KINGAZI BLOG: 03/21/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday, 21 March 2017

Job Opportunity at World Vision, Livelihood Specialist


Livelihood Specialist- Nzega Cluster
Reference :6658-16G12153
Location : Africa - Tanzania
Town/City : Arusha
Application Deadline Date : 03-Apr-17
Category : Food Security & Livelihood
Type :Fixed term, Full-time
International Role :No - Only National applicants will be considered.
Duration : 1-2 Years

Job Description

Purpose of the position:
To provide Leadership and technical support in the implementation of World Vision Tanzania Smallholder Farmer Strategy seeking to achieve Resilient livelihoods of small-holder farmers (agro-pastoralists and pastoralists) to better care and support their households by 2020. S/he will also communicate World Vision's Core values and demonstrate a quality of spiritual life.

Leadership
•    Spearhead rolling out the implementation of Resilient and Livelihood Technical program at the cluster/ ADP to enhance the livelihood security of poor and marginalized households.
•    Effectively follow-up and support Livelihood Facilitators in the Cluster/ Area Development Program (ADP) to perform their duties and take responsibility for performance management.
•    Ensure high quality project implementation and reporting of Resilient and Livelihood interventions, track the targets and shared in a timely manner with Team Leader – Resilient and Livelihood.
•    Provide technical support and leadership needed in Resilient and Livelihood portfolio including concept note for funding development, Project planning, technical document drafting.
•    Coordinate Identification of Resilient Livelihood values chains options in ADPs, and provide guidance on up scaling of innovative technologies to improve food security and income of Smallholder farmers.
•    Ensuring that in all Resilient Livelihood interventions programming, there will be an intentional inclusion of the most vulnerable in the community.
•    In collaboration with DME officer, follow up a monitoring system designed to capture Key Performance Indicator of livelihood programming, and develop a reactive or preventive mitigation response to the identified issues.
•    In collaboration with Cluster Manager develop training modules for capacity building of community groups, and interns of WVT Internship program in the area of livelihoods to improve community livelihoods security.
•    Guide the documentation of livelihood promising practices and share them with partners.
•    Facilitate WVT/GAFCo/VFT integration activities in the Cluster.
•    In collaboration with Cluster Manager prepare and deliver a comprehensive livelihood capacity building curriculum for ADP/Savings Groups and Producer Groups to improve their livelihood strategies.
•    In collaboration with Cluster Manager, maintain close working relationships with various partners at National and District levels aimed at improving the livelihood of poor households especially those of children and vulnerable groups and World Vision Visibility.
•    Prepare weekly, monthly, quarterly and annual activity reports for the supervisor.
Minimum Qualification required:
•    Should have a university degree in Agricultural economics, Agriculture, Rural Development Natural Resources Management, Management or related field.
•    Possession of a Master’s degree in these fields is an added advantage

Other Competencies/Attributes:
•    Must be a committed Christian, able to stand above denominational diversities.
•    Perform other duties as required.

Experience:
•    Should have a minimum of 4 years’ experience in development work with an NGO operating at the National level
•    Prior experience with World Vision an added advantage

Technical Skills & Abilities:
•    Should have been involved in Project Design and Implementation, monitoring, evaluation and reporting.
•    Thorough understanding and experience in Resilient and Livelihood concepts.
•    Prior experience with participatory livelihoods asset inventory and development at the community level
•    Thorough understanding and Experience in quantitative and qualitative data collection methods, including sampling, survey design and data analysis
•    Understanding of a cluster level planning and design of projects
•    Experience in the application of Results-Based Management framework
•    Ability to communicate cross-culturally and be cross-culturally sensitive
•    Computer and Internet skills including word processing, graphic presentation and spreadsheet programs required.
•    Travel is required.

TO APPLY CLICK HERE


SHARE NA MARAFIKI ZAKO

MPYA : Isome Barua Aliyoandika TUNDU LISSU kwa Magufuli Kuhusu Sakata la Makonda

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amemuandikia waraka, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli.

Hii ni barua ya kwanza ya Tundu Lissu kama Rais wa TLS kwenda kwa Rais, ikumbukwe kuwa Rais hapo jana alisema hataki kuambiwa nini cha kufanya kwa sababu yeye ni Rais anayejiamini, na hapangiwi nini cha kufanya. Tusubiri tuone Matokeo ya hili

SOMA HII!! Mwanamke akikwambia haya ujue huyo siyo mkweli, hafai.

Nimefanya 'kautafiti kangu kasicho rasmi' nikagundua maneno haya kutoka kwa wanawake wakikwambia usiwaamini hata kidogo..
Karibuni mchangie mada, ukiwa na la kuongezea ongezea ili tujifunze.

1.Ungejua wala sina haraka ya kuolewa!
Hakuna mwanamke ambaye yuko tayari kuona umri unamkimbia, ameshahudhuria harusi za marafiki zake, pengine ameshaliona mpaka gauni litakalompendeza harusini halafu eti akuambie hana haraka ya kuolewa!

