KINGAZI BLOG: 03/16/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday, 16 March 2017

SHILAWADU!! DIVA WA CLOUDS APIGWA CHINI KIPINDI CHA ALA ZA ROHO NA HUYU NDIYE ALIYEMBADILI...!!!

Eeh ila wambea nimewavulia kofia, wiki kadhaa nilisikia makelele kuwa diva katimuliwa clouds ,diva mwenyewe akatoa mchambo wa haja kukanusha,kumbe kweli bibie kitumbua kimeingia mchanga,looh maskini pole diva[IMG]http://www.jamiiforums.com/mobile-gallery/aefeb3dfe6cff563c34f6f285d53abdf.jpg[/IMG]
SOURCE :JF

PICHA++Ile Ndege ya wanawake pekee kutoka Malawi tayari imetua Tanzania leo


 Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limefanikiwa kukamilisha safari ya ndege iliyosimamiwa na wanawake pekee.

Ndege hiyo imetua katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.

Marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege hiyo wote walikuwa wanawake, na ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuandaa safari kama hiyo.

Ndege hiyo ilianza safari yake mjini Blantyre na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar es Salaam.

Shirika hilo la ndege, lilisema lengo la kuandaa safari hiyo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".

 Ndege hiyo ilikuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.
Bi Mwenifumbo, 24, ambaye alisomea urubani jijini Addis Ababa, Ethiopia amemwambia Munira Hussein wa BBC kwamba alihamasishwa kuwa rubani na baba yake ambaye pia alikuwa rubani.



MAKONDA KUSHTAKIWA MAHAKAMANI WIKI IJAYO SAKATA VYETI FEKI.


HATIMAYE Meya wa Ubungo Mh. Boniface Jacob anakusudia kufungua shauri mahakamani la kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuonesha vyeti vyake ili kuondoa utata uliojitokeza hivi karibuni dhidi ya kiongozi huyo wa mkoa.Kesi hiyo inatarajiwa kufunguliwa Jumatato ijayo ya tarehe 20/03/2017.Stay tuned.Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema Jumanne wiki ijayo atafungua kesi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na madai ya kuwa na vyeti feki.Jacob pia amesema, atamshtaki Makonda katika sekretarieti ya maadili ya utumishi wa umma, tume ya haki za binadamu pamoja na utawala bora. Amesema kesi hiyo ambayo itaongozwa na mawakili Tundu Lissu pamoja na Peter Kibatara.“Tunachosubiri ni wanasheria wamalize mchakato wa uchaguzi Chama cha Wanasheria Tanganyika (TSL) na mara watakaporejea kutoka Arusha tutakwenda mahakamani” amesema Jacob.

Mwananchi

UTATA KIFO CHA BODA BODA,..... IRENE UWOYA ASAKWA NA POLISI.


Ni msala? Nyota wa sinema za Bongo, Irene Uwoya anadaiwa kusakwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni ili kutoa maelezo yake kwa kina kufuatia kifo cha kijana Fahari Colos katika ajali ya gari iliyotokea Masaki jijini hapa.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja, Uwoya anatakiwa kituoni hapo kwa vile, kifo cha Fahari kina utata wa simulizi kutoka kwa ndugu na kwa askari polisi waliokuwepo kwenye eneo la ajali.

Fahari alifariki dunia Machi 12, mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia ajali hiyo mbaya aliyoipata siku hiyohiyo. “Kama umesoma mitandaoni utakuwa umeona kuhusu ajali ya yule dereva wa bodaboda, sasa Irene Uwoya ana sehemu kubwa ya maelezo kutokana na ajali mpaka kifo cha yule kijana.

“Tumekuwa tukimtafuta kuanzia siku ya tukio lengo letu aje kituoni atoe maelezo maana na yeye ana sehemu ya maelezo muhimu. Lakini kama amezima simu au sijui ameiseti kiaina,” alisema afande mmoja na kutaka kusitiriwa kwa jina lake.

