KINGAZI BLOG: 10/10/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday, 10 October 2016

HAYA HAPA MAJINA YA MAJINA YA WANUFAIKA WA MKOPO CHUO KIKUU MUM 2016/2017


Hatimaye chuo cha Muslim University of Morogoro MUM kimetangaza majina ya wanafunzi walioomba mkopo kwa ajili ya masom-o yao chuoni hapo,kwa awamu ya kwanza.
Nimekuwekea hapa list kamili ya wanafunzi waliochaguliwa kupata mkopo chuo kikuu MUM 2016/2017. 
 
KUONA MAJINA YA WANUFAIKA WA MKOPO CHUO KIKUU MUM 2016/2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Octoba 10




NECTA yatoa ratiba ya ukaguzi wa vyeti mkoa kwa mkoa

Hatua ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kutoa ratiba ya kufanya uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu kwa watumishi wote wa umma sasa ni wazi imezidi kupandisha joto kwa vigogo na watumishi mbalimbali ambao hawana sifa za kielimu kushika nafasi walizo nazo.

Katika taarifa yake ya sasa Baraza la Mitihani nchini, limetangaza kuwafuata katika maeneo yao ya kazi watumishi wote walioko katika mamlaka za mikoa, halmashauri na manispaa kwa ajili ya kufanya uhakiki wa vyeti vyao hivyo vya kitaaluma.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na Edga Kasuga kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo kwenda kwa Makatibu tawala wa Mikoa, uhakiki utafanyika katika ofisi za Makatibu Tawala wa mikoa kuanzia Oktoba 10 hadi 14 mwaka huu, ingawa ratiba nyingine ya uhakiki imeonyesha zoezi hilo litafikia tamati Novemba 7 mwaka huu.

“Ili kufanikisha zoezi hilo Baraza limetaka kupata orodha (nakala- laini ya soft copy) ya watumishi wote wa umma waliopo katika mkoa, halmashauri na manispaa.

“Nakala za vyeti vya kidato cha nne, cha sita na ualimu vya watumishi wote walioandikishwa na chumba cha kufanyia uhakiki,” inaeleza taarifa hiyo ya Baraza la Mitihani.

RATIBA YA UHAKIKI

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani, uhakiki huo utafanywa katika makundi matano katika mikoa tofauti tofauti.

Oktoba 10, mwaka huu kundi la kwanza litafanya uhakiki katika Mkoa wa Mtwara, kundi la pili Singida, kundi la tatu Rukwa, kundi la nne Katavi na kundi la tano litakuwa Geita.

Oktoba 17 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Lindi, la pili Manyara la tatu Songwe, la nne Kigoma na la tano litakuwa Mwanza.

Oktoba 24 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Morogoro, la pili Arusha, la tatu Mbeya, la nne Tabora na la tano Mara.

Oktoba 31 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Pwani, la pili Kilimanjaro, tatu Ruvuma, la nne Shinyanga na la tano Simiyu.

Novemba 7 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Dar es Salaam, la pili Tanga, la tatu Njombe, la nne Dodoma na la tano Iringa.

JOTO LA UHAKIKI

Kabla Baraza la Mitihani halijatangaza ratiba hiyo, tayari watumishi wa umma ambao wanatumia majina matatu lakini vyeti vyao vya elimu vinasomeka majina mawili walikuwa wamepewa maelekezo ya kwenda kutafuta hati ya kiapo kwa ajili ya kuapa mahakamani ili kuthibitisha majina yao.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili mmoja wa watumishi hao alisema: “Wakati tunaanza kazi sisi ambao vyeti vyetu tulikuwa tunatumia majina mawili shuleni, tuliambiwa tutumie matatu ambayo pia yanatumika hata kwenye ‘salary slip’, sasa tumeambiwa tunatakiwa kwenda mahakamani kuthibitisha.”

Alisema zoezi hilo tayari limeleta changamoto kubwa mbali na kuzua hofu kwa baadhi ya watu ambao taarifa zao za kitaaluma hazipo sawa sawa.

“Mimi binafsi sina hofu zoezi linakwisha kesho lakini kinachoniuma ni kwamba hiyo hati ya kiapo (affidavit) tukienda Mahakama ya Mwanzo tunaambiwa ni lazima tulipie shilingi 10,000 na kibaya zaidi hatupewi risiti lakini kwa watumishi wengine ambao wanafahamiana wanapata huduma bure,” alisema mtumishi huyo.

