Monday, 9 January 2017
PICHAZ+++HUYU NDIYE MWANAMKE ALIYEIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA
Kundi la kigaidi la ISIS laishambulia Israel.......Wanne Wauawa
Kundi la kigaidi linalojiita ‘Islamic State of Iraq and Syria’ (ISIS) kwa mara ya kwanza limetajwa kufanya mashambulizi ya mlengo wa kigaidi Jerusalem nchini Israel.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema kuwa shambulizi la kutumia roli lililowaua watu wanne na kujeruhi wengine 17 lilifanywa na kijana wa Palestina aliyetumwa na kundi la ISIS.
Israel ilifanya kikao cha dharura cha kabineti ya usalama ambacho ingawa hakikutoa vielelezo kuhusu mtu huyo, kilimtaja kuwa mfuasi wa ISIS.
“Tunajua kumekuwa na mlolongo wa mashambulizi ya kigaidi. Kuna uhakika kuwa kunaweza kuwa na muungano kati yao [ISIS], kutoka Ufaransa hadi Berlin, na sasa Jerusalem,” alisema Netanyahu.
Mshambuliaji huyo aliyetambulika kwa jina la Fadi Qunbar mwenye umri wa miaka 28, raia wa Palestina alitumia lori kubwa kuwagonga watu hao lakini alipigwa risasi na kuuawa papohapo baada ya kutekeleza tukio hilo.
Watu kadhaa wamekamatwa kutokana na tukio hilo wakiwemo majirani zake na wana familia wake watano.
Serikali yafanya mabadiliko tena !!Elimu ya Msingi mwisho Darasa la sita
SERIKALI imefanya mabadiliko makubwa katika mitaala na mfumo wa elimu ya msingi, MTANZANIA imebaini.
* Yaweza kuwa mwisho wa darasa la sita, masomo yapunguzwa
Habari za uhakika kutoka vyanzo vya kuaminika na kuthibitishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, zinasema mabadiliko hayo ambayo utekelezaji wake unaanza leo, yatagusa aina ya masomo yatakayofundishwa kuanzia darasa la tatu.
Kwa mujibu wa habari hizo, upo uwezekano wa elimu ya msingi ambayo imekuwa ikitolewa kwa miaka saba, ikapunguzwa na kuwa miaka sita kwa wanafunzi walioko darasa la tatu hivi sasa.
Habari hizo, zinasema masomo yatakayofundishwa kuanzia leo ni Kiswahili, Hisabati, English, Maarifa ya Jamii, Uraia na Maadili, Sayansi na Teknolojia na somo la dini.
Lakini pia kutokana na mabadiliko hayo, Serikali imeongezea masomo mawili ya ziada kwa wanafunzi wa darasa hilo ambayo ni Elimu ya Sanaa na Michezo na Vilabu vya Masomo ya Usajariamali (Shughuli za uzalishaji mali).
“Utaona idadi ya masomo imepungua kutoka 10 ya awali mpaka 6, haya ni mabadiliko makubwa katika madarasa haya, naamini yataleta mapinduzi kwa wanafunzi wetu.
“Si hicho tu, bali kuna masomo mapya yameingizwa, utaona kuna somo la uraia na maadili na ya shughuli za ujasiriamali..mitaala hii inaonekana itafungua ukurasa mpya wa elimu yetu,”kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kilisema kuanzia sasa wanafunzi hao watakuwa wanaingia shuleni asubuhi na kuruhusiwa saa 6:20 mchana.
“Mbali ya hilo, tayari kuna walimu shuleni kwetu wamepewa mafunzo ya namna ya kuanza kufundisha mitaala hii mipya, tena wametakiwa kukaa kituo cha kazi miaka miwili bila kuhama,”kilisema chanzo chetu.
KAULI YA SERIKALI
Akithibitisha kuwapo mabadiliko hayo, Naibu Katibu Mkuu Wizara Elimu (Msingi), Dk. Leonard Akwilapo alisema wanafunzi wanaoguswa na mabadiliko hayo ni wale walioanza elimu ya msingi mwaka 2015 na mwaka jana walikuwa darasa pili na darasa la tatu mtaala wao unalenga waishie darasa la sita.
“Kimsingi kuna maandalizi tunatakiwa tuyafanye maandalizi ya kimtaala yamekamilika, tunaangalia maandalizi ya miundombinu ndiyo tunayafanyia kazi hapo ili tutoke na ‘statement’ kamliki.