Amani juzi lilimtafuta Uwoya mwenyewe na kumuuliza kuhusu madai ya kutafutwa na polisi ambapo alisema:

“Mimi niko tayari kwenda kutoa meleozo yangu polisi, tena nitayatoa kwa uzuri sana. Kama wananitafuta safi sana.”

Kuhusu simulizi ya tukio hilo, Uwoya alisema:

“Machi 12, usiku nikiwa naelekea Masaki, kufika Colosseum Hoteli nilikuta ajali mbaya sana. Nilimkuta mkaka mmoja kagongwa na gari, yeye alikuwa na pikipiki.

“Nikasimama pale nikakuta polisi wapo na gari lao na ndiyo kwanza wanapiga stori tu, hawana habari watu wanaomba msaada.

“Niliwauliza polisi kwa nini mtu anakufa wanamuangalia tu? Wakajibu wao wafanyaje wakati hakuna gari la kumbeba! Nikawaambia gari lenu si hilo hapo? Wakasema haliwezi kumbeba, basi nikawaambia watu wampakie kwenye gari langu ili nimkimbize hospitali.

“Ile nataka kuondoka tu, wakaniambia nikachukue PF3 kwanza halafu niende hospitali, nikawaambia mtu anakufa nyie mnasema nikafuate PF3? Mimi sifuati PF 3, wakaniambia watapiga simu hospitali wasimpokee.

“Tukaenda na baadhi ya watu mpaka Hospitali ya Mwananyamala, kufika akapokelewa na tulikuta watu wa ajali wawili wamekaa karibu saa nzima.

“Niliumia sana! Tukaandikiwa vitu vya kununua kwa ajili ya majeruhi, kwenda nje hakukuwa na dawa, tukapata baadhi ya vifaa wakaanza kumhudumia! Baada ya muda difenda ikaja ikamchukua dereva wangu eti alikuwa anapiga kelele na kutukana wakati tulikuwa tunapiga kelele wamhudumie mgonjwa.

“Baada ya muda ndugu zake majeruhi wakajitokeza, mgonjwa akahamishiwa Muhimbili. Mimi nikamfuata dereva wangu. Kabla Sijafika kituoni akanipigia simu kwamba wamemuachia.

“Jana asubuhi (Machi 13) napiga simu kwa ndugu wa mgonjwa naaambiwa amefariki dunia. Niliumia sana kwa kweli. Sasa kama wanasema wananitafuta askari ili wanihoji sawa tu mimi nipo sana, nimejaa tele.”

Juzi, Amani lilimpigia simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzana Kaganda ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa madai hayo, lakini simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa

Shilawadu!!!! Inasemekana....Penzi la Lulu na Majizzo tayari lime....!!SOMA ZAIDI HAPA👇👇


Lile penzi mubashara kati ya staa wa filamu nchini, Lulu Michael na Mkurugenzi wa E-fm maarufu kama Majizo, linadaiwa kuingia kidudu mtu.

Za kunyapia nyapia zinadai eti bibie huyo anatuhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina. Hata hivyo chanzo kamili cha wawili hao kuwa katika hali ya sintofahamu bado hakijajulikana ila wawili hao sasa hivi hawakai zizi moja kama zamani.

Tundu Akamatwa Na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma

Mbunge Tundu Lissu amekamatwa na jeshi la polisi asubuhi hii nyumbani kwake na kupelekwa ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma.

 

==>Huu ni Ujumbe wa Tundu Lissu alioutumia mtandaoni

Wandugu wapendwa. Ninaandika haya nikiwa nyumbani kwangu Dodoma. Najiandaa kwenda mahakamani kwa ajili ya uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi wa TLS.

Ninawapa taarifa kwamba nimefuatwa nyumbani na askari wawili kutoka ofisi ya RPC Dodoma. Sijazungumza nao bado lakini ni wazi wana maagizo ya kunikamata na kunizuia kuja Arusha kwenye Uchaguzi wa TLS. Wameshindwa kuzuia uchaguzi wetu mahakamani. Sasa, kama kawaida ya serikali za kidikteta kila mahali, wanatumia mabavu ya kijeshi.