Tangu Serikali itangaze kuwafuatilia watumishi wake wote wenye vyeti feki hali ya wasiwasi na sintofahamu imetawala miongoni mwa vigogo, maofisa na watumishi wengine ambao vyeti vyao vya kitaaluma haviko sawa sawa au haviendani na kazi au nyadhifa wanazoshikilia.

Source: Mtanzania

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Yatupiwa Lawama Kwa Kuchelewa Kutoa Majina ya Wanufaika wa Mikopo

Wakati vyuo vikuu vikikaribia kufunguliwa, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imelaumiwa kwa kuchelewa kutoa majina ya wanufaika huku yenyewe ikisema itahakikisha majina yanatolewa sanjali na tarehe za vyuo kufunguliwa. 

Pia, HESLB imesema miongoni mwa vipaumbele vitakavyozingatiwa kwenye utoaji wa mikopo katika mwaka wa masomo 2016/2017 ni kwa wanafunzi wenye mahitaji makubwa, waliotoka kwenye kaya masikini, waliosoma shule za kata na waliotoka vijijini. 

Kauli hiyo imekuja baada ya bodi hiyo kutupiwa lawama kwa kuchelewa kutoa majina ya wanufaika wa mikopo kabla hawajaripoti vyuoni, hasa wanafunzi wa mwaka wa kwanza.

Mkurugenzi wa mtandao wa haki za wanafunzi (TSNP), Shitindi Venance alisema hadi sasa wanafunzi wanaojiunga na masomo ya elimu ya juu nchini kwa mwaka wa kwanza wa masomo 2016/2017, ambao wameomba mkopo bado hawajui ni kiasi gani wamepewa. 

Malalamiko ya Shitindi yamerejea kilichotokea mwaka jana baada ya wanafunzi kuripoti vyuoni, lakini majina yalipotolewa na bodi hiyo baadhi yao hawakuwa wanu- faika hali iliyosababisha usumbufu. 

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema miongozo ya utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka huu ni tofauti na mwaka jana. 

“Utaratibu wa mwaka huu ni tofauti kwa kuzingatia wanafunzi wanaoanza masomo na wale wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali,”alisema Badru. 

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa majina ya wanufaika wa mikopo yataanza kutolewa kwa kuzingatia tarehe ambayo chuo husika kinafunguliwa.

 “Kila chuo kinafunguliwa kwa mujibu wa tarehe iliyopangwa kwa hiyo na sisi tunatoa majina kuendana na utaratibu wa chuo husika,” alisema. 

Hata hivyo, Badru alisema uta- ratibu wa kupanga viwango vya mikopo kwa wanafunzi na kisha kutoa orodha ya majina ya wanufaika haihusishi bodi ya mikopo peke yake. 

Alisema kabla ya kuidhinisha majina ya wanufaika na mikopo, lazima Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) iwe imeshatoa orodha ya majina wa wanafunzi ambao imewadahili kwa kuzingatia vigezo vyao, halafu majina hayo yatumwe vyuoni. 

Alisema mzunguko wote huo unahitaji muda na umakini wa hali ya juu ndiyo maana huchukua muda.

Waliotimuliwa Udom wakibeba chuo Moro

Morogoro. Baada ya kukaa miaka zaidi ya 50 bila ukarabati, hatimaye Chuo cha Ualimu Morogoro kimeanza kukarabatiwa ili kipokee wanafunzi 1,138 walioondolea Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Ukarabati huo unaofanywa chini ya ufadhili wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi utagharimu Sh700 milioni.

Mkuu wa chuo hicho, Augustine Sahili amesema huo ni mpango wa Serikali unaohusisha vyuo vyote vya ualimu ambavyo vitapokea wanafunzi walioondolewa Udom kutokana na kutokuwa na sifa za kujiunga na chuo kikuu.

Amesema ukarabati huo utakaomalizika mwezi huu unahusisha mabweni, madarasa na mfumo wa majitaka.

Pia, ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kukarabati chuo hicho kwani tangu kilipoanzishwa mwaka 1926 hakijawahi kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Mwalimu Anna Mushi aliyehitimu chuoni hapo, amesema majengo mengi na miundombinu vilikuwa chakavu.

