KINGAZI BLOG: 10/29/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 29 October 2016

KUTANA NA HUYU MWANAMKE ALIYEAMUA KUJIOA MWENYEWE BAADA YA KUKOSA MCHUMBA


Yasmin Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume wake atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe.
Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.
Duru zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake mwenyewe katika makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na wageni wengine waalikwa.Kwa sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio, kwani ni kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati ya watu wawili.

Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida bila ya mchumba.
Kulingana na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo, sherehe hiyo ilionekana kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani makavazi hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi zao hapo.
Aliposikia kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini alikuwa anapanga kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea mwenyewe.


"Eleby alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi na mtu mwenye nia ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr ambaye anasema harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.
Anasema anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba mtu anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu kujipenda kwanza kabla ya kupendwa."watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani.

"ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi.

Ujumbe wa Rais Magufuli kwa Watanzani katika siku yake ya kuzaliwa

Leo Oktoba 29 ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli ambapo alizaliwa Oktoba 29, 1959. 

 

Rais Magufuli alizaliwa mkoani Geita na kitaaluma yeye ni mwalimu aliyebobea katika somo la Chemistry.

 

Katika siku yake hii ya kuzaliwa, Rais Magufuli amewashukuru Watanzania wote kwa kuendelea kumuombea ambapo amesema kuwa ataendelea kufanyakazi kwa bidii na kuwatumikia watanzania wote kwa ajili ya maendelo ya nchi.

 

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Magufuli ameandika jumbe hizi;

MWANAMKE AUAWA KWA KUPIGWA MAWE, KISA KUCHEPUKA NJE YA NDOA

Ripoti zinasema kuwa takriban watu 200 akiwemo gavana wa eneo hilo walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke huyo kwenye mji wa Barowe. Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Wadadisi wanasema kuwa mauaji hayo ni ishara ya ushawishi wa kundi la Al shabaab hata baada ya kushambuliwa na serikali ya Somalia pamoja na vikosi vya muungano wa Afrika. 
Mji wa Barowe ambao uko umbali wa kiomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu umekuwa ngome ya Al Shabaab.

Download Mp3 : Solidstar Ft. Diamond Platnumz - Money [New Song Audio]



Download Mp3 : Solidstar Ft. Diamond Platnumz - Money [New Song Audio] Enjoy Full Music

USIPITWE NA HII!!!! WAUMINI WA KANISA WAKATWA SEHEMU ZAO ZA SIRI ILI WAMUONE MUNGU

Image result for Gurmeet Ram Rahim Singh
Ishu ya imani ni ya mtu binafsi na kila mtu ana uwezo wa kuamini kile anachoona ni sahihi kwa mtazamo wake na mtu anapotokea kumuamini kiongozi wake wa dini kwa asilimia kubwa hutekeleza yale anayofundishwa.Sasa hii ya leo inamuhusu mhubiri maarufu wa dini India

Image result for gurmeet ram rahim
Akiwa katika moja ya mafundisho yake
ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni hamsini duniani.
Image result for gurmeet ram rahim

Gurmeet Ram Rahim Singh anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha majeruhi kwa tuhuma za kuwashawishi wafuasi wake 400 kukata sehemu zao za siri ili waweze kuwa karibu na Mungu.
HII HAPA VIDEO YAKE KATIKA MOJA YA MAHOJIANO ALIYOWAHINKUFANYA NA KITUO KIMOJA CHA TELEVISION.

HIZI HAPA HABARI KUU KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 29

MPYA:HAYA HAPA MAJINA 63,773 YA WANAFUNZI WOTE (BATCH ZOTE) WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO VIKUU MBALIMBALI TANZANIA 2016/2017

 

Gallery

Popular Posts

About Us