Wednesday, 21 December 2016
Habari kuu Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Disemba 21
2G, 3G, 4G na 5G maana yake ni nini?
Katika sekta ya mawasiliano, ni kawaida kuwasikia wataalamu na wakati mwingine watu wa kawaida wakizungumzia kuhusu teknolojia ya 2G, 3G, 4G na 5G. Maana yake ni nini?
G kwenye tarakimu hizi inawakilisha 'Generation', yaani kizazi fulani cha teknolojia ya mawasiliano kwa kuangazia zaidi uwezo wa data kwenye simu.
Hakuna kipimo chochote kinachotumiwa kimataifa kuhusu kasi ya data ya simu.
Lakini wengi wanakubaliana kuhusu baadhi ya sifa za teknolojia hizi.
Teknolojia ya 1G, au kizazi cha kwanza cha data ya simu, ilianza kutumiwa 1991.
Teknolojia ya 2G ilianza pia kutumika katika kipindi hicho, ikiwa kama ndugu wa 1G.
Kwa 1G, ungeweza tu kupiga simu
Teknolojia hii sana ilikuwa analogu na simu za wakati huo zilikuwa kama hizi hapa chini...
Kisha 2G ikaja na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi au arafa
Teknolojia ya 2G ambayo pia huitwa teknolojia ya SMS iliwezesha watu kutuma ujumbe mfupi.
Ungeweza pia kutuma ujumbe wenye picha, ambao uliitwa MMS (multimedia messaging service).
Na pia simu za waka.
Kupiga simu kwa video kuliwezekana 2001
3G na kasi yake ya data ya 2mbit/s (megabaiti 0.25 kila sekunde) ilianza kutumika wakati ambao simu za kwanza aina ya smartphone zilianza kuuzwa madukani.
Huduma yake ya mtandao haikuwa ya kasi sana lakini iliwezesha huduma ya mtandao kupatikana bila kutumia nyaya. Angalau ilikuwa hatua fulani.
Na watu waliweza kupiga simu za video.
Ili kufahamu kasi yake au mwendo wake wa upole ulivyokuwa, iwapo ungetaka kupakua filamu ya ucheshi ya David Brent: Life on the Road kutoka kwenye iTunes, ingekuchukua saa tano kupakua faili hiyo ya 4.26GB.
2010 teknolojia ya 4G ikaanza kutumika
Teknolojia hii ya kasi iliwezesha kuanza kupatikana kwa michezo mingi kwenye simu na ya kiwango cha juu.
Filamu ambayo ingekuchukua saa tano kuipakua kwa teknolojia ya 3G sasa inaweza ikakuchukua dakika 8 pekee kwa teknolojia ya 4G.
Utafiti: Betri zinazotumiwa katika simu zina sumu
Lakini 4G haipatikani maeneo yote, hata katika mataifa yaliyoendelea.
Afrika Mashariki, utaipata katika baadhi ya maeneo ya miji mikubwa.
5G ndiyo mwendo kasi?
Hii ndiyo ya kasi zaidi kwa sasa.
Tume ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee.
Simu za wakati huo nazo zitakuwa na muonekano gani? Kama hii hapa chini labda?
Ahukumiwa Miaka 25 Jela Au Faini Bilioni 3.7 Kwa Kujihusisha na Biashara ya Meno ya Tembo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, imemtia hatiani na kumuhukumu kwenda jela miaka 25 au kulipa faini ya Sh bilioni 3.7 mfanyabiashara Charles Kijangwa kwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo.
Kijangwa alihukumiwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cresencia Kisongo, baada ya kuruka dhamana kwa miaka sita. Alishindwa kulipa faini.
Mshtakiwa huyo alikabidhiwa mahakamani hapo baada ya kukamatwa na askari wa kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Mashariki na Pwani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Lushoto.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Saraji Iboru, alidai mahakamani kuwa mshtakiwa Kijangwa alikuwa akitafutwa na Serikali kwa muda mrefu tangu mwaka 2010 baada ya kuruka dhamana katika shauri la uhujumu uchumi namba 6/2007.
Mshtakiwa alishtakiwa na wenzake Michael Msuya na Nyaisa Makori ambao walitiwa hatiani na mahakama, wakahukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kosa la kumiliki kilo 5,000 za meno ya tembo kwa shtaka la kwanza.
Katika shtaka la pili la kula njama, washtakiwa wote walihukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya Sh 10,950,000 baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha kilo 5,000 za meno ya tembo kwenda nchini Taiwan mwaka 2006.
Iboru aliiambia mahakama kuwa washtakiwa watatu, Kijangwa na wenzake walihukumiwa kwenda jela miaka mitano au faini ya Sh 50,000 katika shtaka la kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali kinyume cha sheria.
Alidai mshtakiwa hakufika mwenyewe mahakamani hapo bali aliletwa baada ya kukamatwa Desemba 11, mwaka huu wilayani Lushoto.
Aliiomba mahakama kumtia hatiani mshtakiwa na kuhakiksha anatumikia adhabu iliyotolewa dhidi yake akiwa hayupo.
Hakimu Kisongo baada ya kusikiliza maombi hayo, alimtia hatiani mshtakiwa na kumuhukumu kwenda jela miaka 25 au kulipa faini ya Sh bilioni 3.7.
Mshtakiwa Kijangwa alitenda kosa hilo Novemba 2005 na Aprili 2006 kwa kusafirisha makontena mawili ya meno ya tembo yenye ujazo wa tani 5,000 yaliyokamatwa katika bandari ndogo ya Konshugi nchini Taiwan.
Makontena hayo ambayo yalitokea katika Bandari ya Tanga yakiwa na shehena ya kamba za katani na meno ya tembo ndani yake, yalikuwa yanapelekwa Manila nchini Philipine.