“Vyuo vingi vya ualimu vya Serikali vilianza kabla ya Uhuru, hivyo vinahitaji ukarabati ili viendelee kuwa katika hali nzuri,” amesema mwalimu huyo.

NECTA Kupigilia Panga la Mwisho Kwa Wenye Vyeti FEKI Kuanzia Kesho.....Watumishi Wote Kufuatwa Vituoni Kukaguliwa


Hatua ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kutoa ratiba ya kufanya uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu kwa watumishi wote wa umma sasa ni wazi imezidi kupandisha joto kwa vigogo na watumishi mbalimbali ambao hawana sifa za kielimu kushika nafasi walizo nazo.

Katika taarifa yake ya sasa Baraza la Mitihani nchini, limetangaza kuwafuata katika maeneo yao ya kazi watumishi wote walioko katika mamlaka za mikoa, halmashauri na manispaa kwa ajili ya kufanya uhakiki wa vyeti vyao hivyo vya kitaaluma.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na  Edga Kasuga kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo kwenda kwa Makatibu tawala wa Mikoa, uhakiki utafanyika katika ofisi za Makatibu Tawala wa mikoa kuanzia Oktoba 10 hadi 14 mwaka huu, ingawa ratiba nyingine ya uhakiki imeonyesha zoezi hilo litafikia tamati Novemba 7 mwaka huu.

“Ili kufanikisha zoezi hilo Baraza limetaka kupata orodha (nakala- laini ya soft copy) ya watumishi wote wa umma waliopo katika Mkoa, Halmashauri na Manispaa.

“Nakala za vyeti vya kidato cha nne, cha sita na ualimu vya watumishi wote walioandikishwa na chumba cha kufanyia uhakiki,” inaeleza taarifa hiyo ya Baraza la Mitihani.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani, uhakiki huo utafanywa katika makundi matano katika mikoa tofauti tofauti.

Oktoba 10, mwaka huu kundi la kwanza litafanya uhakiki katika Mkoa wa Mtwara, kundi la pili Singida, kundi la tatu Rukwa, kundi la nne Katavi na kundi la tano litakuwa Geita.

Oktoba 17 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Lindi, la pili Manyara la tatu Songwe, la nne Kigoma na la tano litakuwa Mwanza.

Oktoba 24 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Morogoro, la pili Arusha, la tatu Mbeya, la nne Tabora na la tano Mara.

Oktoba 31 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Pwani, la pili Kilimanjaro, tatu Ruvuma, la nne Shinyanga na la tano Simiyu.

Novemba 7 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Dar es Salaam, la pili Tanga, la tatu Njombe, la nne Dodoma na la tano Iringa.
==



Taarifa kutoka Ikulu: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mhandisi James Mitayakingi Kilaba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi James Mitayakingi Kilaba umeanza jana Jumamosi tarehe 08 Oktoba, 2016.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba alikuwa akikaimu nafasi hiyo, baada ya uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba kutenguliwa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

09 Oktoba, 2016

WAZIRI NDALICHAKO AZIFUTA SHULE NYINGINE 12.

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imezifuta shule nyingine za awali na msingi nchini ambazo hazijasajiliwa zaidi ya 10 kuanzia Desemba mwaka jana. Aidha, shule tano kati ya 40 zilizokuwa zimefutiwa usajili zimekamilisha taratibu na kurejeshewa usajili wake.

Kaimu Mkurugenzi wa Usajili wa Shule katika wizara hiyo, Khadija Mcheka amesema mpaka sasa bado wanaendelea na ukaguzi kubaini shule ambazo hazijasajiliwa.

Alizitaja shule ambazo zimefutwa kwa kutosajiliwa kuwa ni Mwandai Junior Academy, shule ya msingi DACETE, shule za msingi Malaika na Fares Kisingo (FK) za wilaya ya Kinondoni. Nyingine ni shule ya msingi The Unity, shule ya sekondari Jotac iliyopo eneo la Kipunguni, Verena iliyopo eneo la Pugu zote wilaya ya Ilala, Exodus iliyopo Kigamboni na Havard Junior ya wilaya ya Temeke.

Alisema shule nyingine zilizofutwa kabisa ni shule ya sekondari ya Kahe ambayo imefutwa kutokana na wamiliki kushindwa kuiendesha na pia majengo yake yamebadilishiwa matumizi. 

