
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imezindua mpango maalum unaomuwezesha mteja kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu, na kueleza hatua 13 za kufuata ili kupata huduma hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jana jijini Dar es Salaam, alisema huduma hiyo ni ya hiari na ili mtu...