KINGAZI BLOG: 11/03/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday, 3 November 2016

WCB WAKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA SALOME NA KUSEMA ALIE KUFA SIO YULE VIDEO QUEEN WAO


Habari zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya jana iliripoti tukio la Model Juliana kufariki Dunia baada ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia (kubakwa).(Picha iliyosambaa ikitaarifu tukio hilo)Lakini hali imekuwa tofauti baada ya taarifa zilizotolewa na akaunti moja ya Instagram inayojulikana kwa jina la Young_msafi ambayo imekanusha taarifa hizo.
Akaunti kiyo imeeleza kuwa aliyekutwa na ukatili huo hadi kupelekea kifo chake sio SALOME wa Diamond Platnumz bali ni model ambaye alikuwa Dancer wa chuo kikuu cha Mkumila.
Juliana amekutwa na mauti hayo usiku wa Jumatano ya tarehe 1/11/2016 baada ya Kutekwa wakati akiwa anakwenda kukutana na Marafiki zake kisha akateswa na kubakwa na watu wasiojulikana na kisha wakamtupa kichakani na mwili wake kuonekana asubuhi ya tarehe 2/11/2016.

Kupitia akaunti ya Instagram ya Ma-Model inayojulikana kwa jina la BLACKFOX_MODELS imethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa Misa ya maombezi itafanyika siku ya Jumapili katika ofisi zao.

REST IN PEACE JULIANA

JINSI BIBLIA INAAVYOSEMA KUHUSU MAMBO MBALIMBALI MAOVU YANAYOTUKIA SASA HIVI KA

Kitabu cha Biblia kinaeleza waziwazi huu uchafu unaofanywa
na binadamu kama matendo ya ushoga,kutembea na binamu
yako pamoja na wake za watu,kupitia vifungu vifuatavyo :
USHOGA NA ULAJI TIGO MAMBO YA WALAWI 20:13 Tena mtu
mume akilala pamoja na mtu mume,kama alalavyo na mtu
mke,wote wamefanya machukizo hakika watauwawa
KUTEMBEA NA MKE/MUME WA MTU MAMBO YA WALAWI
20:10 Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine,na
mwanamke aziniye na mtu mume hakika watauwawa
NA WALE MNAOKULA KUKU NA MAYAI YAKE [MAMA NA
MWANA] MAMBO YA WALAWI 20:12 Na mtu mume akilala na
mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauwawa,Tena
mtu mume akimuoa mke pamoja na mama yake ni uovu mkuu
WALE WANAOTEMBEA NA WANYAMA MAMBO YA WALAWI
20:15 Tena mtu mume akilala na mnyama, na mwanamke
akimkaribia mnyama yeyote na kulala pamoja naye,mtamwua
huyo mwanamke
KUTEMBEA NA BINAMU YAKO MAMBO YA WALAWI 20:19
Usifunue utupu wa umbu la mama yako wala umbu la baba
yako

je wajua,zifahamu mbinu mbalimbali za kumpata mwenzi bora

KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana.

Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza.
Ndio ukweli wenyewe

Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea.

Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi.

Maneno ya kusikia kutoka kwa wanawake
Wakati wa kumtongoza mwanamke tarajia maneno kama;

1. Nina mume au mchumba
Inakuwa kuwa ni kweli au njia ya kukataa

2. Niko bize na kazi`
Hii humaanisha kwamba hana muda wa kuzungumza au hata kuonana, ni dalili pia ya kukataa au kuvuta muda ili aendelea kukutafiti

3. Nimeokoka nampenda Mungu
Hii huwa na maana kwamba yeye ni mtu asiyependa uchafu hasa kama unamtongoza kwa lengo la kufanya ngono tu

4.Mimi nasoma, sitaki hayo hadi nimalize
Sitaki! Ni kwamba anaweza kujisemea kwamba hataki uhusiano uwepo. Anaweza kueleza sababu au kutoeleza.

6. Wewe sio mwanaume wa aina yangu;
Hapo huwa mwanamke anamaanisha labda una sifa tofauti na anazotaka, huenda wewe mwanaume ni mfupi, mweusi au tabia zingine zozote ambazo haziendani nae.

Msingi wa kuomba urafiki 
Kwa mwanamume mwenye umakini, huwa hakosi kupata anachotaka. Jiwe lake lazima litapiga anachokitaka, hasa kama atakuwa mwenye kufanya utafiti wa kina kabla ya kuamua kufanya kitu. Msingi sahihi wa kutongoza ni kufanya utafiti na kuongea kwa mitego, kabla ya kumfikia msichana unayemuhitaji.

