Tuesday, 25 April 2017
HIZI HAPA NAFASI ZA SCHOLARSHIP NCHINI CHINA MWAKA 2017/18
Sakata la Bosi wa UN kufukuzwa latua bungeni
Dodoma. Sakata la kufukuzwa nchini la bosi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Awa Dabo, limetua bungeni.
Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga(Chadema) akizungumza bungeni leo, aliitaka serikali kufafanua sababu za kumfukuza nchini Mkurugenzi Mkazi huyo wa UNDP Tanzania kwa kumpa saa 24.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliliambia bunge kuwa serikali ina mamlaka yote katika masuala ya kidiplomasia na hivyo bunge haliwezi kuhoji sababu za mkurugenzi huyo kufukuzwa.
SIRARI: Mzee wa Miaka 78 Ajiunga na Darasa la Kwanza..!!!
Waswahili husema ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni, na elimu siku zote haina mwisho.
Huko Sirari Mkoani Mara Mzee wa miaka 78 amejitosa na kuanza darasa la kwanza mara tu baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu ya awali.
Mzee Nyamhanga Seguta alifikia uamuzi huo baada ya kuteseka sana na mahesabu katika biashara yake ya kuuza ndizi.
KAZI IMEANZA Marekani Watuma Nyambizi Nyingine Kuongeza Nguvu Korea Kaskazini..Inauwezo wa Kurusha Makombora ya Mbali.
Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda kutokana na majibizano makali na vitisho kati ya Marekani na Korea Kaskazini, ambapo meli ya jeshi la Marekani (USS Michigan) imewasili katika Korea Kusini huku hofu ikiongezeka zaidi kuhusu uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora au silaha za nyuklia.
Meli hiyo yenye uwezo wa kushambulia kwa makombora, imewasili kujiunga na kundi jingine la meli za kivita zinazoelekea eneo hilo ambapo zinaongozwa na meli kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson.
USS Michigan hutumia nguvu za nyuklia na hubeba makombora aina ya 154 Tomahawk na wanajeshi 60 pamoja na meli nyingine ndogo.
Aidha, bunge la Seneti nchini Marekani limealikwa kwa kikao cha kupewa habari kuhusu Korea Kaskazini siku ya Jumatano katika ikulu ya White House.
Meli hiyo inatarajiwa kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi pamoja na kundi la meli zinazoongozwa na Carl Vinson, kundi ambalo lilitumwa eneo la Korea kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani.
Hivi karibuni safari ya meli za kivita za Marekani ilizua utata kuhusu iwapo zilikuwa zinaenelekea eneo la Korea, lakini maafisa wa jeshi la wanamaji la Marekani kwa sasa wamesema zinaelekea eneo hilo kama ilivyoamrishwa.
Naye Rais wa Marekani, Donald Trump mapema mwezi huu amesema kwamba atatuma kundi kubwa la meli zenye nguvu.
Kimenuka!!..JB Amtolea Povu Wema Sepetu na Wenzake Ambao Hawakuandamana na Makonda Kupinga Uuzaji wa CD Feki na Za Nnje.
Muigizaji mkongwe nchini Jacob Stephen 'JB amefunguka na kudai hawakufanya maandamano ya kuzuia movie za nje ya nchi kuuzwa nchini bali waliandamana kuzitaka zilipiwe kodi au serikali itoe msamaha kwenye filamu za ndani.
JB amezungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano na wanahabari wakati wa uzinduzi wa filamu ya Tunu na kudai kuwa watu wengi wamehusisha maandamano yao na siasa kitu ambacho hakina ukweli na kuongeza kuwa tasnia ya filamu kwa sasa inahitaji watu watakaowasaidia kumaliza kilio chao.
