KINGAZI BLOG: MICHEZO

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Saturday, 27 May 2017

Klabu ya Everton Yathibitisha Kutua Tanzania Kucheza na Simba na Yanga..!!!


Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter wa klabu ya soka ya Everton, umethibitisha kuwa klabu hiyo kuwasili nchini mwezi Julai na itakuwa ni timu ya kwanza inayoshiriki Ligi kuu nchini Uingereza kucheza na timu za Afrika mashariki.

Ujio wa Everton ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi, Vilabu vinavyo tarajiwa kunufaika na ujio huo ni vile ambavyo vipo chini ya udhamini wa kampuni ya Michezo ya kubashiri ya SportPesa. Kwa hapa nchini mpaka sasa kampuni hii imeingia mkataba na klabu tatu ambazo ni Simba SC, Yanga SC pamoja na Singida United .

Kwa mujibu wa Kampuni ya SportPesa, wameandaa ligi ijulikanayo kama SportPesa  Super Cup , inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 5  / 6 / 2017, kwa kushirikisha jumla ya timu 8  kutoka mataifa mawili, Tanzania na Kenya, na mshindi wa mashindano hayo atacheza na timu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Mshindi wa michuano hiyo mikubwa atapata kiasi cha Dola za kimarekani Elfu thelathini (USD 30,0000) na mshindi wa pili wa michuano hiyo anatarajia kupata kiasi cha Dola za kimarekani Elfu kumi (USD 10,000).

Kutokana na kuthibitisha kwa klabu ya Everton bilashaka mshindi wa mashindano hayo atacheza na klabu hiyo kongwe iliyoanzishwa  mwaka 1978.

Tuesday, 23 May 2017

Taarifa ya Yusuf Manji Kutangaza Kujiuzulu Yanga, Tamko Rasmi la Klabu Hili Hapa

Baada ya taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kueleza kuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuf Manji ameachia ngazi kuiongoza Yanga, tamko rasmi limetolewa juu ya ukweli wa suala hilo.

Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Mkwasa ametoa tamko kwa kusema kuwa hajapata taarifa rasmi juu ya ukweli wa suala hilo lakini amethibitisha kuwa bado hajawasiliana na Manji kama kweli amechukua uamuzi huo.

Akizungumza juu ya taarifa hizo, Mkwasa alisema: “Sijapata taarifa hizo rasmi, mimi ndiyo mtendaji mkuu wa klabu, bado sijakabidhiwa barua kwa kuwa sifanyi kazi kwa kutumia mitandao.

“Tunajua kuwa mitandaoni kuna taarifa nyingi ambazo siyo za kweli na zipo nyingine ambazo zimesababisha baadhi ya wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, hivyo nasubiri kuona kama ni kweli, basi nitapatiwa barua rasmi na nitatoa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo.”

Alipoulizwa kama amewasiliana na Manji hivi karibuni, alisema: “Nimekuwa nikiwasiliana naye kwa njia ya barua pepe kwa masuala ya kiofisi lakini sijakutana naye siku mbili hizi.”

Tangu mapema leo Jumanne kumekuwa kukisambaa barua ambayo inaonekana imesainiwa na mwekiti huyo akielezea uamuzi wake wa kutangaza kujiuzulu. Barua yenyewe inayosambaa hii hapa:





Thursday, 11 May 2017

Nani anakwenda fainali ya Europa League leo?


Mechi ya kwanza ambapo Manchester United walisafiri kwenda nchini Hispania Marcus Rashford alifanikiwa kuwapa Manchester United bao la ugenini dhidi ya Celta Vigo.

Leo Celta Vigo wako Old Traford huku mashabiki zaidi ya 30,000 wakiwa wamesafiri na timu kutoka Hispania hadi Uingereza jambo linalompa faraja kocha wao Eduardo Berizzo.

“Ni faraja sana kwetu kwani inaonesha mashabiki hawa wako bega kwa bega na sisi, baada ya kufungwa mchezo wa kwanza hawajatuacha wamekuja na sisi hapa leo” alisema Berizzo.

Lakini Manchester United ambao wamerudi katika nafasi ya 6 kwenye ligi baada ya ushindi wa Arsenal hapo jana, watahitaji sana ushindi ili kucheza fainali ambayo inaweza kuwasaidia kushiriki Champions League msimu ujao.

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema ni muhimu sana kwao kama Manchester kushinda kombe hilo kwani ndio kombe pekee ambalo hawajawahi kulishinda.