Kwa mfano badala ya kusema twende tukale chakula cha mchana, sema utakuwa na muda kweli tukale, au uko bize? Maana yake ni kwamba huenda ni kweli akawa bize au la, lakini kama hataki atakwambia niko bize kama ndivyo unaweza kumuuliza nikuletee nini ninapotoka kula. Kwa namna anavyojibu vibaya au vizuri unaweza kupata mwelekeo wa nini unaweza kujibiwa kama unaongea wazi unachokitaka kwake.

Wanawake wanajua fika nini ambacho mwanaume anakitaka anapoanza kuongea hiki na kile, mara nyingi huwa wanafanya kana kwamba hawajui.

Mambo ya kuzingatia katika hatua ya uchumba
Ukweli ni kuwa uchumba ni wakati mzuri sana wa kuangaliana tabia ili hatimaye kuwa na chaguo jema. Hata hivyo ili kuwa na uhusiano mzuri ni lazima kufahamu kuwa wanadamu wanatofautiana, aidha kitabia au kimuonekano. Ni lazima kujifunza namna gani unaweza kuishi na watu wengine wenye hali tofauti.

Unaweza kuona watu wanatofautiana kitabia, huyo ni mzunguzaji sana, mwingine ni mpole, kiasi kwamba hata ukiwa nae ni kama uko peke yako. Kumlazimisha asiye na uwezo wa kuzungumza sana, awe mzungumzaji, sio sahihi sana, wala kumzuia mzungumzaji asifanye hivyo, pia sio sahihi
Wachumba wanaweza kutofautiana kwa kiwango cha elimu, uchumi, ufahamu juu ya mambo mbalimbali, kikabila, umri na hata kwa rangi pia. Kufahamu hili ni suala la msingi sana ili kuhakikisha.

Ingawa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakilazimisha kwamba wawe wanaoana na wale ambao ni wa kutoka kwenye madhehebu yao tu, wachumba wanaweza wakatoka katika madhehebu/makanisa tofauti na hili ni kwa kuzingatia madhehebu/makanisa mengi yaliyopo.

COPIED FROM  MUUNGWANA BLOG

Hiki ndicho kinachoendelea bungeni ...... "Mawaziri Wasulubiwa"


Bunge la Jamhuri ya Muungano jana liliweka kando tofauti zao za kisiasa wakati lilipowaweka kwenye kibano mawaziri watano kutokana na utendaji wao.

 Wabunge wa chama tawala na upinzani walionyesha makali yao wakijadili Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2017/18 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao, ikiwa ni mwaka mmoja tangu Serikali ya Rais John Magufuli iingie madarakani.

 Mbali na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, mawaziri wengine waliowekwa kwenye hali ngumu ni Ummy Mwalimu, ambaye ni Waziri wa Afya, Angellah Kairuki (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi), Charles Mwijage (Viwanda, Biashara na Uwezeshaji) na Profesa Joyce Ndalichako (Elimu, Sayansi na Teknolojia). 

Mwongozo huo wa mpango wa kuandaa bajeti unaonyesha Serikali itatumia Sh32.9 trilioni kwa mwaka ujao wa fedha, ikiwa ni ongezeko la Sh3.4 trilioni kulinganisha na bajeti ya mwaka huu. 

Mjadala wa wabunge hao ulijielekeza katika kuchambua utendaji wa mawaziri hao na hali ilivyo kwenye wizara zao, hasa kiuchumi ambayo inaelezwa kuwa ngumu kutokana na wananchi kudai fedha zimepotea kwenye mzunguko.

Aliyefungua mashambulizi hayo ni mbunge wa Busega (CCM), Dk Raphael Chegeni aliyesema Dk Mpango ni msomi, lakini ana “kiburi, si msikivu na hataki kushauriwa”. 

Dk Chegeni alisema wabunge walimshauri mambo mengi waziri huyo katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2016/17, lakini hakutaka kusikiliza na ndiyo maana hali imekuwa ngumu kila eneo. 

‘’Dk Mpango unapaswa kuwa msikivu na kuacha kiburi. Tunayokushauri yachukue (kwa kuwa) tunakusaidia ufanye kazi.Tulikuambia mambo mengi, ukatudharau sasa yanatokea, kila kona hakuna unafuu,’’ alisema.

