KINGAZI BLOG: 10/30/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday, 30 October 2016

MPYA: BODI YA MIKOPO KUANZA TENA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO KWA WANAOKATA RUFAA NA WALIOKOSA.

Bodi ya mikopo ya vyuo vikuu imetangaza kuanza kupokea tena maombi ya mikopo kwa wanafunzi waliokosa mna wale wanaokata rufaa, akizungumzana waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya mikopo ya vyuo vikuu ABDULRAZAQ BADRU, amesema bodi hiyo itaanza awamu nyingine ya kupokea maombi ya mikopo kwa ili wote walio na vigezo vya kupata mkopo wapate na waweze kusoma vizuri.
Abdul-Razaq Badru, Mkurugenzi wa HESLB
Abdul-Razaq Badru, mkurugenzi wa HESLB akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO jijini Dar es Salaam amewambia waandishi wa habari kuwa bodi hiyo lazima ipitie upya majina ya wanafunzi waliopewa mikopo hata kama wapo katika mwaka wao wa mwisho wa masomo.

Pia akaongeza kwa kusema Wote walioomba na kupitishwa na bodi kupta mkopo tayari wamekwisha pewa mikopo yao na fedha hizo tayari zmekwisha wekwa kwenye akaunti za vyuo husika, 
Sambamba na hilo amesisitiza wale wote wanaonufaika na mikopo hasa wale wanaoendelea na masomo wanatakiwa kujaza dodoso au form ya uhakiki wa mnufaika, na Zoezi hilo la uhakiki wa wanufaika litaanza mwanzoni mwa mwezi novemba mwaka huu na litachukua muda wa siku 30 
Wanufaika wote wanatakiwa kuingia kwenye akaunti binafsi za HESLB ili kuweza kujaza na kuweka taarifa sahihi 
"HESLB tutahakiki upya wanufaikaji wa mikopo waliopo mwaka wa pili, tatu na hata wale wa mwaka wa nne ili kuondoa kila asiye na sifa na kwa wale wa mwaka wa kwanza waliokosa mikopo na wanadhani wanazo sifa wakate rufaa  kuanzia Novemba Mosi,” amesema Badru."

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YATOKEA,BASI SAFARI NJEMA LATEKETEA KWA MOTO KIMARA STOP OVER LEO BAADA YA KUGONGANA NA LORI USO KWA USO, PICHA NA VIDEO.





Basi lenye namba za usajili T990 AQF la kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kuja jijini Dar, limeteketea kwa Moto maeneo ya Kimara Stop Over-Suka,mara baada ya kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake za usajili hazikujulikana mara moja),jioni ya leo,Inaelezwa kuwa mali zote zilikowemo katika basi vimeteketea kabisa kwa moto,hali ya abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo tutawaleta taarifa kamili itakayotolewa na Jeshi la Polisi.
 Pichani Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili kuwaka moto. 
 Baadhi ya mashuhuda wakishuhudia tukio hilo lilivyokuwa.
 Gari la zima moto likiwa eneo la tukio kuuzima moto huo.
 Baadhi ya vijana wasio waaminifu walivamia eneo hilo la ajali na kuanza.
 Pichani Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili kuwaka moto. 

