KINGAZI BLOG: 01/22/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday, 22 January 2017

Mwanamke Atupa kichanga chooni baada ya kujifungua kisa kuokoa ndoa

MATUKIO mawili ya mama kutupa vichanga chooni baada ya kujifungua, yametikisa katika wilaya za Sikonge na Shinyanga. Katika tukio la wilayani Sikonge, mama akichukua uamuzi huo ili kulinda ndoa isivunjike, baada ya kupata ujauzito nje ya ndoa.

Katika tukio jingine, mtoto wa siku moja mwenye jinsia ya kiume, amekutwa ametupwa kwenye tundu la choo la Kanisa la African Inland Tanzania (AICT) lililopo Kitangiri Manispaa ya Shinyanga na kutofahamika mara moja mtu aliyefanya kitendo hicho.

Kutoka Sikonge inaelezwa kuwa Polisi wilayani humo mkoani Tabora, inamshikilia mkazi wa kitongoji cha Ukanga katika kijiji cha Sikonge mjini, Paulina Mussa (21) kwa tuhuma ya kumtupa mtoto aliyejifungua kwenye shimo la choo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Sikonge, Mselemi Maulidi akizungumza na waandishi wa habari, alisema kwamba tukio hilo ni la Januari 19, saa 10 usiku katika Kitongoji cha Ukanga wilayani Sikonge.

Maulidi alisema mtuhumiwa, Paulina Mussa alishikwa na uchungu majira ya usiku wa saa 10, ambapo alitoka nje na kumuacha mume wake akiwa amelala ndani, lakini baada ya muda alirudi ndani.

Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa akiwa ndani, alimueleza mume wake, Saulo Kaombwe kuwa mimba aliyokuwa amebeba, imeharibika huku akimuomba ampeleke hospitali akatibiwe, ambapo mume wake alikubali kumpeleka.

Alisema akiwa Hospitali ya Wilaya, mama mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwenye gazeti, alikwenda kujisaidia katika choo hicho cha jirani yake, ambapo alisikia kichanga kikiwa kwenye shimo la choo kikilia .

Kutokana na hali hiyo, alitoka haraka chooni na kuomba msaada kwa majirani, ambao walifika katika choo hicho na kuamua kukivunja na kukikuta kichanga hicho, kikiwa kimewekwa kwenye mfuko wa saruji uliokuwa tupu.

Baada ya kukitoa kichanga hicho, walikipeleka katika Hospitali ya Wilaya, alipokwenda kutibiwa mama wa kichanga hicho, na walipomhoji alikiri kujifungua na kukitupa kichanga kwenye shimo la choo, jambo ambalo baadhi ya akinamama liliwakera na kuanza kumtembezea kipigo mama huyo, huku baadhi ya wananchi wakituliza ghasia hizo.

Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo, alidai alikuwa anaokoa ndoa yake, kwa kuwa mimba aliyobeba, ilikuwa si ya mume aliyekuwa akiishi naye.

Mmoja wa majirani wa mama huyo, Lameck Benjamin alisema jambo hilo ni la aibu na kuiomba serikali ichukue hatua kali dhidi ya akinamama, wanaofanya tabia ya kutupa watoto huku akiwataka kuacha kubeba mimba, endapo hawataki kuzaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Hamisi Selemani Issa, alithibitisha kutupwa kwa kichanga hicho na kusema kuwa tayari mtoto huyo, anaendela kupatiwa huduma na mama yake huku wakisubiri kuchukua hatua za kisheria.

Kamanda Issa alitoa wito kwa akina mama, kuacha tabia hiyo ya kuwatupa watoto pasipo kuwa na sababu ya msingi kwani nao wana haki ya kuishi.

