KINGAZI BLOG: 05/11/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday, 11 May 2017

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Udahili Wa Wanafunzi Wa Astashahada Na Stashada Katika Programu Mbalimbali Kwa Mwaka Wa Masomo 2017/2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na  vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.

Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali  utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

Aidha vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.

Baraza linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017. Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Septemba, 2017.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 10/05/2017

HIVI Ndivyo Magufuli Anavyong'aa Ulaya..Wazungu Wamwagia Misifa Kedekede.


Nimekaa Mahali Fulani Hapa Mtaa wa Poznańska Street Katika Mji wa Warsaw Poland, Yani Wazungu Fulani Nikawaskia Wanazungumzia Tanzania Kwamba Hivi Sasa Ina Rais Mzuri Ambaye Anasimamia Vizuri Uwajibikaji Katika Masuala ya Fedha za Umma na Kuanzisha Elimu Bure. 

Nikapata Hamu ya Kuwasogelea na Kuwauliza Iweje Wanaizungumzia Tanzania Hivyo, Wanaijua? Nikajibiwa Kwamba Wao (wako 9 wamekaa meza moja) wana kikundi chao walifika TZ mwezi April kwa ajili ya utalii na kwamba walipata fursa ya kuitembelea TZ na pia kutengeneza urafiki na baadhi ya watu na kwamba walifurahi kuona TZ inapiga hatua. 

Kumbuka hawa hawakutembelea TZ nzima ila wanasema walienda Zenji, Kilimanjaro, Arusha na Serengeti. Kiukweli wanaisifu sana Tanzania pamoja na Rais JPM. Nimefurahi kuona Nchi yangu inazungumzwa vizuri na baadhi ya watu hapa Poland.

Nani anakwenda fainali ya Europa League leo?


Mechi ya kwanza ambapo Manchester United walisafiri kwenda nchini Hispania Marcus Rashford alifanikiwa kuwapa Manchester United bao la ugenini dhidi ya Celta Vigo.

Leo Celta Vigo wako Old Traford huku mashabiki zaidi ya 30,000 wakiwa wamesafiri na timu kutoka Hispania hadi Uingereza jambo linalompa faraja kocha wao Eduardo Berizzo.

“Ni faraja sana kwetu kwani inaonesha mashabiki hawa wako bega kwa bega na sisi, baada ya kufungwa mchezo wa kwanza hawajatuacha wamekuja na sisi hapa leo” alisema Berizzo.

Lakini Manchester United ambao wamerudi katika nafasi ya 6 kwenye ligi baada ya ushindi wa Arsenal hapo jana, watahitaji sana ushindi ili kucheza fainali ambayo inaweza kuwasaidia kushiriki Champions League msimu ujao.

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema ni muhimu sana kwao kama Manchester kushinda kombe hilo kwani ndio kombe pekee ambalo hawajawahi kulishinda.

“Hakuna aliyewahi kubeba kombe hilo hapa, nadhani itakuwa muhimu sana kwa wachezaji na timu kwa ujumla, hatupaswi kuwaza kuhusu mchezo uliopita bali tunapaswa kuwaza nini kinafuata” alisema Mourinho.

Katika mchezo mwingine Lyon ambao mchezo wa kwanza walikubali kipigo cha bao 4 kwa 1 toka kwa Ajax, leo watakuwa nyumbani kujaribu kubadili matokeo hayo.

ALICHOSEMA Askofu Gwajima Baada ya Kuzungumza na Maalim Seif Kuhusu Mgogoro wa CUF



Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dr Josephat Gwajima amefunguka na kusema Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ni rafiki yake hivyo alitaka kuonana naye ili aweze kujua Professa Ibrahim Lipumba anaharibu vipi chama

Mchungaji Gwajima amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo na Katibu Mkuu huyo wa CUF na kusema aliamua kukutana na rafiki yake huyo ili ajue hilo baada ya hapo yeye atajua anafanyaje.