Dk Chegeni alisema uchumi ambao anauzungumziwa kwenye mpango wake hauendani na hali halisi ya maisha ya wananchi, akisema hata halmashauri hazijapewa fedha hadi sasa. 

“Wananchi hawana fedha, wabunge hawana fedha. Fedha ambazo Mamlaka ya Mapato (TRA) inaeleza kuwa inakusanya, ziko wapi wakati madeni yameongezeka?”

Alimtaka waziri huyo kutimiza wajibu wake kwa unyenyekevu na kwa kusikiliza ushauri wa wabunge kuhusu wizara yake.

“Umekuwa ni tatizo sana. Hata ukiitwa na jumuiya za wafanyabiashara huendi, ukiitwa na kamati ya Bunge ya Bajeti huendi.Umekuwa mgumu kupatikana, dhamana uliyopewa ni kubwa, usitumie vibaya mamlaka yako,” alisema Dk Chegeni. 

Mbunge mwingine aliyechangia alikuwa John Heche (Tarime Vijijini-Chadema), ambaye alisema mtu wa pili kutumbuliwa na Rais John Magufuli baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga atakuwa Dk Mpango. 

“Kwa sababu gani utakuwa ni wa pili kutumbuliwa? Kwa sababu mambo yanapokwama, mipango yote mliyopanga inapokwama, wewe ndiye unabebeshwa zigo hilo ili yeye aonekane yuko sawa wakati mnakosea wote,” alisema. 

Heche alisema wamesimamisha ajira kutafuta watumishi hewa kwa mwaka mzima, lakini wako vijana waliosomeshwa na baba zao wako mitaani kwa kukosa ajira. 

“Dada zetu wanajiuza, mikopo nayo hakuna, mnatafuta wanafunzi hewa. Kilimo nako mnatafuta wakulima hewa. Cha msingi mseme kuwa Serikali yenu imefilisika na hamuwezi kutekeleza kitu chochote, msaidiwe,” alisema. 

Mbunge wa Solwa (CCM), Ahmed Salum aliwataka wabunge wa CCM kumwambia ukweli Dk Mpango kuwa wanakwenda kugonga mwamba katika uchumi.

“Unajiuliza fedha zimekwenda wapi? Unakuja hapa unasema kuwa uchumi umekua, how (kwa vipi)? Twiga imeshakuwa taken over (imeshachukuliwa), CRDB imetangaza hasara na TIB hasara,” alisema. 

Alisema hali hiyo inaonyesha kuwa baada ya miaka miwili benki hizo zinakwenda kufungwa na huo utakuwa ni mgogoro wa kiuchumi nchini. 

Alisema hilo huenda linatokana na mawaziri kutokwenda kuomba kura na hivyo hawafahamu joto la maisha lililopo kwa wananchi majimboni. 

“Mimi natoka Jimbo la Solwa, unaahidi, unadanganya hadi unachoka. Alikuwa JK ameondoka, anakuja Magufuli ataondoka hakuna lililofanyika,” alisema. 

Aliitaka Serikali kurejesha fedha za mifuko ya hifadhi ya jamii ilizoziweka “kabatini” Benki Kuu na mifuko hiyo iziweke fedha hizo kwenye benki za biashara ili fedha zianze kuzunguka.

Aliitaka Serikali kulipa madeni ya ndani ili fedha zianze kuzunguka na kwamba kumekuwa na joto hata ndani ya Bunge, akisema kuna ukata.

Salum alisema makusanyo ya kodi yanayotangazwa na kuonekana kuwa makubwa yanatokana na watu kulipa madeni ya nyuma na mara baada ya kuisha kwa malimbikizo hayo, makusanyo yatabaki kama ilivyokuwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne. 

“Watalipa itafika mahali itakwisha na kubaki na makusanyo ya siku hiyo, cash revenue (fedha taslimu). Hapo ndipo itashuka kutoka Sh1.5 trilioni hadi Sh800 bilioni iliyoachwa na Rais Jakaya Kikwete,” alisema. 

“Haya madeni yakiisha tutarudi kukusanya bilioni. Hatuwezi kufika trilioni hizo za leo. Tuna matatizo. Kipindi cha Kikwete, TRA ilikuwa inakusanya Sh850 bilioni, lakini nchi ilikuwa nzuri na mambo mengi yalienda vizuri kuliko sasa.” 

Alisema Rais Magufuli amekuwa na maono mazuri ya kuifanya nchi kufikia mafanikio ya Thailand, lakini tatizo wasaidizi wake hawamwambii ukweli ama wanaogopa kufukuzwa. 