Alisema shule nyingine za Deogrolius International School iliyopo Kitunda, Desinity na Almustakim zote za jijini Dar es Salaam nazo zimefutiwa usajili. Alisema awali yalitolewa majina ya wamiliki.

Mcheka alisema pia shule mbili hazitakiwi kuwa za bweni ambazo ni Heritage iliyopo Banana Ukonga na Hellens iliyopo Kinondoni.

Akizungumzia shule zilizorejeshewa usajili, alisema ni Gisera, Rose Land, Conerstone na Grace za jijini Dar es Salaam na Must Lead na Qunu zilizopo mkoani Pwani huku shule ya Fountain Gate ikifutiwa usajili wa kuendesha shughuli za bweni.

Akifafanua kuhusu shule ya Coner Stone alisema baada ya ukaguzi na kufutiwa usajili kuanzia mwezi Julai zipo shule ambazo zilikamilisha utaratibu na kurejeshewa usajili, na kwamba hakuna shule iliyoelezwa kufutiwa usajili kwa uongo.

“Kuhusu shule zinazolalamika kutangazwa kimakosa si kweli isipokuwa jambo lililofanyika baada ya kuwapelekea barua kuwataka kutawanya wanafunzi baada ya kufutiwa usajili walikamilisha utaratibu ndipo wakasajiliwa,“ alisisitiza.

Alisema ukaguzi huo wa shule unaendelea katika mikoa yote nchini kwa kuwatumia wakaguzi wa Kanda na watakaobainika watafutwa mpaka watakapokidhi vigezo vinavyotakiwa. 

Hivi karibuni Mcheka alisema kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana, waligundua kuwepo kwa shule 35 zisizosajiliwa na kuzifuta na baadaye walizifungia shule nyingine 12. 

Mcheka alisema shule zinaweza kufutwa kwa sababu mbili zikiwamo zilizosajiliwa, lakini zikakiuka vigezo ambapo zikitimiza vigezo zinaweza kuomba upya usajili na kupewa.

“Lakini aina ya pili ni zile ambazo hazijasajiliwa na zinaendeshwa kinyume cha sheria ambazo nazo zikifuata taratibu zikatimiza vigezo zinaweza kupewa usajili,”alifafanua Kaimu Mkurugenzi huyo wa Usajili wa Shule.

Alisema katika kipindi hicho mpaka Agosti mwaka huu baada ya tangazo la kuwataka kusajiliwa shule za awali nne, zile za awali na msingi 105 na sekondari 19, walifika wizarani kwa ajili ya kupata taratibu za usajili ambapo zipo zilizosajiliwa na nyingine kupewa vibali.

Alisema katika usajili, wapo waliokidhi viwango na wengine walipatiwa maelekezo na kupatiwa vibali vya kutumia majengo yaliyopo huku wengine wakipewa vibali vya kujenga majengo ya shule kabla ya kupata usajili. 

Alisema kwa shule walizozifungia, waliwaandikia barua za kuwafungia na kuwataka kuhakikisha wanawatawanya wanafunzi katika shule zilizosajiliwa kwa gharama zao bila kuwaathiri wanafunzi.

Alitaja shule zilizofungiwa kwa kuendesha shughuli zake bila usajili kuwa ni shule ya awali na msingi Must Lead ya mkoa wa Pwani, kwa upande wa mkoa wa Dar es Salaam ni Brainstorm, Pax, Lassana, Grace, Rose Land, Julius Raymod, St Thomas, Mary Mother of Mercy, Noble Sinkonde, Immaculate Heart of Mary, St Columba, Corner Stone, Dancraig, Mwalimu Edward Kalunga, Edson Mwidunda, Gisela, Kingstar, St Columba, Bilal Muslim, Thado, Hocet , Elishadai, Lawrance Citizen, Comrade, Dar Elite Preparatory, Golden Hill Academy na Hekima.

Nyingine ni Pwani Islamic, St Kizito na Rwazi Encysloped za Kagera, Dancraig na Qunu za Pwani, Hellen’s ya Njombe, Joseph ya Arusha, Samandito na Maguzu za Geita. Alizitaja shule za sekondari zilizofungiwa kwa sababu hiyo kuwa ni Hananasif, Elu, Hocet, Safina za Dar es Salaam na Namnyaki ya Iringa.

 

Gallery

Popular Posts

About Us