“Hakuna aliyewahi kubeba kombe hilo hapa, nadhani itakuwa muhimu sana kwa wachezaji na timu kwa ujumla, hatupaswi kuwaza kuhusu mchezo uliopita bali tunapaswa kuwaza nini kinafuata” alisema Mourinho.

Katika mchezo mwingine Lyon ambao mchezo wa kwanza walikubali kipigo cha bao 4 kwa 1 toka kwa Ajax, leo watakuwa nyumbani kujaribu kubadili matokeo hayo.

Ni Juventus vs Real Madrid fainali ya Champions League.


Atletico Madrid walionekana tishio kwa Real Madrid na walionekana kama wanaenda kubadili matokeo ya mwanzo ya mchezo wao baada ya mabao mawili ya haraka haraka.

Alianza Saul Niguez dakika ya 12 kuzichungulia nyavu za Real Madrid kabla ya Antoine Griezman dakika ya 16 kuiandikia Atletico bao la pili kwa mkwaju wa penati.

Lakini wakati Atletico wakiamini wangemaliza kipindi cha kwanza wakiongoza kwa goli 2 kwa 0, dakika ya 42 Isco alifanikiwa kuipatia Real Madrid goli na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa bao 2 kwa 1.

Bao la Isco lilikuwa la kwanza kwake katika michezo yake 31 iliyopita katika Champions League, na bao hilo liliifanya Real Madrid kufunga mfululizo goli katika mechi 67 mfululizo.

Kipindi cha pili Atletico iliwapasa kufunga mabao mengine matatu ili kuitoa Real Madrid na Atletico waliingia wakijitahidi kutafuta mabao hayo lakini ikashindikana na mchezo kuisha 2 kwa 1.

Matokeo hayo yameifanya Real Madrid kufudhu kwenda katika fainali ya Champions League msimu huu na hii ikiwa ni mara mbili mfululizo katika misimu miwili.

Real Madrid sasa wanaifuata Juventus ambao usiku wa Jumanne waliitoa Monaco katika fainali itakayopigwa mwezi ujao tarehe 6 katika mji wa Cardiff nchini Wales.

 

Saturday, 6 May 2017

Klabu ya Man City yafungiwa Usajili Miaka miwili

KLABU ya Manchester City imefungiwa kwa miaka miwili kusajili wachezaji wa umri chini ya miaka 18 sambamba na kutozwa faini ya Pauni 300,000 na Bodi ya Ligi Kuu England kwa kuvunja sheria ya maendeleo ya vijana.

Uvunjaji huo wa sheria unahusu kufanya mazungumzo na wachezaji wawili wa akademi tofauti kwa ajili ya kuwasajili huku wakiwa wamesajiliwa na klabu nyingine. 

Adhabu hiyo ni sawa na waliyopewa Liverpool mwezi uliopita baada ya kukutwa na hatia ya 'kuiba' mchezaji mwanafunzi wa shule wa Stoke City.

Kufuatia uchunguzi wa Bodi ya Ligi Kuu, ushahidi umepatikana kwa City ambao wamevunja sheria za Ligi.

Kuwasilia na mchezaji wa akademi yoyote akiwa amesajiliwa na klabu yake ya wakati husika ni kosa, ambalo City wamefanya na sasa linawagharimu. 

Monday, 6 February 2017

Hawa ndio mabingwa wa Afcon 2017

Timu ya Taifa ya Soka ya Cameroon imetawazwa kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2017 baada ya kuilaza timu ya Taifa ya Misri kwa mabao 2-1,  yaliyofungwa na Nicolas N'Koulou na Vincent Aboubakar.

Cameroon imepata ubingwa huo katika fainali za mashindano hayo yaliyofanyika nchini Gabon, ukiwa ni ubingwa kwa mara ya tano na ni mara ya kwanza tangu mwaka 2002.

Katika mtanange huo uliovuta hisia za mashabiki na wapenzi wengi wa soka,  Misri ndiyo ilianza kutikisa nyavu za Cameroon baada ya Mohamed Elneny kufunga goli kwa shuti kali katika dakika ya 21.

Hata hivyo, katika dakika ya 58, N'Koulou aliamsha matumaini ya Cameroon kutwaa ubingwa huo, baada ya kuisawazishia timu yake kwa kichwa, kabla ya Aboubakar kuihakikishia ubingwa kwa kupachika wavuni bao la pili katika dakika ya 88 na hivyo kuzamisha kabisa jahazi la Misri.

