KINGAZI BLOG: 03/22/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Wednesday, 22 March 2017

ALICHOKISEMA ASKOFU GWAJIMA LEO ALIPOTEMBELEA CLOUDS MEDIA LEO TAR 22 ,





Askofu wa kanisa la Ufufuo na uzima Joseph Gwajima 

Dar es Salaam. Askofu wa kanisa la Ufufuo na uzima Joseph Gwajima amezungumza na waandishi wa habari  wa Clouds Media Group  na kusema kilichomfanya afike katika ofisi hizo ni kutoa pole kwa kuwa yeye ni sehemu ya sababu za uvamizi huo.

“Isingekuwa busara watu wavamiwe na mimi ni mhusika mkuu halafu nisije kutoa pole,” alisema

Hatua ya Gwajima imekuja baada ya tukio la kituo hicho kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiwa na polisi wenye silaha.

Gwajima amewasilia saa 4:00 asubuhi akiwa na msafara wa magari zaidi ya manne na walinzi wake takribani 30 na alipofika alipokelewa na Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na kufanya mazungumzo na waandishi wa habari  na baadaye na uongozi wa kituo hicho.

Amewataka Clouds kuendelea na kazi zao za kawaida na kutaka suala hilo lisichukuliwe kisiasa huku akikisitiza kuwa Mkuu wa mkoa alikosea.

Kimenukaa..!!Vyombo vya Habari vyamfungia Makonda,vyakubalians Kutoonekana Kwenye Tv,Magazeti na Kusikika Redioni.


Jukwaa la Wahariri Tanzania limelaani kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar na kutangaza atakayeshirikiana naye, *hawatarusha matangazo yake.*

"Utekelezaji agizo la kutokufanya kazi na RC Dar unaanza mara moja kwa vyombo vyote vya habari nchini, uamuzi huu waungwa mkono na UTPC"-TEF.


kwa upande mwingine tena 

RC Makonda amefunguliwa Mashtaka matano

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob amemfungulia mashitaka matano Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambayo ameyawasilisha kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.


Mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya Makonda ni pamoja na kughushi vyeti, kupokea zawadi bila kutangaza, jambo ambalo ni kinyume na sheria za utumishi wa umma, kujipatia mali kutoka kwa watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya, kuwadhalilisha watu kwa kuwataja kwenye tuhuma za madawa ya kulevya bila kuwa na vielelezo na kutumia madaraka vibaya.

Hatua hiyo ya meya Jacob, imekuja siku chache baada ya mkuu huyo wa mkoa, kudaiwa kuvamia kwenye ofisi za Clouds Media, kushinikiza kipindi kilichorekodiwa kikiwa na habari ya Mchungaji Josephat Gwajima, kirushwe hewani wakati kipindi cha Shilawadu kikiendelea.

Kitendo hicho kilimlazimu Waziri Nape Nnauye, mwenye dhamana ya kuwalinda waandishi wa habari, aunde tume maalum kuchunguza sakata hilo, ambayo ilipewa muda wa saa 24 kukamilisha kazi yake, lakini mpaka sasa bado ripoti yake haijatoka.

Jinsi ya Kuokoa Simu Iliyoingia Maji






Unaweza ukawa mwangalifu sana ila, bahati mbaya inatokea na simu zetu zinaingia maji.

Sasa, kwa kuwa simu zisizoingia maji bado ni ghali sana, simu yako ikiingia maji unaweza ukaiokoa kwa kufanya yafuatayo.

Itoe kwenye maji
Izime alafu ilaze kwenye kitambaa laini au tishu nzito alafu toa kava la nyuma na betri (kama unaweza kufungua simu yako)
Pia, ondoa SIM card, memory card, kava za simu uziache zikauke.
Kausha simu kwa ndani kwa kutumia kitambaa laini au tishu nzito. Hakikisha unaikausha haraka iwezekanavyo.
Weka simu ya ndani ya mfuko wa mchele kwa masaa 24. Mchele inanyonya maji.
Angalia kama eneo la kuchomeka chaji na headphone zimekauka. Kama bado, rudia  hatua 4 na 5.
Baada ya masaa 24, jaribu kuiwasha alafu angalia kama ina fanya kazi inavyotakiwa.

