
WAKATI Dunia ikiwa imeaminishwa kuwa binadamu aliyeishi miaka mingi alikuwa anatoka nchini Italia na amefariki hivi karibuni, ameibuka mzee mmoja mkazi wa Kijiji cha Majengo, Kata ya Ihanda Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya ambaye ana miaka 127.
Mzee Ambilikile Mwanyaluke Panja, anaishi kitongoji cha Izyiga takribani kilomita mbili kutoka Kituo cha Mabasi cha Ihanda upande wa Magharibi, na hajiwezi kwa...