“Magufuli tulikuwa naye hapa kwa zaidi ya miaka 10, namfahamu. Ukienda na data (takwimu) ukamueleza kukimbiwa na wafanyabiashara bandarini, atakuelewa,”alisema. 

Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussen Bashe alisema mipango ya Dk Mpango haifanani na ahadi walizozitoa kwa wananchi kuwa watawaboreshea hali ya uchumi watakapowachagua. 

“Kwa sababu kaka yangu (Dk Mpango) hujaenda kuomba kura? Dunia imebadilika tunaenda kufa tunapaswa kubadilika,” alisema Bashe. 

Alisema miradi mingine kama wa chuma wa Liganga na makaa ya mawe wa Mchuchuma ameanza kuisikia muda mrefu, lakini hajaona utekelezaji. 

Bashe alisema Waziri Dk Mpango anazungumzia bajeti ya Sh33 trilioni na kwamba eneo la kwanza ni makusanyo ya kodi kuongezeka kwa asilimia 16, wakati siyo mazuri. 

Alisema wabunge waliwahi kuwaambia wasiweke kodi kwenye uhamishaji wa fedha, utalii na maeneo mengine, lakini hawakuwasikia. 

 

Ndalichako 

Wakizungumzia hali ya elimu, wabunge walimkosoa Waziri Ndalichako kutokana na hali inavyoendelea, hasa suala la mikopo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu. 

Akichangia eneo hilo, Heche alianza kwa kukosoa kitendo cha Profesa Ndalichako kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam. 

“Leo elimu ni majanga. Mimi nilikuwa nakuheshimu sana Profesa Ndalichako ukiwa Katibu wa Baraza (la Mitihani la TaifaNecta). Umewahi kuonyesha watu wamechora mazombi kwenye mitihani,” alisema. 

“Wewe umepewa wizara hii, umechora Zombie kubwa kuliko wale waliochora kwenye mitihani, sijui hata wizi wa mitihani utazuiaje kama wewe Profesa ulitoka hapa kwenda kuiba kura Kinondoni.” 

 Alisema hivi sasa Bunge wamelifanya kama idara fulani ya Ikulu inayohusika na umwagiliaji maji katika maua. 

Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Wataira alisema Ndalichako alipiga kura za kuwachagua mameya wa halmashauri za manispaa za Kinondoni na Ilala. 

“Ulikuwapo juzi kwenye uchaguzi wa meya Kinondoni wakati ulishapiga kura katika umeya wa Ilala, Profesa mzima unahusika katika wizi wa kura,” alisema. 

Mwijage

Pia Waziri Mwijage alikuwa kwe- nye kikaangio hicho. Akichangia suala la mpango wa Serikali kuifanya Tanzania iwe nchi ya viwanda, Dk Chegeni alisema Mwijage ni “mzee wa sound” ambaye anafanya porojo. 

“Waziri wetu anajulikana kama mzee wa porojo, sijui hiyo Tanzania ya viwanda tutafika lini. Acheni maneno maneno na kusigana wenyewe kwa wenyewe. Mnatofautiana kauli, kila mmoja anaongea lake.  Fanyeni kazi kwa pamoja kila wizara itoe maoni yake katika huo Mpango,” alisema Dk Chegeni. 

Naye Heche alisema hata kwa Watanzania wanamjua Mwijage kwa jina la “Mzee wa Sound”. “Ukikutana naye hapo nje ukamsimamisha waziri, anauliza ‘vipi unataka nikupe kiwanda’ na kutoa mkono mfukoni. 

Anataka kuchomoa kiwanda mfukoni? Mpango wenu hamjajenga kiwanda hata kimoja,” alisema. 

Alisema kiwanda ndicho kitaajiri watu wengi wakiwemo mamantilie, wahasibu wahandisi na wengine wengi, lakini hadi sasa hakuna kiwanda hata kimoja. 

Kairuki 

Akizungumzia suala la watumishi hewa, mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo) Zitto Kabwe alionyesha kushangazwa na kitendo cha mawaziri kutoa taarifa zinazotofautiana. 

 “Monthly Economic Review (taarifa ya uchumi ya mwezi) ya Agosti 2015 inaonyesha kwamba wages and salaries (mishahara) ambazo Serikali ililipa Juni mwaka 2015 zilikuwa Sh456 bilioni. 

"Monthly Economic Review ya Agosti 2016 inaonyesha kwamba wages and salaries ambazo Serikali imelipa kwa mwezi Juni 2016 ni Sh534 bilioni,”alisema Zitto.