Wito wangu kwenu mawakili wa Tanzania:

Nendeni Arusha mkachague viongozi wa TLS watakaopigania haki za binadamu, utawala wa sheria na demokrasia. Msipofanya hivyo hakuna mtu yeyote, hata ninyi mawakili, atakayepona kwenye utawala wa aina hii.

Kumbuka, kama Nimrod Mkono anaweza kufungiwa ofisi na TRA ni wakili gani mwingine aliye salama??? Kama wakili anaweza kukamatwa mahakamani kwa kufanya kazi yake ya uwakili, ni nani miongoni mwetu aliye salama??? Nendeni mkapige kura kukataa mfumo wa aina hii.

Mimi naenda mahabusu, na pengine, gerezani. Nawaombeni kura zenu ili niweze kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu. 

Hiki sio kipindi cha kuwa na viongozi wanaojipendekeza kwa wanaokandamiza haki za watu wetu na haki za mawakili wetu. 

Hiki ni kipindi cha kuwa na viongozi watakaopigania haki zenu na haki za watu wetu. Mnanifahamu. Nipeni jukumu hili la kuwaongoza kwenye giza hili nene. Msikubali kuyumbishwa.

Na wachagueni pia Makamu wa Rais, Mweka Hazina wajumbe wa Governing Council watakaokuwa na msimamo kama wa kwangu.

Nawatakieni kila la kheri. I'll think of you all wherever they'll take me to, wherever I'll be incarcerated. This too shall pass. The race of man shall rise again. It always has. Nimemwambia na mke wangu naye aende Arusha akapige kura. So, everybody to Arusha. Go vote your consciences.

All the best.

TL

Makonda azidi kukaliwa kooni Sakata la Vyeti.


Rais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe Spunda amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi juu ya utata wa jina lake unaozidi kuvuma mitandaoni

Utata huo unadaiwa kutokana na mkuu huyo wa mkoa kutumia cheti cha mtu mwingine cha kidato cha nne kujiendeleza kielimu. 

Rungwe ametoa ushauri huo  kupitia kipindi cha maswali na majibu cha Kikaangoni , akimsisitiza Makonda kuweka ukweli mezani na kuacha kupiga chenga za mchangani kwa maana akiendelea kukaa kimya watu wanazidi kuamini uvumi huo.

"Namshauri Mkuu wa mkoa ambaye ni kama mwanangu, atoke azungumze ili kumaliza huu utata wa vyeti, asimsumbue Rais ana mambo mengi" Amesema Rungwe

Pia, amemtaka kuacha kulia madhabahuni, kwakuwa hilo halitamsaidia kwa kuwa kulia siyo jibu, na atambue kuwa ofisi hiyo aliyopo sasa siyo yake bali ni wananchi, hivyo kila alichokikuta atakiacha.

"Siku moja nafungua 'ipad' yangu namuona Mkuu wa Mkoa analia mbele ya kanisa halafu mchungaji anambembeleza kama mjukuu wangu, mimi namwambia kulia kwake hakusaidii kitu yeye anapaswa kusema ukweli tu kama hilo jina siyo la lake halisi ila ni la kisanii sisi tutamuelewa". Alisema Rungwe

Kwa upande mwingine, Rungwe ambaye ni wakili msomi, ametoa ushauri wa kisheria kwa watu wenye ushahidi na suala hilo kwenda mahakamani kwa kuwa sheria inaruhusu mashtaka binafsi, ingawa bado Jamhuri itahitajika zaidi kuisimamia kesi hiyo.

Aidha Rungwe aliendelea kufunguka kwa kumtaka Makonda kuacha kung'ang'ania nafasi ambazo anastahili katika nafasi hiyo huku akimpiga kijembe kuwa mwanaume hachagui kazi aende akabebe hata zege kama hana ujuzi wa kufanya.