“Kwa hiyo siwezi kuconfirme (kuthibitisha) kwa sababu tunajalidiliana katika uongozi wa juu na wizara yetu pamoja na Tamisemi kuangalia je miundombinu itakuwa imekaa vizuri?
“Yaani wakati wale wanafika darasa la sita ili wote waende ‘form one’ na tuwe na madarasa mawili pale yote yanakwenda form one, kwa hiyo tunajiandaa sasa hivi na tunataka tutoe nyaraka ambazo zitatoa maelekezo namna ya kutekeleza, kwa hiyo ni matarajio yetu yaende namna hiyo.
“…siwezi kuconfirm sasa hivi mpaka yatakapokuwa tayari na uhakika wa miundombinu itakapokuwa tayari kuwapokea,” alisema.
Alipoulizwa kama taarifa za kuwapo walimu waliopewa semina kwa ajili ya mitaala mipya, akiri kufanyika kwa semina hizo.
“Yaaah tumewapa semina walimu wawili katika kila shule wa darasa la tatu na la nne na tumetoa mafunzo kwa walimu 22,950 kwa hiyo kimsingi ni kama mwalimu mmoja kwa kila shule, lakini kuna shule zimetoa walimu wawili kwa sababu zipo 16,000 na mia kidogo…ina maana kuna shule zimetoa walimu zaidi ya mmoja kwa sababu ya idadi ya wanafunzi kama ni wengi, lakini shule zote zilitoa walimu zipo zilizotoa mmoja zingine wawili wawili.
Alipoulizwa kama darasa la saba halitakuwapo rasmi kama wakikamilisha maandalizi, Dk. Akwilapo alisema. “eeeh kama tutakamilisha maandalizi hayo tutatangaza, kimsingi ni kwamba wanafunzi hao ukumbuke walianza na mtaala mpya ule ambao ulianza na masomo ya kusoma, kuandika na kuhesabu yaani KKK kwa darasa la kwanza na la pili tulitoa masomo ya tehama sijui sayansi, yote sasa yanaanzia darasa la tatu.
“Tulisema darasa la kwanza na la pili, wanafunzi wafundishwe kusoma, kuandika na kuhesbu kwa kuwa mahiri wanaingia darasa la tatu wanatumia stadi hizo ili kuyaelewa masomo sayansi, jiografia, tunaingiza uraia na maadili.
“ Sasa maana yake ni nini, baada ya darasa la kwanza na pili kuwa wameimarishwa kuwa mahiri katika kusoma, kuandika na kuhesabu, wanapoingia darasa la tatu wanatumia stadi hizo ili tunaingiza masomo na huo mtaala unaozungumza umeishia darasa la sita.
“Lakini utakuwa flexible kama miundombinu yetu bado kuna mahitaji muhimu tunaweza kuspendi mwaka mmoja, ila lengo ni hilo,”alisema Dk. Akwilapo.
Kuhusu walimu kuhama, Dk. Akwilapo alisema Serikali ingependa kuona walimu wanakaa kwenye vituo vya kazi kwa sababu wamepewa mafunzo.
“Tungependa wakae katika kituo hicho kwa sababu tumewapa mafunzo kwa ajili ya kituo hicho, lakini wanaweza wakahama kwa sababu tuna uwezo wa kufundisha wengine… maelekezo ni kwamba wakifa kule shuleni wenyewe wanakuwa wakufunzi kwa wenzao, si wao wanaweza kufanya mambo haya shule nzima, kuhama si sheria kama ya Mungu, wanaweza kuhama.
Kuhusu shule binafsi kutumia mitaala hiyo, Dk. Akwilapo alisema tayari shule hizo zimepewa mtaala mpya ambao umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza na tayari wamepewa mafunzo.
Alipoulizwa tena kama nia ya Serikali ni kufuta darasa la saba, Dk. Akwilapo alisema. “Matarajio yako namna hii, lakini ule mtaala ni flexible wanaanza na mtaala mpya ambao umethibitishwa,” alisema.
CWT
Akizungumzia mabadiliko hayo, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba alieleza kushtushwa na taarifa hiyo huku akitaka kupewa muda wa siku mbili ili alizungumzie jambo hilo.
“Hayo ni mabadiliko makubwa na ni mshtuko…ndio nasikia kwako sijasikia wala kuona popote. Naomba unipe muda wa kutulia kama siku mbili halafu nitapata cha kuongea,”alisema Mukoba.
Kwa upande wake mdau kutoka taasisi binafsi ya elimu, Benjamin Nkonya alisema mabadiliko hayo yapo katika sera ya elimu ya mwaka 2014.