‘Mimi huyu ni rafiki yangu kwa hiyo nilitaka kujua Professa Lipumba anafanya nini kuvuruga CUF, hivyo nilitaka kujua Lipumba amepatwa na nini mpaka amevuruga chama chako na kiukweli mimi nilikuwa siufahamu vizuri huu mgogoro ila saizi Seif ameniambia kwa hiyo na mimi nataka nitafakari alichoniambia rafiki yangu ni ‘digest’ baada ya hapo nitajua nafanya nini” alisema Gwajima

Kwa upande wake Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa amekaa na askofu Gwajima na kuzungumza naye kwa kina juu ya mgogoro huo na kila mmoja amemueleza mwenzake kile anachokifahamu na kusema ameamuchia askofu ili na yeye atafakari juu ya jambo hilo baada ya hapo anaamini huenda askofu akafanya jambo.

“Nimekaa na askofu na kila mmoja akamweleza mwenzake yale ambayo anayajua, kwa hiyo nimemweleza saizi kiundani kwa hiyo yeye ana ‘digest’ halafu askofu yeye ataamua juu ya kile tulichuzungumza” alisema Maalim Seif Sharif Hamad

-EATV

Kitwanga Aikaba Koo Serikali......Atishia Kuhamasisha Wananchi Kwenda Kuzima Mtambo wa Maji ulioko Ziwa Victoria.

Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga (CCM), amewapiga mkwara mawaziri bungeni kuwa atahamasisha wananchi wa jimbo lake kwenda kuzima mtambo wa maji ulioko Ziwa Victoria.

Kitwanga ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa kwanza katika serikali ya awamu ya tano, alilieleza Bunge jana kuwa mtambo huo upo kwenye chanzo cha maji cha Iherere, kilichoko jimboni kwake Misungwi mkoani Mwanza.

Katika mjadala wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji bungeni mjini Dodoma jana mchana, mbunge huyo aliyekuwa wa kwanza kupewa nafasi ya kuchangia, alitoa onyo hilo kwa Waziri Gerson Lwenge na msaidizi wake, Mhandisi Isack Kamwele, kwamba yuko mbioni kuuzima mtambo huo ikiwa wananchi wake hawatakuwa sehemu ya mradi huo wa maji.

“Mheshimiwa Naibu Spika, jimboni kwangu hakuna maji ya uhakika na tangu mwaka 2008 wananchi wamekuwa wakiyasubiri bila mafanikio," Kitwanga alisema.

“Kwa hiyo, nitakachokifanya safari hii, sitatoa shilingi kwenye bajeti, bali nitakwenda kuwahamasisha wananchi wa Misungwi wapatao 10,000, twende tukazime mtambo katika kile chanzo cha maji ili wote tukose.

“Wanamchi wa Misungwi hawana maji na katika bajeti yenu leo (jana) mmesema Nyang’omango kuna maji wakati hakuna, sasa nawaambia, sitatoa shilingi 'nita-mobilize' (nitahamasisha) wananchi tukazime ule mtambo.

“World Bank' (Benki ya Dunia) walifika pale kijijini, wakasema hawa wananchi walioko kwenye kile chanzo wanatakiwa kupata maji, lakini nyie hamuoni, hivi nyie mkoje?

“Nakipenda chama changu (CCM), nampenda Rais wangu (John) Magufuli, lakini lazima tutendeane haki kwa sababu hii nchi ni yetu sote.

“Hamuwezi kupeleka maji sehemu nyingine kwa gharama ya Sh. bilioni 600 halafu mkashindwa kuwapa wananchi wangu hata mradi wa Sh. bilioni 10.

“Mshukuru kwamba nilipokuwa waziri, nilikuwa siwezi kusema kitu, lakini sasa nimetoka, tutapambana kwa sababu lazima tuwe na mipango mizuri ya kuwapelekea wananchi wetu maji kama inavyofanyika katika umeme kupitia REA (Wakala wa Umeme Vijijini).”

Kitwanga alitumbuliwa na Rais Magufuli Mei 20, mwaka jana kwa tuhuma za kuingia bungeni na kujibu swali linalohusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Kitwanga pia alilalamikia kile alichokiita tabia ya baadhi ya viongozi wa wizara hiyo kukwamisha upatikanaji wa maji kupitia kwa marafiki zake kutoka nchini Austria.

“Rais alipokuja Misungwi, aliwaambia wananchi, kwamba nina marafiki zangu huko nje wanaoweza kunisaidia kupata maji," alisema. "Ule mradi ulipokuja, nikawekewa figisu wakasema mimi nina 'interest' (maslahi) nao.

"Ni kweli nina 'interest' nao kwa sababu wananchi wangu wa Kolomije wanahitaji maji, wananchi wa Bukumbi wanahitaji maji.