Mwingine atupwa kwenye choo cha kanisa Katika tukio jingine, mtoto wa siku moja mwenye jinsia ya kiume, amekutwa ametupwa kwenye tundu la choo la Kanisa la African Inland Tanzania (AICT) lililopo Kitangiri Manispaa ya Shinyanga na kutofahamika mara moja mtu aliyefanya kitendo hicho.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Habiba Jumanne aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa majira ya saa 11 jioni ya Januari 20, mwaka huu, alipigiwa simu na baadhi ya waumini wa kanisa hilo, kuwa kuna mtoto mchanga wanasikia sauti yake ndani ya tundu la choo.

Jumanne alisema kuwa mtoto huyo mwenye siku moja, alikutwa kweli kwenye tundu la choo akiwa hai, huku waumini wa kanisa hilo na askari walibomoa choo na kumtoa mtoto huyo, kisha kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

“Tulifanya jitihada za kuvunja choo na kumtoa mtoto akiwa hai, tukamkimbiza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

Chakusikitisha leo asubuhi tumekwenda kuona hali ya mtoto, daktari ametueleza mtoto amefariki dunia, hatuna jinsi aliyefanya kitendo hicho hafahamiki.

Tunachotaka ni kuomba kibali cha polisi na kwenda kumzika kwa kushirikiana na Kanisa la AICT,” alisema Jumanne.

Mzee wa Kanisa la AICT, David Madata alisema kuwa wakati alipokuwa akifundisha watoto somo la Injili, alimuona mwanamke mmoja akiwa amelala karibu na choo hicho, lakini hakumdhania kama alikuwa na nia ovu.

Alisema baada ya muda, mwanamke huyo aliondoka na kuelekea mahali kusikojulikana na baadaye watu waliokuwa wanaenda chooni, walianza kusikia sauti ya mtoto mchanga akilia chooni, hivyo waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi na serikali ya mtaa.

Kaimu Kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo alieleza kuwa mtoto huyo alitupwa kwenye tundu la choo la Kanisa la AICT na mtu ambaye hajafahamika.

Alisema bado wanaendelea na uchunguzi kumbaini aliyehusika na kitendo hicho. Habari hii imeandikwa na Lucas Raphael, Sikonge na Kareny Masasy, Shinyanga.

PICHA 16 +Hivi Ndivyo Trump Alivyosherehekea Mara Baada ya Kuapishwa Kuwa Rais wa 45 wa MAREKANI


Rais mpya wa Marekani, Donald Trump aliungana na First Lady Melania Trump kwenye hafla ya kusherehekea kuapishwa kwake, Ijumaa hii. 

Aliungana na wanajeshi wa nchi hiyo mjini Washington. Familia yake pamoja na Makamu wake, nayo ilikuwepo. Kwenye hotuba yake fupi kwenye hafla hiyo, Trump ameahidi mabadiliko makubwa kwenye sera za nchi yake. Tazama picha zaidi.


Kutana na Mpakistani Mwenye Nguvu Zaidi Duniani,Anakula Mayai 36 ,Kuku 4 na Maziwa Lita 5 Kwa Siku..!!!


TANGU vikatuni vya Hulk, jitu la kutisha na lenye nguvu ijapokuwa la kufikirika vilipoanzishwa mapema katika miaka ya 1960, mashabiki wamekuwa wakishangazwa na ushupavu au nguvu zaidi kuliko ghadhabu zake.

Tangu hapo kikatuni hiki kikapata nafasi katika tasnia ya filamu, ambako alizidi kujipatia umaarufu miongoni mwa mashabiki kwa namna alivyo.

Kuanzia hapo wale binadamu halisi wenye nguvu na maumbo makubwa wakajipatia au kujipachika u-Hulk hususani nchini Marekani.

Katika Bara la Asia kulikuwa na Hulk wa Iran na sasa amejitokeza Hulk wa Pakistan, ambaye ndiye makusudio ya makala haya.

Akiwa na uzito wa kilo 436, Arbab Khizer Hayat ameonesha matendo mengi kama vile kusimamisha trekta kwa mikono mitupu.

