KINGAZI BLOG: 03/14/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday, 14 March 2017

Taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu kuondolewa na Kurejeshwa Jeshini


Aliyekuwa  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi, ameondolewa katika wadhifa huo na kurejeshwa jeshini.

Akithibitisha habari hizi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu (DAS), Titus Mughuha, amesema Kanali Mkisi alitoa taarifa za uhamisho huo katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na kusema kuwa, anarejea makao makuu ya jeshi alikokuwa awali kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

‘Ni kweli Kanali Martin Mkisi amepata barua ya kurudi makao makuu ya jeshi, uhamisho huo ni wa kawaida na haupaswi kuhusishwa na uzushi ama sababu zozote,” alisema Mughuha.

Kutokana na mabadiliko hayo, Mkuu wa Wilaya ya  Buhigwe mkoani humo, Kanali Marko Gaguti, atakaimu nafasi hiyo hadi uteuzi mwingine utakapofanyika kujaza nafasi hiyo.

Kanali Martin Mkisi amedumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi tisa, akitokea makao makuu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), kutokana na uteuzi wa Rais, Dk. John Magufuli kwa wakuu wa wilaya 139 alioufanya Juni, mwaka jana.

Kumbe Wimbo ‘Niambie’ ilikuwa ni dedication ya Harmonize kwa Wolper.


Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize amedai idea ya wimbo wake mpya ‘Niambie’ ilitokana na aliyekuwa mpenzi wake, Jacqueline Wolper.

Muimbaji huyo amedai alishindwa kujua ni kwanini malkia huyo wa filamu alimpenda na kuwatosa wenye pesa zao ambao walikuwa wanamnyapia nyapia.

“Watu wamekuwa wakisema hatuendani mimi na Wolper huenda kwa sababu yeye alianza kuwa staa kabla yangu wakati huo nikiwa kijijini au hatuendani kwa kuwa yeye anapesa nyingi pengine kuliko mimi!,” Harmonize aliiambia Global TV Online.

Aliongeza, “Licha ya hayo yote lakini alikuwa ananionesha ananikubali, kunifanya niwe mwanaume hata kunitangaza kwenye jamiii. So sometime nikiwa nazi-appreciate zile treatment anazonipa kwa sababu wengi wenye pesa walikuwa wanamtaka. So nikapata idea ningependa siku moja uniambie kitu ambacho kinakufanya mimi unipende wakati mimi sina chochote,”

Wimbo huo mpya wa muimbaji huyo unapatikana kwenye mtandao wa www.wasafi.com.

Mourinho asema ""nitabaki Yuda namba moja""

Kocha wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amewajibu mashabiki wa Chelsea waliokuwa wakimuita ‘Yuda’ katika mechi ya Kombe la FA robo fainali dhidi ya Chelsea.

Sehemu moja ya mashabiki ilipiga kelele “F*** off Mourinho”, “Wewe si Special tena” na “ni Yuda” wakimaanisha msaliti katika ushindi wa Chelsea wa 1-0 katika uwanja wa Stamford Bridge.

Katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo Mourinho alijibu.

“Wanaweza kuniita chochote wapendacho. Hadi watakapopata meneja anayewashindia mataji manne ya Ligi ya Uingereza, Mimi ni nambari moja,” alisema Mourinho ambaye alitupiwa virago Chelsea msimu uliopita.

Katika vipindi viwili tofauti kama meneja wa Chelsea (2004-2007 na 2013-2015), Mourinho aliinoa Chelsea na kuipa mataji manne ya ligi, moja la FA na matatu ya Kombe la Ligi.

“Watakapopata mtu wa kuwapa mataji manne ya Ligi ya Uingereza, basi nitakuwa namba mbili. Lakini hadi sasa Yuda bado ni namba moja.”

Fake News: Watangazaji 9 wa TBC Waliotangaza Trump Amsifia Rais Magufuli, Wasimamishwa Kazi...!!



Wafanyakazi tisa wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wamechukuliwa hatua za kinidhamu kufuatia kurusha habari ya uongo kuhusu Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Wafanyakazi hao wamesimamishwa kazi kufuatia kurusha taarifa ya uongo kutoka tovuti ya fox-channel.com ambayo ilidai kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump  amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa utendaji wake mkubwa na vita dhidi ya dawa za kulevya. Tovuti halali ya Fox ni foxnews.com na si hiyo iliyonukuliwa na TBC.

Mkurugenzi wa TBC, Dk. Ayoub Riyoba amethibitisha kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa wafanyakazi hao kufuatia kosa hilo walilolifanya.

“Ni kweli watu kadhaa wamesimamishwa kazi kutokana na suala hilo.”

Wafanyakazi tisa waliosimamishwa ni pamoja na Elizabeth Mramba, Gabriel Zacharia, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhani Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai.

Rais Magufuli amepiga simu Clouds Tv na kuzungumza na mwanamuziki Diamond Platnumz baada kusikia maombi yake

Mwanamuziki Diamond Platnumz amepata nafasi ya kuzungumza na Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kuhusu hali ya wasanii ilivyo nchini na kuomba serikali kuunga mkono juhudi zao ili kulisaidia taifa kuongeza pato na wasanii kupata faida kutokana na kazi wanazozifanya.

Diamond amezungumza na Rais Magufuli kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa katika kituo cha runinga cha Clouds Tv na kumwambia wamekuwa wakifanya jitihada lakini zaidi wanahitaji msaada wa serikali ili wapate kipato ambacho kinastahili kutokana na kazi wanayoifanya.

“Mkuu tunaomba utusaidie sana maana tunaamini wewe ni Rais ambaye unatetea wanyonge na kusaidia wanyonge na sisi vijana wako kwa unyonge wetu tunaomba utusaidie kwasababu utakuwa umesaidia familia nyingi, sababu tuna familia tuna watoto na watu wengi tunategemea mziki ili tujiajiri na kuliingia pato taifa,

“Nafikiri tuweke system nzuri ya kulipa kodi kama mimi ni mlipa kodi mzuri na wengine nimeweka mfumo wafate hivyohivyo nafikiri itasaidia sana kuliingizia pato taifa na sisi pia atleast kupata riziki na kujenga nchi  yetu,”alisema Diamond.

Rais Magufuli alimjibu kwa kumpongeza kwa kazi nzuri ambayo wasanii wanaifanya ya kuitangaza Tanzania kimataifa, “Asante sana nimekusikia lakini pia nakupongeza na uzidi kuitangaza Tanzania katika muziki na hata wasanii wengine hata wale wanaoigiza nawapenda kama shilawadu na kadhalika.”

Lakini awali akizungumza na mtangazaji wa kipindi hicho Babbie Kabae alisema kuwa amepanga kukutana na wasanii ili kusikiliza changamoto zinazowakabili,“Maombi yake nimeyasikia nimepanga siku moja kukutana na hao wasanii ili tuone jinsi gani tunawasadia.”
Credit ..Mpekuzi.

 

Gallery

Popular Posts

About Us