“Kwamba kuna nyongeza ya gharama za mishahara ya kila mwezi ya Sh78 bilioni. Waziri wa Utumishi jana ameeleza wanaokoa Sh19 bilioni kila mwezi kwa kuondoa watumishi hewa. Taarifa ya Benki Kuu inaonyesha kuwa tangu Serikali hii iingie madarakani, gharama za watumishi kwa mwezi zimeongezeka kwa Sh78 bilioni.”

 Zito alisema pamoja na watumishi hewa kuondolewa, ajira mpya kuzuiwa na nyongeza ya mishahara kusimamishwa, gharama za mishahara zimeongezeka kwa Sh78 bilioni. “Haiekeweki. 

Kuna mmojawapo kati ya hawa wawili (Waziri Kairuki na BOT) anadanganya umma. Ama zoezi la watumishi hewa ni publicity stunt (la kujitafutia umaarufu) au Serikali inatumia fedha kwa matumizi mengine, halafu BOT inasema ni mishahara,”alisema Zitto.

Watiwa Mbaroni Kwa kuvujisha mtihani FEKI wa kidato cha nne


Walimu wa Shule ya Sekondari Hasanga, iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe na wafanyabiashara wawili, wanahojiwa na vyombo vya usalama mkoani Mbeya kwa tuhuma za kuhusika na utengenezaji wa mitihani feki ya kidato cha nne.

Watuhumiwa hao, James Kapinga (36) ambaye anadaiwa kufanya kazi Shule ya Sekondari ya Hasanga pia anajitolea kufundisha Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Sangu, Baraka Mwazambe (28), mfanyabiashara na mkazi wa Tunduma na mtaalamu wa masuala ya Tehama (IT), Alex Mochi.

Watu hao kwa pamoja inadaiwa walikamatwa juzi usiku baada ya mwanafunzi mmoja ambaye jina lake na la shule vimehifadhiwa kukutwa na mtihani wa somo la Kiingereza na alipobanwa, inadaiwa aliwataja wahusika hao.

“Mwanafunzi huyu ni wa shule nyingine tena si ya Mbeya, alikutwa na mtihani feki wa somo la Kiingereza, alipohojiwa alieleza mtihani huo ulitoka Mbeya na Serikali ilipofuatilia iliwabaini wahusika ambao walikuwa wanasambaza mitihani feki,” kilisema chanzo kimoja cha habari hii.

Akizungumzia sakata hilo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariamu Mtunguja, alikiri ofisi yake kupokea taarifa juu ya uvujaji wa mitihani na walipofuatilia walibaini mitihani hiyo ni feki.

“Mbeya hakuna mitihani iliyovuja kama inavyoelezwa katika mitandao, ukweli ni kwamba suala hilo lilifuatiliwa ilibainika mitihani inayosambazwa si ile iliyochapishwa na Baraza la Mitihani la Taifa, ni feki na baadhi ya wahusika wanahojiwa na vyombo vya dola,” alisema.

Naye Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Benedict Sandy, alisema hakuna mitihani iliyovuja.

“Mitandao imekuwa ikitoa taarifa za upotoshaji eti mitihani imevuja, mitihani iliyosambaa na kukutwa na baadhi ya wanafunzi tena si wa Mkoa wa Mbeya ni feki na wahusika wanaodaiwa kuisambaza wamekamatwa.

“Nawaomba wanafunzi wazingatie yale waliyofundishwa, mitihani hiyo inakuja kwa lengo baya la kuwapotezea muda wao na mwisho wa siku kuishia kufeli, watu wanaofanya kazi hiyo wapo kimasilahi,” alisema.

Kesi mpya  ya SCORPION Yapigwa Kalenda tena


Upande wa Jamhuri kwenye kesi ya Salim Njwete  maarufu kama 'Scorpion' anayetuhumiwa kumwibia Saidi Mrisho na kumtoboa macho kwa kisu umedai mahakamani hapo kwamba upelelezi haujakamilika na kuomba siku nyingine ya kukamilisha.

Mshitakiwa Njwete 34,  anashitakiwa kwa kumwibia Mrisho na kumjeruhi kwa kumchoma tumboni, mabegani na machoni.

Taarifa ya upelelezi kutokamilika ilielezwa jana na Mwendesha Mashitaka Chensensi Gavyole mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule kesi hiyo ilipotajwa na kuangaliwa kama upelelezi umekamilika.