Pia ana kundi kubwa la wafuasi katika mji wake wa nyumbani wa Mardan, Pakistan.

Arbab Khizer Hayat, maarufu kama Hulk wa Pakistan mwenye umri wa miaka 25 na urefu wa futi 6 na inchi 3 ana ndoto za kuiwakilisha Pakistani katika mchezo wa mieleka wa uzito wa juu unaotambuliwa na Chama cha Mchezo wa Mieleka Duniani (WWE).

Hayat ni mtu mwenye mwili mkubwa, anayehaha kuhakikisha analinda umbo lake hilo la kutisha.

Mieleka na unyanyuzi wa vitu vizito ni mchezo unaopendwa na wengi.

Hata hivyo, linapokuja suala la mtu kudai kuwa na nguvu kuliko wote Pakistan huku akijiaminisha kuwa ni mwenye nguvu dunia bila kuthibitisha hilo, kunashangaza wengi.

Hayat alianza kunenepa katika umri mdogo na akavutiwa na mchezo wa mieleka na kunyanyua vitu vizito na hivyo kujiwa na ndoto ya kuwa mtu mwenye nguvu duniani.

Nilianza kunenepa nikiwa mdogo lakini nilitambua kwamba nahitaji kujiunga na mchezo wa kuinua vitu vizito na kuwa mtu mwenye nguvu duniani. Hivyo, niliendelea kuongeza uzito,” Hayat anasema.

“Namshukuru Mungu kwa kunipa umbo hili. Haitachukua muda kabla ya kuingia katika uwanja wa unyanyuaji vitu vizito duniani,” anasema.


Hayat, ambaye pia anajulikana kama Baba Khan, amejipatia umaarufu katika mitandao ya jamii baada ya kuweka video zenye kuonesha nguvu zake kwa kuzuia magari pasipo kutumia nguvu nyingi na au kuyainua kirahisi rahisi.

Mnyanyua vitu vizito huyo hivi karibuni alidai kunyanya kilogramu 5000 (tani 5) katika tukio lililofanyika nchini Japan mwaka 2012.

Anadai kutumia zaidi ya kalori 10,000 kwa siku ikiwamo mayai 36 kwa ajili ya kifungua kinywa, kuku wanne, kilo tatu za nyama nyekundu na lita tano za maziwa.

Tajiri huyu kutoka Mardan amekuwa akitukuzwa katika mji wake huo wa nyumbani.

Hata hivyo, watu wengi wanadai kwamba jitu hili linalofanana na hulk ni feki.

Kuna watu wengi duniani wanasema kwamba madai ya Hulk huyu wa Pakistan ni feki na kwamba uhalisia wa video zake unazua maswali mengi.

Video za Hayat, ambazo zinaonesha mtu huyo mzito akidhibiti magari kwa kutumia nguvu kidogo huku magari yakijaribu kufurukuta kuchomoka kutoka mikononi mwake bila mafanikio.

Lakini kiuhalisia nguvu kubwa inayotumiwa na magari hayo ilipaswa kukata kamba, ambazo zilichomekwa tu, lakini hakuna kitu kama hicho kinachoonekana kutokea.

Lingine linalozua maswali ni kwamba Hayat daima anaonekana kuvaa nguo za kitamaduni za jamii ya Pathani nchini humo na kujifunika kwa kashida (shali).

Hilo linampatia fursa ya kuuonesha mwili wake kuwa mnene mno kuliko uhalisia.

Madai ya rekodi yake ya kunyanyua uzito wa kilogramu 5000 haijathibitishwa popote na imedaiwa ni uongo.

“Hakuna mtu anayeweza kuvunja rekodi hii,” alisema. Baba pia alidai kwamba alipata medali kutoka WWE na jina lake liko katika Kitabu cha Rekodi za Dunia (Guinness Book of World Records. Hata hivyo madai yake hayo hayajathibitishwa.