Kutokana na hilo, Nkonya alikiri kwamba wapo walimu ambao wamekwishaanza mafunzo kwa ajili ya mabadiliko hayo.
“Lakini katika mabadiliko hayo sisi kama wadau wa shule binafsi tulipinga kwamba wanafunzi wa darasa la kwanza na pili wasisome kiingereza. Lakini baadaye tukakubaliana na sera ikatamka kwamba shule inayo uhuru wa kuchagua lugha sasa wasije wakapindisha.
“Sisi shule zetu za binafsi Kiingereza ni kuanzia chekechea. Pia tunapinga hili la wanafunzi kwenda sekondari bila kufanya mtihani, tunapinga kwa nguvu zote kwa sababu kipimo cha mwanafunzi ni mtihani,”alisema Nkonya.
Karoti na tangawizi vinavyoweza kukuondolea upungufu wa nguvu za kiume
Juisi ya karoti na mchanganyiko wa tangawizi huupatia mwili vitamin A, K, ambazo kwa pamoja husaidia na kulinda afya zetu.
Uwepo wa tangawizi ndani ya juisi hii umekuwa ukiifanya juisi hii kuwa suluhisho la matatizo ya kukatika kwa nywele na kuzifanya kuwa imara zaidi.Hivyo ni juisi nzuri kwa wanawake wanaopenda urembo wa nywele.
Hukinga dhidi ya saratani, matumizi ya juisi ya karoti yenye mchanganyiko wa tangawizi husaidia sana kuukinda mwili dhidi ya matatizo ya saratani za aina mbalimbali kwani husaidia kuua seli zinazoweza kuchangia matatizo ya saratani.
Huimarisha kinga za mwili, juisi hii pia husaidia kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na vitamin A ndani yake hivyo kumfanya mhusika kutozongwa na magonjwa ya mara kwa mara.
Hulinda meno na fizi, karoti pekee yake kwanza inatosha kwa kuwa mlinzi mzuri wa kinywa, hivyo matumizi ya glasi moja ya juisi ya karoti iliyochanganywa na tangawizi baada ya kula husaidia sana kulinda afya ya kinywa kwa ujumla.
Pamoja na hayo, pia huweza kuongeza nguvu za kiume kutokana na kuwa na tangawizi ndani
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam Dr. Valentino Mokiwa Avuliwa uaskofu
Sakata la Mgogoro wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es salaam, linazidi kuchukua sura mpya,kufuatia Askofu wa Dayosisi hiyo,Dokta Valentino Mokiwa,kugoma kujiuzulu na kustaafishwa kwa manufaa ya Kanisa hilo kama alivyotakiwa na Mhasham Askofu wa Jimbo kuu la Tanzania,Dokta Jacob Erasto Chimeledya.
Hatua ya Dokta Mokiwa,kutakiwa kufanya hivyo,ni agizo la nyumba ya maaskofu la kuundwa tume ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo,kuchunguza tuhuma kumi zilizokuwa zinamkabili Dokta Mokiwa,pamoja na nyinginezo, za ukosefu wa maadili,ikiwemo kufuja mali za kanisa na kuingia mikataba kiholela yenye viashiria vya rushwa katika maeneo ya Buza,ikiwemo pia kutoa daraja la Ushemasi,Upadre,na Ukanon,kwa katibu wa Dayosisi,Mkristo ambaye ametengana na mkewe na kuoa mke mwingine kiserikali kinyume na kanuni ya kanisa kuhusu ndoa.
Waandishi wa Channel Ten,wamefika katika nyumba zinazodaiwa kutelekezwa na Dokta Mokiwa ikiwemo Silver Oak ya Upanga,na ya Mtaa wa Uganda Ostabei, ambapo imedaiwa kuwa ameiacha na kwenda kupanga huku kanisa likimlipa pango la shilingi milioni 3 kwa mwezi miaka zaidi ya miaka sita.
Dokta Mokiwa jana aligoma kupokea barua yake kutoka kwa Dokta Jacob Erasto Chimeledya,na baadhi ya waamini wa kanisa hilo katika nyakati tofauti,wamezungumzia hatua ya kutakiwa kujiuzulu na kustaafishwa Dokta Mokiwa.
Katika hatua nyingine,Dokta Valentino Leonard Mokiwa,kupitia kwa Afisa habari wake,Yohana Sanha,amedai kuwa mchakato uliotumika kumuhukumu ni batili na kwamba bado yeye ni Mkuu wa Dayosisi ya Dar es salaam.