KINGAZI BLOG: KIMATAIFA

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Saturday, 27 May 2017

Wakristo 23 wa kanisa la Coptic wauawa wakienda kanisani kwa maombi Misri

Watu takriban 23 wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kufyatulia risasi waumini wa kanisa la Coptic waliokuwa wakisafiri kwa kutumia basi katikati mwa Misri, vyombo vya habari vya serikali ya nchi hiyo vimesema.

Kisa hicho kilitokea katika mkoa wa Minya, takriban kilomita 250 (maili 155) kusini mwa Cairo, basi hilo lilipokuwa linawasafirisha kwenda kanisani.

Kumetokea visa kadha vya waumini wa kanisa la Coptic kushambuliwa, mashambulio ambayo kundi la Islamic State limedai kuhusika.

Mashambulio mawili ya mabomu ya kujitoa mhanga katika makanisa Tanta na Alexandria mnamo 9 Aprili yalisababisha vifo vya watu 46.

Waumini hao waliuawa walipokuwa wakisafiri kwenda kanisa la Mtakatifu Samuel kuomba.
Basi lao lilikuwa katika msafara mdogo wa magari na taarifa zinasema gari hilo lilisimamishwa na watu kati ya wanane na kumi waliokuwa wamevalia sare za kijeshi.

Watu hao wenye silaha walifyatulia risasi basi hilo kwa kutumia bunduki za rashasha kisha wakatoroka kwa kutumia magari matatu ya 4x4.

Afisa Mkristo kutoka Minya Ibram Samir ameambia gazeti la New York Times kwamba kulikuwa na watoto kwenye basi hilo na ni miongoni mwa waliofariki.

Gavana wa Minya Essam al-Bedawi amesema maafisa wa usalama walifika eneo hilo na wanaweka vizuizi kwenye barabara hiyo ya kulekea kanisa la Mtakatifu Samuel pamoja na kufanya msako mkali.

Wakristo wa Coptic hujumuisha asilimia 10 ya raia wote 92 milioni wa Misri.
Mashambulio ya mwezi jana yalimfanya Rais Abdul Fattah al-Sisi kutangaza hali ya hatari ya miezi mitatu kote nchini humo na kuahidi kuchukua hatua kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu, wengi ambao hutoka maeneo ya kaskazini ya Sinai.

Lakini wengi wa waumini wa Coptic wamekuwa wakilalamika kwamba serikali haifanyi juhudi za kutosha kuwalinda, anasema mwandishi wa BBC aliyepo Cairo Orla Guerin.

Kwa sasa kuna hali ya wasiwasi miongoni mwa Wakristo ambao wanahisi kwamba wanawindwa, anasema.

Kanisa la Coptic ni gani?
Kanisa la Coptic ni la Kiothodoksi na ndilo kanisa kuu la Kikristo nchini Misri.
Ingawa wengi wa waumini wa Coptic huwa Misri, kanisa hilo lina waumini karibu milioni moja nje ya nchi hiyo.

Wengi wa waumini wa kanisa hilo huamini kwamba asili ya kanisa lao ni mwaka 50 AD (Baada ya kuzaliwa kwa Kristo) pale Mtume Mark alipozuru Misri.

Mkuu wa kanisa hilo huitwa Papa na huchukuliwa kuwa mrithi wa Mtakatifu Mark.
Kanisa hilo lilijitenga na Madhehebu mengine ya Kikristo katika Mkutano wa Chalcedon (451 AD) baada ya mzozo kuhusu sifa za utu na umungu za Yesu Kristo.

Kagame Atangaza Kuachia Madaraka ya Urais Rwanda..Awataka Wanyarwanda Kufikiria Mtu Sahihi Ili Kuziba Nafasi Yake..!!!


Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Rwanda unaotarajiwa kufanyika Agosti 3 mwaka huu, Rais wa Rwanda Paul Kagame ameeleza kinaga ubaga kuwa ukomo wake wa kutawala ni mwaka 2024.

Rais Kagame amethibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wa Jeune Afrique kuwa awamu hii ya miaka saba ndiyo ya mwisho na Wanyarwanda wanatakiwa waanze kufikiria mtu mwingine atakayewaongoza baada ya mwaka 2024.

“Inawezekana natakiwa niliangazie suala hili katika siku chache zijazo nitakapoanza mbio za urais. Kuna aina ya makubaliano kati yangu mimi na RPF-Inkotanyi kwa upade mmoja, na raia wa Rwanda kwa upande mwingine“,alisema Kagame na kuendelea kuweka wazi kuwa

“Raia, kupitia kura ya maoni ya Disemba 2015, waliniomba niendelee kuwaongoza nikakubali, ila muda mwafaka wa kupumzika umewadia na waomba waanze kufikiri nje ya mimi baada ya miaka saba“,alisema Kagame kwenye mahojiano yake na mtandao wa Jean Afrique.

Kwa sasa hakuna shaka yoyote kuwa Rais Kagame atashinda uchaguzi wa urais mwaka huu na ni ushindi ambao umekuwa ukitabiriwa kwa muda mrefu na Wanyarwanda.

Mwaka 2015 Wanyarwanda wapatao milioni 4 ambao ni zaidi ya asilimia 70% ya wapiga kura, walipaza sauti zao kulitaka Bunge lirekebishe katiba ili Kagame apate nafasi ya kuendelea kutawala.