Kwa upande mwingine Mzee Spunda amemuomba Rais Magufuli kuliingilia kati suala hilo kama alivyofanya kwa maafisa wengine wa serikali.

Rungwe alilazimika kutoa ushauri huo kutokana na swali aliloulizwa kuhusiana na maoni yake kuhusu vita dhidi ya dawa kulevya ambapo amesema kuwa anaunga mkono vita hiyo, isipokuwa njia iliyotumika ya kutaja majina ya watu hadharani bila uhakika, haikuwa nzuri.

Wolper Azidi Kufunguka Mambo Juu ya Harmonize,Safari Hii Kayaanika Haya Hadharani Kweupee!!


Jacqueline Wolper amevitaja vitu vitatu ambavyo vimemvutia kuwa kwenye mahusiano na Harmonize.

Muigizaji huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, vitu hivyo ni upole wake, ukarimu pamoja na kuijua dini.

“Upole, Ukarimu na anapenda dini na anaijua dini kabisa. Mimi naamini asingekuwa mwanamuziki angekuwa maalimu fulani hivi,” amesema Wolper.

Wakati huo huo Harmonize kwa sasa ameachia wimbo mpya ‘Niambie’ ambao amemuimbia mpenzi wake Wolper.

Kauli ya Vanessa Mdee kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kutoka 'Selo'


Vanessa Mdee amezungumza kwa mara ya kwanza tangu atoke rumande Jumatatu hii baada ya kushikililiwa na polisi jijini Dar es Salaam kuanza Jumatano ya wiki iliyopita.

Muimbaji huyo wa Cash Madame amewashukuru wote waliompa pole wakati alipokuwa ameshikiliwa na kudai kuwa ataachia wimbo mpya wiki hii.

“I love you all sooo much 😚,” ameandika kwenye Twitter.

“It is by his Grace alone 💜 Utukufu kwa Mungu wetu wa miujiza.

Thankyou for your kind tweets and posts. I got a glimpse of some of them and this kinda loooooove 😍,” ameongeza.

“AND incase you were wondering. I am doing so fine. Infact new music out THIS WEEK 😙.”

Maneno ya Paul Makonda Baada ya Kutimiza Mwaka Mmoja Kama Mkuu wa Mkoa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Machi 15, 2017 anatimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Machi 13, 2016 na kuapishwa Machi 15, 2016.

==>Haya ni Baadhi ya Maneno Yake

1.Namshukuru Rais Magufuli kwa kusikiliza kauli ya Mungu na kunikabidhi mamlaka ktk mkoa huu wa Dar.

2.Navishukuru sana Vyombo vya Habari kwa kuwa daraja kati ya Serikali ya Mkoa na wananchi. Wamefanya kazi kubwa!

3.Nawashukuru sana vijana tuliowakamata wa mwanzo(TID na wenzake), wamekuwa mfano mzuri kwa wenzao na Mungu awasaidie

4.Mwaka wangu wa II nikiwa kama RC wa Dar, kasi itaongezeka maana nimekomaa sasa. Nitahakikisha jiji linarudi kwny mstari.

5.Kuna makampuni ya barabara mawili nimeshayapiga marufuku kwa sababu ya kujenga barabara chini ya viwango.

6.Katika vitu nimeweka msingi mzuri ni kinondoni, kesi za ardhi zinasikilizwa mpaka jumamosi

7.Kazi hii nimepewa na Mungu, acha idadi ya wanaomchukia Makonda waongezeka lakini niwe na uhakika na Mungu wangu

8.Tumeamua kufanya vitu hadharani kwa sababu hatutaki kupokea rushwa wala fedha haramu

9.Hatuna kisasi na mtu, ndio maana upande huo wanapigana sisi tunacheka

10.Kupitia fedha za dawa za kulevya, watu wamejenga maghorofa yanakwenda kwa kasi sana na wamefanya hata thamani ya viwanja ipande

11.Fedha hizi za dawa za kulevya zinaenda kukauka DSM ili kila mtu ale kwa jasho lake