Anasema kwamba hakuna utamaduni wa kunyanyua vitu vizito Pakistan na hivyo yeye amelenga kubadili utamaduni huo.

Wakati Hayat anadai kuwa ni mtu mwenye nguvu kuliko wote Pakistan pia anadai hana tatizo lolote la kiafya linalotokana na unene na uzito wake huo mkubwa.

Hata hivyo, kwa kuzingatia masuala ya kiafya, mnyanyua vitu vizito huyo anaweza asidumu katika ulingo wa WWE, ambako stamina ni muhimu zaidi kuliko nguvu.

Chaguo la Hayat kuwa na uzito mkubwa wa kiasi hicho, kwa mujibu ya wataalamu wa afya ni hatari na hauna afya, hata kama umelenga ubingwa wa WWE au kuweka rekodi ya kuwa mtu mwenye nguvu kuliko wote duniani.

Kuna tofauti kati ya kuwa na uzito mkubwa na kuwa mwenye nguvu na ni wazi jitu hilo la Pakistan liko mbali na ukweli.

Nyama Yaanza Kutengenezwa Maabara,Inafanana na Nyama ya Ng'ombe Hadi ladha.

DUNIA inabadilika kwa haraka kutokana na maendeleo katika sekta mbalimbali. Teknalojia nayo inakua kwa kasi huku ikitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya binadamu. Siku hizi Dunia inashuhudia uvumbuzi wa teknalojia za kisasa katika nyanja za kilimo, afya, nishati na nyingine nyingi.

Leo katika safu hii, nitajadili namna ambavyo wanasayansi walivyofanya jitihada za kutengeneza nyama katika maabara. Ndiyo, sasa si lazima kuhangaika kufuga na kupata usumbufu wa kutunza wanyama ili uweze kupata nyama.

Wote mtakubaliana na mimi kuwa, aina zote za vyakula vinavyotumiwa na binadamu inatokana na mimea na wanyama. Mamilioni ya wanyama huchinjwa kila siku duniani kwa ajili ya kupata kitoweo.

Uchinjaji wa wanyama umekuwa mkubwa kuliko uzalishaji jambo ambalo limewafanya wanasayansi kufikiri namna ya kutengeneza kitoweo hiki muhimu pasipo kuhusisha kuchinja mnyama.

Rasilimali nyingi zimekuwa zikitumika kulisha wanyama, kuwachinja na kusafirisha, pia kumekuwapo upotevu mkubwa wa maji na nishati katika mzunguko mzima wa kupata kitoweo hiki.

Ufugaji wa wanyama ambao hutupatia nyama unazalisha gesi ya methane ambayo inamchangio mkubwa katika mabadiliko ya tabianchi, wanasayansi wanataka kuondokana na haya yote kwa kutafuta mbinu mbadala ya kuzalisha nyama.

Kwa upande mwingine, wanyama hufungiwa ndani kwa maisha yao yote. Wanyama pia huchinjwa kikatili ili kuweza kupata nyama. Pamoja na haya yote, ni vigumu kufikiri maisha ya binadamu bila kula nyama.

Utamaduni wa kula nyama ni mkongwe duniani na kwa vyovyote vile haitakuwa rahisi kuufuta. Kwa kutambua ukweli huu, wanasayansi wameaanza kutengeneza nyama maabara waliyoipa jina la nyama ya Vitro au Vitro meat kwa kimombo.

Nyama ya Vitro huzalishwa maabara. Kwa kawaida nyama hutengenezwa kutokana na kemikali ndogo inayojulikana kitaalamu atoms. Kama unaweza kutengeneza atoms kwa njia tofauti na ya kawaida, basi pia unaweza kutengeneza nyama.

Ukipewa vipande viwili vya nyama kimoja kilichotokana na mnyama aliyechinjwa na nyingine aina ya Vitro ambayo hutengenezwa maabara ni vigumu kuelezea tofauti yake kutokana na kufanana kwa muonekano na hata ladha.