2.Ngoja Nikavae, nipe dakika tano tu!Ukiambiwa hivi, basi Kama hujanywa soda muda mrefu huu ndo muda muafaka! Tafuta sehemu yenye utulivu upate kinywaji chako maana hizo dakika tano ni dakika hamsini!

3.Wala sioni wivu ukiwa unawaangalia wanawake wengine
Akikuambia hivi, anataka tu akuonyeshe ni jinsi gani amekua kiakili, na ni mtu muelewa saana.. lakini moyoni mwake anatamani kukupiga makofi unapomuangalia msichana mwingine huku akijiuliza moyoni,  kwani huyo anaemuangalia amenishinda nini?

4.Hata kama unapata mshahara mdogo, mi nimeridhika kabisa.. (mmmh Kweli?)

5.Mbona dada yako hajaja kututembelea muda mrefu? Nime”mmiss” sana! Mara chache sana kutakuwepo na  upendo kati ya mpenzi wako na dada yako au hata mama. Kwa mwanamke ni  bora umletee  wadogo zako wa kiume kumi nyumbani atawalea ila sio dada yako mmoja!

6.Napenda kila kitu kutoka kwako
Unadanganywa!  lazima kuna kitu angalau kimoja angependa ubadilike au anapanga kukubadilisha.. mara nyingine atataka hata uwe kama Yule kaka anayemuona kwenye tamthilia!

7.Sihitaji kuwa na mwanaume kwa sasa.Niko “busy” sana! Au utaambiwa nimeumizwa sana hata kama yeye ndiye mgonvi namba moja!

8.Wala sina njaa, mi nikila kidogo tu nashiba!

9.Niko sawa tu, hamna shida! Ukweli ni kwamba anataka uongeze juhudi kumbembeleza ili akuambie ni nini shida.

10.Simuambii yeyote! Hapo imekula kwako usitegemee atakaa nalo moyoni!

Gwajima Afunguka Mengine Mapya Aliyofanyiwa Polisi..Adai Walitaka Kumchoma Sindano!!


Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima ameieleza mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuwa ofisa wa jeshi la polisi alitaka kumchoma sindano bila ridhaa yake wakati alipolazwa kwenye hospitali ya polisi Oysterbay.

Askofu Gwajima ameyasema hayo wakati akiongozwa na wakili wake Peter Kibatala alipokuwa akitoa utetezi katika kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha inayomkabili na wenzake watatu, mbele ya hakimu mkazi mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Mbali ya Gwajima washtakiwa wengine ni mfanyabiashara anayedaiwa kuwa mlinzi wake, George Mzava, msaidizi wake, Yekonia Bihagaze na mchungaji Georgey Milulu ambao wanakabiliwa na kosa la kumiliki silaha isiyokuwa yao.

Katika utetezi wake, Gwajima alibainisha kuwa machi 27, 2015 anakumbuka alikuwa safarini kuelekea Arusha kwenye kikao cha maaskofu, ambapo aliondoka jijini Dar es Salaam, machi 26,2015.

Alieleza kuwa wakati alipokuwa njiani kuelekea Arusha aliona taarifa kwenye mtandao wa kijamii kuwa askofu Gwajima anatafutwa na jeshi la polisi.

Alieleza kuwa alishangaa kuiona taarifa hivyo, hivyo akafika hadi Arusha lakini alishindwa kushiriki katika mkutano huo badala yake alianza safari ya kurudi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kwenye kituo kikuu cha polisi kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuripoti.

Gwajima alibainisha kuwa alifika jijini Dar es Salaam ambapo alikwenda kituoni hapo na kukutana na ofisa mpelelezi wa kanda hiyo na baada ya muda alianza kuhojiwa, wakati mazungumzo yakiendelea kulikuwa na mtu aliyekaa nyuma yake akisoma gazeti ambapo kulikuwa na kitu kikimpalia.

Ameeleza kuwa kutokana na hatua hiyo, alianza kupiga kelele kwamba kuna kitu kinamkera ndipo ghafla akajikuta amepoteza fahamu na hakujua nini kilichoendelea, alipopata fahamu alijikuta yupo hospitali ya polisi Oysterbay ambapo wakati akiwa kitandani alimuona mtu aliyevalia mavazi ya kipolisi ambaye alikuwa na nyota tatu.

Ambaye alitaka kumchoma sindano lakini alikataa na kuanza kubishana naye kwamba yeye ana daktari wake katika hospitali ya TMJ hivyo apelekwe huko na kwamba wakati akiendelea kubishana na askari huyo ghafla alijikuta kapoteza fahamu na alipozinduka alijikuta yupo hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.

Baada ya kueleza hayo, hakimu Mkeha ameahirisha kesi hiyo hadi aprili 10 hadi 11, mwaka huu itaendelea kusikiliza ushahidi wa kesi hiyo. 

Magufuli amkingia kifua Makonda...Habari kuu Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 21.