Bunge lilifanya hivyo ili limruhusu rais huyo ambaye ana umri wa miaka 59 kuwania awamu zingine mbili hadi mwaka 2024.

Friday, 19 May 2017

Mgahawa Wakumbwa na Kashfa ya Kuuza Nyama ya Binadamu

Mgahawa wakumbwa na habari bandia za kuuza ''nyama ya binadamu''

Mgahawa mmoja mjini London umekumbwa na habari bandia za kuuza nyama ya mtu.

Wafanyikazi katika mkahawa wa Karri Twist katika eneo la New Cross nchini Uingereza wamehangaishwa kwa kupigiwa simu kutoka kwa wateja wanaosema ''Kwa nini hamujafunga''?.

Mkahawa huo wa chakula cha jioni ni mwathiriwa wa habari za mzaha zilizodai kwamba mmiliki wake alikamatwa kwa kuweka nyama ya binadamu katika chakula na kwamba miili 9 ilipatikana katika jokovu la mkahawa huo.

Na watu wengine waliamini mzaha huo.

Habari hiyo ilichapishwa katika chombo cha habari cha channel23news.com, mtandao ambao wateja wake wanaweza kuchapisha habari za uwongo ili kuwafanyia mzaha rafiki zao kwa kuchapisha moja kwa moja katika mtandao wa fecbook.

Shinra Begum ambaye ndio mmiliki wake aliambia Newsbeat kwamba biashara hiyo ya familia imekumbwa na wakati mgumu tangu habari hiyo ilipochapishwa siku ya Alhamisi.

''Wakati watu walipoanza kunipigia simu na kuuliza iwapo tulikuwa tukiuza nyama ya binadamu sikuamini''.

''Nilishtuka nilipoaana habari hiyo katika mtandao na kuendelea kusambazwa katika mtandao wa facebook''.

Sasa watu wametishia kulivunja jengo letu na nimelazimika kuketi chini na mteja ili kumuelezea kwamba yote hayo ni madai ya uwongo.

Shinra anasema kuwa alilazimika kuripoti kwa maafisa wa polisi kwa sababu lilikuwa swala lililomtia wasiwasi mkubwa.

Njia ya pekee ambapo Karri Twist iliweza kukabiliana na chuki hiyo ni kupitia kuchapisha katika mtandao wao ili kuhakikisha kwamba watu wanajua kwamba hilo halikuwa la kweli.

Friday, 12 May 2017

IMEBAINIKA..Kumbe Robert Mugabe Huwa Halali Bali Hupumzisha Macho tuu

Msemaji wa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kiongozi huyo huwa anapumzisha macho tu na si kulala wakati wa mikutano kama wanavyoamini watu wengi.Kiongozi huyo amekuwa akionekana kusinzia katika mikutano mingi."Rais huwa anasumbuliwa na mwanga mkali," George

Charamba amenukuliwa akisema na gazeti la serikali la Herald.Rais huyo kwa sasa yupo nchini Singapore akipokea matibabu maalum kwenye macho yake.Bw Mugabe, 93, anapanga kuwania tena urais katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.

"Huwa najihisi kama mtu ambaye amekosa kutekeleza kazi yake vyema ninaposoma (kwenye vyombo vya habari na mtandaoni) kwamba rais alikuwa anasinzia katika makongamano - la hasha," Bw Charamba amesema.Alilinganisha tatizo la Bw Mugabe na matatizo ya macho ambayo yalikuwa yanamsibu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela.

Bw Mandela alikuwa anatatizwa na mwanga mkali na wapiga picha hawakuruhusiwa kutumia mwanga wa kamera wakati wanapiga picha katika hafla zake.Matatizo ya Bw Mandela yalitokana na kufanya kazi kwa muda mrefu katika timbo na pia kufungwa jela muda mrefu Robben Island.

miliki ya pichaAFPImage captionMacho ya Robert Mugabe hutatizwa na mwanga, msemaji wake amesema. Hapa Mugabe anaonekana akiwa Bamako Januari 13, 2017.Safari za Bw Mugabe za mara kwa mara nje ya nchi zimekuwa zikishutumiwa sana na wakosoaji wake.Sekta ya afya nchini Zimbabwe imedorora na wahudumu wa afya hulalamika kwamba huwa hawalipwi vyema.

Thursday, 11 May 2017

HIVI Ndivyo Magufuli Anavyong'aa Ulaya..Wazungu Wamwagia Misifa Kedekede.


Nimekaa Mahali Fulani Hapa Mtaa wa Poznańska Street Katika Mji wa Warsaw Poland, Yani Wazungu Fulani Nikawaskia Wanazungumzia Tanzania Kwamba Hivi Sasa Ina Rais Mzuri Ambaye Anasimamia Vizuri Uwajibikaji Katika Masuala ya Fedha za Umma na Kuanzisha Elimu Bure. 

Nikapata Hamu ya Kuwasogelea na Kuwauliza Iweje Wanaizungumzia Tanzania Hivyo, Wanaijua? Nikajibiwa Kwamba Wao (wako 9 wamekaa meza moja) wana kikundi chao walifika TZ mwezi April kwa ajili ya utalii na kwamba walipata fursa ya kuitembelea TZ na pia kutengeneza urafiki na baadhi ya watu na kwamba walifurahi kuona TZ inapiga hatua. 