“Kwa hiyo, Mheshimiwa Naibu Spika, narudia tena, safari hii sitatoa shilingi, nitakwenda kuwahamasisha wananchi wangu tukazime ule mtambo wa maji ili wote tukose,” alisisiza Kitwanga.

Hata hivyo, muda mfupi kabla ya kusitisha shughuli za Bunge jana mchana, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, alimtahadharisha Kitwanga kuwa, uamuzi wake huo huenda ukamsababishia matatizo kwa kuwa unakiuka sheria za nchi.

Dk. Tulia alisema kuwahamasisha wananchi ili wavunje sheria ni kosa la jinai, hivyo mbunge huyo anapaswa kuwa makini kwa kuwa anaweza kuchukuliwa hatua kabla hata hajawahamasisha wananchi wa maeneo ya Kolomije na jimbo zima la Misungwi.

Walimu Wawili Watiwa Mbaroni Jijini Dar Kwa Kuvujisha Mtihani wa Kemia wa kidato cha sita

Jeshi la  Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia walimu wawili na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Chang'ombe (Mazoezi) kwa tuhuma za kukutwa na mtihani wa Kemia wa kidato cha sita. Mitihani hiyo inaendelea kufanyika nchini.

Kamishna wa Kanda hiyo, Simon Sirro, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Musa Elius na Innocent Murutu ambao ni walimu wa shule hiyo. Mwanafunzi ni Ritha Mosha.

Kamishna Sirro alisema wiki iliyopita saa 1:00 usiku Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa Ofisa wa Baraza la Mitihani, Aron Mweteni, aliyesema alimkuta kwenye shule hiyo mwalimu Elius na mtahiniwa Ritha wakiwa na karatasi yenye maswali na majibu ya somo la vitendo la kemia.

Alisema baada ya kuwatilia shaka na baadaye kuwatia mbaroni, walifanya ufuatiliaji wa awali kwa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) ambako ilibainika kuwa mtihani huo ni miongoni mwa ile ya kidato cha sita inayofanyika mwaka huu.

"Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa polisi na upelelezi ukikamilika tutawachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani,"Sirro alisema.

Katika tukio lingine, Kamishna Sirro alisema mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimesababisha kifo cha mkazi wa Gulani Suka, Alice Genadi ambaye alitumbukia kwenye shimo la choo cha jirani yake ambacho kilikuwa kimejaa maji na hakikuwa kimefunikwa.

Kamanda Sirro alisema msichana huyo alikuwa akimfuata dada yake dukani.

Wakati huo huo, Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wawili kwa kukutwa na vipande sita vya meno ya tembo.

Pia kamanda Sirro alisema wanawashikilia watuhumiwa watatu waliodaiwa kukutwa na lita 36,000 za gongo yenye thamani ya Sh. milioni 72.


Polisi Watumia Risasi Kumkamata Mtuhumiwa Aliyetoroka Chini ya Ulinzi wa Askari Magereza

Mshtakiwa anayekabiliwa na kesi ya kujaribu kubaka Allen Robert (33), ametoroka akiwa chini ya ulinzi wa askari Magereza baada ya kutoka kusikiliza ushahidi wa kesi inayomkabili na kusababisha taharuki kwa baadhi ya wananchi waliokuwa eneo hilo.

Tukio hilo lilitokea jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar  saa tisa alasiri na askari Magereza walilazimika kurusha risasi hewani ili kumkamata.

Wananchi waliohudhuria mahakamani  kwa shughuli mbalimbali baadhi walikimbia baada ya kusikia milio ya risasi.

Mmoja wa wananchi waliokuwa eneo hilo, Alex Simon alisema baada ya kusikia milio ya risasi aliingia chini ya meza na alilala chini akihofia usalama wake.

“Wakati nikiwa nimeagiza chakula kwenye mgahawa  ghafla niliona mtu akitoka hapo kwenye geti la Mahakama kisha nikasikia sauti ya askari Magereza wakisema lala chini wakati huo yule mshtakiwa akikimbia katikati ya watu. Nililala chini ya meza baada ya dakika 15 hali ilikuwa shwari,” alisema Simon.

Baada ya Robert kukamatwa alifunguliwa shtaka na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kwa kutoroka akiwa chini ya ulinzi.

