KINGAZI BLOG: 04/14/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday, 14 April 2017

Audio | Rich Mavoko X Harmonize – Show Me | Mp3 Download

DOWNLOAD VIA wasafi.com

AJALI Mbaya Imetokea Maeneo ya Mbwewe na Manga Tanga..

Kuna ajali ya Gari imetokea kati ya Mbwewe na Manga Tanga kuhusisha RAV 4 no T 455 CLA ya kugongana na lori. Taarifa za awali zinasema kuna waliofariki na kujeruhiwa.. Mungu awalaze mahali pema Marehemu na kuwapa uponaji majeruhi.
Taarifa kamili itawajia baadae

RIPOTI: Wanasayansi wamegundua uhai kwenye sayari hii

Mwezi wa Enceladus ambao uko kwenye sayari ya Saturn huenda ukawa mahali bora zaidi pa kwenda kutafuta maisha nje ya dunia.

Tathmini hii inatokea kufuatia uchunguzi katika sayari hiyo yenye kilomita 500 uliofanywa na Cassini.

Uchambuzi wa kemia wa Cassini unaonyesha matundu ya maji moto kwenye sakafu ya bahari ya Enceladus, maeneo ambayo yanahusishwa na kuwepo kwa maisha, hapa duniani.

Kuwepo kwa maji haya sio thibitisho kamili kwamba vitu vilivyo na uhai vinaishi katika mwezi huo mdogo lakini teknolojia zinaweza kutumika kupima maji hayo na kutoa ushahidi zaidi.

"Tuna uhakika kuwa kitu chenye uhai kinaweza kuishi kwenye bahari ya Enceladus lakini lazima tufanye utafiti zaidi," alisema mwanasayansi wa Cassini kutoka Taasisi ya Utafiti ya Southwest, San Antonio, Dkt. Hunter Waite.

"Iwapo hakuna maisha huko, ni sawa, lakini ikiwa maisha yapo itakuwa bora zaidi," alieleza BBC.

Bahari iliyopo kwenye Enceladus inakisiwa kuwa na kina kirefusana sana na yapo majimaji kwa sababu ya joto linalotokana na mvuto wa mara kwa mara kutoka kwenye sayari ya Saturn.

Cassini tayari amedhibitisha kwamba maji hayo yanashikana na sakafu ya bahari kutokana na aina ya chumvi na silika ambayo pia imeonekana katika mashimo.

Lakini wanachotaka kujua sana wanasayansi ni ikiwa maswala fulani yanayotendeka duniani pia yanaweza kufanyika katika Enceladus - kitu kinachoitwa serpentinisation, ambayo hutengeneza gesi ya hidrojeni.

"Kwa viumbe hai, hidrojeni huwa ni kama kama pipi - ni chakula wanachokienzi," alieleza Dkt Chris McKay, mwanabiolojia wa maswala ya anga wa shirika la Nasa.

"Ni nzuri sana kwa kuvipa nguvu, na inaweza kusaidia viumbe vidogo sana. Kupata hidrojeni itakuwa vizuri sana na itakuwa moja ya ushahidi utakaoonyesha uwezekano wa kuwepo na uhai."

Viumbe hai anavyozungumzia Dkt McKay vinaitwa methanojeni kwa sababu vinatengeneza gesi ya metheni vinapogusana na hidrojeni na gesi ya kaboni .

Nasa, ambayo inaongoza ujumbe wa Cassini , ilitakikana kufanya tangazo la hidrojeni miezi michache baada ya uchunguzi wa mwisho waroketi ya mwezini, Oktoba mwaka wa 2015.

Ziara ya Cassini sasa inakamilika . Baada ya kuizunguka Saturn kwa muda wa miaka 12, inaendelea kuishiwa na mafuta na sasa itawachiliwa kuingia kwenye anga ya dunia hiyo ya Saturn mwezi Septemba, kuhakikisha kuwa haiwezi kugongana na Enceladus na kusababisha kuchafuka kwake.

MAJAMBAZI Wanne Walioua Askari 8 Kibiti Wauawa, Msako Waendelea

Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8 wilayani Kibiti mkoani Pwana jana usiku.

Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya majambazi hao.

Amesema baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi, ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao.

Akielezea tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9 waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8 kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi.

Amewataja askari waliuawa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub, ambapo pia walipora bunduki 7 zikiwemo SMG 4.

Kufuatia tukio hilo, Kamishna Marijani ametangaza vita na waharifu wote katika maeneo hayo, ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaanza oparesheni maalum katika mkoa wa Pwani, kuhakikisha vinawasaka na kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua.

“Mpaka sasa jeshi limekwisha poteza skari zaidi ya 10, inatosha…. Tunakwenda kwenye oparesheni maalum, hatutakuwa na mzaha, tutawasaka popote walipo na kuwashughulikia kikamilifu, ,,, watajua tofauti ya moto na maji… mpaka jana idadi ilikuwa ni 8 kwa nne, lakini nawahakikishia kuwa ndani ya wiki moja idadi hiyo itakuwa imebadilika, na tutakuwa na hesabu tofati,” amesema Marijani

Kuhusu hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki katika maeneo yote ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji zaidi ya saa 12:00 jioni. Amesema usafiri wa boda boda utaruhusiwa kati ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni

Kauli ya Rais Magufuli Baada ya Askari Nane Kuuawa Mkoani Pwani..!!!

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi.

Mhe. Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu, familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo. 

“Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao  wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa, naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu. 

“Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amelaani tukio hilo na matukio yote ya kuwashambulia askari polisi ambao wanafanya kazi kubwa na muhimu ya kulinda raia na mali na ametaka Watanzania wote watoe ushirikiano katika kukomesha vitendo hivyo.

Mhe. Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

MAJAMBAZI Wanne Walioua Askari 8 Kibiti Wauawa, Msako Waendelea

Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8 wilayani Kibiti mkoani Pwana jana usiku.

Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya majambazi hao.

Amesema baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi, ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao.

Akielezea tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9 waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8 kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi.

Amewataja askari waliuawa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub, ambapo pia walipora bunduki 7 zikiwemo SMG 4.

Kufuatia tukio hilo, Kamishna Marijani ametangaza vita na waharifu wote katika maeneo hayo, ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaanza oparesheni maalum katika mkoa wa Pwani, kuhakikisha vinawasaka na kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua.

“Mpaka sasa jeshi limekwisha poteza skari zaidi ya 10, inatosha…. Tunakwenda kwenye oparesheni maalum, hatutakuwa na mzaha, tutawasaka popote walipo na kuwashughulikia kikamilifu, ,,, watajua tofauti ya moto na maji… mpaka jana idadi ilikuwa ni 8 kwa nne, lakini nawahakikishia kuwa ndani ya wiki moja idadi hiyo itakuwa imebadilika, na tutakuwa na hesabu tofati,” amesema Marijani

Kuhusu hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki katika maeneo yote ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji zaidi ya saa 12:00 jioni. Amesema usafiri wa boda boda utaruhusiwa kati ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni

Gallery

Popular Posts

About Us