Kumbuka hawa hawakutembelea TZ nzima ila wanasema walienda Zenji, Kilimanjaro, Arusha na Serengeti. Kiukweli wanaisifu sana Tanzania pamoja na Rais JPM. Nimefurahi kuona Nchi yangu inazungumzwa vizuri na baadhi ya watu hapa Poland.

Saturday, 6 May 2017

Picha za utupu za mgombea urais Rwanda zavuja mtandaoni

Baada ya siku chache Mrembo Diane Shima Rwigara kutoka Rwanda kutangaza kugombea urais nchini humo,hatimae akutwa na skendo ya kuvujisha picha zake za utupu mtandaoni.

Mrembo Diane 35, ambae ni msomi wa Uchumi na mtoto wa aliyekuwa tajiri maarufu nchini Rwanda Asinapol Rwigara, picha zake za utupu zilianza kusambaa mapema jana nchini Rwanda hususani kwenye mitandao ya kijamii kama WhatsApp na Facebook na baadae kutapakaa Duniani kote.

Kwa mujibu wa mtandao wa Habari Pevu umeeleza kuwa picha hizo zilitumwa awali kwa njia ya E-mail na mtu aliyejiita ni Muandishi wa habari aliyejulikana kwa jina la Twahirwa Emmy huku akishinikiza kuwa mrembo huyo hafai kuchaguliwa kuwa Rais kwa vitendo vyake  vichafu vya kupiga picha za utupu.



Hata hivyo Jitihada za kumpata mrembo huyo kuzungumzia picha hizo zilizovuja ziligonga mwamba baada ya waandishi wa habari nchini Rwanda kumsaka bila mafanikio.

Uchaguzi mkuu wa Rais nchini Rwanda unatarajiwa kufanyika mwaka huu mwezi wa Augosti, na mpaka sasa kuna wagombea watatu tuu ambao ni Mpayimana Philippe ambae ni mgombea binafsi na Franck Habineza kutoka chama cha Green pamoja na Diane Rwagira wote wakitarajiwa kuleta upinzani mzito kwa Rais Paul Kagame .

Friday, 5 May 2017

Binti wa Miaka 35 Ajitokeza Kuwania Urais Nchini Rwanda


Mwanadada Diane Rwigara, ametangaza azma yake ya kuwania Urais nchini Nchini Rwanda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.

Huyu ni Binti wa mfanyabiashara maarufu wa Kinyarwanda Assinapol Rwigara aliyefariki miaka 2 iliyopita katika mazingira ya kutatanisha .

Bi Diane mwenye umri wa miaka 35 amesema, anataka kukomesha uonevu na kuleta haki na uhuru wa watu kujieleza nchini Rwanda.

Amesema, kuna suala la usalama mdogo ambapo baadhi ya watu hutoweka na wengine kuuwawa katika mazingira ya kutatanisha, na kwamba huwezi kusema uko katika nchi yenye amani na usalama wakati watu wanauawa huku wengine wakikimbia nchi.

Huyu ni Mnyarwanda wa tatu kutangaza rasmi nia ya kutaka kugombea urais nchini Rwanda wengine wakiwa ni Bwana Mpayimana Philippe aliyetangaza kuwa mgombea binafsi na Franck Habineza kutoka chama cha Green.


Sunday, 30 April 2017

Ma'admin' wa makundi Whatsapp kukiona cha moto India


Kuwa msimamizi wa kundi katika whatsApp (WhatsApp Group Chat Admins) kwa wengi sio kitu kikubwa sana. Kimsingi ni kuwezesha kuongeza wanachama katika Kundi au kumuondoa yeyote katika kundi husika.

Hata hivyo nchini India ni zaidi ya hivyo, kuwa msimamizi wa kundi huko ni jambo linalomtaka msimamizi kuwa makini zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Economic Times serikali ya India na mahakama inataka kuwafanya wasimamizi wa makundi ya WhatsApp kuwa wasimamizi ambao watadhibiti taarifa za uongo zinazoenezwa na watu wengi kupitia whatsApp.

Kwa mujibu wa sheria mpya Msimamizi wa kundi anaweza kutupwa gerezani kama muhusika wa kusambaza habari za uongo endapo kama hakuchukua hatua ya kumtoa katika kundi lake na kumripoti Polisi.

Kama itatokea mtu ametoa habari ya uzushi katika Kundi basi msimamizi anatakiwa kumtoa (removed) katika kundi na kumripoti haraka zaidi Polisi ili hatua dhidi yake zifuate.

Kama habari ya uongo itazidi kuenea kwa kusambazwa kutokea kundi husika na msimamizi wa kundi hakufuata hatua hizo basi atachukuliwa hatua za kisheria kama aliyesaidia kupotosha umma.

Lengo la hatua hii ni kusaidia kukabiliana na kuenea kwa taarifa za uongo. Nchini India watu zaidi ya milioni 200 wamejisaJIli katika WhatsApp.

Wakati wa kampeni za uchaguzi wa Marekani kulikuwa na taarifa nyingi za uongo na uzushi kupitia makundi ya whatsapp.

Na hata hivi karibuni pia iliripotiwa kwamba Ufaransa ilikuwa na mafuriko ya habari za uongo zilizokuwa zinapikwa kutokea makundi ya WhatsApp katika kampeni za uchaguzi unaopigiwa kura leo.

Facebook nao wameanza mpango wa kupambana na taarifa za uongo kupitia mtandao wao.

