Saturday, 15 October 2016
PICHAZ++: MSANII TUNDA AFUNGA NDOA RASMI HEBU ONA HAPA
Madee (kutoka kulia), Tunda Man na mke wake (katikati’ Kassim Mganga pamoja na Dogo Janja
Mkali wa wimbo ‘Mama Kijacho’ kutoka Tip Top Connection, Tunda Man amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu aitwae Sabrah
Ndoa hiyo ambayo imefanyika Ijumaa hii huko mkoani Morogoro nyumbani kwa Bi Sabrah, ilihudhuriwa na mastaa wa muziki kutoka Tip Top Connection. Angalia picha.
Miadee akwa na shemeji yake
Tunda Man akipongezwa na mtu wake wa karibu
HIVI HAPA VIGEZO VYA UTOAJI MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWA 2016-2017
Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, imekuwa ikiwakopesha wanafunzi wenye sifa za kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini kugharimia masomo yao. Katika utekelezaji wa jukumu hili, Serikali huandaa Sifa na Vigezo vya Utoaji Mikopo kila mwaka ili kuendana na malengo na matarajio yaliyopo katika mipango na mikakati ya kitaifa kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17 -2020/21),Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) na Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Kwa kuzingatia mipango mikakati na sera hizo, pia Mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2016/2017 katika mwaka wa masomo 2016/17, Serikali imetoa vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji mikopo kama ifuatavyo:
(i) Vipaumbele vya kitaifa vinayoendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mafunzo ambayo yatazalisha watalaamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele kama vile:
Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia
Sayansi Asilia na Mabadiliko ya Tabianchi
Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu
(ii) Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji maalum kama vile Ulemavu na Uyatima
(iii) Ufaulu wa waombaji katika maeneo ya vipaumbele na umahiri Kwa hivi sasa Bodi imekamilisha uchambuzi wa majina ya waombaji ambao wana sifa zilizoainishwa hapo juu na majina ya wanufaika wapya yatatangazwa leo tarehe 14 Oktoba, 2016.
Aidha, kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao (means tested) katika vipengele vyote vya mikopo.
Samsung Galaxy Note 7 marufuku kwenye ndege Marekani.
Idara ya uchukuzi nchini Marekani imepiga marufuku simu za Samsung aina ya Galaxy Note 7 kwenye ndege zote nchini humo.
Hii ni baada ya visa vya simu hizo kushika moto kuripotiwa.
Abiria hawataruhusiwa kubeba simu hizo ndani ya ndege au hata kwenye mizigo yao wakiingia au kutoka Marekani kuanzia Jumamosi saa 16:00 GMT.
Idara ya uchukuzi ya Marekani ilikuwa awali imewashauri abriia dhidi ya kuweka simu hizo kwenye mikoba yao.
Samsung ilitangaza kwamba haitaunda tena simu hizo wiki hii.
"Tunatambua kwamba kupigwa marufuku kwa simu hizi ndegeni kutatiza baadhi ya abiria, lakini tunazingatia sana usalama wa watu walio ndani ya ndege," karibu wa uchukuzi Anthony Foxx alisema kupitia taarifa.
Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.
Walipewa simu mpya ambazo zilidaiwa kuwa salama
Lakini taarifa zilitokea baadaye kwamba hata simu hizo zilizodaiwa kuwa salama zinashika moto.