Mbele ya Hakimu Marko Mochiwa, Mwendesha mashtaka wa Polisi, Mrusha Warioba alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Mei 10 katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.

“Mshtakiwa unakabiliwa na shtaka la kumtoroka askari Magereza Koplo John Chale, ulifanya hivyo ukijua kwamba ni kinyume na sheria,” alidai Warioba.

Baada ya maelezo hayo mshtakiwa hakujibu chochote licha ya kuulizwa zaidi ya mara mbili.

Hakimu Mochiwa aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 16 kesi hiyo itakaposikiliza. Mshtakiwa alipelekwa rumande.

Katika kesi ya msingi iliyopo mbele ya Hakimu Issa Kasailo, mshtakiwa anakabiliwa na shtaka la kujaribu kumbaka binti  mwenye umri wa miaka 24.

Kesi hiyo ilitajwa mahakamani hapo jana kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na shauri liliahirishwa hadi Mei 24.

WAZIRI wa Katiba na Sheria Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Atajwa Kwenye Orodha ya Watumishi Wenye Vyeti Feki..!!!!


Sakata la watumishi wa umma waliofanyiwa uhakiki wa vyeti limezidi kuchukua sura mpya kila iitwapo leo ambapo awamu hii, Waziri wa serikali ya awamu ya tano amebainika kuwa miongoni mwa watumishi ambao vyeti vyao vina utata.

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi ametajwa katika orodha ya watumishi ambao vyeti vyao vina matatizo ambapo uhakiki wake ulifanyika wakati akiwa mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla ya kuteuliwa kuwa mbunge na kisha waziri.

Waziri Prof. Kabuni ambaye amebobea katika sheria, pamoja na waafanyakazi wengine wa UDSM wametajwa katika orodha ya watumishi wa umma ambao vyeti vyao havijakamilika.

Katika orodha aliokabidhiwa Rais Dkt Magufuli na Waziri wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, jumla ya watumishi 9,932 walikutwa na vyeti vya kughushi, huku wengine zaidi ya 1,500 wakiwa na vyeti vyenye utata na wengine walikuwa wamepeleka vyeti pungufu kwenye uhakiki.

Akizungumza suala hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Mukandala alisema kwa Prof. Kabudi ametajwa katika orodha hiyo kwa sababu cheti chake cja kidato cha nne hakikuonekana wakati wa uhakiki. Aidha, Prof. Mukandala alisema kuwa tayari Prof. Kabudi ameshawasilisha cheti hicho na kwamba watakipeleka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa ajili ya uhakiki.

Wakati Rais Magufuli akikabidhiwa ripoti ya uhakiki wa watumishi wenye vyeti feki alisema kuwa, kwa wale ambao wanavyeti pungufu, wanaendelee kubaki kazini lakini uhakiki ufanyike vizuri kwa sababu si kila mtu alipita kidato cha sita kiweza kufika chuo. Hivyo kama hakupita kidato cha sita alafu ukamwambia akuletee cheti, hatokuwa nacho.

Diva Amjibu Dkt. Mwakyembe Kuhusu Kupinga Wasanii kuimba Nyimbo za Kisiasa

Ni muda mchache baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kusema wasanii waachane na tabia ya kuimba nyimbo za kisiasa kwani hakuna msanii aliyewahi kufikia mafanikio makubwa kwa kufanya hivyo.

Mtangazaji Diva the Bawse kupitia mtandao wake wa twitter ameandika ujumbe ambao unasadikika pengine amejibu kauli ya waziri huyo.




TAMBUA Faida Kuu 4 Utakazozipata Kama Ukiacha Kulala na Simu Yako Kuanzia Leo..!!!


Wengi wetu naamini tumekuwa na kajitabia kakulala na karibu na simu usiku kwenye vitanda vyetu pasipo kufahamua madhara ya kijitabia hicho.

Sasa leo ninayo mambo kadhaa yakukwambia msomaji wangu wa www.dkmandai.com kuhusu hii tabia ya kulala na simu usiku.

Zifuatazo ni faida utakazozipata endapo utaacha kulala na simu usiku kitandani kwako.

1.Utalala usinginzi mzuri na wa kutosha.