Maabara sasa inafanya kazi ya kutengeneza nyama ambayo ni sawa na nyama uliyozoea kununua buchani. Profesa wa Molecular Biology, katika Chuo Kikuu cha Stanford, alinukuliwa na gazeti la The Gurdian la Uingereza akisema inawezekana kuondokana na usumbufu wa kufuga na kuchinja wanyama kwa kuwa nyama sasa inaweza kutengenezwa maabara.

“Sina nia ya kutengeneza vyakula vipya kwa watu wasiokula nyama. Natengeneza chakula kwa ajili ya wanaokula nyama na ambao wana nia ya kula nyama. Hii itawasaidia kupata nyama bila shurba.

“Nyama ya Vitro haitokani na kiumbe hai hivyo haiwezi kufa na hii naletea tofauti kubwa katika upatikanaji wake. Kiuchumi, gharama za uzalishaji wake ni kubwa na hivyo kufanya uzalishaji mkubwa kuwa changamoto.

Pia kutokana na ushawishi wa wafugaji wakubwa Marekani na sehemu nyingine duniani, inawezekana kuwa na vikwazo vya kisheria,” anasema Profesa huyo.

Gharama kubwa za uzalishaji wa nyama ya Vitro inaweza kuwa ndiyo kikwazo kikubwa katika uzalishaji wake. Hata hivyo, ugunduzi zaidi kwenye teknalojia ya uzalishaji wake itaweza kupunguza gharama.

Kampuni kubwa ikiwamo New Harvest na Modern Meadow zinafanya kazi kuhakikisha kuwa nyama hii inazalishwa kwa wingi na kuwafikia walaji wengi.

Breaking News ..!! Rais Magufuli Amteua Anne Kilango Malecela kushika nafasi hii serikalini


Rais John Magufuli amemteua Anne Kilango Malecela kuwa mbunge, huku akiwa mkuu wa mkoa pekee kwenye utawala wa awamu ya tano aliyedumu na wadhifa huo kwa muda mfupi wa siku 29.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Rais Ikulu, imeeleza kuwa Kilango ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za Bunge.

Uteuzi huu unakuja siku chache kabla ya Rais Magufuli kumteua aliyekuwa  mbunge wa kuteuliwa ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Kazi, Dk Abdallah Possi kuwa balozi. Tayari, Dk Possi amekabishi barua ya kujiuzulu ubunge.

Hata hivyo, Kilango anarudi katika ulingo wa siasa huku akiwa amepitia katika misukusuko kadhaa ikiwamo kupoteza kiti cha ubunge Same Mashariki, mkoani Kilimanjaro.

Kilango aliteuliwa Machi 13, 2016 na uteuzi wake kutenguliwa Aprili 11 mwaka huohuo, kutokana na kutoa taarifa kwamba Mkoa wa Shinyanga aliokuwa akiuongoza haukuwa na watumishi hewa.

Safari yake ya kisiasa

Mbunge huyo mteule alizaliwa Januari 9, 1956 Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Mwaka 1979-1983 alikuwa mwalimu Sekondari ya Kisutu jijini Dar es Salaam; 1983-1991 alikuwa Mhasibu Msaidizi Shirika la Ndege Tanzania (ATC); na 1991-1993 alikuwa Mdhibiti wa Fedha Shirika la Ndege la Gulf.

Pia, mwaka 1993-1994 alikuwa Mhasibu Shirika la Ndege la KLM; 1994-2000 alikuwa akijishughulisha na ujasiriamali kwenye kampuni yake ijulikanayo kama Ninna Bridal Centre; 2000-2005 aliteuliwa ubunge na Rais Benjamin Mkapa; na 2005-2015 alikuwa mbunge wa kuchaguliwa Same Mashariki

 

Gallery

Popular Posts

About Us