Kwa sasa Dunia imekumbwa na wimbi la taarifa za uongo na uzushi kupitia mitandao ya kijamii. Kuanzia taarifa mpaka picha nyingi zimekuwa za uongo na uzushi.

Kwanini watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wako mbele katika kuzusha na kusambaza habari za uongo? tatizo ni nini au msukumo wao ni upi?

Thursday, 27 April 2017

Picha!! China imtengeneza meli kubwa ya kivita

China imetangaza kwamba imefanikiwa kuzindua manowari yake ya kwanza ya kujiundia yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita, Meli hiyo ya kivita ina uzani wa tani 50,000.

Hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya karibuni zaidi ya kujiimarisha kwa taifa hilo katika nguvu za jeshi lake la majini.

Vyombo vya habari nchini China vinasema meli hiyo, ambayo inawezesha ndege kuruka na kutua juu yake, ilisafirishwa kutoka eneo ambalo ilikuwa ikiundiwa Dalian na kuwekwa baharini, Inatarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka 2020.






Makubwa!!!Huyu ndiye Rais Mpya wa Ufaransa Emmanuel Marcon..Amemuoa Mwalimu Wake Aliyemzidi Zaidi ya Miaka 24..Alianza Kutembea Naye Toka Akiwa na Miaka 17..!!


EMMANUEL MARCON mwenye umri wa miaka 39 ndiye anayetarajiwa kuwa rais ajaye wa Ufaransa.

Pamoja na hayo, Marcon ambaye ameoa mke mwenye umri wa miaka 64 ,ana mambo mengi ya kufurahisha na kuvutia maishani mwake hususan kuhusiana na mkewe huyo ambaye anamzidi umri kwa kiasi cha miaka  zaidi ya 24.

Mkewe huyo alikuwa ni mwalimu wake wa darasa miaka ipatayo 24 iliyopita ambapo mwalimu wake wa darasa wakati huo alikuwa na binti ambaye alikuwa mwanafunzi mwenzake darasa moja.  Wakati huo, kila mtu, wakiwemo wazazi wake Marcon, walifikiri binti huyo wa mwalimu alikuwa rafiki yake, wakati hawakuwa hivyo.

Katika mlolongo huo wa vituko, Marcon alijikuta katika mapenzi na mwalimu wake wakati yeye akiwa na umri wa miaka 15 ambapo wakati huo, mwalimu huyo alikuwa ameolewa akiishi kwa furaha na akiwa na watoto watatu

Alipofikisha umri wa miaka 17, aliamua kumuoa mwalimu huyo, wakati huo akiwa na umri wa miaka 42.

apendanao hao walifunga pingu za upendo mwaka 2007 wakati huo ‘mlume’ huyo akiwa na umri wa miaka 30 na ‘mrembo’ wake akiwa anapiga hodi katika umri wa miaka 55.

Mwanandoa huyo wa kiume anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa Ufaransa mwezi ujao akiwa amebakiza miezi sita kufikisha umri wa miaka 40 wakati ambapo kipenzi chake, yaani mkewe,  ana watoto  (watu wazima) watatu na wajukuu saba sasa.

Ni vyema pia kufahamu kwamba mtoto wa kwanza wa mkewe huyo anamzidi Marcon kwa umri wa miaka miwili, wakati ambapo mtoto wake wa pili, aliyekuwa kipenzi na mwanafunzi mwenzake  na Marcon wakiwa darasa moja, wanalingana umri.

Tuesday, 25 April 2017

KAZI IMEANZA Marekani Watuma Nyambizi Nyingine Kuongeza Nguvu Korea Kaskazini..Inauwezo wa Kurusha Makombora ya Mbali.


Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda kutokana na majibizano makali na vitisho kati ya Marekani na Korea Kaskazini, ambapo meli ya jeshi la Marekani (USS Michigan) imewasili katika Korea Kusini huku hofu ikiongezeka zaidi kuhusu uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora au silaha za nyuklia.

Meli hiyo yenye uwezo wa kushambulia kwa makombora, imewasili kujiunga na kundi jingine la meli za kivita zinazoelekea eneo hilo ambapo zinaongozwa na meli kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson.

USS Michigan hutumia nguvu za nyuklia na hubeba makombora aina ya 154 Tomahawk na wanajeshi 60 pamoja na meli nyingine ndogo.

Aidha, bunge la Seneti nchini Marekani limealikwa kwa kikao cha kupewa habari kuhusu Korea Kaskazini siku ya Jumatano katika ikulu ya White House.

Meli hiyo inatarajiwa kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi pamoja na kundi la meli zinazoongozwa na Carl Vinson, kundi ambalo lilitumwa eneo la Korea kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani.

Hivi karibuni safari ya meli za kivita za Marekani ilizua utata kuhusu iwapo zilikuwa zinaenelekea eneo la Korea, lakini maafisa wa jeshi la wanamaji la Marekani kwa sasa wamesema zinaelekea eneo hilo kama ilivyoamrishwa.

Naye Rais wa Marekani, Donald Trump mapema mwezi huu amesema kwamba atatuma kundi kubwa la meli zenye nguvu.

Wednesday, 19 April 2017

Kenya Nao Waiga usafiri wa Mwendokasi kama Tanzania..!!


Mara nyingi watanzania wamekuwa wanataja mafanikio ya nchi nyingine wakilinganisha na mazingira hafifu ya hapa nchini katika masuala ya Maendeleo.

