KINGAZI BLOG: 10/22/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 22 October 2016

DIAMOND: Nitaudhihirishia Ulimwengu Afrika Mashariki Kuna zaidi ya Wasanii


Diamond Platnumz yupo kwenye mission – ya kuuonesha ulimwengu kuwa Afrika Mashariki si ya mchezo mchezo kwenye muziki.
Akipost picha akifanya rehearsal na dancers wake kwenye ukumbi wa Ticket Pro jijini Johannesburg patakapofanyika tuzo hizo, Diamond ameandika, “Tafadhali sana ndugu zangu naomba kesho msikose kutazama tunzo za MTVMAMA…. kijana wenu nimepanga kuwadhihilishia Ulimwengu Kuwa Africa Mashariki kuna zaidi ya Wasanii

BREAKING NEWS: MSANII JB AJALI YA GARI

Mwigizaji wa filamu na mtayarishaji, Jacob Stephen ‘JB’ Ijumaa hii amenusurika kifo katika ajali ya gari.
Mwigizaji huyo ambaye hivi karibuni alikuwa mkoani Arusha katika shindano la Mama Shujaa, amewataka mashabiki wake kutambua kwamba anaendelea vizuri pamoja na wanzake ambao walikuwa kwenye gari hilo.
Asanteni wote mlionipa pole kwa ajali ya jana,” aliandika JB instagram. “Hakika Mungu ni Mwema, nipo poa mimi na wenzangu wote. Namshukuru sana Mungu.Thank you JESUS,”
Kwa sasa mwigizaji huyo anafanya vizuri na filamu yake, ‘Kalambati Lobo’.
Ajali za barabarani nchini Tanzania zinatajwa kuwa ni moja kati ya matukio ambayo yanasababisha vifo vingi nchini.

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA DIPLOMA-AFYA CHUO KIKUU UDOM BATCH 1 2016/2017.

Logo

KUONA MAJINA 

MPYA: HII HAPA TAARIFA MUHIMU TOKA TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU) KUHUSU AWAMU YA TAU YA UDAHILI.


tcu banner



                            
                               TCU - TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES

          TAARIFA KWA UMMA 

Tume ya vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa baada ya kukamilisha mchakato wa maombi ya waombaji wa vyuo vikuu, vyuo Vikuu Vishiriki na Taasisi za elimu ya juu kwa awamu ya Kwanza, ya Pili na ya Tatu, na matokeo ya waombaji wote waliofanikiwa kupata nafasi vyuoni kukamilika, Tume ya vyuo Vikuu imebaini kuwa bado kuna waombaji takribani 5,301 ambao bado wako kwenye mfumo na hawajakamilisha maombi yao. 

Tume imebaini pia kuwepo kwa idadi kubwa ya waombaji hasa wenye Stashahada ambao hawakuomba kabisa kutokana na matokeo yao ya mitihani kuchelewa kufika Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE). Awamu hii itawahusu:

         • Waombaji ambao bado wako ndani ya mfumo ambao hawajachaguliwa; 
         • Waombaji wapya ambao hawakuwahi kuomba awali;
 na 
        • Waombaji walio na sifa linganifu ambao hawakukamilisha taratibu za uombaji hapo awali Kutokana na sababu tajwa hapo juu, Tume inautangazia Umma kuwa itafungua Mfumo (CAS) kwa siku tatu tu, kuanzia Jumatatu tarehe 24 hadi Jumatano tarehe 26 Oktoba 2016 ili kuruhusu Makundi tajwa hapo juu kuingia kwenye mfumo kutuma maombi. Waombaji wa Awamu ya Nne wanasisitizwa kuzingatia yafuatayo: 

    • Kuhakikisha wanaomba kozi walizo na sifa stahiki 
    • Kuhakikisha wanakamilisha maombi yao kiufasaha

     • kuhakikisha wanajiridhisha na nafasi zilizopo kwa kuzingatia viwango vyao vya ufaulu. Aidha Tume inapenda kuujulisha Umma kwamba kozi zote zisizoonekana kwenye mfumo kwa sasa kuwa zimejaa. Baada ya tarehe tajwa hapo juu Tume itafunga rasmi zoezi la udahili kwa mwaka 2016/17 ili kuruhusu mchakato mingine ya Bodi ya Mikopo na Vyuo kuendelea. 



Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
21/10/2016


Download: Tekno – Diana (Official Video)

screen-shot-2016-10-21-at-15-37-28
screen-shot-2016-10-21-at-15-37-28As expected Tekno serves up  the official video to his latest single “Diana”.
The Triple MG superstar is ending the year on a very high note, same way he started the year. Dropping chart-topping singles and accompanying them with amazing visuals.
Enjoy!download-video-pink

PICHA++ MAZOEZI YA KIJESHI YALIYO MAGUMU ZAIDI ULIMWENGUNI



Mazoezi kwa wanajeshi ni kitu cha muhimu sana. Majeshi duniani huhakikisha kuwa wanawafunza wanajeshi wao mafunzo ya kuikakamavu kuweza kuwajenga kimwili na kiakili ili kuweza kupambana na hali tofauti tofauti wanazokumbana nazo wakiwa vitani au katika mazingira mengine.


Hizi hapa ni picha za majeshi tofauti tofauti duniani zikionyesha mazoezi magumu ambayo huwa wanfanya.


Wanajeshi wa China wakifanya mazoezi kwenye matope.
Mwanajeshi wa China akitambaa chini ya nyaya zinazowa waka moto wakati wa mazoezi.
Baada ya kutambaa na kufanya mazoezi kwenye moto, sasa wanafanya mazoezi ya viungo.
Mazoezi wakati mwingine huwa ni adhabu kwa wanajeshi. Hapa wanajeshi wa China wakitakiwa kubana pumzi na kuweka uso ndani ya maji.
Wanajeshi wa China wakifanya mazoezi yao kwenye barafu. Maeneo haya yana baridi ya hali ya juu.
Wanajeshi wa kitengo maalum cha kivita nchini Korea ya Kusini wakifanya mazoezi yao kwenye barafu.
Mwanajeshi wa nchini Canada akifanya mazoezi katika maji yenye barafu ikiwa ni mazoezi ya NATO.
Wanajeshi wa majini wa Marekani pamoja na Korea Kusini wakifanya mazoezi pamoja katika milima nchini Korea Kusini.
Wanajeshi wa Marekani wakiwa mazoezi Thailand. Katika kujifunza namna ya kushi katika hali ngumu, wanajeshi hao hulazimika kunywa damu ya Chatu.
Mwanajeshi wa Marekani wakiwa mazoezini ambapo anaruka kutoka kwenye helikopta akiwa na mbwa anayemfanyia mazoezi.
Wanajeshi nchini Japan wakifanya mazoezi ya kuning’ia kwenye helikopta kwa kutumia kamba.
Ili mwanajeshi ahitimishe mafunzo ya wiki tisa nchini Taiwan, unatakiwa kutembea umbali wa futi 150 juu ya mawe na miamba.
Belarus, ili uweze kuwa mmoja wa kundi la Red Berets, unatakiwa kupita kwenye vikwanza mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupita juu ya boma kwa kutembea.
Mmoja wa wanakundi wa Red Berets akiwa amefukiza kichwa chake ndani ya matofali yenye moto ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya kundi hilo kila mwaka.
Mazoezi ya uvumilivu ni muhimu sana, wanajeshi wa Israel kila mmoja analazimika kutembea umbali wa maili 43 (69 km) ikiwa ni sehemu ya mazoezi.
Wanajeshi wa Palestina wakifanya mazoezi ya kuruka angani.
Kundi la Kurdish YPG nchini Syria likifanya mazoezi katika viunzi vyenye moto
Wanajeshi wa Kishia nchini Iraq wakifanya maonyesho ya mazoezi yao wakati wa mahafali yao.
Wanajeshi wengine wa Kishia nchini Iraq ili kuweza kuhitimu mafunzo yao wanalazimika kutambaa kwenye mchanga/udongo jangwani.

Picha: Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete Alipokutana na Mtoto Aliyepewa Jina Lake Nchini Msumbiji.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Maputo nchini Msumbiji amepata nafasi ya kukutana na mtoto aliyepewa jina lake kama heshima kwake.
Rais Jakaya Kikwete kupitia akaunti yake ya Twitter aliandika “I have met in Maputo a boy named after me. His name is Kikwete.”
Mtoto huyo aliyekutana na Rais Jakaya Kikwete ambaye na yeye anaitwa ‘Kikwete.’

