KINGAZI BLOG: 02/04/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 4 February 2017

DOWNLOAD VIDEO: Ben Pol ft. Mr Eazi – PHONE







 

USIPITWE NA HII, TRENI ZA UMEME KULETWA TANZANIA. SERIKALI YATOA NENO


Hatimae serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya uchukuzi imesaini mkataba wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa Reli ya kisasa itakayowezesha Treni zinazotumia umeme kuanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza Tanzania.

Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawaamesema ‘Sasa hivi kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza unatumia saa 36 ambapo kuna kilometa 1219 lakini Treni mpya za umeme zikianza kufanya kazi safari itakua rahisi zaidi‘

Leo tunashuhudia utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa sehemu ya kipande cha reli kati ya Dar es salaam na Morogoro chenye urefu wa kilometa 300 na mkataba huu utakua baina ya RAHACO kampuni hodhi ya rasilimali za reli na ubia kati ya kampuni ya UTURUKI na URENO’

Kwa Wenzetu

‘Itakua kwa gharama ya USD BILIONI 1, Milioni 215, laki 2 na 82 ikijumuisha VAT USD Milioni 185 na laki 3, hii ni kwa ajili ya gharama za ujenzi kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro

Katika Afrika Treni kubwa ambayo itakwenda spidi kubwa itakua ni ya Tanzania (Kilomita 160 kwa saa), Treni nyingine itayokua na spidi kubwa itakua ni Morocco itakua kilometa 200 kwa saa, naamini na sisi Tanzania tutabadilisha mawazo kwenye Treni ya Dar Mwanza tutakua Kilometa 200 kwa saa

Kwa Wenzetu

Kama hufahamu, wakati wa utawala wa Uingereza marekebisho kidogo yalifanyika kwenye usafiri wa Treni Tanzania kutoka Treni inayotumia mvuke kuja kwenye injini ya Diesel, hata hivyo miundombinu hii kwa sasa ni chakavu na mwendokasi sio chini ya Kilomita 30 kwa saa ambayo kutoka Dar kwenda Mwanza unachukua saa 36‘ – Profesa Mbarawa

Mda wa mradi huu wa Umeme kukamilika ni miaka miwili na nusu baada ya ujenzi kuanza, kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro Treni mpya ya umeme itatumia saa moja na dakika 16, Dar es salaam kwenda Dodoma itakua masaa mawili na nusu, Dar-Mwanza saa saba na nusu’ – Profesa Mbarawa

Millard ayo

Makonda Amtaja Na Vee Money na Tunda Ishu ya Madawa ya Kulevya....Waliokaidi Agizo Lake Leo Kukamatwa


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameagiza kukamatwa kwa watu aliowataja jana kuhusika na dawa za kulevya ambao hawajajisalimisha kituo cha polisi leo, kama alivyoagiza

Makonda aliyefika katika Kituo Kikuu cha Polisi, amesema watu wao ambao hawajajisalimisha, wasakwe kokote waliko, na wawekwe ndani.

"Kuna watu tuliwaita, baadhi nimeambiwa hawajafika, ambao hawajafika nimeagiza wakachukuliwe wakae ndani mpaka siku ya Jumatatu" Amesema Makonda.

Amesema kati ya watu waliotajwa jana, ni wasanii watano pekee ndiyo wamejisalimisha siku ya leo katika kituo hicho wakiongozwa na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Wema Sepetu, Nyandu Tozi (Hamidu), TID, Babuu wa Kitaa.

Pia kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, jumla ya polisi 7 wamekwisha kamatwa huku watatu wakiendelea kutafutwa na wengine wawili ambao hawako katika jiji la Dar es Salaam watakamatwa ndani ya muda mfupi ujao.  

 Katika hatua nyingine, Makonda ametaja orodha nyingine tofauti na aliyoitaja jana ya watu wanadaiwa kuhusika katika dawa za kulevya akiwemo msanii bongo fleva Vanessa Mdee, mwanamitindo anayefahamika kwa jina la Tunda.

Mbali na wasanii hao, makonda amewataja pia askari wengine watatu wa Jeshi la Polisi Tanzania ambapo amedai kuwa askari hao wanatuhumiwa kwa kupokea pesa kiasi cha shilingi bilioni 1 hivi karibuni kutokana na kuhusika na dawa za kulevya pamoja na kukamata dawa za kulevya kisha kuziuza tena.

Pia amemtaja anayejulikana kwa jina la Omari Sanga kuwa ni mmoja anayehusishwa na uletaji wa dawa ya kulevya na amesababisha asilimia 60 ya watanzania kufungwa katika magereza ya china.

Makonda amesema "Waliofika tutajadiliana nao kuona namna gani wanatupatia yale tunayoyataka kuyafanyia kazi kutokana na taarifa tulizo nazo. Vita hii ya dawa za kulevya haiishi leo, inaisha pale dawa zinapokuwa zimeisha"

Naye Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kamishna Simon Sirro amesema kuwa Jeshi hilo limeunda tume ya kushughulika na mapambano dhidi ya dawa za kulevya mkoani humo


Wale Wanajeshi waliochangia kifo cha Kondakta Kwa Kipigo,Sasa Serikali Imechukua Hatua Hii Dhidi yao.


ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Sajini John Komba na wenzake wanne wakiwemo mgambo na wanafunzi wa jijini hapa, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga kwa kosa la kusababisha kifo cha aliyekuwa kondakta wa daladala inayosafiri kati ya Nguvumali na Raskazoni, Salim Kassim (18) mkazi wa Mwamboni.

Wakili wa Serikali, Donata Kazungu akisoma shitaka hilo la mauaji linalowakabili watuhumiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Hilda Lyatuu alisema Januari 26, mwaka huu katika Kambi ya JWTZ iliyoko Kata ya Nguvumali jijini Tanga, Komba mwenye namba MT 69500 na wenzake watatu walimuua Kassim katika eneo la kambi hiyo.

Wakili Kazungu aliwataja washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Adam Juma (20), Sofia John (20) ambao ni mwanafunzi, Yohana Warioba na Bernard Nicholaus ambao ni wanamgambo wanaolinda katika kambi hiyo.

Hata hivyo, watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji. Aidha, upelelezi kuhusu kesi hiyo haujakamilika na hivyo itatajwa tena Februari 26, mwaka huu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya February 4



 

Gallery

Popular Posts

About Us