NILAMBE HUMO HUMO ===7

chombezo: nilambe humohumo
MTUNZI: HUSSEIN WAMAYWA
SEHEMU YA SABA
Nikijua mtego ndio unakaribia kufyatuka, sikumgusa!
Badala yake nilikwapua mwanamke mwingine nikatokomea nae migombani na kwenda kuneng’eneka nae, Nikamuacha Havijawa pale pale uwanjani. Mwanamke niliyemchukua hakuwa haba, alikuwa bora kwa kila hali.
Nikamuuliza kama ameolewa akasema bado, nikamuomba niwe mgeni wake kwa siku hiyo akakubali. Sikurudi uwanjani nikaenda kulala kwa mwanamke huyu mpya.
Asubuhi na mapema nilikuwa ndani ya gari nikielekea Daresalaam.
Ukawa mwisho wa kuwasiliana na Havijawa. Ikawa mwanzo wa mawasiliano na yule mpiga ngoma, nikaendelea kuhudhuria katika ngoma hata iwe wapi. Ni hapa nilipojua ni kwanini ngoma inapendwa sana uzaramuni.
Nami nikawa mfuasi mtiifu na mkamilifu wa ngoma!.
* * *
Naam, niliyainua tena macho yangu na kuutazama ubao wa matangazo No! Ubao wa matokeo. Nao haukunidanganya. Uliniambia tena kama unaonidhihaki. Kwamba nilipata alama F katika mitihani yangu ya mwisho pale chuoni.
Kwa sekunde kadhaa niliduwaa nikiwa siuoni ubao huo wa matokeo sawasawa. Akilini niliona kama kitu cha kawaida huku nikitabasamu kiwazanga kama niliyefurahishwa na matokeo yale. Wenzangu wachache niliofeli pamoja nao walikuwa wakilia. Wengine wakisikitika.
Wachache waliokuwa na roho ya paka wakaniangalia kwa mshangao.
‘’He Ibra anacheka!” Mmoja aliropoka ’’Wakati amefeli vibaya!” mwingine akadakia ‘’Lazima kuna analotarajia sio bure!” Mwingine akahitimisha.
Shamsa alikuwa miongoni mwa wanafunzi wachache waliofanya vizuri sana kiasi cha kupata A+. Wakati huu alikuwa hajiwezi kwa furaha machozi yakimtoka hovyo asiyaamini macho yake.
Wengine wakashangaa, aliyefeli anacheka, aliefaulu analia! Akimu alikuwa mbali sana, alikuwa na alama za wastani hazikuwa mbaya wala nzuri sana alipata grade C, yeye pia alikuwa akisononeka. Alitaka apate grade A!
Wabongo kwa kutoridhika? Mie niliyepata mswaki je?
Kadiri muda ulivyokuwa ukipita ndivyo nami nilivyokuwa nikipambazukiwa na ukweli, ukweli kwamba nimefeli vibaya! Ukweli kwamba miaka yangu mitatu pale chuoni ilikuwa bure, bure kabisa! Bure kwa maana ya kwenda na maji.
Nikawafikiria wazazi wangu waliopoteza mamilioni kwa malaki ya shilingi kunisomesha mwana wao. Kunisomesha nisihangaike na maisha kwa namna itakayoikwaza mioyo yao na kuwasononesha.
Kunisomesha ili nije niwatunze wao mara nguvu zitakapowaishia. Kunisomesha ili nije nitimize wajibu wangu kama binadamu wa kuisaidia jamii kupata unafuu katika sekta fulani. Kunisomesha… kunisomesha…! Niliendelea kutafakari pasipo kupata majibu.
Sikuwa nimewahi kufeli kwa mtindo huu toka nilipoanza elimu ya Awali, chekechea kwa maana halisi. Nikafuatia ile ya msingi hadi sekondari! Lakini leo… My God nitawaambia nini wazazi wangu?
Chozi la uchungu likateleza na kuanguka shavuni.
Roho na moyo vikaniuma kwa pamoja na kuufanya mwili wangu kuwa handaki la mateso kwa muda.
Nikiwa katika hali hii mwili ulitikisika na kutetemeka kwa nguvu wakati mawimbi ya kilio yakitoka kifuani mwangu na kunifanya nitoe mlio mithili ya gari ndogo yenye mzigo mkubwa inayopanda mlima na kushindwa kuumaliza.
Nililia na kulia na kulia! ’’Hatimae mapenzi yameniliza!” Niliwaza kwa uchungu nikiendelea kulia kwa nguvu.
‘’Ibra… Ibra… Ibra!’’
Sauti nzuri nzuri ikapasua anga, ikakizidi kilio changu na kuzifikia mboni za masikio yangu, mwito huu ulienda sambamba na mtikiso wa bega langu la kushoto. Sio siri ulikuwa mguso wa faraja. Nikainua uso na kumwangalia huyu aliyeingia chumbani kwangu bila hodi na kujipa mamlaka ya kuniita.
Ana kwa ana na Shamsa Nuhu, msichana wa maisha yangu!
”Pole!’’ Akaniambia kwa upole hali akinihurumia.
Huruma hii ikanifanya niangue kilio upya. Kilio cha nguvu, kilio cha simanzi. Nililia haswa, nililia mno. Ukweli nililia kweli kweli. Shamsa alijaribu kunibembeleza kwa muda mfupi akashindwa na kuniacha nilie. Nadhani aliniacha nafasi nimalize machungu niliyo nayo moyoni.
Na niliyamaliza.
Ilikuwa baadae sana niliponyamaza na kupitiwa na usingizi moja kwa moja. Shamsa aliniamsha jioni kabisa nikaamka! Alikuwa ndani ya vazi la usiku! Mwili wake mzuri ulionekana vizuri zaidi ndani ya vazi lile la kulalia.
‘’Amka ukaoge!’’ Akaniambia, nikamtazama kwa matamanio.
‘’Nataka nikutoe out!‘’ Akaongezea akitabasamu alipoona namwangalia tu pasipo kuinuka. Nikainuka, nikajinyoosha nikatwaa taulo, mswaki pamwe na sabuni na kuelekea bafuni.
Nilipotoka yeye, akaingia.
Akanichagulia nguo za kuvaa alipotoka bafuni, nae akavaa za kwake ambazo zilikuwa katika mkoba aliokuja nao. Tulipokuwa tayari akainua simu akabofya nambari kadhaa na kuipeleka sikioni. Akatamka neno moja tu
“Unaweza kuja!’’ Halafu akakata simu.
“Huyo ni Tax Drive ambae huwa anapaki gari lake hapo nje. Anaitwa Sudi’’ akaniambia. Nilimjua vizuri sana dereva huyo na nilikuwa nikimtumia sana mara kwa mara katika harakati zangu.
‘’Hutaki nikutoe out?’’ akaniuliza tena
‘’Hata kama sitaki unafikiri mbele yako nitakuwa na ubavu wa kukataa?’’ Nikamwambia kiutani, akatahayari na kunikabili tena.
‘’Ina maana hutaki?’’
‘’Hapana nataka sana, fursa hii nimeililia kitambo, nasikitika imekuja wakati mbaya! Wakati nimefeli!’’
‘’Usijali, kupanda na kushuka ni mojawapo ya safari za kimaisha, na ili mwanadamu ukamilike kabla hujaumbika haswa ni lazima uzipitie!‘’ Akatua. Nikamuuliza.
“Kuumbika haswa?! Unamaana gani?”
‘’Umesahau ule msemo?”
‘’Msemo gani?’’
‘’Hujafa hujaumbika!’’
‘’Naufahamu, kwa hiyo una maana kuumbika hasa ni kufa siyo?’’
‘’Yes!’’
Akajibu kwa bashasha. Nikatabasamu naye akatabasamu. Tukatengeneza njozi mbili adimu sana. Nilipotaka kusema kitu, akaangalia simu na kuniambia “Sudi yuko nje!”
‘’Mie nipo tayari!”
Akaukwapua mkoba wake toka pale sofani na kuutia begani, nikauchukua ufunguo wa chumba nikafunga mlango na kutoka.
‘’Kwa nini uliniuliza vile?’’ Nikamuuliza tukitoka nje.
‘’Vipi?!”
‘’Kwamba sitaki nikutoe out?’’
‘’Ulionekana kuwa na fikara sana Ibra. Sijui ulikuwa ukifikiria nini’’
Tukaifikia gari, tukaingia nyuma na kumsalimia Sudi, akawasha gari na kumuuliza Shamsa ‘’Haya niambie wapi Shamsa?’’
‘’Sudi bwana, unakuwa kama sio Born Town?! Nimekwambia sehemu yoyote tulivu!’’
