Mchezaji wa West Ham United, Michail Antonio ndiye mchezaji pekee ambaye hakuwahi kuchezea kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza ambaye kajumuishwa kwenye kikosi cha sasa cha Uingereza.
Pamoja na Antonio, wapo pia Luke Shaw na Phil Jagielka ambao wanarejea kikosini baada ya kukosekana katika kikosi cha Roy Hodgson kilichoshiriki mashindano ya Euro 2016 kutokana na majeraha.
Antonio ameonekana kuwa mchezaji anayeweza kucheza nafasi nyingi kwani msimu huu ameshacheza katika nafasi za kiungo na beki wa pembeni vyema kwa upande wa West Ham. Hata hivyo Allardayce amemtwaa mchezaji huyu kama kiungo katika kwa ajili ya mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Slovakia utakaopigwa Trnava, September 4.
Wachezaji wengine waliozua maswali kwenye kuachwa kwao na Hodgson, Walcott ppamoja na Drinkwater wameitwa kikosini huku Jack Wilshere na Ross Barkley ambaye anaonekana kurejea kwenye kiwango cha hali ya juu chini ya Ronald Koeman wakitemwa.
KIKOSI KAMILI.
Makipa: Forster (Southampton), Hart (Man City), Heaton (Burnley)
Mabeki: Cahill (Chelsea), Clyne (Liverpool), Jagielka (Everton), Rose (Tottenham), Shaw (Man Utd), Smalling (Man Utd), Stones (Man City), Walker (Tottenham)
Viungo: Alli (Tottenham), Antonio (West Ham), Dier (Tottenham), Drinkwater (Leicester), Henderson (Liverpool), Lallana (Liverpool), Rooney (Man Utd), Sterling (Man City), Walcott (Arsenal)
Washambuliaji: Kane (Tottenham), Sturridge (Liverpool), Vardy (Leicester)
0 comments:
POST A COMMENT