Lakini  orodha ya mazuri yanayoigwa na nchi nyingine kutoka Tanzania itakuwa imeongezeka kwa jambo moja lingine ambalo ni Mabasi ya mwendo kasi.

Aidha, Mamlaka ya usafiri jiji la Nairobi imefufua mpango kupunguza foleni za magari kwa  kuanzisha usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi kama yanayotumika kwa sasa nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Katibu wa Masuala ya usafirishaji Mwangi Mariga alisema ujenzi wa  mradi huo wa Mabasi ya  Mwendokasi  utahusisha miji mitano.

Naye  Katibu wa Baraza la Mawaziri James Macharia alishauri   mwaka jana kwamba mapendekezo maalum ya mfumo wa Mabasi ya  usafiri yalikuwa na changamoto kutokana na miundombinu iliyopo ya  barabara  kwa mabasi kuwa na msongamano.

Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi   umebuniwa kufuatia idadi ya watu wa Nairobi kuongezeka hadi milioni 3.3 kutoka 350,000 mwaka 1963 na idadi ya magari inakadiriwa kufikia 300,000 bila ongezeko sawa katika mtandao wa barabara.

Huu ndo Uwezo wa Korea Kaskazini Kivita..Ana Makombora Zaidi ya 1000 Yanayoweza Kurushwa Toka Bara Moja Hadi Jingine

Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani.

Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90.

Mifumo ilio na uwezo mkubwa inadaiwa kufanyiwa utafiti.

Hivi karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambayo yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi.

Taifa la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa marefu zaidi ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong-13.

Makombora ya Hwasong yakiwa katika maonyesho

Ishara za kwanza kuhusu utengenezaji huo ulifanyika Septemba 2016 ambapo taifa hilo lilifanyia majaribio mashine mpya ya roketi ambayo baadhi ya watu wanasema inaweza kurusha kombora kutoka bara moja hadi jingine.

Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon inaamini kwamba Korea Kaskazini inamiliki makombora 6 aina ya KN-08, ambalo lina uwezo wa kufika hadi Marekani.

Korea kaskazini inaaminika kutengeza toleo jipya la kombora hilo linalojulikana kama KN-14. Haahivyo makombora hayo hayajafanyiwa majaribio.

Lakini mnamo mwezi Januari 2017, kulikuwa na ishara ya jaribio, muda mfupi baada ya kiongozi Kim Jong un kudai kwamba taifa hilo lilikuwa katika awamu ya mwisho ya kutengeza kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.

Mpango wa kisasa wa kutengeza makombora yaa Korea Kasakzini ulianza kwa kutengeza makombora ya scud ambapo yalipitia Misri mwaka 1976.

Kufikia 1984, taifa hilo lilikuwa likitengeza makombora yake kwa jina Hwasong.

Inaaminika kuwa na makombora tofauti tofauti ya masafa mafupi ambayo yanaweza kulenga taifa jirani la Korea Kusini.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya Korea umeharibika na yamekuwa yakijiandaa kukabiliana kivita.

Kombora la Hwasong 5 na Hwasong 6 ambayo pia hujulikana kama Scud B na Scud C yana uwezo wa kwenda kilomita 300 na 500 mtawalia kulingana na kituo cha Marekani kinachofanya utafiti wa kuzuia kuenea kwa nuklia.

Makombora hayo yanaweza kubeba makombora ya kemikali na nyuklia.

Silaha hizo zimejaribiwa na kupelekwa katika maeneo yanayohitajika na kombora la Hwasong-6 limeuzwa nchini Iran.


Ramani ya Korea Kaskazini na majirani zake wa Korea Kusini

Korea Kaskazini ilianza mpango huo mapema miaka ya 80 kutengeza kombora la masafa ya kadri kwa jina Nodong likiwa na uwezo wa kusafiri urefu wa kilomita 1000.

Kombora hilo limetengezwa kwa muundo wa Scud ,lakini ni asilimia 50 kwa ukubwa na lina mashine yenye uwezo mkubwa.

Uchanganuzi wa mwezi Aprili 2016 wa taassii ya kimataifa kuhusu utafiti wa mikakati ,unasema kuwa makombora hayo yalithibtishwa yanaweza kupiga maeneo yote ya Korea Kusini na Japan.

Imeongezea kuwa maonyesho ya Oktoba 2010 yalithibitisha kuwa kombora hilo linaweza kufika urefu wa kilomita 1,600 ikimaanisha kwamba linaweza kupiga kambi kadhaa za Marekani zilizopo katika eneo la Okinawa.

Makombora hayo ya Nodong yanadaiwa kujaribiwa 2006, 2009, 2014 na 2016.


Kombora la Musudan

Korea Kaskazni imekuwa ikitengeza makombora ya Musudan kwa miaka kadhaa, na hivi karibuni ilifanya majaribio 2016.

Makadirio yanatofautiana kuhusu viwango vyake, huku ujasusi wa Israel ukitaja uwezo wake kuwa kilomita 2,500 nacho kitengo cha ulinzi wa makombora nchini Marekani kikikadiria kuwa na uwezo wa kufika kilomita 3,200.

Duru nyingine zinasema kuwa kombora hilo lina uwezo wa kwenda kilomita 4,000.