“Sehemu tulivu ziko nyingi Shamsa! Kuna hoteli za kitalii, majumba ya kifahari na makumbusho, fukwe na n.k.!”
Ukazuka mjadala mfupi wa wapi atupeleke kutokea pale chang’ombe. Mjadala ambao ulimalizika kwa kuamuliwa atupeleke Coco beach. Hii ni kwa vile watu wangekuwa wachache sana kwa kuwa sio mwisho wa wiki. Hivyo iliaminika kule tungeweza kupata utulivu wa haja.
Tukaondoka.
Njiani nilimwambia Shamsa kuwa chanzo cha fikara zangu kule bwenini ni kumfikiria yeye, kwamba aliwezaje kuingia katika bweni la wanaume, akapata hadi ujasiri wa kubadili na kuvaa night dress achilia mbali kuniandalia maji kana kwamba nilikuwa mpenzi kama sio mume wake!
Shamsa akatabasamu kabla hajaniambia kuwa aliamua kuhamishia kambi katika chumba changu kwa muda kabla ya kunitoa out ili awe pamoja na mimi katika kipindi hiki kigumu.
Ilitosha! Alikuwa kama amenitonesha donda upya. Sura yangu ikasawijika na kupoteza nuru, alipoligundua hili akabadili mada haraka na niliporejea katika mood yangu, hatukuzungumza tena hadi tulipofika Coco Beach.
* * *
Image result for booty ebony’Katika mambo yote, hili sikulitarajia!’’ Shamsa alianza taratibu mara tu tulipochagua mahala patulivu pa’ kuketi pale Coco Beach na kufungua vinywaji vyetu vya kopo, ‘’Naapa hili sikulitarajia kabisa!”
Image result for booty ebony
Sauti yake ilikuwa ndogo yenye mchanganyiko wa mizizimo ya upendo wa dhati, huruma pamoja na uchungu. Machozi pia yalikuwa yakitafuta njia katika kingo za macho yake. Kwa kila hali alikuwa katika majonzi!
‘’Ibra niliyekuamini, Ibra niliyekuthamini, Ibra niliyekutegemea ukweli wa kukutegemea! Bado siamini dear! Kwanini ukafanya hivi? Enhe kwa nini Ibra?’’
Machozi yakamtoka.
Moyo wangu ukazizima kwa simanzi ingawa nilihisi nitakuwa namuumiza, nikajikakamua na kumuuliza
‘’Kufanya nini Shamsa?”
Akageuka na kuniangalia kwa mshangao, akafuta machozi na kuniuliza,
‘’Bado hujui tu? Hujui ulichofanya?! My God are you serious Ibra?”
‘’Sijui!” Nikajibu na kuapia
“Mungu mmoja sijui!! Ningejua nisingeuliza!” Nikatua.
Akaendelea kunitazama nikaona kama hanielewi, nikamsogelea na kumshika mkono kwa upendo uliotukuka, “Shamsa?” Nikaita taratibu nikingali nimeushikiria mkono wake
“Mimi ni miongoni mwa watu wachache sana wasiopenda kuwakwaza wenzao hasa wewe! Kuendelea kunilaumu kana kwamba nimeua bila kunieleza nilililolifanya, hunitendei haki Shamsa! Unaniweka katika kimuhemuhe ambacho kinanifanya nishindwe kujua nastahili kuwemo katika fungu gani kati ya wastaarabu na washenzi. Tafadhali niambie, niambie tu usihofu!’’
Shamsa akashusha pumzi na kuzivuta tena akauliza
“Kwa hiyo hujafanya kitu?’’
‘’Kitu gani? kwa kadiri ninavyokumbuka na kufahamu, sijafanya lolote la kumchukiza mtu yeyote! Na kama nilivyokwambia sipendi kumkwaza mtu!’’
‘’Kweli!?’’
‘’Kabisa!’’
‘’Sasa kule Chuoni ulikuwa unalia nini?”
Akili ikazibuka.
Macho yakazibuka pia na fahamu kufunguka. Masikio, moyo na hata vinyweleo vya mwili ambavyo wakati huu vilikuwa vikikiruhusu kijasho chembamba kupenya na kuteleza juu ya paji la uso wangu, juu ya mashavu, juu ya mikono, juu ya kila mahali, sasa nikaelewa! Kwamba Shamsa alikuwa akizungumzia kufeli kwangu.
ITAENDELEA 

