KINGAZI BLOG: 03/28/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday, 28 March 2017

Baada ya Rais Magufuli Kuamuru Wimbo wa Wapo wa Nay wa Mitego Uchezwe Redioni,Basata nao Wameibuka na Haya.


Baraza la Sanaa Taifa ‘BATASA’ limerudi tena na kuufungilia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego kwa madai waliufungia ili kupisha uchunguzi wa kipolisi upite baada ya jeshi hilo kumshikilia rapa huyo kwa siku mbili kutokana na wimbo huyo.

Awali baraza hilo lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai hauna maadili kabla ya Rais Magufuli kutoa tamko la wimbo huo kuendelea kupigwa kwa kuwa hauna tatizo lolote.

Baraza hilo limedai kuwa msanii kama ilivyo kwa raia yeyote anaweza kukamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kama kazi yake ikibainika kuwa na kosa la jinai.

“Tulifanya mazungumzo na wenzetu jeshi la polisi waliokua wanamhoji msanii Nay wa Mitego na kuchunguza jinai katika wimbo wake wa Wapo,” Basata walitweet.

Aliongeza, “Baada ya ushauri kutoka kwa Waziri Mwakyembe na baadaye taarifa ya jeshi la polisi na mazungumzo na msanii Nay kituo cha kati cha polisi.Tunaruhusu wimbo wa ‘Wapo’ wa msanii Nay kuchezwa katika vyombo vya habari. Kama taarifa yetu ilivyoeleza, ulisitishwa kupisha taratibu za kipolisi,”

Rapa huyo aliachiwa jana jioni na jeshi la polisi kwa kauli ya Rais Magufuli baada ya kushikiliwa kwa siku mbili.

Pichaz 4 Nape Alivyokabidhi Ofisi Kwa Mwakyembe leo

Aliyekuwa Waziri wa Habari Nape  Nnauye amemkabidhi ramsi ofisi Waziri mpya wa Habari, Dkt Harrison George Mwakyembe.




Kumbe Aliyemtishia Nape kwa bastola sio polisi Waziri Mwigulu anena!!


Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema mtu aliyemtishia kwa bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye si askari wa Jeshi la Polisi, lakini ameshapatikana na atashughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa ulinzi na usalama.

Mwigulu alisema hayo baada ya kufungua mkutano wa kazi wa mwaka wa maofisa waandamizi wa polisi, makamanda wa mikoa na wakuu wa vikosi wa Jeshi la Polisi ambao unafanyika mjini hapa.

“Ameshapatikana (aliyemtishia Nape) na atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za ulinzi na usalama ambazo zimekuwa zikifanyika ndani, lakini hazitangazwi,”alisema.

Hata hivyo, Mwigulu alikataa kuelezea kwa undani kuhusu mtu huyo kwa kubainisha anatoka taasisi gani wala jina la mtuhumiwa kwa madai kuwa ni kwa sababu ya usalama wake.

Baadhi ya taasisi za ulinzi na usalama nchini ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Usalama wa Taifa na Takukuru.

Mtu huyo alifanya kitendo hicho wakati Nape, ambaye alikuwa Waziri wa Habari, alipokuwa anaelekea Hoteli ya Protea alikopanga kuzungumza na waandishi wa habari baada ya mbunge huyo wa Mtama kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Mtu huyo alikuwa pamoja na wenzake wawili ambao kwa pamoja walikuwa wakimlazimisha arudi kwenye gari lake na kuondoka, lakini Nape alibisha na ndipo mtu huyo aliporudi nyuma, kuchomoa bastola kutoka kiunoni na kisha kumtishia kabla ya kutulizwa na mwenzake.

Watu hao walitoweka eneo hilo muda mfupi baadaye.

Siku moja baada ya tukio hilo Mwigulu alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu kumtafuta mtu huyo.

Mwigulu aliandika katika ukurasa wake wa twitter akisema:

“Mh Nape sio jambazi, hana record za uhalifu. Kitendo cha kutolewa bastola si cha Kitanzania na si cha kiaskari. Nimemuagiza IGP achukue hatua.”

