vyake, huku ujasusi wa Israel ukitaja uwezo wake kuwa kilomita 2,500 nacho kitengo cha ulinzi wa makombora nchini Marekani kikikadiria kuwa na uwezo wa kufika kilomita 3,200.
Duru nyingine zinasema kuwa kombora hilo lina uwezo wa kwenda kilomita 4,000.
Kombora la masafa mafupi la Musudan ambalo pia linajulikana kama Nodong B ama Taepodong-x linaweza kulishambulia taifa lote la Korea Kusini na Japan.
Kombora hilo linaweza kushambulia kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Guam.
Kombora la masafa marefu la Taepodong linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine
Korea Kaskazini inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la masafa ya kadri, kwa jina Pukguksong, mnamo mwezi Agosti 2016 likirushwa kutoka kwa manuwari.
Kombora la pili lilirushwa kutoka ardhini mnamo mwezi Februari 2017.
Pyongyang ilisema kuwa ilitumia mafuta ,na kufanya kuwa rahisi kuliwasilisha na kurusha. Hatahivyo maelezo kuhusu uwezo wake hayajulikani.
Credit: BBC
Picha: Mwigizaji Shamsa Ford Apasuka Uso Kisa Ugomvi
Msanii wa filamu Shamsa Ford amepokea kichapo Jumanne hii katika harakati za kuamlia ugomvi wa watu ambao walikuwa wanapigana.
Malkia huyo wa filamu amekutwa na mkasa huo ikiwa ni mwezi mmoja toka aibiwe akaunti yake na Instagram yenye follows 2.
Muigizaji huyo amedai alipigwa ngumi ya uso katika harakati za kutafuta usalama wa watu hao ambao walikuwa wakipigana.
“Jana kwa moyo mmoja nimeenda kuamlia ugomvi watu wasipigane mwisho wa siku nikaambulia Mimi ngumi..HUYU mtu alishiba sana aiseee ngumi ilikuwa nzito sana..😃😃 niombeeni ndugu zangu panauma,” aliandika Shamsa Instagram.
Kwa sasa muigizaji anaendelea vizuri na matibabu.
Hatimaye Yule Jamaa Aliyerekodi Tukio Akimuua Mzee Amejiua Mwenyewe
Yule Jamaa ambae alirekodi tukio live akimuua mzee wa miaka 79 kwa bastola hatimae amejiua mwenyewe .
Tukio hilo la kujiua limetoa muda tu baada ya polisi kumpata na kuanza kulikimbiza gari lake ila kabla hawajamkamata alijipiga risasi na kukatisha uhai wake hivyo.... Jamaa kabla ya kifo chake inasemekana ameua watu kumi na tano bila sababu kisa tu anamaumivu ya kuachwa na mpenzi wake..