"Sisi hatupingi movie za nje kuingia nchini, mimi mwenyewe nazipenda na ninaziangalia. Hapa ugomvi uliopo ni wao watozwe kodi au na sisi tuondolewe hizo kodi, wakifanya hivyo hakuna mtu ambaye atapiga kelele tena. Sasa hivi nakatwa asilimia 30 lakini bado natakiwa nitoe asilimia tano na wakati huo huo, nikitaka kutoa movie mpaka nikaombe kibali kama ni wewe ungekubali? Na jambo hili lisihusishwe na siasa kwani sisi mtu yoyote ambaye ataweza kutusaidia kutusemea tutamsikiliza hata akiwa wa upinzani hatuna shida" Alisema Jb
Aidha msanii huyo ameongeza kuwa wasanii wenzao wanaowakejeli kwa kuandamana wengi wao hawategemei movie kuwaingizia kipato na ndio maana wanaongea maneno ya ajabu huko nje.
"Msanii yoyote ambaye filamu ndiyo chakula chake hawezi kuwa nje ya hili kwa sababu hataweza kuishi. Mimi niseme tu siwezi kuishi bila filamu ndiyo maana tunapiga kelele. Sitaki kuwataja majina lakini angalia tu wewe mwenyewe huyo mtu ambaye hataki kupiga kelele anaishi bila filamu?" JB alimaliza
CCM Wamshitaki Nape ..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 25/4/2017..!!!
Umesikia Alichokisema Nape Nnauye Kuhusu CCM?? soma hapa
Usiku wa kuamkia Leo Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia tiketi ya CCM Nape Moses Nnauye ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe wake wa wazi aliyowahi kuandika kipindi cha nyuma kuhusu CCM, lengo likiwa ni kuweka kumbukumbu sawa kwa watu kuhusu CCM.
“Watu wengi wanaamini nimeisaidia sana CCM lakini ukweli ni kuwa CCM imenisaidia sana mimi kuliko mimi nilivyoisaidia, CCM ni SHULE.
“Bahati niliyopata kwa kuwa muenezi CCM ni kufanya kazi na ndg Kinana ni mwema, mzalendo, hodari, uwezo mkubwa, upendo na maarifa mengi” Ameandika Nape
JOH Makini Afunguka Haya Baada ya Mashabiki Kumfananisha na Jay Z wa Marekani..!!!
Msanii wa miondoko ya 'Hip hop' kutoka kampuni ya Weusi, Joh Makini amefunguka ya moyoni na kusema anajisikia faraja kwa mashabiki zake kumfananisha na msanii Jay Z.
Joh Makini amesema ufananisho huo uko wazi kwa kuwa kiwango cha muziki wake ni mkubwa kiasi ambacho watu wanaomzunguka na wapenzi wa kazi zake hawaoni mtu mwingine wa kumfananishia naye isipokuwa msanii huyo kutoka Ughaibuni.
"Jay Z ni 'role model' wangu...mimi naimba maisha ya sinoni daraja mbili na Tanzania na Jay Z anaimba maisha ya Brooklyn na Marekani, nafikiri nipo katika 'level' ambayo hawaoni mtu mwingine wa kunifananisha naye...Kwahiyo mimi naona poa kwa sababu kama unanifananisha na Jay z 'yeah i like it' kuliko ungenifananisha na mtu mwingine". Alisema Joh Makini
Kwa upande mwingine msanii huyo amedai changamoto na vikwazo anavyokutana navyo katika kufanya kazi zake za kila siku huwa ndiyo vinamfanya aweze kutengeneza mambo mazuri zaidi.
JB: Simfahamu Ney wa Mitego Wala Sisikilizagi Bongo Fleva
JB amedai hamfahamu mwanamuziki huyo na wala hasikilizagi bongo fleva, ila kwa kauli yake hiyo amesema anampenda sana japo amemdiss.
Yeye pamoja na kusema hasikilizi Bongo Flevaila hawachukii wanamuziki wa Bongo Fleva
Pia amesema sio kwamba hawataki movie za nje zisije ila wanataka zilipe kodi kama wao wanavyofanya, kwa kuwa mtu anadownload movie ya nje kisha anaizalisha copy nyingi na kuiuza bila kulipa kodi na amesema hii ikiendelea na wao hawatalipa kodi kwa movie zao pia