Ubingwa wa mwaka huu kwa Cameroon unaandika rekodi mpya na ya kwanza baada ya timu hizo kukutana katika hatua ya fainali mwaka 1986 na 2008, ambazo zote Misri iliibuka mbabe.

Monday, 5 December 2016

Mchezaji wa Mbao FC afariki baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui FC

Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao FC U-20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki  Dunia jana jioni  baada ya kuanguka uwanjani Kaitaba wakati wa mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui FC ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.

Ismail Khalfan  alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Serikali ya mjini Bukoba.

Ismail Khalfan kabla ya kufikiwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.

Kabla ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui FC  na baadae akiwa peke yake alianguka chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa katika Uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta.



Sunday, 6 November 2016

Zlatan atupia 2, Pogba atupia 1, Man United Yaibamiza Swansea 3-1, Picha 8 ziko hapa













Monday, 31 October 2016

Breaking News: Bondia Thomas Mashali Auwawa,

Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali amefariki dunia usiku wa kuamkia leo October 31 2016 maeneo ya Kimara DSM, Taarifa zinadai kuwa alishambuliwa na wananchi baada ya madai ya kuitiwa mwizi kwa kushambuliwa na wananchi kwa madai ya kuitiwa mwizi.
Promota Siraji Kaike amesema watu aliokuwa anagombana nao walimwitia mwizi na wakapiga mapanga akawa ametupwa na bodaboda waliokuwa wanamjua Thoams Mashali walimuokota na kumpeleka hospitali ambapo baadaye zilitolewa taarifa kuwa amefariki.
Yassin Abdallah maarufu kama Ustaadhi, mmoja wa viongozi wakongwe wa mchezo wa ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
"Tumethibitishiwa hizo taarifa za majonzi kabisa, mwili upo Muhimbili na msiba upo kwao Tandale," alisema Ustaadhi.

Saturday, 22 October 2016

Man U yang'ara ligi ya Europa..Paul Pogba Afuta Nuksi ya mda mrefu

Paul Pogba alifunga mara mbili wakati Manchester United walipoibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya klabu ya Fenerbahce katika kundi A.

Pogba mchezaji ghali zaidi duniani alifunga goli la kwanza kwa penalti baada ya Juan Mata kuangushwa ndani ya eneo la hatari, kisha baadaye kuandika bao la pili baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Jesse Lingard.

Bao la Robin Van Persie lilishangiliwa na mashabiki wa pande zote mbili

Goli la Pili kwa United liliwekwa kimiani na Anton Martial kwa njia ya penalti baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari huku la mwisho likipachikwa na Jesse Lingard kwa shuti kali la chinichini.

Robin Van Persie aliiandikia timu yake ya Fenerbahce goli la kufutia machozi lililoshangiliwa na mashabiki wa pande zote akiwemo kocha wake wa zamani Sir Alex Ferguson.

Matokeo mengine katika michezo ya ligi ya Europa

THURSDAY 20TH OCTOBER 2016
FC Steaua București 1-1 FC Zürich
FK Krasnodar 0- 1 Schalke
FC Slovan Liberec 1-3 Fiorentina
Hapoel Be'er Sheva 0-1 Sparta Prague
Inter Milan 1-0Southampton
Osmanlispor 2-2 Villarreal
FK Qarabag 2-0 PAOK Salonika
Celta Vigo 2-2 Ajax
Standard Liege 2-2 Panathinaikos
Konyaspor 1-1 Sporting Braga
Shakhtar Donetsk 5-0 KAA Gent
FC RB Salzb 0-1 Nice

Friday, 9 September 2016

Mourinho avurugana na staa wake mwengine ndani ya united, wakati mvurugano wake na schwaeinsteiger haujakaa sawa

Wakati mvutano kati ya Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho na kiungo wake, Bastian Schweinsteiger ukiwa haujakaa sawa, kocha huyo inadaiwa ametibuana na beki wake kikosini hapo, Matteo Darmian.

Beki huyo raia wa Italia ambaye ana umri wa miaka 26 amekuwa hana nafasi aktika kikosi cha kwanza cha timu yake hiyo, ambapo amekuwa akimtumia zaidi Antonio Valencia katika nafasi yake ya beki wa kulia.

Kutokana na hali hiyo inadaiwa kuwa kuna uwezekano mkubwa Darmian akarejea Italia kujiunga na Juventus.

