Friday, 24 March 2017
VIDEO: Rais Magufuli Katoa ONYO Kwa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Wakati akiwaapisha Dr Harrison Mwakyembe na Prof Palamagamba Kabudi, Ikulu
Umeipata hii!! Tanzania kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza Mabasi.
Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya Mhe. Lazaro Eduard Mathe amemhakikishia Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuwa nchi yake ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza sekta ya viwanda
Pia Balozi huyo amemuhakikishia kwamba wawekezaji kutoka Hungary wameanza kufanya mchakato wa kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya abiria.
Mhe. Lazaro Eduard Mathe amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Mhe. Rais Magufuli muda mfupi baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho akiwa ni miongoni mwa Mabalozi sita waliokabidhi hati hizo.
Pamoja na nia ya kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya abiria, Mhe. Lazaro Eduard Mathe amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi kubwa anazofanya kujenga uchumi wa Tanzania na ameahidi kuwa Hungary itakuza na kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania kwa kuleta teknolojia katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda na kilimo pamoja na kuwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania.