Dodoma. Sakata la kufukuzwa nchini la bosi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Awa Dabo, limetua bungeni.
Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga(Chadema) akizungumza bungeni leo, aliitaka serikali kufafanua sababu za kumfukuza nchini Mkurugenzi Mkazi huyo wa UNDP Tanzania kwa kumpa saa 24.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliliambia bunge kuwa serikali ina mamlaka yote katika masuala ya kidiplomasia na hivyo bunge haliwezi kuhoji sababu za mkurugenzi huyo kufukuzwa.
0 comments:
POST A COMMENT