KINGAZI BLOG: 11/27/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday, 27 November 2016

Wakosoaji wa Castro wafurahia kifo chake

Wakosoaji wa mwanamapinduzi, aliyekuwa kiongozi wa Cuba, Fidel Castro, wanaoishi Miami, nchini Marekani, kilomita 200 kutoka ufuo wa Bahari wa Cuba, walifanya maadhimisho ya hadharani kufuatia kutangazwa kwa kifo cha kiongozi huyo.

Wengi wao walihamia Miami baada ya Castro kupindua Serikali yenye ufisadi mkubwa, iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani mwaka 1959.

Wengine wengi waliungana nao baada ya muungano wa Sovieti, taifa lililokuwa likifadhili Cuba, kusambaratika na kusababisha mfumuko mkubwa wa bei.

Wakaazi wengi waliokumbuka umaskini na mateso ya kisiasa na kidini aliyokuwa akiwalimbikizia Castro, wengi waliendesha magari yao wakipiga honi kwa shangwe
Wengi walisikika wakipiga makelelewa wakisema Cuba sio Castro No!.

Tabia ya wizi imeibuka mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam

Abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam wameomba waendesha mradi UDA-RT kuimarisha ulinzi katika vituo vya mabasi hayo kutokana na kuibuka kwa tabia ya wizi katika vituo hivyo jambo ambalo hapo awali halikuwepo.

Wakizungumza na Channel Ten abiria hao wamesema wanadhani tatizo hilo limeibuka katika kipindi hiki kutokana na kusitishwa kwa daladala zinazotumia barabara ya morogoro hivyo vibaka waliokuwa wakifanya vitendo hivyo katika vituo vya daladala kuhamia katika vituo vya mbasi yaendayo haraka na kuwaibia abiria pindi wanapogombania kuingia kwenye mabasi hayo.

Licha ya kuwepo kwa wizi katika mabasi hayo baadhi ya abiria wameiomba mamlaka husika kukamiliksha miundombinu iliyosalia hususn kufunguliwa kwa milango ambayo kwa asilimia kubwa bado haijakamilishwa mashine za kukagulia tiketi hivyo kutoruhusu abiria kutumia milango hiyo jambo ambalo limekuwa na usumbufu kwani abiria hulazimika kutumia mlango mmoja na kupanga foleni ndefu.

Mmoja wa watumiaji wa usafiri ameshauri kuwepo kwa utaratibu wa kupanga foleni wakati wa kuingia kwenye mabasi hayo ili kuepuka msongamano na kuumizana wakati wa kugombania usafiri huo.

KUFUATIA Agizo la Waziri wa Elimu Wanafanzi wa IFM Wavuliwa Majoho Katikati ya Mahafali

Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeanza utekelezaji wa agizo la Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kwa kuwazuia wahitimu wa ngazi ya cheti na stashahada kuvaa majoho na kofia wakati wa mahafali yao.

Kitendo hicho kilitokea katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam juzi baada ya mratibu wa mahafali ya 42 ya IFM, Dk. Godwin Kaganda, kutangaza utaratibu huo licha ya wahitimu wao kuvaa majoho yao.

Dk. Kaganda alisema utaratibu huo ni kwa mujibu ya miongozo iliyotolewa na Serikali kuhusu uvaaji wa majoho, ambao unataka yavaliwe na wahitimu wa kuanzia ngazi ya shahada na kuendelea.

“Wahitimu wote wa ngazi ya cheti na stashahada hamtovaa majoho wala kofia pamoja na kwamba mlishapewa awali, tunaomba radhi kwa sababu ndiyo miongozo tuliyopewa,” alisema Dk. Kaganda.

Wiki iliyopita, Profesa Ndalichako  alipokuwa akiwatunuku vyeti wahitimu wa mafunzo ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa njia ya masafa, iliyotolewa na Wakala wa Usimamizi na Uongozi wa Elimu (ADEM) mkoani Mbeya, alisema kumekuwa na matumizi holela ya majoho suala linaloshusha hadhi yake na kuagiza yavaliwe kuanzia ngazi ya shahada.

“Siku hizi hata mwanafunzi akimaliza chekechea anavalishwa joho. Nafikiri haya majoho yangebaki kwa wanaohitimu digrii peke yake, ili hawa wengine nao watamani kufika ngazi hiyo na si kila mtu anavaa,” alisema Profesa Ndalichako.

Katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 2,857 wa ngazi za cheti, stashahada, shahada, stashahada ya uzamili na shahada ya uzamili walihitimu masomo yao.

Akizungumza katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la IFM, Profesa Letisi Rutashoga, alielezea changamoto katika utekelezaji wa mpango wa muda mrefu wa chuo hicho, ikiwamo kupanua miundombinu na utoaji wa taaluma.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni uhaba wa fedha za kuanza mradi wa ujenzi wa kampasi mpya ya Msata iliyopo Bagamoyo na kuiomba Serikali kuupangia Sh bilioni 2.5 katika mwaka ujao wa fedha.

Pia aliomba kuyafanyia kazi mapendekezo ya kubadilisha sheria namba 3 ya mwaka 1972 iliyoanzisha chuo hicho, ili iweze kuendana na malengo ya sasa ya uendelezaji wa chuo.

 

Gallery

Popular Posts

About Us