Tukio hilo lilitokea siku chache baada ya RC Paul Makonda kuvamia kituo cha televisheni cha kampuni ya Clouds Media, akiwa na askari wenye silaha za moto na kulazimisha arekodiwe mahojiano baina ya watangazaji wa kipindi cha Shirika la Wambeya Duniani (Shilawadu) na mwanamke anayedai kuzaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ambaye ameibukia kuwa mpinzani wa kiongozi huyo.

Hadi sasa, Jeshi la Polisi halijaeleza kuhusu askari hao waliojumuika kufanikisha uvamizi huo.

Kali ya Mwaka hii!!!...Aliyemfunga mbwa wake mdomo atupwa jela miaka 5

Mwanamume mmoja raia wa Marekani ambaye alifunga mbwa wake kwenye mdomo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

William Dodson, mwenye umri wa miaka 43, anasema alimfunga mbwa huyo mdomoni kwa sababu alibweka sana. Ililazimu mbwa huyo kufanyiwa upasuaji mara kadha baada ya kupoteza sehemu ya ulimi wake.

Siku moja baada ya hukumu hiyo kutolewa, William Dodson pia alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela, kwa mashtaka tofauti ya bunduki.

Vifungo hiyo viwili vitafuatana Kulingana na polisi William Dodson alimnunua mbwa hiyo kwa jina Caitlyn kwa dola 20.

Dodson, ambaye alikuwa huru kwa dhamana wakati huo, alimfunga mbwa huyo nje baada ya kumfunga mdomo wake mara tisa.

Lakini mbwa huo alifanikiwa kutoroka mwezi Mei mwaka 2015, na alikuwa mgonjwa sana wakati alipatikana akirandaranda barabarani.

Kamba aliyotumia kumfunga mbwa hiyo ilizuia damu kufika hadi kwenye ulimi wake, na iliwachukua madaktari wa mifugo karibu saa 36 kuiondoa.

Wakati huo chama cha wanyama cha Charleston, kibadilisha picha ya akaunti yake na kuweka picha ya mbwa hiyo, kama njia ya kuonyesha uzalendo.

Wamekuwa wakichapisha taarifa jinsi mbwa huyo anavyoendelea katika kisa hicho kilichoangaziwa kimataifa.

Caitlyn, alikuwa na umri wa miezi 15 wakati alipatikana na sasa amehitimu miaka mitano akiwa anaishi na familia tofauti.




Post ya kwanza ya Soudy Brown baada ya Tukio la Uvamizi wa Makonda Clouds.


MTANGAZAJI na mwanachama wa Shirika la Wambeya Duniani ‘Shilawadu’, Soudy Brown leo ameweka picha ya kwanza mtandaoni baada ya kutoka likizo iliyosababishwa na sekeseke la kuvamiwa kwa kituo chao cha kurushia matangazo, Clouds Televisheni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Jamaa huyo ameweka picha ya aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye na haijafahamika ni kwanini ameweka picha hiyo.




Nay wa Mitego kukutana na JPM Ikulu

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ameitwa Ikulu jioni hii kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Nay amepata mwaliko huo ikiwa ni sasa chache baada ya kuachiwa huru na Jeshi la Polisi lililokuwa likimshikilia tangu jana.

Katika mahojiano yake na kituo cha Televisheni cha Azam Two,  Nay alikiri kupata mwaliko huo na kueleza kuwa ataitumia vyema nafasi hiyo kumuelezea Rais Magufuli hali halisi ya maisha ya Watanzania.

“Nimepokea mwaliko bado nafikiria nini cha kuongea naye endapo nitapata hiyo nafasi ya kuzungumza naye, nadhani itakuwa nafasi nzuri ya kumweleza vile ambavyo Watanzania sisi tunaishi mtaani,”alisema.

Nay alikamatwa na polisi jana mkoani Morogoro na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kutunga wimbo wenye maudhui yanayoikashifu Serikali.

Mapema leo mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema Rais Magufuli ameagiza msanii huyo aachiwe huru na wimbo wake uendelee kuchezwa na kusambazwa.

Bunge kumng'oa Makonda...Habari katika Magazeti ya leo tar 28 march 2017.

























 

Gallery

Popular Posts

About Us