Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dr Josephat Gwajima amefunguka na kusema Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ni rafiki yake hivyo alitaka kuonana naye ili aweze kujua Professa Ibrahim Lipumba anaharibu vipi chama
Mchungaji Gwajima amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo na Katibu Mkuu huyo wa CUF na kusema aliamua kukutana na rafiki yake huyo ili ajue hilo baada ya hapo yeye atajua anafanyaje.
‘Mimi huyu ni rafiki yangu kwa hiyo nilitaka kujua Professa Lipumba anafanya nini kuvuruga CUF, hivyo nilitaka kujua Lipumba amepatwa na nini mpaka amevuruga chama chako na kiukweli mimi nilikuwa siufahamu vizuri huu mgogoro ila saizi Seif ameniambia kwa hiyo na mimi nataka nitafakari alichoniambia rafiki yangu ni ‘digest’ baada ya hapo nitajua nafanya nini” alisema Gwajima
Kwa upande wake Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa amekaa na askofu Gwajima na kuzungumza naye kwa kina juu ya mgogoro huo na kila mmoja amemueleza mwenzake kile anachokifahamu na kusema ameamuchia askofu ili na yeye atafakari juu ya jambo hilo baada ya hapo anaamini huenda askofu akafanya jambo.
“Nimekaa na askofu na kila mmoja akamweleza mwenzake yale ambayo anayajua, kwa hiyo nimemweleza saizi kiundani kwa hiyo yeye ana ‘digest’ halafu askofu yeye ataamua juu ya kile tulichuzungumza” alisema Maalim Seif Sharif Hamad
-EATV
0 comments:
POST A COMMENT