Vifaru
Takriban raia 35 wameuawa katika mashambulio kadha ya ndege za Uturuki kaskazini mwa nchi hiyo.
Shirika la kutetea haki za kibinaadamu, limesema kijiji cha Jeb el-Kussa kilipigwa mabomu huku watu 20 wakiuawa na 50 kujeruhiwa.
Inaripotiwa kuwa watu wengine 15, waliuawa baada ya shamba moja kulipuliwa karibu na al-Amarna.
Lakini jeshi la Uturuki linasema ndege zake zilizoshambulia Syria, ziliuwa watu 25, iliyowataja kuwa magaidi wa Ki-Kurd.
Katika shambulio liloanza juma lilopita, vifaru na wanajeshi wa Uturuki, wakisaidiwa na wapiganaji wa Syria, wameteka ardhi iliyokuwa chini ya kundi la Islamic State, na walipambana na YPG, wapiganaji wa Ki-Kurd wanaosaidiwa na Marekani.
Uturuki inataka wapiganaji wa Kikurd wa YPG, warejee nyuma hadi mashariki ya Mto Euphrates.
YPG inapigana kusini mashariki mwa Uturuki.
0 comments:
POST A COMMENT