Katika jamii mtu anapokuwa amepewa jina kama la kwako mara nyingi humaanisha au huonyesha kukubalika kwako ndani ya jamii husika na kuyakubali yale yote ambayo umekuwa ukiyafanya. Hivyo kama kuonyesha heshima na kuendelea kukuenzi mtoto hupewa jina lako ili uendelee kuwa katika kumbukumbu miongoni mwao.
Rais Kikwete yupo mjini Maputo nchini Msumbiji ambapo ni mmoja wa wajumbe wanaoshughulikia masuala ya amani.

Tangu alipotoka madarakani Novemba 5, 2015 Rais Jakaya Kikwete amekua akijishughulisha na masuala ya kurejesha amani Afrika hasa nchini Libya, masuala ya Elimu na kupiga vita ugonjwa wa Malaria barani Afrika.

MAAJABU!!!!!! MWANAMKE WA MIAKA 65 AJIFUNGUA WATOTO WATATU...HEBU MSHUHUDIE HAPA

Mwanamke mwenye umri wa miaka 65 nchini Ujerumani amejifungua watoto watatu baada ya kutunga mimba kwa njia za kupandikiza kisayansi.
Kituo cha runinga cha RTL nchini Ujerumani kimesema mwanamke huyo Annegret Raunigk, amejifungua watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike kwa njia ya upasuaji Jijini Berlin.
Watoto hao wamezaliwa kabla ya muda wao wakiwa na wiki 26, hata hivyo madaktari wamesema wote wapo katika hali nzuri ya kuweza kuishi.
Annegret Raunigk ambaye alikuwa na watoto 13 pamoja na wajukuu saba, ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza duniani mwenye umri mkubwa kujifungua mapacha watatu.

Man U yang'ara ligi ya Europa..Paul Pogba Afuta Nuksi ya mda mrefu

Paul Pogba alifunga mara mbili wakati Manchester United walipoibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya klabu ya Fenerbahce katika kundi A.

Pogba mchezaji ghali zaidi duniani alifunga goli la kwanza kwa penalti baada ya Juan Mata kuangushwa ndani ya eneo la hatari, kisha baadaye kuandika bao la pili baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Jesse Lingard.

Bao la Robin Van Persie lilishangiliwa na mashabiki wa pande zote mbili

Goli la Pili kwa United liliwekwa kimiani na Anton Martial kwa njia ya penalti baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari huku la mwisho likipachikwa na Jesse Lingard kwa shuti kali la chinichini.

Robin Van Persie aliiandikia timu yake ya Fenerbahce goli la kufutia machozi lililoshangiliwa na mashabiki wa pande zote akiwemo kocha wake wa zamani Sir Alex Ferguson.

Matokeo mengine katika michezo ya ligi ya Europa

THURSDAY 20TH OCTOBER 2016
FC Steaua București 1-1 FC Zürich
FK Krasnodar 0- 1 Schalke
FC Slovan Liberec 1-3 Fiorentina
Hapoel Be'er Sheva 0-1 Sparta Prague
Inter Milan 1-0Southampton
Osmanlispor 2-2 Villarreal
FK Qarabag 2-0 PAOK Salonika
Celta Vigo 2-2 Ajax
Standard Liege 2-2 Panathinaikos
Konyaspor 1-1 Sporting Braga
Shakhtar Donetsk 5-0 KAA Gent
FC RB Salzb 0-1 Nice

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI YA TAR 22 OKTOBA

.
20161022_042441
20161022_042456
20161022_042509
20161022_042518
20161022_042533
20161022_042543
20161022_042552
20161022_042601
20161022_042611
20161022_042620
20161022_042629
20161022_042638
20161022_042638
20161022_042646
20161022_042655
20161022_042704
20161022_042713
20161022_042723
20161022_042732
20161022_042744
20161022_042803
20161022_042813
20161022_042822
20161022_042829
20161022_042840
20161022_042849
20161022_042913
20161022_042923
20161022_042948
20161022_042956
 

Gallery

Popular Posts

About Us