Darmian ameshacheza mechi 39 kikosini hapo lakini msimu huu Antonio Valencia ameiteka nafasi yake.

Tuesday, 30 August 2016

Mchezaji Mpira Avunjiwa Mkataba Baada ya Kugundulika Ana Virusi vya Ukimwi

Zikiwa zimepita siku nne tu tangu asajiliwe na klabu ya Al Ittihad inayoshiki ligi kuu ya Misri, Samuel Nlend, 21, mkataba wake umevunjwa baada ya klabu yake mpya kugundua mchezaji huyo anamaambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Jarid linalojulikana kwa jina la KingFut.com limeripoti kuwa, afisa habari wa klabu hiyo amethibitisha taarifa hiyo ya kusikitisha kwa vyombo vya habari.

Mshambuliaji huyo ameitumikia Cameroon katika michezo mitano, alifunga goli January kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kabla ya kujiunga na Al Ittihad majira ya kiangazi.

Samuel Nlend alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Al Ittihad tangu tarehe 24 August. Licha ya hayo yote kutokea bado amepata support ya kutosha kutoka kwa klabu yake mpya ya Misri.

Monday, 29 August 2016

ASAMOH GYAN arudi kwa kishindo Uingereza.

Nahodha wa kikosi cha soka nchini Ghana Asamoah Gyan anatarajiwa kujiunga na klabu ya Reading kwa mkopo kutoka timu ya China Shanghai SIPG.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Sunderland anafanyiwa ukaguzi wa matibabu na klabu hiyo ya daraja la kwanza.

Gyan aliifungia mabao 30 Sunderland alipoichezea timu hiyo kwa misimu miwili,kutoka mwaka 2010 kabla ya kuelekea Al-Ain ya Umoja wa Milki za kiarabu UAE.

Alijiunga na Shanghai 2015 wakati huo na alikuwa miongoni mwa mchezaji wanaolipwa zaidi duniani.


SHKODRAN MUSTAFI ALIITOSA CITY, AKABANIWA NA MOYES SASA YUPO NA WENGER

Na Athumani Adam

Tetesi zimekuwa kweli mapema wiki hii pale Arsene wenger alipokamilisha usajili wa beki Shkodran Mustafi. Usajili wa beki huyo Mjerumani mwenye miaka 24 kutoka klabu ya Valencia ya kule nchini Hispania utasaidia kuziba nafasi zilizopo kwenye safu ya ulinzi ya Arsenal ukizingatia Per Mertesacker bado anasumbuliwa na majeraha

Ikiwa bado mashabiki wa Arsenal wana furaha ya ujio wa Mustafi, makala hii inakupa historia fupi kabla ya kuja Arsenal

HISTORIA

Shkodran Mustafi alizaliwa tarehe 17 April 1992 kule Bad Hersfeld nchini Ujerumani. Wazazi wake ni raia wa Albania wenye asili ya Marcedonia. Mwaka 2006 alijiunga na timu ya vijana ya Hamburger SV

AKATAA OFA YA MAN CITY NA NEWCASTLE

Mwaka 2009 klabu za Man City pamoja na Newcastle United zilitaka kumsajili Mustafi lakini akataa na kuelekea zake kule Merseyside kwenye klabu ya Everton

ACHEZA GAME MMOJA TU EVERTON

Tangu ajiunge na Everton hadi anaondoka mwaka mwaka 2012, Mustafi alicheza mechi moja tu.   Mechi ambayo Mustafi alicheza ilikuwa dhidi ya Bate Borisov michuano ya Europa League.  Ilikuwa kwenye uwanja wa Goodson Park December 16, 2009 mchezo ambao Everton ililala 1-0

Baada ya kuona hapati nafasi ya kutosha kucheza, mustafi alimwomba kocha David Moyes kuhama Everton na kulelekea kwenye klabu ya Sampdoria.

AFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA SAMPDORIA (MECHI 53, GOLI 1)

Mustafi alifunga goli lake la kwanza kama mchezaji “professional” kwenye mechi ya Serie A dhidi ya Atlanta October 2013. Sampdoria ilikuwa imepanda daraja kutoka Serie B tangu iliposhuka mwaka 2011. Mbali na Mustafi pia Samporia walikuwa na wachezaji vijana  Simon Zaza na Mauro Icardi

DAU LA USAJILI LAWA SIRI VALENCIA (MECHI 78, GOLI 6)

Mustafi alijiunga na Valencia mwaka 2014 akitokea Sampodria bila dau la usajili kuwekwa wazi. Zipo tetesi kwamba japo haikuwekwa wazi, lakini Mustafi alitua kwa Euro milioni 8. Ndani ya Valencia Mustafi alicheza mechi 78 na kufunga goli 6.