Kombora la masafa mafupi la Musudan ambalo pia linajulikana kama Nodong B ama Taepodong-x linaweza kulishambulia taifa lote la Korea Kusini na Japan.

Kombora hilo linaweza kushambulia kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Guam.

Kombora la masafa marefu la Taepodong linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine

Korea Kaskazini inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la masafa ya kadri, kwa jina Pukguksong, mnamo mwezi Agosti 2016 likirushwa kutoka kwa manuwari.

Kombora la pili lilirushwa kutoka ardhini mnamo mwezi Februari 2017.

Pyongyang ilisema kuwa ilitumia mafuta ,na kufanya kuwa rahisi kuliwasilisha na kurusha. Hatahivyo maelezo kuhusu uwezo wake hayajulikani.

Credit: BBC

Tuesday, 18 April 2017

Kimenuka!!!Kikosi hatari cha US NAVY 'SEAL' chatua rasmi Korea Kasikazini tayari kwa Mapambano.


NI wazi kuwa jaribio lilifanywa na Korea Kaskazini la Makombora yake ya Nukria  limeshtua  Marekani ambapo sasa ni rasmi Kikosi hatari cha Makomandoo wa Kimarekani ambacho ndicho "The Most Feared Force" katika ulimwengu huu cha US NAVY SEAL inasemekana tayari kiko katika Peninsula ya Korea tangu Jana usiku kikitokea jimbo la Florida nchini Marekani.

Hiki ni kikosi hatari zaidi duniani ambacho kazi yake ni kufanya operations ambazo ni hatari zaidi mno na za mwisho. US Navy Seal ni mjumuisho wa makomandoo hatari zaidi wanaotumia ujuzi wa hali ya juu na wenye mafunzo ya kitaalamu zaidi kuliko makomandoo wengine wa majeshi yote ya kimarekani.

Makomandoo hawa ni wale tu wenye uzoefu wa hali ya juu wa kupambana popote pale iwe angani, ardhini au majini, na katika hali yoyote ile iwe barafu, mvua au jua. Na ndio maana ya neno SEAL ambayo kirefu chake ni Sea, Air and Land.

Ni Mara chache sana kutumika. Hawa ni tofauti na majeshi mengine kama US Army Rangers, US Delta Force na mengine. Katika utawala wa Obama, ametoa ruhusa MARA MOJA tu kwa US Navy Seal kutumika. Mara ya mwisho kilitumika usiku wa manane kwa takribani dakika 45 tu kumuangamiza Osama na ni askari mmoja tu alijeruhiwa kwa ajali ya helkopta zisizotoa sauti ambayo ilikosewa ikagonga ukuta wakati makomandoo wakidrop kwenye makazi ya Osama.

Na baada ya Operation Makomandoo hao waliilipua haraka helicopter yao iliyopata hitilafu ili maadui wasigundue teknolojia iliyotumika kutengenezea helicopter hiyo na baada ya kuilipua wakaondoka. Makomandoo wa Navy Seal waliotumika katika Operation hiyo ni 11 tu na Marubani Watatu ambao nao ni kutoka Navy Seal. Na ikumbukwe kuwa Operation hii ilikuwa ikitazamwa live (mubashara) kutoka White House ambapo Obama alikuwa akifuatilia (nilirusha tukio hili), kofia za makomandoo hawa zilikuwa na kamera mbele ambazo zilitumika kurekodi kila kitu kinachoonekana mbele na kurusha kwenye satelaiti had White House. Mkakati huu ulisimamiwa na Mwanamke hatari zaidi anayejulikana kama Alfreda Frances Bikosky ambaye ni Afisa mwandamizi wa CIA na jasusi aliyebobea na pia ni komandoo lakini si memba wa Navy Seal. Bibi Alfreda anajulikana zaidi katika jeshi la Marekani kama MALKIA WA MATESO. Serikali ya Marekani inajitahidi kudhibiti mitandao ya kijamii na google isisambaze picha za mama huyu hatari.

Kikosi hiki cha US Navy Seal hutumika baada ya makomandoo wengine wa majeshi tofauti ya marekani kusoma Jiografia ya sehem husika, ramani ya ngome za adui na silaha zake then Raisi wa Marekani hutoa ruhusa ya NAVY SEAL kutumika kumalizia Operation. Baadhi ya majukumu/kazi za Navy Seal ni Direct Operations (kama wanavyotaka kumfanyia North Korea), Strategic Special Missions (kama walivyofanya kwa Osama), Hostage Rescue (kama walivyofanya miaka ya nyuma kuwaokoa Ma-Intelligensia wa Kimarekani waliotekwa Iran) na Foreign Internal Defence.

Mpaka sasa Navy Seal ina jumla ya Makomandoo 8985 ambao ni hatari mno na wenye roho za kinyama. Makomandoo hawa huwa wapo kwenye mazoezi makali ya special operations na trainings ngumu muda wote huko Virginia, Marekani. Mara chache sana Navy Seal huwa Recruited kwenda CIA kufanya kazi za Kiintelligensia wanapotakiwa. Makamu wa Rais wa Marekani Bwana Pence yuko Korea Kusini na inasadikika ujio wake umeambatana na NAVY SEAL waliojichimbia katika Nyambizi zisizoonekana katika pwani ya Korea..