“Mshitakiwa yuko mbele ya Mahakama hii lakini upelelezi haujakamilika, tunaomba Mahakama itupangie siku nyingine ya kutajwa kutokana na upelelezi kuendelea,”alisema Gavyole.

Kutokana na sababu hizo, Hakimu Haule aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 16 itakapotajwa tena.

Mshitakiwa huyo maarufu kama Scorpion alifikishwa mahakamani hapo akiwa kwenye gari dogo la mizigo tofauti na siku za nyuma ambapo alikuwa akiletwa akiwa kwenye basi la Magereza.

Awali ilidaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 9 Buguruni Sheli alipomwibia Mrisho fedha na vitu vyenye thamani ya Sh 476,000 na kumjeruhi kwa kumchoma kisu tumboni, mabegani na machoni.

Hii hapa Video ya undani wa Msichana huyu Aliyebakwa Hadi Kufa chuo cha Makumira University ARUSHA.


Mapema jana zimesambaa Picha kwenye Mitandao ya kijamii ikimuonyesha Msichana anayefahamika kwa jina la JULIANA ISAWAFO Ambaye Amebakwa hadi Kufa na Kutupwa Nje ya eneo la Chuo Kikuu cha Tumaini (Makumira Arusha).

Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho ambapo amethibitisha kwamba ni kweli Ameokotwa Msichana huyo Majira ya Saa tano asubuhi ya Leo akiwa Amekufa na mwili wake Kutelekezwa kwenye Shamba la Mpunga hatua chache nje ya Eneo la Chuo.

Hata hivyo Amenithibitishia kwamba Msichana huyo ni Mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila sio Mwanafunzi rasmi kama watu wanavyodai.

Anasema Msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la Chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa waalimu wa Sanaa Chuoni hapo.

Hata hivyo hakusita kuweka wazi kwamba Wanasikitika sana Kwa Tukio hilo kwani Msichana huyo alikuwa kama Dancer wa Matamasha ya Chuo cha Makumira.
 Sikiliza Hapa chini: i: 

Habari Kuu zilizopo kwenye Magazeti ya Leo Alhamisi ya Novemba 3







USIACHE KUTEMBELEA BLOG HII , PIA SHARE HABARI HIZI NA WENZAKO WAZIPATE.

Shirikisho la vyuo Vikuu lataja Hujuma bodi ya Mikopo- (HESLB)

Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini limemuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa hesabu za Sh bilioni 1.74 za ada ya uombaji mikopo kwa mwaka huu katika Bodi ya Mikopo (HESLB) ili kujua matumizi ya fedha hizo kwa kuwa kuna mapungufu.

Aidha, shirikisho hilo limedai kubaini hujuma katika bodi hiyo zinazofanywa kwa makusudi ili kuchafua utendaji wa serikali iliyopo madarakani.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mtendaji wa shirikisho hilo, Daniel Zenda alipokuwa anazungumzia tuhuma za hujuma hizo, akidai zinafanywa kwa makusudi ili kurudisha nyuma jitihada njema za serikali.

Alisema ofisi ya CAG inapaswa kufanya ukaguzi wa Sh bilioni 1.74 fedha ambazo zilitokana na ada ya uombaji wa mikopo kwa mwaka huu ambapo kila mwanafunzi alitoa Sh 30,000 kwa waombaji 54,000.

Alisema ni muhimu kujua matumizi ya fedha hizo kutokana na upungufu uliojitokeza katika upitiaji wa sifa na vigezo vya wanaostahili kupata mkopo.

Alifafanua kuwa wanatambua hatua ya serikali katika kuhakikisha wanafunzi wenye sifa wanapata mikopo kwa wakati ambapo takribani Sh bilioni 80 zimeongezwa kwenye bajeti ya bodi hiyo ili kuwezesha mikopo kwa wanafunzi wote wenye sifa.

Zenda alisema Sh bilioni 487 zimepitishwa katika bajeti ya mwaka huu na mwaka jana ilikuwa chini ya makadirio ya Sh bilioni 350, lakini pamoja na kuongezeka kwa fedha hizo idadi ya wanafunzi walionufaika na mikopo imekuwa pungufu.

“Mwaka uliopita wanufaika wa mikopo walikuwa 53,000 na mwaka huu wanufaika wanafunzi 25,700 pamoja na ongezeko la makadirio ya zaidi ya Sh bilioni 137 kwenye bajeti ya Mikopo bado wanafunzi wengi hawajafikiwa,” alisema.

 

Gallery

Popular Posts

About Us