KINGAZI BLOG: 01/20/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday, 20 January 2017

SHILAWADU!!!!Dimpoz afunguka skendo ya kuwekwa kinyumba na jimama mitaa ya mbezi

Ommy Dimpoz

Msanii wa muziki wa bongo fleva Ommy Dimpoz amekanusha tetesi zilizozagaa kwamba amewekwa ndani kimapenzi maeneo ya mbezi  na jimama ambalo lina mahusiano naye kumapenzi.

Akiongea kupitia eNEWZ ya EATV, Ommy amesema kwa sasa anaishi Mikocheni Dar es Salaam na hajawahi kuwekwa ndani na mwanamke yeyote kwa kuwa anasema mpenzi wake wa sasa ni mchina na hajawahi kuwa na mahusiano na mwanamke wa kizungu na kwamba hizo ni story za watu ambao waliamua kuvumisha.

Hata hivyo Ommy amesema kwa sasa anajenga nyumba yake maeneo ya Mbezi na Kigambona hivyo hana nyumba ambayo amepangisha au kupangishiwa Mbezi na mambo yatakapokuwa wazi atamuweka wazi mpenzi wake.

Sallam atangaza ujio wa tamasha la Diamonds Are Forever 2017

Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK aka ‘Fundi Mitambo’ ametangaza ujio mpya wa tamasha kubwa la Diamonds Are Forever 2017 ambapo safari hii litafanyikia katika uwanja wa Taifa.

Muimbaji huyo alifanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2012 katika ukumbi wa Mlimani City show ambayo ilihudhuriwa na watu wengi kwa kiingilio cha Tsh 50,000.

Sallam akizungumza live na mashabiki katika mtandao wa Istangam (Insta Live) alisema show hiyo ipo kwenye maandalizi na itafanyika uwanja wa Taifa.

“Mjiandae na Diamonds Are Forever 2017, Diamonds Are Forever 2017 is back,” Sallam aliwaambia mashabiki.

Meneja huyo alidai safari hii tamasha hilo litafanyika uwanja wa taifa ili kuwapa fursa watu wengi zaidi ya kuudhuria.

Hata hivyo hakuweka wazi ni lini au mwezi gani tamasha hilo litafanyika.

Pitia Hapa Ratiba ya Tukio Zima la Kuapishwa kwa Rais wa 45 wa Marekani Donald Trump Leo..!!!


Mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba Donald Trump anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani leo Ijumaa tarehe 20 Januari, 2017.

Bw Trump wa Chama cha Republican anatarajiwa kuapishwa mbele ya watu 750,000 mbele ya majengo makuu ya bunge la Marekani, Capitol Building, Washington D.C.

Kisheria, rais anafaa kuapishwa kabla ya saa 6:00 mchana saa za Amerika Mashariki ambazo Afrika Mashariki ni saa mbili usiku.

Hii hapa ni ratiba fupi ya matukio yanayotarajiwa siku hiyo.

Saa 17:30 (Saa za Afrika Mashariki) Wanamuziki walioalikwa wataanza kutumbuiza.

19:30 Hotuba za kufungua sherehe zitaanza kutolewa.

20:00 Muda mfupi kabla ya saa Mbili Afrika Mashariki Donald Trump atalishwa kiapo cha kuwa rais wa Marekani na Jaji wa Mahakama ya Juu John Roberts.

Baadaye, kutakuwa na msafara baada ya sherehe ya kuapishwa ambao utaanza katika vidato vya jumba la Capitol Building kuelekea ikulu ya White House kupitia barabara maarufu ya Pennsylvania Avenue.

Bw Trump na mkewe Melania baadaye watacheza densi katika matamasha matatu, mawili katika ukumbi wa mikutano wa Walter E Washington na jingine katika ukumbi wa Jengo la Makumbusho ya Taifa.

Miaka minane iliyopita, Rais Obama alipokuwa anaapishwa kura rais, waliohudhuria walikuwa 1.8 milioni.

Siku moja baada ya kuapishwa kwa Bw Trump, wanawake takriban 200,000 wanatarajiwa kuandamana Washington DC na miji mingine kumpinga Bw Donald Trump.