Monday, 17 April 2017

Hatari !! Mwanaume aliyefanya mauaji huku Akionyesha Live Marafiki zake Kupitia Facebook asakwa

Steve Stephens muuaji anayesakwa Marekani

Polisi katika jimbo la Ohio nchini Marekani wanamtafuta mtu anayedaiwa kufanya mauaji,huku akionyesha moja kwa moja mauaji hayo kupitia mtandao wa Facebook.

Maofisa katika mji wa Cleveland wamesema kuwa Steve Stephens anaonekana akionyesha moja kwa moja mauaji wakati akimpiga risasi mwanaume mmoja mtu mzima kupitia Facebook.

Mkuu wa Polisi mjini Cleveland Calvin Williams amemtaka Stephens ajisalimishe mwenyewe.

Williams alisema kuwa mtu huyo ni hatari kuendelea kuwa mafichoni kwake.

Polisi wanasema hawajapata ushahidi madai ya Stephen kuwa amewauwa watu kumi na mmoja.

Sunday, 2 April 2017

Watu 250 wahofiwa kufa kwenye maporomoko ya ardhi

Mamlaka ya jeshi la Colombia inasema idadi ya waliofariki katika maporomoko ya ardhi nchini humo imefikia watu 250 huku waliojeruhiwa wakiwa 400.
Hata hivyo idadi hiyo huenda ikaongezeka kwani bado kuna zaidi ya watu 200 ambao hawajapatikana .
Vikosi vya wafanyikazi wanaoendesha shughuli za uokoaji wanasema nyingi ya barabara za kulipotekea maporomoko hayo huko eneo la mji wa kusini mwa taifa hilo, Mocoa hazipitiki kutokana na mkasa huo.

Maporomo hayo yametokea baada ya mvua kali kunyesha kwa saa nyingi.
Viongozi wa mataifa jirani wa Mexico na Argentina walikuwa wa kwanza kutoa ujumbe wa pole na kuahidi kwenda kuisaidia Colombia.

Rais Juan Manuel Santosa alitangaza hali ya tahadhari eneo hilo na kusafiri kuangalia shughuli za uokoaji.

Picha zilizochapishwa kwenye mitandao na jeshi zilionyesha baadhi ya majeruhi wakiokolewa kwa kutumia ndege.
Maporomo koya ardhi yamekumba eneo hilo mara kadha miezi ya hivi karibuni.

Mwezi Novemba, watu 9 waliuawa kwenye mji wa El Tambo, karibu kilomita 140 kutoka Mocoa kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyosababiswa na mvua kubwa.

Tuesday, 28 March 2017

Kali ya Mwaka hii!!!...Aliyemfunga mbwa wake mdomo atupwa jela miaka 5

Mwanamume mmoja raia wa Marekani ambaye alifunga mbwa wake kwenye mdomo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

William Dodson, mwenye umri wa miaka 43, anasema alimfunga mbwa huyo mdomoni kwa sababu alibweka sana. Ililazimu mbwa huyo kufanyiwa upasuaji mara kadha baada ya kupoteza sehemu ya ulimi wake.

Siku moja baada ya hukumu hiyo kutolewa, William Dodson pia alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela, kwa mashtaka tofauti ya bunduki.

Vifungo hiyo viwili vitafuatana Kulingana na polisi William Dodson alimnunua mbwa hiyo kwa jina Caitlyn kwa dola 20.

Dodson, ambaye alikuwa huru kwa dhamana wakati huo, alimfunga mbwa huyo nje baada ya kumfunga mdomo wake mara tisa.

Lakini mbwa huo alifanikiwa kutoroka mwezi Mei mwaka 2015, na alikuwa mgonjwa sana wakati alipatikana akirandaranda barabarani.

Kamba aliyotumia kumfunga mbwa hiyo ilizuia damu kufika hadi kwenye ulimi wake, na iliwachukua madaktari wa mifugo karibu saa 36 kuiondoa.

Wakati huo chama cha wanyama cha Charleston, kibadilisha picha ya akaunti yake na kuweka picha ya mbwa hiyo, kama njia ya kuonyesha uzalendo.

Wamekuwa wakichapisha taarifa jinsi mbwa huyo anavyoendelea katika kisa hicho kilichoangaziwa kimataifa.

Caitlyn, alikuwa na umri wa miezi 15 wakati alipatikana na sasa amehitimu miaka mitano akiwa anaishi na familia tofauti.




Saturday, 28 January 2017

Serikali Yapiga Marufuku Wanafunzi kufundishwa Somo la Dini ya Kiislamu Mashuleni..!!!



 SERIKALI nchini Swaziland imeziagiza shule zake kufundisha somo la dini ya Kikristo pekee, hatua iliokosolewa na wadau mbalimbali kwa kuwa haiheshimu dini nyengine.

Agizo hilo lilitolewa wiki iliyopita na Wizara ya Elimu nchini humo, ambapo ilipita shuleni ikiwaagiza walimu wakuu wote kuhakikisha mtaala hautaji dini nyingine zaidi ya Kikristo.

Sahid Matsebula, ambaye ni Muislamu anayefanya kazi msikitini karibu na Mji Mkuu wa Mbabane, alinukuliwa akisema kwamba sera hiyo huenda ikazua wasiwasi wa kidini katika ufalme huo.

''Serikali ina mpango gani kwa watoto wetu ambao si Wakristo? Ambao licha ya kujifunza wakiwa nyumbani, mambo mengine wanapaswa wajifunze wakiwa shuleni,” alisema.

