Wednesday, 10 May 2017
MSANII Nikki Aiweka Sawa Kauli yake ya Uchunguzi wa Ajali iliyoua 32
Msanii wa muziki wa hip hop, Nikki wa Pili amefafanua kauli yake ya uchunguzi ufanyike katika ajali iliyoua 32 Arusha baada ya kudai kuna baadhi ya watu wameshindwa kuielewa kauli yake hiyo.
Rapa huyo amedai kuwa ni jambo la utu kama tatizo litajulikana na kufanyiwa marekebisho kwa vitendo na siyo kuhukumu watu au kumtafuta mchawi nani kipindi hiki, huku akitaka asinukuliwe vibaya.
“Nasikitika watu wameninukuu vibaya sana niliposema uchunguzi ufanyike wengine wameniponda lakini sijachukia kwani hawajanielewa,” Nikki alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio. “Uchunguzi ukifanyika sina maana ya kumhukumu mtu mmoja hapana bali tuweze kujifunza. Watu wengi waliokusanyika uwanjani kuaga walimu na wanafunzi wameonyesha utu lakini pasipo tukio hili kuchunguzwa utu wao utakua hauna thaani kwani matatizo haya yatajirudia mara kwa mara,”
Aliongeza, “Inawezekana kuwa mikanda ilikosekana kwenye ‘bus’ walilokuwa wamepanda wanafunzi na walimu wa Lucky Vicent Academy au mwendo haukuwa mzuri lakini tatizo linaweza kuwa hali ya hewa hivi ni vitu ambavyo vikifanyiwa uchunguzi vinaweza kutukumbusha tabia zetu na tutajifunza wakati mwingine,”
Katika hatua nyingine Nikki amewaona watu wanaoweka mitandaoni picha za ajali na kusema kuwa ni vitendo vya udhalilishaji na kuongeza kwamba zipo njia nyingi za kutoa taarifa kwenye mitandao lakini siyo kwa ku- ‘share’ picha za ajali ambazo watu wanakuwa wameumia vibaya.
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watakiwa kuzingatia mipaka ya madaraka yao
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kuzingatia mipaka ya madaraka yao na kuhakikisha hatua wanazochukua katika utendaji wao zinafuata Sheria ,Kanuni na Taratibu katika Utumishi wa Umma.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana Mei 9, 2017 wakati akifungua mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
Majaliwa alisema kuwa viongozi hao wanatakiwa kusimamia kikamilifu nidhamu katika Utumishi wa Umma kwa sababu wenyewe ni kioo katika kuishi kwa kuzingatia miiko ya Utumishi wa Umma.
Aidha, viongozi hao wametakiwa kutoa kipaumbelea katika kufuatilia na kusimamia kwa makini sekta za afya, kilimo, elimu na maji kwa kuwa ndizo zinazogusa zaidi maisha ya wananchi.
Pia, Majaliwa aliwaelekeza wasimamie na kuziba mianya yote ya upotevu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya na kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira katika maeneo yao.
Naye Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Suleiman Jafo alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha viongozi hao wanapata mafanikio makubwa katika utendaji wao wa kazi ili Serikali iweze kupata tija.
Gobless Lema Alifikisha Bungeni Sakata la Kukamatwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35.
Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda.
Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.
RAIS Zuma Kutua Nchini Leo!
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anatarajiwa kuwasili nchini leo (Jumatano) saa 10.00 jioni.
Rasi Zuma atakuwa nchini kwa ziara ya siku tatu kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais John Magufuli.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
Katika ziara hiyo Rais Zuma ataandamana na mawaziri sita pamoja na wafanyibiashara zaidi ya 80 kutoka Afrika Kusini.
Pia atashirikia mkutano wa wafanyabiashara, atazindua jengo Ubalozi wa Afrika Kusini na kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
FAHAMU Jinsi ya Kusafisha Pasi Yako Endapo Itachafuka kwa Kuunguza Nguo!
Mara nyingi tumekuwa tukipata shida juu ya kusafisha pasi zetu za umeme punde tu inapokuwa imeanza kiushika uchafu.
Pasi za umeme huchafuka kutokana na moto kuwa mwingi, kitendo kinachopelekea nguo, hasa za mpira, kunga’ang’ania na kuharibu pasi kwa kuifanya iwe ina mabaki ya nguo yaliosababishwa na moto wa pasi ya kunyooshea kuwa mkubwa.
Tumesikia na pengine tumeshuhudia tukitumia steel wire, (dodoki la kusugulia sufuria), kusafishia pasi zetu tukiamini ni njia nzuri au kutumia kidonge cha panadol kusugulia pasi ili iwe safi. Huenda ikawa ni sahihi kwa wakati huo.
Leo nitakupatia njia rahisi za kuweza kusafisha pasi yako kwa kutumia vitu ambavyo ni rahisi, na vyepesi kuvipata, huku hata vingine vikipatikana nyumbani.
Chumvi:- Hii hutumika kama kiungo cha mboga hapo nyumbani lakini huleta matokeo mazuri ukitumia kusafisha pasi.
Jinsi ya kutumia chumvi;
Weka kiasi cha chumvi kuanzia kijiko kimoja cha chakula, kisha washa pasi yako na uwe unanyoosha pale ulipo weka chumvi, mpaka uchafu utoke. Ni kitendo kisicho zidi dakika 20.
Dawa ya meno:-Pakaa dawa ya meno yoyote kwenye pasi yako, kisha washa pasi, hakikisha pembeni kuna kitambaa chenye maji maji maana kitatumika kufuta pasi ikiwa kama njia ya kusafisha pasi hiyo.
Vinegar:- Hii hutumika kuweka katika kachumbari au salad. Chukua kitambaa kisha kimwagie vinegar na uwashe pasi mpaka ipate moto, kisha tumia kitambaa chenye maji maji ya vinegar kusafishia pasi yako.
Hakikisha pasi inasafishwa ikiwa na moto ili iweze kusafishika vizuri.
WAZIRI a Magufuli Atajwa kwenye Sakata la Vyeti Feki..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 10/5/2017.
MBUNGE: Diamond Anadaiwa Milioni 400 Na TRA.
Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia ameliambia Bunge kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platinumz’, anadaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zaidi ya Sh. milioni 400.
Mbunge huyo aliyasema hayo bungeni jana wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Amesema Wilaya ya Kinondoni ina wasanii wengi maarufu na wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana na mauzo ya kazi zao na kwamba Diamond Platinumz amemueleza kuwa kwa sasa anadaiwa kodi ya zaidi ya Sh. milioni 400.
Naiomba serikali kuhakikisha inaimarisha mapambano dhidi ya wizi wa kazi zao badala ya kutilia mkazo kwenye ukusanyaji wa kodi pekee kwani msanii huyo na wenzake wanaingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na kazi zao za sanaa,
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Walipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema suala hilo liko kwenye uchunguzi.
“Hilo liko kwenye hatua ambayo hatuwezi kulizungumzia kwenye vyombo vya habari. Liko katika ‘investigation’ (uchunguzi),” amesema
Gobless Lema Alifikisha Bungeni Sakata la Kukamatwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35.
Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda.
Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.