Hillary Clinton na mumewe Bill wamethibitisha kwamba watahudhuria sherehe hiyo, sawa na George W Bush na mkewe Laura.

Wamesema wanataka “kushuhudia kukabidhiwa madaraka kwa rasi mwingine kwa njia ya amani.”

Rais mwingine wa zamani Jimmy Carter atahudhuria pia, lakini George HW Bush, 92, na mkewe Barbara hawataweza kwa sababu za kiafya.

Wanaosoma Diploma Sasa Kupewa Mikopo na Bodi ya Mikopo (HESLB)

Serikali imewasilisha pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuwezesha wanafunzi wanaochukua Stashahada katika vipaumbele vya kitaifa, kupewa mikopo ya kuwawezesha kuchukua elimu husika.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema mabadiliko hayo, yamelenga kuwezesha kasi katika uchumi wa viwanda.

Profesa Ndalichako alisema mabadiliko katika Sheria Namba 4 ya Mwaka 2016 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), yamelenga kutoa nafasi ya kada ya Stashahada inayohitajika ambao wamekuwa hawapati mikopo.

“Kwa lengo la kupata balance (mizania) na kwa kuwa Diploma nayo iko kwenye elimu ya juu, watoto ni wale wale. Kuna wengine nao wanashindwa kumudu gharama na ili serikali ipate uwiano mzuri tumeona ni vizuri kuwe na marekebisho ya sheria,” alieleza Profesa Ndalichako.

Profesa Ndalichako alisema kuna umuhimu mkubwa wa kada ya Stashahada, hasa wanaokwenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa kwenye msukumo wa Serikali ya Awamu ya Tano wa ujenzi wa taifa la vijana, kama ilivyo kwa wenye Shahada.

“Kama taifa tunazungumzia uchumi wa viwanda,wadau wote hata wale wa ngazi ya kati ni muhimu katika kuhakikisha kwamba ajenda hii inafanikiwa kama vile ambavyo wale wa digrii wangelifanya,” aliongeza waziri huyo.

Mwaka 2004, kulikuwepo na mabadiliko katika sheria hiyo iliyowezesha wanaochukua masomo ya sayansi, hisabati na elimu ya msingi (kwenye msisitizo wa sayansi na hisabati), kupata mikopo ya elimu, nafasi iliyoanza kutumika mwaka 2014, lakini hatua hiyo ilisimamishwa wakati wa muhula wa masomo wa mwaka 2016/17.

Hata hivyo, HESLB ilikaririwa ikisema kwamba maamuzi ya kusitisha utoaji wa mikopo, ililenga kutekeleza maagizo ya serikali.

Hata hivyo, jana Profesa Ndalichako alisema kwamba uamuzi wa kusimamisha mikopo hiyo,ulitokana na nia ya serikali kufanya mabadiliko katika sheria hiyo ili kuipa wigo mpana zaidi kuliko kujikita katika eneo la sayansi pekee.

“Mwaka 2004 tuliingiza diploma, lakini kwa masomo ya sayansi pekee sasa, tunataka kuwa na kipengele kinachopanua wigo ili tuweze kuhusisha kozi nyingine za diploma ambazo zinaenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa,” alifafanua waziri huyo.

Kwa mwaka wa masomo 2016/17, serikali ilipanga bajeti ya Sh bilioni 483 ambazo zitakopeshwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea. Katika mwaka huo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo walikuwa ni 25,715.

Umeipata Hii ya Toleo Jipya la Simu ya iPhone 8,Eti Itakuwa na Uwezo wa Kutambua Sura za Watu..!!

Toleo lijalo la simu za Apple, iPhone 8, itakuja na uwezo wa kutambua sura za watu.

“Other features appear to include some form of facial/gesture recognition supported by a new laser sensor and an infrared sensor mounted near the front-facing camera and, as expected, should also finally include wireless charging,” alisema, Timothy Arcuri toka kampuni ya utafiti ya Cowen and Company.

Simu hizo zinatarajiwa kuzinduliwa September mwaka huu na zinatarajiwa kushuka bei zake kwa asilimia 30 hadi 50.

 

Gallery

Popular Posts

About Us