Sera hiyo mpya imekuja baada ya raia kulalamika kuhusu wahamiaji wa Bara la Asia na wale wa Kiislamu kwamba wamekuwa wakiingia nchini humo hatua iliyolazimu Bunge kuunda kamati ya kuchunguza tukio hilo.

Wahamiaji wengine tayari wamerudishwa makwao na Waziri wa Biashara, Jabulani Mabuza ameliambia Bunge kwamba wameanza kutunga sheria itakayowazuia wahamiaji kuanzisha biashara nchini Swaziland.

Rais wa Baraza la Makanisa nchini humo, Stephen Masilela ameunga mkono mtaala huo mpya.

''Ukristo ndio msingi wa kujengwa kwa taifa hili,” alisema.

Hata hivyo, Taifa la Swaziland linaloongozwa na Mfalme Mswati wa tatu tangu mwaka 1986, lina idadi ndogo ya waumini wa Kiislamu.

Sera hiyo ya kufundisha dini ya Kikristo pekee shuleni, pia imekosolewa na mwandishi Nomsa Mbuli wa gazeti la Times of Swaziland.

“Kinachoinua dini moja juu ya nyengine ni nini wakati ambapo Katiba inaagiza usawa wa kidini?” alihoji.

Wednesday, 25 January 2017

Wasomali 90 na Wakenya wawili watimuliwa Marekani

 Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Wote wamewasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba raia hao wa Somalia watasafirishwa moja kwa moja hadi Mogadishu.

"Ni watu 90 kulingana na habari ambazo tulipewa. Wakati unaondolewa nchi fulani kurejeshwa kwenu, huwa unarejeshwa hadi kwenu," ameambia BBC.

Kuhusu sababu iliyowafanya kufurushwa, Bw Kiraithe amesema: "Inategemea sheria za nchi ambayo walikuwa wamehamia (Marekani),"

Bw Trump alisema Jumatano itakuwa siku muhimu kwa usalama wa Marekani.

Anatarajiwa kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotafuta viza za kwenda Marekani.

Wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.

Aligusia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita dhidi ya ugaidi. Baadaye alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.

 Anatarajiwa kufika katika wizara ya usalama wa ndani baadaye leo na anatarajiwa kusaini maagizo hayo ya kuimarisha usalama katika mpaka wa Mexico na taifa lake na baadaye wiki hiii taarifa zinaashiria atawajibikia ahadi yake ya kupunguza idadi ya wakimbizi wanaoingia Marekani.

Na hiyo ni hadi pale ukaguzi mkali utakapoanzishwa na kuzuia raia wa mataifa saba ya Afrika na kutoka eneo la Mashariki ya Kati yote yalio na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu.

Rais wa Mexico akiwa na Rais Trump

Ubaguzi wa kidini unapigwa marufuku kwa mujibu wa katiba ya Marekani lakini inadhaniwa utawala wa Trump utaidhinisha marufuku hiyo kwa misingi kwamba ni hatua za dharura kukabiliana na tishio lililopo la ugaidi.

Awali, Bw Trump aliandika kwenye Twitter kueleza kusikitishwa kwake na kiwango cha juu cha ghasia na mauaji katika jiji la Chicago.

Vyombo vya habari wiki hii viliripoti kwamba tayari watu 228 wamepigwa risasi na wengine zaidi ya 40 kuuawa mwaka huu.

Bw Trump ameandika kwamba iwapo watawala wa Chicago hawatatua tatizo hilo la mauaji, basi atawatuma 'Feds' akimaanisha maafisa wa FBI.

Tuesday, 24 January 2017

Rais Donald Trump kawafuta kazi Mabalozi wote wa Marekani duniani

Kwa mujibu wa  The Independent naParsToday wanasema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote duniani na wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa ambapo uamuzi huo umefanyika katika siku yake ya kwanza kazini.
 

Trump ambaye aliapishwa Ijumaa January 20, 2017 kuwa Rais wa 45 wa Marekani, amewataka mabalozi wote walioteuliwa na mtangulizi wake, Barack Obama kuondoka kazini mara moja bila hata kuwapa muda wa kujitayarisha kuondoka kama ilivyo kawaida.
 

Inaelezwa kuwa zaidi ya mabalozi 80 wa Marekani katika nchi mbalimbali duniani walifutwa kazi Ijumaa tarehe 20 Disemba saa sita mchana ikiwa ni mara baada ya Trump kuapishwa.
 

Hatua hiyo ya Trump inatazamiwa kuvuruga uhusiano na washirika muhimu kama vile Ujerumani, Uingereza na Canada ambapo ripoti zinasema nchi hizo zinaweza kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwani baada ya Trump kuteua mabalozi wapya watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Congress kabla ya kuanza kazi zao.
 

Donald Trump anakosolewa kwa kuacha nafasi nyingi wazi na hivyo kuvuruga shughuli za kawaida za serikali ya Marekani na hii haya yanajiri huku maandamano yakiripotiwa kuendelea sehemu mbalimbali kupinga utawala wa kiongozi huyo. 
 

Nchini Marekani katika siku ya pili ya utawala wa Trump kumeripotiwa maandamano ya watu milioni tatu na imeripotiwa kumefanyika maandamano 637 katika maeneo mbalimbali ya Ulaya, Asia na Afrika kumpinga rais mpya wa Marekani.

 

Gallery

Popular Posts

About Us