PICHAZ+++ HUYU HAPA NDIYE MISS TANZANIA MWAKA 2016

  Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward akiwapungia Mkono wananchi wa Jiji la Mwanza mara baada ya kutangazwa Mshiindi wa Miss Tanzania 2016 Jijini Mwanza Leo wakati wa Kuhitishimisha hindano la Miss Tanzania 2016.
 Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward  katikati akiwa na mshindi wa pili na watatu Grace Malikita na Maria Peter mara baada ya Msindi wa shindano la Miss Tanzania 2016 kutangazwa Mshindi jijini Mwanza leo.

 Warembo wakionesha mavazi ya ubinifu.
Warembo waliokua wameingia hatua ya tano bora moja kwa moja kwa kushinda mataji mbalimbali.

Hivi ndivyo Wanawake wanavyosababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Image result for WANAWAKE NA NGUVU ZA KIUME

Kesi ya wanaume kupungukiwa nguvu za kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa ya kuongeza nguvu hizo kuwa maarufu na yenye mahitaji makubwa katika jamii.

Waganga wa kienyeji wamekuwa wakitumia dawa hiyo kama tiba ya msingi ya kuwavutia wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa wanaume wengi.

Hata hivyo, utafiti unaonesha kuwa wengi kati ya wanaume waliowahi kutumia dawa za asili na zile za hospitali kuondokana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hawakufanikiwa kupata tiba ya kudumu, matokeo yake wamegeuzwa watumwa wa kila wanapotaka kushiriki tendo lazima wabwie ‘kolezo’ la kuwasaidia kuamsha hisia zao.

Kwa wanaume ukosefu wa nguvu ni jambo linalouma na kuondoa kabisa ujasiri. Wengi kati yao wako tayari kutumia pesa na uwezo wao wote kuhakikisha kuwa heshima ya tendo la ndoa wanaimiliki daima.

Lakini, watafiti wa masuala ya mapenzi nikiwemo mimi, tumegundua kuwa wengi kati ya hao wanaolalamika kupungukiwa nguvu, hawafahamu chanzo cha matatizo na namna wanavyoweza kuepukana na kasoro hiyo.

Ushahidi uliopatikana kwa waathirika wa tatizo hili, unaonesha kuwa wanaume wanapokabili upungufu wa nguvu za kiume huishia kujuta na kujilaumu wenyewe bila kutazama upande wa pili wa washirika wao, namaanisha wanawake.

Zipo kesi za wanaume kujiua au kujinyofoa sehemu za siri kwa sababu ya kushindwa katika tendo. Hali hii inatoa picha kwamba mzigo wa lawama hujitwika wenyewe.

Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara anasema, wanawake huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo nami nalithibitisha kwa ushahidi wa kitaalamu ufuatao:

1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litamfanya aanze kupoteza nguvu za kiume taratibu.

Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwabia hawezi, bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”

2 : UJUZI
Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume husika kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.

Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo.Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.

3: USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi ni muhimu sana katika mapenzi.

MAMBO 6 YAKUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

Image result for mahusiano ya mapenzi

Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu.  Wanawake wengi wanalalamika kuwa  hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao.

Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika,  muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala.  Wengi walioachana au kutalikiana nao  walipitia njia hii pia.

Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu.

Njia za kukusaidia

1.       kucheka pamoja

Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote.  Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu.  Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea.  Kama utaanza kujizoeza  hivi ukiwa nyumbani, taratibu  utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.

Image result for mahusiano ya mapenzi


2.       Jifunzeni kutiana moyo

Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake.  Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo.  Onyesha heshima katika vitu hivyo pia.  Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu.  Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye.  Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo.  Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua  na sisi pia.



3.       Jifunzeni kupenda kugusana

Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote.  Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala.  Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili.   Wengi wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu? au nidhamu mbaya? au  dhambi?

Kugusana ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.

Mguso huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa  tendo la ndoa katika  mahusiano yenu.


4.       Zungumzeni hisia zenu

Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano.  Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao.  Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu.  Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu.  Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu.  Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.


5.       Samehe na kubali kusamehewa

Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu.  Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia.  Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu.  Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu.  Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.


6.       Linda muonekano wa mpenzi wako

Mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko.  Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano  wetu lazima ume halisi na sio feki.  Vile tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi.  Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu.  Ukianza kupata  ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.

Lengo liwe kuvitafuta vile vyote  mpenzi wako alivyonavyo ambavyo  hukuza ukaribu wenu.  Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako.Image result for mahusiano ya mapenzi

MPYA: BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU TANZANIA IMETANGAZA RASMI KWA WANAFUNZI WOTE WALIOOMBA MKOPO KUANGALIA SASA MIKOPO WALIYOPANGIWA 2016/2017


Image result for bodi ya mikopo ya wanafunzi

>>>BONYEZA HAPA KUONA MAJINA YOTE YA MKOPO<<<
 N.B. 
NAMBA YAKO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE INAHITAJIKA 

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU SAUT 2016/2017,BOOM LARUDISHWA 8500 KWA SIKU.


SAUT

  





<<KUONA MAJINA YOTE 
BONYEZA HAPA>>

Habari kuu Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Octoba 30




 

Gallery

Popular Posts

About Us