Pichaz++ Usipitwe na hii ya Magufuli alivyopanda basi la mwendokasi akielekea ubungo jana.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 20 Machi, 2017 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam (Ubungo Interchange).

Sherehe za kuweka jiwe la msingi katika mradi huo zimefanyika kando ya makutano ya barabara hizo na kuhudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia Mhe. Dkt. Jim Yong Kim, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mawaziri wa Tanzania, Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigala King na viongozi wengine wa Wizara na Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Bw. Paul Makonda.

Ujenzi wa barabara hizo utagharimu Shilingi Bilioni 188.71 ambapo kati yake Shilingi Bilioni 186.725 ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia na Shilingi Bilioni 1.985 zitatolewa na Serikali ya Tanzania, na mradi huo utakaochukua muda wa miezi 30 unatekelezwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza katika sherehe hizo, Rais wa Benki ya Dunia Mhe. Dkt. Jim Yong Kim amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya katika uongozi wake iliyomjengea sifa nzuri duniani kote.

“Nilivutiwa na hotuba za Mwalimu Julius Nyerere hasa aliposemabila uhuru hakuna maendeleo na bila maendeleo utapoteza uhuru wako, kwa maana hiyo Nyerere aliona kuwa maendeleo ndio njia pekee ya kulifanya Taifa kuwa imara na kujitawala na kuwawezesha watu kujua mwelekeo wa maisha yao.

“Nipo hapa kwa sababu viongozi wengi wa Afrika na wengine wengi duniani, wameniambia unatakiwa kwenda Tanzania, kuona kileanachofanya Rais Magufuli, ikiwemo kuzuia rushwa na kujenga uchumi wa nchi ambayo ni huru” amesema Dkt. Jim Yong Kim.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuunga mkono juhudi za maendeleo za Tanzania na ameahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na benki hiyo kwa kuendelea kukopa na kulipa madeni yake.

Mhe. Dkt. Magufuli amesema ataendelea kutekeleza ahadi yake ya kukabiliana na msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam ambapo pamoja na kujengwa kwa barabara za juu katika makutano ya Ubungo, maandalizi yanaendelea kujenga njia ya barabara 6 za kuanzia Dar es Salaam hadi Chalinze Mkoani Pwani, kujenga kilometa 305 za reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro, kujenga bandari kavu katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani na kujenga daraja la Salenda litakalounganisha Agha Khan na Coco Beach kupitia baharini.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla kuunga mkono juhudi hizo nzuri na muhimu kwa maendeleo, na kuachana na ushabiki usio na manufaa unaochochewa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari.

Amewataka wakandarasi watakaojenga barabara za juu katika makutano ya Ubungo kuharakisha ujenzi huo, ikibidi kumaliza kabla ya miezi 30 na pia amewasihi wananchi watakaopata kazi katika mradi huo kuwa waaminifu na waadilifu wakati wote wa ujenzi.

“Tujielekeze katika masuala ya msingi na ya maendeleo, tuache kujielekeza katika udaku, tunapoteza muda mwingi katika masuala ambayo yanatupotezea muda” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Pamoja na kuweka jiwe la msingi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mhe. Dkt. Jim Yong Kim wameshuhudia utiaji saini wa miradi 3 itakayopatiwa mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia ambayo ni mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam, mradi wa kusambaza maji safi, mazingira na ukusanyaji wa maji taka, na mradi wa uendelezaji wa miji ya Arusha, Dodoma, Kigoma, Mbeya, Tanga, Mwanza na Mtwara, yote ikiwa na thamani ya Jumla ya Shilingi Trilioni 1.74.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na mkopo wa Shilingi Trilioni 1.74 Tanzania inatarajia kunufaika na mkopo mwingine wa Shilingi Trilioni 2.79 zitakazotumika katika miradi ya endelezaji bandari ya Dar es Salaam, umeme, gesi, kilimo, afya na elimu kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakiwa wamepanda basi la mwendokasi huku wakibadilishana mawazo wakielekea Ubungo kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipanda basi la DART-Maarufu kama Mabasi ya Mwendokasi katika eneo la Kivukoni wakati akielekea Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kabla ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilia Prof. Makame Mbarawa kwa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim walipokwenda kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi alipokwenda kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017


Baadhi ya wananchi wakisikiliza hotuba ya Rais alipokwenda kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakifungua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakikata utepe ikiwa ni ishara ya kuanza kwa ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuzindua mitambo na magari yatakayotumika katika ujenzi wa makutano ya barabara za juu za Ubungo (Ubungo interchange) jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakipata maelezo jinsi barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo zitakavyokuwa baada ya kujengwa March 20,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye Makutano ya Ubungo March 20,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye Makutano ya Ubungo March 20,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakiwapungia wananchi mkono wakati wakielekea kuweka jiwe la msingi ujenzi wa makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kabla ya kwenda kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli katika mazunzumzo Ikulu jijini Dar es salaam na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kabla ya kwenda kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017 

 

Gallery

Popular Posts

About Us