Kuna uwezekano kwamba utabidi kuipeleka kwa fundi

Ukiona kwamba haifanya kazi baada ya pitia hatua hizi, bora uipeleke kwa fundi. Ipeleke kwa wakala wa aina ya simu (au mtandao) ya simu yako au kwa duka la kutengeneza vifaa vya umeme linaloaminika.

Ila, kuzuia ni bora zaidi ya tiba. Kwa hiyo, nunua kava ya simu inayozuia maji kuingia kwenye simu.

Forbes: Hawa ndio Mabilionea 25 matajiri zaidi Afrika 2017

Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea mwaka 2017 iliyoandaliwa na jarida la Forbes.

Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni.
Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana.

Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.

Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni.

Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ndiye mabilionea wanawake pekee katika orodha hiyo mwaka huu.

Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.
Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020.

Dangote pia anamiliki hisa katika kampuni za chumvi, sukari na unga.
Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970. Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta. Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika.

Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017:

1. Aliko Dangote, Nigeria

    Utajiri: $12.2 bilioni

2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini

    Utajiri: $7 bilioni

3. Mike Adenuga, Nigeria

   Utajiri: $6.1 bilioni

4. Johann Rupert, Afrika Kusini

   Utajiri: $6.3 bilioni

5. Nassef Sawiris, Misri

   Utajiri: $6.2 bilioni

6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini

    Utajiri: $5.9 bilioni

7. Nathan Kirsch, Swaziland

    Utajiri: $3.9 bilioni

8. Naguib Sawiris, Misri

    Utajiri: $3.8 bilioni

9. Isabel dos Santos, Angola

    Utajiri: $3.1 bilioni

10. Issad Rebrab, Algeria

     Utajiri: $3 bilioni

11. Mohamed Mansour, Misri

      Utajiri: $2.7 bilioni

12. Koos Bekker, Afrika Kusini

      Utajiri: $2.1 bilioni

13. Allan Gray, Afrika Kusini

      Utajiri: $1.99 bilioni

14. Othman Benjelloun, Morocco

      Utajiri: $1.9 bilioni

15. Mohamed Al Fayed, Misri

      Utajiri: $1.82 bilioni

16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini

      Utajiri: $1.81 bilioni

17. Yasseen Mansour, Misri

      Utajiri: $1.76 bilioni

18. Folorunsho Alakija, Nigeria

      Utajiri: $1.61 bilioni

19. Aziz Akhannouch, Morocco

     Utajiri: $1.58 bilioni

20. Mohammed Dewji, Tanzania

      Utajiri: $1.4 bilioni

21. Stephen Saad, Afrika Kusini

      Utajiri: $1.21 bilioni

22. Youssef Mansour, Misri

      Utajiri: $1.15 bilioni

23. Onsi Sawiris, Misri

      Utajiri: $1.14 bilioni

24. Anas Sefrioui, Misri

     Utajiri: $1.06 bilioni

25. Jannie Mouton, Afrika Kusini

      Utajiri: $1 bilioni



Ishu ya kutaja majina ya mashoga waziri afunguka haya.Soma hapa👇👇



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla kwa mara ya kwanza ametoa sababu ya yeye kushindwa kuweka wazi orodha ya watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga)

Amesema hakuweza kuyataja hadharani majina hayo kwa kuwa alisikiliza ushauri aliopewa na jamii inayomzunguka.

“Mimi nashaurika, sikuweka majina hadharani kwa sababu nashaurika, listi ya watu ninayo na tunachukuwa hatua kimya kimya hili ni kosa la jinai na mtu anayekutwa na hatia anafungwa kifungo cha miaka 30 jela” Amesema Dkt. Kigwangalla

Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema, hayo wakati akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam.

Katika maadhimisho hayo Kigwangalla ameeleza kuwa kufanya mapenzi ya jinsia moja ni kosa kibaiolojia na hairuhusiwi mtu kuvutiwa na mtu wa jinsia yake.

Aidha, amesema katika sheria iliyotungwa mwaka 2012 ya kukazia adhabu ya mapenzi ya jinsia moja, kuna kipengele kinachotaka mtu achukuliwe hatua endapo ikithibitika amekaa mapozi yasiyoeleweka na ikabainika kuwa ni kwa lengo la mapenzi ya jinsia moja atafunguliwa mashtaka.

Mhe. Kigwangalla amewaonya wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kusisitiza kwamba serikali inawachukulia hatua kimya kimya

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 22

 

Gallery

Popular Posts

About Us