ALIKUWEPO WORLD 2014, EURO 2016

Mustafi alikuwepo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia kule nchini Brazil mwaka 2014. Alipata kuitwa kwenye kikosi na kocha Joackim Low baada ya kuumia kiungo Marco Reus. Mustafi aliingia kutokea sub kwenye mechi dhidi ya Portugal na Ghana. Bahati mbaya aliuumia wakati mashindano yanaendelea

Mbali na kombe la dunia pia mustafi alikuwepo kwenye mashindano ya euro 2016 kule nchini Ufaransana.

STERLING AJA KIVINGINE, CITY YALA VYA KUCHINJA

Ni kama vile Guardiola anatengeneza timu ambayo itakuwa tishio sana katika ligi kuu ya Uingereza kwa namna ambayo amekuwa akipangilia kikosi chake na namna ambavyo wachezaji wamekuwa wakitoa matokeo kwa klabu hiyo.
Timu imeongeza kujiamini kwa ujumla na pia baadhi ya wachezaji wamepanda kiwango huku majukumu kwa baadhi pia yakiwa yamebadilika na kuwa tofauti kiasi. Sergio Kun Aguero anaonekana kupunguziwa mzigo wa ufungaji na ndio maana sio ajabu kuona watu kama Raheem Sterling na Nolito wakiwa tayari wameona wavu zaidi ya mara mbili.
Uhuru uliopo kati ya Kevin De Bryune na Silva unawapa City sababu nyingine ya kucheza vyema wanapokuwa wanaelekea eneo la ushambuliaji huku pia Fernandinho akiweza kupatia vyema mfumo wa kucheza kama kiungo pekee wa chini na mkabaji huku akiwa jirani zaidi na John Stones.
Jumapili dhidi ya West Ham United, klabu ya Man City iliendeleza ushindi wake wa asilimia 100 kwa kushinda kwa jumla ya mabao 3-1. Mabao mawili ya Raheem Sterling (7, 90+2) pamoja na lile la Fernandinho yaliwabeba City huku Michail Antonio akifunga bao pekee a West Ham ambao hawajaanza vyema msimu kutokana na majeruhi wengi kikosini.
HIGHLIGHTS

ALLARDAYCE ATANGAZA KIKOSI TIMU YA TAIFA UINGEREZA, MICHAIL ANTONIO NDANI

Mchezaji wa West Ham United, Michail Antonio ndiye mchezaji pekee ambaye hakuwahi kuchezea kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza ambaye kajumuishwa kwenye kikosi cha sasa cha Uingereza.

Pamoja na Antonio, wapo pia Luke Shaw na Phil Jagielka ambao wanarejea kikosini baada ya kukosekana katika kikosi cha Roy Hodgson kilichoshiriki mashindano ya Euro 2016 kutokana na majeraha.

Antonio ameonekana kuwa mchezaji anayeweza kucheza nafasi nyingi kwani msimu huu ameshacheza katika nafasi za kiungo na beki wa pembeni vyema kwa upande wa West Ham. Hata hivyo Allardayce amemtwaa mchezaji huyu kama kiungo katika kwa ajili ya mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya  Slovakia utakaopigwa Trnava, September 4.

Wachezaji wengine waliozua maswali kwenye kuachwa kwao na Hodgson, Walcott ppamoja na Drinkwater wameitwa kikosini huku Jack Wilshere na Ross Barkley ambaye anaonekana kurejea kwenye kiwango cha hali ya juu chini ya Ronald Koeman wakitemwa.

KIKOSI KAMILI.

Makipa: Forster (Southampton), Hart (Man City), Heaton (Burnley)

Mabeki: Cahill (Chelsea), Clyne (Liverpool), Jagielka (Everton), Rose (Tottenham), Shaw (Man Utd), Smalling (Man Utd), Stones (Man City), Walker (Tottenham)

Viungo: Alli (Tottenham), Antonio (West Ham), Dier (Tottenham), Drinkwater (Leicester), Henderson (Liverpool), Lallana (Liverpool), Rooney (Man Utd), Sterling (Man City), Walcott (Arsenal)

Washambuliaji: Kane (Tottenham), Sturridge (Liverpool), Vardy (Leicester)

 

Gallery

Popular Posts

About Us