Inaaminika kuwa mtu ambaye hulala karibu na simu  usiku hulala usingizi wa mang'amng'amu kwa kuwa muda mwingi huwa akihisi huenda kunasimu itaingia. Hivyo endapo kuanzia leo ukiacha kulala na simu usiku itakusaidia kulala usingizi mzuri na wa kutosha usiku.

2. Hautakuwa mtumwa wa msongo wa mawazo tena

Kwa kawaida unapolala na simu unakuwa unamawazo mengi pengine bila wewe mwenyewe kujijua huenda unawaza kwanini fulani haja kupigia usiku huo au atakupigia saa ngapi kukwambia usiku mwema hivyo unajikuta unajipatia msongo wa mawao usio na sababu na hivyo kuathiri afya yako bure. Ili kuondokana na hilo ni vyema kuweka mbali simu yako wakati wa kulala au kuweka silent kabisa.

3. Utafanya kazi / biashara zako vizuri

Kwasababu sasa unapoacha kulala na simu inamaana utapata mda mzuri na wakutosha wa kulala vizuri hivyo hata kazi zako au biashara utazifanya kwa ufanisi zaidi.

4. Utajisikia mwenye afya zaidi 

Kwa sababu utakuwa unalala vya kutosha na watu wenye kulala vizuri huwa ni wenye afya.

KITWANGA Aitwanga Serikali Bungeni..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 11/5/2017..!!!


Ni Juventus vs Real Madrid fainali ya Champions League.


Atletico Madrid walionekana tishio kwa Real Madrid na walionekana kama wanaenda kubadili matokeo ya mwanzo ya mchezo wao baada ya mabao mawili ya haraka haraka.

Alianza Saul Niguez dakika ya 12 kuzichungulia nyavu za Real Madrid kabla ya Antoine Griezman dakika ya 16 kuiandikia Atletico bao la pili kwa mkwaju wa penati.

Lakini wakati Atletico wakiamini wangemaliza kipindi cha kwanza wakiongoza kwa goli 2 kwa 0, dakika ya 42 Isco alifanikiwa kuipatia Real Madrid goli na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa bao 2 kwa 1.

Bao la Isco lilikuwa la kwanza kwake katika michezo yake 31 iliyopita katika Champions League, na bao hilo liliifanya Real Madrid kufunga mfululizo goli katika mechi 67 mfululizo.

Kipindi cha pili Atletico iliwapasa kufunga mabao mengine matatu ili kuitoa Real Madrid na Atletico waliingia wakijitahidi kutafuta mabao hayo lakini ikashindikana na mchezo kuisha 2 kwa 1.

Matokeo hayo yameifanya Real Madrid kufudhu kwenda katika fainali ya Champions League msimu huu na hii ikiwa ni mara mbili mfululizo katika misimu miwili.

Real Madrid sasa wanaifuata Juventus ambao usiku wa Jumanne waliitoa Monaco katika fainali itakayopigwa mwezi ujao tarehe 6 katika mji wa Cardiff nchini Wales.

 

KAULI ya Msanii Diamond baada ya Profesa Jay Kusimama Bungeni na Kumtetea Kuhusu Kudaiwa Kodi ya Milioni 400 na TRA


Mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye juzi aliandikwa na gazeti la NIPASHE kwamba anadaiwa shilingi milioni 400 za kodi na TRA, amepost kipande cha video fupi ambacho Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay‘ amemuongelea bungeni.

Kwenye video hiyo, Profesa Jay amesema;"Juzi Msanii Diamond alikua analalamika TRA wamempelekea kodi ya Milioni 400, unaweza kujiuliza anadaiwa milioni 400 kwa kiasi gani alichoingiza?‘

"Downloads zinazofanyika mnaweza kuona Wasanii sasa hivi wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna kutoka kwa Wasanii kitu ambacho bado hawajakipandikiza, tumekua na ule msemo kama wa zamani kwamba shamba likiwa na bangi ni lako lakini likiwa na dhahabu ni la serikali… tunataka kuchuma kitu ambacho hatujakipanda, inabidi Serikali ianze kuwekeza na kuwajenga Wasanii kutoka shule za msingi mpaka Chuo kikuu"

Baada ya maneno hayo ya Profesa Jay kwenye video, Diamond Platnumz aliichukua video hiyo na kuandika; "Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni bro…kwakuwa niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo"

KITWANGA Aitwanga Serikali Bungeni..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 11/5/2017..!!!


 

Gallery

Popular Posts

About Us