Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limefanikiwa kukamilisha safari ya ndege iliyosimamiwa na wanawake pekee.
Ndege hiyo imetua katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.
Marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege hiyo wote walikuwa wanawake, na ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuandaa safari kama hiyo.
Ndege hiyo ilianza safari yake mjini Blantyre na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar es Salaam.
Shirika hilo la ndege, lilisema lengo la kuandaa safari hiyo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".
Ndege hiyo ilikuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.
Bi Mwenifumbo, 24, ambaye alisomea urubani jijini Addis Ababa, Ethiopia amemwambia Munira Hussein wa BBC kwamba alihamasishwa kuwa rubani na baba yake ambaye pia alikuwa rubani.
0 comments:
POST A COMMENT