Iliwashangaza wengi baada ya Vanessa Mdee naye kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya mastaa wanaohusishwa na biashara ya madawa ya kulevya. Ni shutuma nzito, na hata kabla uthibitisho rasmi haujatoka, madhara ya kutajwa majina yao yameanza kuonekana katika maisha yao
Wito huo umemkutia Vee Money akiwa nchini Afrika Kusini anakoshoot tamthilia ya MTV Shuga, na bila shaka atalazimika kukatisha kwa muda na kurudi Tanzania kwenda kituo cha polisi central, anakotakiwa Jumatatu ya kesho.
Pamoja na hivyo, Vee ameonesha kuvuta pumzi ndefu na kuacha maisha yaendelee kama yalivyo. Kupitia Instagram, Vee amepost picha hizo juu na katika ile aliyokaa ameandika: The show must go on … bomb ass dress from @asos #FILA.
Kwenye hiyo black and white ameandika: The night is darkest before the dawn. #Breakthrough #Juu #CashMadame #SheKing.”
Kwenye picha hizo amezima comments ili kuepuka maneno ya kejeli kutoka kwa baadhi ya watu ambao tayari wamefanya hivyo kwenye picha zingine. Vee anaungana na mastaa wengine wakubwa wakiwemo Wema Sepetu, Mr Blue, TID na wengine kwenye orodha hiyo.
0 comments:
POST A COMMENT