12.Tutaanza mfumo wa kutumia kadi ili tukusanye kodi yetu na kila mtu ale kwa jasho lake, kuna watu wanaficha fedha

13.Kipindi hiki ni cha kazi. Nawapongeza wote wanaofanya kazi kwa bidii na kuifanya Serikali isimame kidete

14.Changamoto mojawapo niliyokutana nayo ni MUDA! Muda hautoshi, nahitaji hata miaka kadhaa ili kumsikiliza kila mwananchi

15.Changamoto nyingine ni mazoea ya Watendaji wa Serikali ktk kutoa huduma. "Njoo kesho" imekuwa kero kwangu na kwa wananchi

16.Kuzungushwa kwa wananchi kunapelekea changamoto katika za Serikali za Mitaa kuletwa ofisini kwangu. Hili nalo ni tatizo!

17.Nampongeza sana Kamishna Sirro na Awadhi (wa Usalama barabarani) kwa kusimamia ulinzi na usalama jijini Dar

18.Milio ya risasi ilikuwa kawaida Dar, watu waliogopa hata kwenda Mlimani City kwa hofu ya kuporwa. Tumeyakomesha yote hayo

19.Mtu anataka nikae kimya wakati wananchi wangu Dar wanateseka kwa matumizi ya DawazaKulevya... Nauliza "Wewe ni NANI?"

20.Tunapambana kupigania ndoto za vijana na matumaini ya wazazi wao. Haijalishi tumechelewa kiasi gani lakini hatutoacha!

21.Wapiga dili wa Bandarini jijini Dar wamekuwa wakisumbua kwa fedha zisizo halali na kuwasumbua wafanyabiashara halali

22.Sibabaishwi na watu wanaonichukia wakati nikitekeleza majukumu niliyopangiwa na Rais Magufuli kama Mkuu wa Mkoa.

23.Bureau de Change zinatumika kufichia pesa haramu. Wiki ijayo moto utawaka, lazima tushughulikie maficho haya.

24.Sasa foleni jijini Dar imepunguzwa kwa kiwango kikubwa na askari. Ukifurahishwa na trafiki toa shukrani zako, tuwape moyo.

25.Mwaka huu wa pili tutakazia sana kwenye utumishi. Nitaanzia kwenye Serikali za Mitaa nione jinsi wanavyowasaidia wananchi.

26.Nataka mwananchi apate majibu kamili aendapo Ofisi ya Umma. Kama hawawezi kumsaidia waende wao ofisi ya juu sio mwananchi.

27.Wanaoishi mabondeni jijini Dar na wana hati halali nitawapa viwanja. Watendaji waliotoa hizo hati nitawashughulikia!

28.Najua wengi wanaoishi mabondeni wamepangishwa na waliolipwa fidia. Huwezi kuwa na akili timamu ukakubali kupanga bondeni

29.Hivi karibuni nitaelekeza wapi showroom za magari zinatakiwa ziwe jijini Dar. Nataka magari yote yauzwe eneo moja

30.Ninawashukuru wanasheria wetu 35 wanaotoa msaada na ushauri wa kisheria bure kwa wananchi wa jiji la Dar wasio na uwezo

31.Tumepewa eneo kubwa la kujenga kambi kwa ajili ya wahanga wa DawazaKulevya. Hii itatusaidia kufuatilia mienendo yao

32.Hadi sasa tuna watu 11,854 jijini Dar waliokubali kuacha matumizi ya DawaZaKulevya kwa hiari. Haya ni mafanikio makubwa

33.Wengine tukiwaita Kituo cha Polisi wanatumia Colgate na Chumvi ili wasigundulike ktk vipimo. Tuna mbinu mpya za kuwapima

34.Kuna wanaowatumia watoto wadogo kufanya uhalifu na kabla ya hapo wanawavutisha bangi. Tunawasaka na tutawakamata!

HABARI KUU KATIKA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI YA TAR 16 / 3 / 2017



































 

Gallery

Popular Posts

About Us