Saturday, 3 September 2016
ALIYEAMUA KUMUUZA MKEWE ANUNUE iPHONE 6
Daktari Apatikana na Video ya Watu Wakishiriki Ngono na Nyoka
UINGEREZA: Daktari mmoja nchini Uingereza amepatikana na hatia ya kuwa na video za ngono, ikiwemo moja ya mwanamume akishiriki ngono na nyoka.
Cyprian Okoro, 55, kutoka Kusini Magharibi mwa London alipatikana na makosa matano ya kuwa na video za ngono ya kuchukiza zaidi pamoja na picha moja ya utupu ya mtoto.
Kwenye moja ya video hizo, kulikuwa na wanawake wakishiriki ngono na mbwa na nyingine ya mwanamke akifanya ngono na farasi.
Mshtakiwa, ambaye anatoka Cameron Place, Streatham, amekanusha mashtaka hayo na amepewa dhamana lakini atahukumiwa tarehe 30 Septemba.
Lakini, baada ya kutafakari kuhusu kesi yake kwa chini ya siku moja, baraza la wazee wa mahakama lilimpata na hatia kuhusia na mashtaka yote ila lile la watu ksuhiriki ngono na mbwa.
Mahakama iliambiwa kwamba Okoro alikuwa na picha na video hizo kwenye simu yake baada ya kuzipokea kupitia WhatsApp.
Ni mara ya pili kwa Okoro kupatikana na hatia wakati mnamo mwaka 2014, alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi 18 baada ya mwanamke kuwasilisha tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi yake.
Okoro alihitimu kama daktari Lagos, Nigeria, mwaka 1986.
TCU Yatangaza Kuanza Udahili Awamu ya PILI Kwa Wanafunzi wanaojiunga Vyuo Vikuu Ambao Wamekosa Nafasi Kwenye Awamu ya Kwanza
MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI KWENYE HABARI ZA KITAIFA NA UDAKU NA MICHEZO
Bodi ya Mikopo Kuwapa mkopo kwa Waombaji wote mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema hayo juzi mjini hapa wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa watu watano waliorejesha mkopo wa elimu ya juu kwa mkupuo na kwa hiari.
Badru alisema idadi ya walioomba mkopo mwaka huu ni wanafunzi 88,000 ambao bodi itahakikisha wale wote waliokidhi vigezo, wanapatiwa fedha kwa ajili ya elimu ya juu.
Mkurugenzi huyo ambaye amehimiza walionufaika na mikopo kulipa madeni yao, alisema mwaka jana, wanafunzi waliokopeshwa ni 55,000.
Kuhusu waliopewa vyeti ikiwa ni hatua ya kuwatambua, ni pamoja na mfanyakazi wa VETA Shinyanga, Richard Jafu aliyerejesha kwa mkupuo Sh 14,749,950 na Francis Mwilafi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo aliyelipa Sh 15,115,200.
Wengine ni Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga aliyerejesha Sh 255,000; Profesa Peter Msoffe ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM) aliyerejesha Sh 1,430,749.
Mwingine ni Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa ambaye kiasi alichorejesha hakikutajwa ingawa mkurugenzi mtendaji wa HESLB, alisema amerejesha kiasi kikubwa kwa mkupuo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao walisisitiza umuhimu wa wanufaika wa mikopo kuirejesha kwa hiari ili kuiwezesha bodi hiyo kukopesha wanafunzi wengine.
Mbunge wa Biharamulo, Mukasa alishauri bodi hiyo kuangalia uwezekano wa kurekebisha vigezo kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi watokao maeneo ya pembezoni kunufaika na mikopo hiyo ya elimu. Kwa upande wake, Mbunge wa Vwawa, Hasunga alisisitiza wabunge wanaodaiwa warejeshe mkopo kwa mkupuo.
HIZI HAPA SIFA PEKEE ZA MWANAMKE WA KUMUOA NA KUDUMU NAYE KATIKA MAISHA
Daraja la Kioo China Lasitishwa Kutumika Baada ya Wiki 2
Daraja la kioo ambalo limeelezwa kuwa liko juu zaidi liliziduliwa hivi karibuni nchini China ambapo lina urefu wa zaidi ya futi 1400, upana wa futi 20 na karibu futi 1000 kutoka kwenye ardhi na imeripotiwa kuwa kioo chake ni imara zaidi mara 25 zaidi ya kioo cha dirisha.
Daraja hilo la wapita kwa miguu lijulikanalo kwa jina la daraja la Zhangjiajie lilizinduliwa August 20 mwaka huu ambapo lina uwezo wa kuchukua watu hadi 800 kwa wakati mmoja. Imeelezwa kuwa daraja hilo limekuwa likitumika kwa shughuli mbalimbali za kiutalii.
Daraja hilo limelazimika kufungwa ili kufanyiwa maboresho ya ndani baada ya idadi kubwa ya watalii waliokusanyika kutembelea kweye daraja hilo. Daraja hilo ambalo liko Kusini mwa China liligharimu dola million 48 kujengwa, na lilifunguliwa August 20 na limesitishwa huduma zake leo.
Msemaji wa kivutio hicho aliiambia MailOnline kuwa daraja lilitengenezwa ili kuweza kuchukua kiwango cha juu cha watu ambao ni 800 kwa wakati mmoja, na limepokea takribani watu 10,000 ambao ni watalii tangu lifunguliwe, msemaji huyo alisisitiza kuwa ni sehemu ya kioo ya daraja ni salama.