KINGAZI BLOG: 02/05/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday, 5 February 2017

Happy birthday Lop's Miraculo. Live long brother

Leo ni siku ya kuzaliwa mwanangu wa nguvu artist mkubwa mwenye asili ya bongo ila yuko kwa Nkurunzinza akifanya yake huko. HAPPY BIRTHDAY BROTHER, ongeza juhudi kupitia kipaji chako.Utafika mbali

Hii hapa kauli yaVanessa Mdee baada kutajwa na makonda sakata la madawa ya kulevya

Iliwashangaza wengi baada ya Vanessa Mdee naye kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya mastaa wanaohusishwa na biashara ya madawa ya kulevya. Ni shutuma nzito, na hata kabla uthibitisho rasmi haujatoka, madhara ya kutajwa majina yao yameanza kuonekana katika maisha yao

Wito huo umemkutia Vee Money akiwa nchini Afrika Kusini anakoshoot tamthilia ya MTV Shuga, na bila shaka atalazimika kukatisha kwa muda na kurudi Tanzania kwenda kituo cha polisi central, anakotakiwa Jumatatu ya kesho.

Pamoja na hivyo, Vee ameonesha kuvuta pumzi ndefu na kuacha maisha yaendelee kama yalivyo. Kupitia Instagram, Vee amepost picha hizo juu na katika ile aliyokaa ameandika: The show must go on … bomb ass dress from @asos #FILA.

Kwenye hiyo black and white ameandika: The night is darkest before the dawn. #Breakthrough #Juu #CashMadame #SheKing.”

Kwenye picha hizo amezima comments ili kuepuka maneno ya kejeli kutoka kwa baadhi ya watu ambao tayari wamefanya hivyo kwenye picha zingine. Vee anaungana na mastaa wengine wakubwa wakiwemo Wema Sepetu, Mr Blue, TID na wengine kwenye orodha hiyo.

Maajabu ya mwaka!!! Auawa Kwa Kutopiga Mswaki.


IRIS HERNANDEZ-RIVER (20) mwanamke mkazi wa Gaithersburg, Jimbo la Maryland, Marekani, alimwua binti yake, Nohely Alexandra Martinez Hernandez mwenye umri wa miaka minne kwa kutopiga mswaki.

Mama huyo alikasirishwa na kitendo hicho jana ambapo alimpiga teke la tumboni binti yake huyo na kusababisha binti huyo kudondoka na kugonga kichwa chake ukutani.

Ilimchukua Iris muda wa saa moja kupiga namba 911 ili binti yake apatiwe msaada ambapo Nohely alifikishwa hospitali akiwa mahututi na baadaye kufariki jana hiyo hiyo.

MUNGU SI ATHUMANI!!! HEBU JIONEE PICHA YA MTOTO ALIYEOKOLEWA KUTOKA KATIKA HALI MBAYA MTAANI ALIVYO SASA HIVI

Sura ya furaha inaendelea kuonekana kwa mtoto Hope aliyechukuliwa mtaani nchiniNigeria wakati huo akiwa na miaka miwili baada ya kuachwa na Wazazi wake ikisemekana ni Mchawi.

Inasemekana alitelekezwa na familia yake kwa sababu walidhani yeye ni mchawi ambapo baadae akapatikana mtaani na kuchukuliwa na Mwanamke raia wa Denmark Anja Ringgren Loven aliyejitolea kumlea na kuishi nae.

Baada ya kuchukuliwa kutoka mtaani January 2016 picha mbalimbali zimekua zikitoka zikionyesha maendeleo ya Hope akionekana amenawiri kiafya na hata shule anasoma.

Hapa chini ni picha zake za kabla na baada ya kuokotwa…

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya February 5



 

Gallery

Popular Posts

About Us